Joseph Kibwetere and Ugandan Cult Mass Murder/Suicide

Dini ni moja ya njia zinazotumiwa na watu kuteka akili za wengine, mtu akija kwa gear ya dini wengi wetu tunakua wadhaifu sana hata kufikiria mita moja mbele yetu tunashindwa
 
Kibwetere inasemekana hakufa katika tukio hilo na akakimbilia kusikojulikana, japo madai haya hayana ushahidi
 
Mwalimu wangu wa Divinity miaka ya nyuma aliwahi kutusimulia hiki kisa akiwa anatufundisha ila nilisikitika sana hakika Mungu mkubwa hawa viongozi walifanya jambo baya
 
Hawa nawafananisha na pool of siloam na viimani vyao vya ajabu ajabu, wale tusishangae siku moja wamejilipua kama hawa Wa Kibwetele
 
Kibwetere ni mmoja wa Magurru( walimu wa dini) hatari sana....
Dunia imefanikiwa kuwapata GURRUS wawili tu wakweli ambao ni Yesu Kristo wa Nazareth na Mtume Mohamed SAW.
Kibwetere alifanikiwa kuwateka akili hata wasomi wa Phd (viongozi wa dini wakiwemo kwamba anayofikiri na kuyatamka yeye ndio sahihi).
Sasa tusubiri UNYAKUO ujao muda si mrefu...
@Gentaaaaa
 
WAFUASI WA KIBWETERE NA MAUAJI YA HALAIKI (Part 2)
IMG_20180807_125124_229.jpg

Mawazo ya kuwa watu walijiua kwa kujichoma moto yalififia taratibu baada ya uchunguzi kuanza kufanyika . siku chache baada ya mauaji polisi waligundua vyoo vya shimo vitano vikionekana kusakafiwa siku chache tu. Kimoja kilikuwa wazi na vingine vilikuwa vimefungwa.

Bwana afya Richard Opira alinukuliwa akisema wamekuta miili mitano vyooni na walipochungulia ndani ya vyoo waliona miili mingine mingi zaidi. hawakuwa na majeraha hivyo inadhaniwa walinyongwa au kupewa sumu. Hadi kufikia machi 21, miili sita ilikuwa imeondolewa ndani ya vyoo, mitatu kati yao ikiwa imechanwa tumboni ,mmoja ukiwa una fuvu lililopasuka. Daktari Sam Birungi alisema baadhi walikuwa wamepigwa Vibaya wengine wakiwa wameunguzwa na baadhi kulishwa sumu na miili yao kutupwa chooni.
Miili 153 iligundulika katika eneo lingine linalomilikiwa na kundi hili karibu na mji wa Buhunga, miili 155 ilikuwa imezikwa katika kaburi la pamoja Katika shamba la miwa la padre Dominic kataribabo .
Inasemekana walikufa kama mwezi mmoja Kabla ya tukio .
Miili mingine 81 ikiwemo watoto 44 iligundulika katika shamba la Joseph Nyimurinda .

Mpaka kufikia Aprili 3 ,2000 baadhi ya maeneo ya viongozi yalikuwa hayajachunguzwa kwa kina kwa kile kilichosemekana kukosekana kwa vifaa vya kisasa vya uchunguzi.
Wafuasi wa kibwetere waliaminishwa kuwa viongozi walikuwa wakipokea maono ya bikira maria ambaye ndiye Kiongozi wa safari ya mbinguni kuelekea mwisho wa dunia mwaka 2000.
Walihubiri kuhusu siku ya mwisho wakiwaelezea namna matofali makubwa yatakavyoporomoka na nyoka wakubwa kama matairi ya trekta, watashuka toka mbinguni kuadhibu watu wasiokuwepo katika kundi lao .
Walihubiri juu ya siku tatu za giza ambazo zitaikumba dunia na Kanisa lao litakuwa kama safina ya Noah , waliomo ndani tu ndiyo wataokolewa na ndiyo sababu ya kupigilia misumari madirisha na milango ili waokolewe wao tu .
Waliishi katika maombi yenye usiri kubwa na hivyo kuondoa ukaribu na watu wa nje .wengine wakijitenga na ndugu na familia zao kwa kuwa ni wadhambi waliokataa kulifuata kundi.

Waliaminishwa wao ni watu wa kipekee waliosafi wanaosubiri kuiona mbingu na watu wengine ni wadhambi wanaongoja kuadhibiwa na mungu hivyo wale waliokuwa ndani ya kambi waliishi wakijiona bora sana kuliko wengine wote. Walifunga Kwa Siku tatu na walipunguziwa idadi ya milo kwa Siku ,walisafirishwa Usiku tu na hivyo kutoonekana kwa majirani mara kwa mara na kambi yao ilizungushiwa fensi iliyozuia muingiliano na watu wa nje, kuna Wakati hawakuruhusiwa kuongea kabisa ila waliambiwa watumie lugha ya ishara ili wasivunje amri inayosema usimshuhudie jirani yako uongo.

Kushiriki tendo la ndoa hata kwa wanandoa ilikuwa dhambi kubwa, hawakuruhusiwa kuzaa watoto zaidi baada ya kujiunga na kundi, walioshindwa waliondoka mapema . walijengewa hofu na hali ya utegemezi kiimani na kimali wapo waliochomewa mali zao kwa madai bikira maria alitoa maono kuwa wanaomiliki mali hizo wamemkasirisha kwa matendo yao, kadiri watu walivyokuwa masikini na kuwa tegemezi kwa viongozi ikawa kama faraja yao, ndiyo viongozi walivyoweza kuwatawala kifikra na kimaisha.

Kuna mengi ya kusikitisha ........ikiwemo watu kukataliwa kutumia dawa za hospitali wakati viongozi wao wakitibiwa hospitali ,kutenganisha familia Kwa kuwagawa watoto kwenda kuishi mbali na familia Sambamba na mauaji ya kinyama ya kisirisiri yalipobainika baada ya mauaji. Walilazimishwa watu kuvaa sare hasa baada ya kuhamia kambini, kundi hili lilijitahidi mno kujiweka karibu na viongozi na kufuata sheria ili wasichunguzwe wala kutuhumiwa kwa lolote.

Theresa kibwetere mke wa Joseph kibwetere kabla ya kutengana ,alipohojiwa alisema ,yeye na mumewe walihudhuria mkutano wa credonia mwerinde . baada ya ibada mwerinde ambaye alishatengana na mumewe ,alimfuata kibwetere na kumweleza maono aliyopokea kuwa aliambiwa amtafute mtu aitwaye kibwetere na aambatane nae.
Na hivyo ndivyo walivyoanza kumshawishi mumewe kuingia katika harakati , wakati huo mwerinde akiwa na wanawake wengine wawili ,walianza kuishi nyumbani kwake na wiki moja baadae nyumba iligeuka kituo cha maombi credonia akileta watu alivyotaka yeye huku akilazimisha kulala pamoja nao na kumzuia Theresa tendo la ndoa na mumewe. Walileta imani zao, wakipunguza milo katika familia ,kuadhibu vikali watoto pale waliposhindwa kufuata kanuni walizowekewa ikiwemo kufunga kwa siku kadhaa alizotaja yeye.

Hali ilizidi kuwa mbaya Mwerinde alipoanza kumueleza Joseph kibwetere namna yeye Theresa alivyo mwanamke mdhambi atakayemzuia kwenda mbinguni . Joseph akaanza kumchukia mkewe, Mugambwa Kijana wa kibwetere anasema mwerinde alianza kuwa katili kwao, akilipuka kwa hasira mara kwa mara na kutoa adhabu ngumu kwa watoto kama vipigo vikali mno ambavyo alidai alitumwa na Bikira Maria kwa kuwa hawakutaka kumtii ,baada ya miezi kadhaa ya mateso na mabadiliko ya ajabu katika familia yao ,ndugu waliingilia kati na kuwatimua mwerinde na wanawake aliokuja nao na Joseph kibwetere akaikana familia yake na kuambatana na Mwerinde, Theresa anasema haamini mumewe alishiriki katika mauaji hayo, anachojua, hiyo ilikuwa kazi ya Credonia mwerinde mwanamke kichaa aliyekuja kumvurugia ndoa yake ya miaka 30.

Tofauti na mama yake ,Mary kibwetere ,binti wa kibwetere anasema baba yake alikufa kabla ya tukio hilo na kwamba alikuwa akiugua ugonjwa wa akili ambao daktari aliyemtibu alithibitisha hili la Joseph kuwa mgonjwa wa akili .
Mary anasema padre Dominic kataribabo akamuondoa hospitali kimya kimya na kwenda kumfungia katika moja ya nyumba zao hadi alipokufa na kuzikwa kama mbwa.
Familia imekuwa ikijaribu mno kumsafisha Joseph kibwetere lakini imeshindikana kabisa kutenganisha "Kanungu massacre" na jina la kibwetere .
Kuna "warrant" ya kutafutwa Joseph kibwetere ,Inasemekana Credonia na Joseph walikimbia baada ya tukio, wapo wanaoamini kuwa walikufa katika moto huo na wapo wanaoamini kuwa kibwetere yupo hai akiishi mafichoni Malawi, na mara kadhaa mwaka 2001/2002 ilidaiwa kuonekana Kwa kibwetere nchini Tanzania .

Hakuna mwenye uhakika kama kibwetere alikufa pamoja na wafuasi wake au alitoroka na pesa alizochuma kwenda kuishi na mwerinde, hakuna anayefahamu hilo mpaka leo.
Baada ya miaka 18, sasa kumekuwa na taarifa tofauti tofauti kuhusu tukio hili la kuhuzunisha ,moja ya ripoti ilisema polisi waliarifiwa juu ya mpango unaotia shaka katika Kanisa hili lakini hakuna hatua zilizochukuliwa .eneo lilipotokea mauaji haya kumekuwa na stori za kuonekana kwa mizimu ya watu walioungua ,palikuwa na mpango wa kujenga makumbusho ,mpango ambao unazidi kuwa ndoto kadiri miaka inavyokatika. Serikali ya Uganda kwa kukosa vifaa bora na weledi katika hatua za kuchunguza ,mambo mengi yamebaki kama kitendawili alichoachiwa mungu kujibu. Mamia ya miili iliyofukuliwa ilizikwa upya pasipo kutambuliwa kujua ni akina nani na hivyo kuachia watu vitendawili vingi kuhusu ndugu zao wasiojua walipo, eneo lilipotokea tukio limegeuka kuwa pori,na kuna nyumba kadhaa za kuhesabika.

Pia soma >Wafuasi wa Kibwetere na mauaji ya halaiki (part one) - JamiiForums
 
WAFUASI WA KIBWETERE NA MAUAJI YA HALAIKI (Part 2)
View attachment 833605

Inahizunisha sana,na kusikitisha sana,haitasahaulika milele
 
Back
Top Bottom