Shyshii
JF-Expert Member
- May 19, 2013
- 439
- 540
Kisaikolojia wewe ni kwamba umebabaika sana na sasa una waya waya tu! Kila chaka lina shetani wake na Magufuli ni shetani wa chaka la mafisadi yaani magufuli ni mzee wa kudeliver na style yake ya uongozi ni kiboko kwa watu wa aina yetu huku bongo ambao hatuwezi kufanya kazi wenyewe kwa hiari yetu hadi tukaliwe kooni. Kuna step tulipitishwa haraka haraka tukadhani tumekomaa kujisimamia kumbe bado tulihitaji kusimamiwa na kuelekezwa kabla ya kusimama wenyewe. Mwenye kipaji cha kutugeuza tuwe chombo cha ku deliver ni Magufuli peke yake maana haogopi mtu yeyote kwake kazi tu na kutoa na matokeo makubwa sasa. Haogopi, hachoki, hasahau, hatanii, hapotezi muda na yuko very focused. Waulize mafisadi wametimkia chadema kwa nini? Ni kwa sababu ya utisho wa Magufuli na kwamba hawana mkono katika kupatikana kwake hivyo they can't ever control him. Hapa kazi tu hayo mengine bakini nayo huko kwenye sewage system na dampo la taka za ccm.
Kama usemayo yana ukweli ndugu yangu jaribu kumwambia mkuu wa kaya wamkate huyu fisadi wetu sielewi ni nini kinachomshinda mkuu wa kaya kumkamata na kumfunga na kurudisha hela zetu au kutaifisha mali za huyu fisadi mkuu
Yaani kama leo mi ndo nimechefuka kabisa kwenye taarifa ya habari ya saa mbili eti Magufuli anasema " umeme huu unao katika katika ni matokeo ya ufisadi wa huyu huyu mamvi" ina maana mr.mamvi ana nguvu kuliko mkuu wa kaya???? huyu mtu ana jeshi la kukodi marekani au???? kwanini kutuaminisha ni fisadi halafu serikali haiwezi kumkamata???? nachefuka kusikia uongo wa KIWANGO cha juu namna hii, Mungu ibariki Tanzania.