John Mashaka Ni Mbunge Mtarajiwa!

Status
Not open for further replies.
i currently endorse Mashaka as the new chairman of CHADEMA !! uchumi inaelekea anaujua, na hatokopa na kushindwa kulipa kama current chairman !
 
MTANZANIA ANAYEISHI MAREKANI BWANA JOHN MASHAKA AMEKUWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI HASA BLOGS MBALIMBALI KUWA NI MTU ATAYEWEZA KUISAIDIA NCHI YETU KWA KIASI KIKUBWA AKIWA MBUNGE 2010.

IKIWA ATAFANIKIWA KUUKWA UBUNGE BASI WATANZANIA TUTAKUWA NA KICHWA KINGINE TOKA MAREKANI BAADA YA AMANI WALID KABOUR MBUNGE WA AFRICA MASHARIKI KWA SASA.

TUNAOMBA MAONI YETU JEE KIZAZI CHA DIASPORA KINA UWEZO MZURI WA KULIKOMBOA TAIFA LETU?
KABOUR ALILETA MABADILIKO YA KWELI?

INTERVIEW YA MASHAKA IKO MICHUZI BLOG AU INAPATIKANA HAPA.

http://issamichuzi.blogspot.com/2008/04/john-mashaka.html#comments

Kwani kila Mtanzania anayefanya vizuri lazima aingie kwenye siasa!? :confused:
Prof Sarungi alikuwa anafanya vizuri sana pale Muhimbili kama Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili na alikuwa kipenzi cha kila mfanyakazi wa pale. Sifa zake zikavuma 'vingunge' wakamwambia akagombee ubunge matokeo ya yeye baada ya kuingia kwenye siasa tunayajua. Mwacheni aendelee kufanya vitu vyake na msitake kumuhusisha na mafisadi.
 
Huyu John anatarajia kugombea ubunge jimbo gani?amejiandaaje kuwasaidia watu mahali husika?
Wengi wameingia na gia nzuri ya kujieleza watafanya hiki na kile,hatimaye imekuwa ziiiii?
 
Ungetuambia umepewa ngapi kwa debe hili ndani ya JF halafu tuendelee na mjadala vinginevyokutumbia mtu yupo marekani anataka kuja kugombea ubunge bongo So?
nenda kijijini kwake au jimbo analotarajia kugombea mkadanganye watu its nothing 2 do with us
 
i currently endorse Mashaka as the new chairman of CHADEMA !! uchumi inaelekea anaujua, na hatokopa na kushindwa kulipa kama current chairman !

KadaMpinzani hapo sasa unazidi.....

Unawaambia watu kwenye hii thread wanyamaze, kumbe wewe ndo unatakiwa kunyamaza.

Kuna wakati una good points, lakini tatizo huo ukada ndo umekuzidi....Nasikia kwenye chama mnalipwa bonuses kulingana na namba ya posts hapa JF, si bure...
 
Ufisadi wa EPA, Richmond wadhalilisha Watanzania Marekani
Na James Magai (Mwananchi)
Mashaka alisema, Watanazania waishio Marekani, wameridhika na juhudi za Rais Jakaya Kikwete kuboresha maisha ya wananchi na kuweka Tanzania katika ramani nzuri.

Hapa I can smell a very big RAT kwa nini mtu usifie pale ambapo hapana sifa! Huyu hafai kabisa kuwa mbunge. Kila mtu anaona hakuna kitu cha maana JK amefanya kumridhisha mtu yeyote yule aliyepo hapa TZ au kokote kule duniani. Na kuhusu kuiweka tz katika ramanai hapa nampa JK mia ya mia he is all over the place huku akitembeza smile and nothing else.

Pia, alielezea kuridhishwa na jinsi wabunge wa chama tawala na vyama vya upinzani, walivyoungana na kushirikiana katika sakata la Richmond na kufanikiwa kuwang'oa mafisadi.
Na hakuna fisadi yeyote aliyengolewa as always too much talk and no action. Mafisadi wameketi tu upande wa kushoto wakiendeshwa na dereva anayesubiri maelekezo kutoka kwao.
 
Ungetuambia umepewa ngapi kwa debe hili ndani ya JF halafu tuendelee na mjadala vinginevyokutumbia mtu yupo marekani anataka kuja kugombea ubunge bongo So?
nenda kijijini kwake au jimbo analotarajia kugombea mkadanganye watu its nothing 2 do with us

Nimeleta hoja si kupiga debe tizama vizuri maandiko yangu, hoja yangu ni kuwa jee kila king'aacho ni dhahabu? kwenye Blog nyingi wanaweka positive zake tu nataka hapa tupate bothsides.
 
John Mashaka ,

nilisikia toka sehemu kuwa anautaka Ubunge wa jimbo la Ubungo toka mwaka juzi wakati ambapo na marehemu amina naye alikuwa anataka kujitosa katika pilika za kujianda na kulikamata jimbo hili.

karibu ila nakuaambia kazi unayo,2010 nadhani Mnyika JJ umri utakuwa umetosha na atakamata jimbo la Ubungo.Hii ni wazi hata mie kama Kada najua Mnyika is going to win that Jimbo.

Kampeni Nzuri kijana na endela tu
 
Tumeshavamiwa tayari...!

Raya yangu ni kuwa, JF ina vichwa hatari hata mtu angekujana mbwembwe nyingi kiasi gani... ataelezwa mbwembwe zake.

I like/love you guys!

Kama mheshimiwa haelekei kuelewa, mwelekezeni blogs za kampeni, mbona pia zipo!
Hapa tuko kazini actively, sio kisiasa. mpaka ukachaguliwe, ukarudishe gharama zako, na kujiweka sawa kama wengine, ndipo utukumbuke sisi tutakuwa wap? marekani, marekani, mnajua wengine tuliko lakini? Siku hizi sio dollar tena ni...! wajanja wanajua wala sio Pound..!
 
Hahahaha week end hii itakuwa tamu....well put mazee....ama ni mwenyewe Mashaka alitundika hii kuangalia upepo JF kweli tupo kazini, blog za kampeni zipo nyingi hahahahah
 
Nataka tutumie mjadala huu kunoa vichwa vyetu.mara nyingi watu toka nje huwa wanatuleta habari za kujikweza zaidi kuliko uhalisia wa mambo.

Bwana Jack Pemba alisema anakuja kusaidia vipaji vya mpira wa miguu matokeo yake sasa hivi anashinda Twanga Pepeta au Akudo Impact.

Jack Pemba ni mwana DIASPORA..

Jamani ujumbe wa hii thread uko hapo juu! mbona mnapindisha mada? wana diaspora mko wapi..twambieni mnakuja kuchangia haya maendeleo ya taifa kivipi? tupeni mikakati yenu...maana tunaambiwa nyinyi ndugu zetu mlio nje mna exposure, kizungu kinapanda (ambacho ndo wawekezaji wanataka) na mengineyo...jamani tupeni insights basi. Ni kweli kwamba tuna mengi ya kujifunza kwenu, labda mnaweza mkaja na MUAROBAINI WA MATATIZO YETU maana juhudi za akina KADA na wenzake tulio hapa mjini hali ni ngumu!!!! We need you guys....

Mi nawasubiri wana wa diaspora waje watupe vitu hapa na mikakati yao....kwa wenye mpango wa kurudi bongo.

Kuhusu Mashaka sina comment..ila sasa naona wana diaspora wenzake wamemgeuka kwamba hawakumtuma kumpongeza Kikwete..kazi ipo...
 
Habari zenu wazee wa Jambo Forum?

Ama Hakika Mmeniangusha sana hamjamjua Mashaka ni Mwanakijiji, yeye anacheka kuona Kada Mpinzani ameshindwa kumtambua.

Mwanakijiji kama nilivyosema siku za nyuma huko ni kijana toka mkoa wa Musoma na amekuwa akivutiwa sana na Mwalimu Nyerere, kwenye mada hii amechangia kwa kumuunga Mkono Mashaka ambaye ni yeye Mwenyewe.

Ushahidi wa wazi inapotokea mjadala kama huu angeingia na majina yake mengine lakini amekuwa kimya kuona upepo uko vipi.
Kila siku watu wanasema kuwa JF ni mwisho wa yote kwanini mmeshindwa kumjua Senior member wetu?

Mwanakijiji

Naona saa yako ya ukombozi imefika karibu sana mwaka jana alikuja live Kitila Mkumbo na 2008 umekuja live, nani atakupa ubunge labda Mbowe na Chadema, huna shule wala nini.

naona Jambo Forum imekuua macho kiasi cha kuvaa miwani kama kobe,ulitegemea nini unakesha kwenye computer 24 hrs hizo ndizo disadvantages za Computer bwana M.M. MWANAKIJIJI=MASHAKA MASUMBUKO MWANAKIJIJI ameanza kuharibiwa macho.

jina la John amekuwa akilitumia kama John Almas kwenye redio yake.
sasa utagombea jimbo gani?
 
Mwanakijiji unamjua mheshimiwa Mashaka? ikiwezekana mfanyie interview tumjue zaidi.

makala nyingine inasema kuwa MASHAKA ni mfano wa kuigwa click hapa chini,

http://issamichuzi.blogspot.com/2008/03/mashaka-ni-mfano-wa-kuigwa.html

Vizuri tujue wapi kasaidia kama alivyosema mjumbe mmoja kuwa MAMA THEREZA alikuwa akijitolea na tunajua wapi alisaidia kama vile Mburahati kituo cha Yatima.

haitoshi kwa Mashaka kusema anajitolea ila hataki kusema wapi kapeleka lakini kutokea kwenye mitandao hakatai.

Tanzania kuna NGO karibu elfu hamsini zote zinasema zinasaidia masikini lakini hatujui wapi zinafanya kazi.

turudi kwenye swali la msingi kizazi cha DIASPORA kinaweza kutuongoza?

Mzee K.
Labda niseme ni uzee wako, atajifanyia vipi interview yeye mwenyewe? msaada katoa kwenye JF ana post zaidi ya elfu nane na anaandika makala magazeti,anamiliki redio na website.
 
Tumeshavamiwa tayari...!

Raya yangu ni kuwa, JF ina vichwa hatari hata mtu angekujana mbwembwe nyingi kiasi gani... ataelezwa mbwembwe zake.

I like/love you guys!

Kama mheshimiwa haelekei kuelewa, mwelekezeni blogs za kampeni, mbona pia zipo!
Hapa tuko kazini actively, sio kisiasa. mpaka ukachaguliwe, ukarudishe gharama zako, na kujiweka sawa kama wengine, ndipo utukumbuke sisi tutakuwa wap? marekani, marekani, mnajua wengine tuliko lakini? Siku hizi sio dollar tena ni...! wajanja wanajua wala sio Pound..!

Hatujavamiwa Mashaka ni senior Member, hapa ni nyumbani kwake, lazima sisi tuanze kum support na wengine waige kutoka kwetu.
wewe ndio umevamia hapa sababu umemkuta Bwana Mashaka akifanya vitu kila siku kwani analipwa na Mbowe kushinda hapa JF.
 
Habari zenu wazee wa Jambo Forum?

Ama Hakika Mmeniangusha sana hamjamjua Mashaka ni Mwanakijiji, yeye anacheka kuona Kada Mpinzani ameshindwa kumtambua.

Mwanakijiji kama nilivyosema siku za nyuma huko ni kijana toka mkoa wa Musoma na amekuwa akivutiwa sana na Mwalimu Nyerere, kwenye mada hii amechangia kwa kumuunga Mkono Mashaka ambaye ni yeye Mwenyewe.

Ushahidi wa wazi inapotokea mjadala kama huu angeingia na majina yake mengine lakini amekuwa kimya kuona upepo uko vipi.
Kila siku watu wanasema kuwa JF ni mwisho wa yote kwanini mmeshindwa kumjua Senior member wetu?

Mwanakijiji

Naona saa yako ya ukombozi imefika karibu sana mwaka jana alikuja live Kitila Mkumbo na 2008 umekuja live, nani atakupa ubunge labda Mbowe na Chadema, huna shule wala nini.

naona Jambo Forum imekuua macho kiasi cha kuvaa miwani kama kobe,ulitegemea nini unakesha kwenye computer 24 hrs hizo ndizo disadvantages za Computer bwana M.M. MWANAKIJIJI=MASHAKA MASUMBUKO MWANAKIJIJI ameanza kuharibiwa macho.

jina la John amekuwa akilitumia kama John Almas kwenye redio yake.
sasa utagombea jimbo gani?

Very interesting M.M Mwanakijiji = John Mashaka = Kitila Mkumbo, hii Kali kumbe Musoma ni mkoa vile vile, ama Kweli JF inaelimisha....
 
Jamani ujumbe wa hii thread uko hapo juu! mbona mnapindisha mada? wana diaspora mko wapi..twambieni mnakuja kuchangia haya maendeleo ya taifa kivipi? tupeni mikakati yenu...maana tunaambiwa nyinyi ndugu zetu mlio nje mna exposure, kizungu kinapanda (ambacho ndo wawekezaji wanataka) na mengineyo...jamani tupeni insights basi. Ni kweli kwamba tuna mengi ya kujifunza kwenu, labda mnaweza mkaja na MUAROBAINI WA MATATIZO YETU maana juhudi za akina KADA na wenzake tulio hapa mjini hali ni ngumu!!!! We need you guys....

Mi nawasubiri wana wa diaspora waje watupe vitu hapa na mikakati yao....kwa wenye mpango wa kurudi bongo.

Kuhusu Mashaka sina comment..ila sasa naona wana diaspora wenzake wamemgeuka kwamba hawakumtuma kumpongeza Kikwete..kazi ipo...

Mashaka anamiliki redio inaitwa KLH NEWS,ana website ana suti nyeusi toka Majuu ana makochi meupe huo ndio mkakati wake,swali KLH NEWS itaweza kupambana na Times FM au Clouds?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom