John Keto historia yangu kuhusu elimu yangu na uzoefu katika kazi za kujenga taifa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,924
30,272
JOHN KETO
HISTORIA YANGU KUHUSU ELIMU YANGU NA UZOEFU
KATIKA KAZI ZA KUJENGA TAIFA
(Kwa hisani ya Dr. Nzige)

Waliosimama wa nne kulia ni John Keto University of Edinburgh 1953

Nilizaliwa Misozwe katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga (wakati ule ukiitwa Jimbo la Tanga tarehe 15/08/1917.

Kwa kuwa baba yangu alikuwa mwalimu nilipata bahati ya ya kuanza elimu katika shule ya misheni ya U.M.C.A (University Mission to Central Africa)pale Misozwe mwaka 1922.

Baba alipohamia Magila Msalabani kwa ajili ya kusomea kazi ya ushemasi,ikabidi nihamie huko na kuendelea na masomo yangu ya shule ya msingi kwenye shule ya St. Martins (zamani ikiitwa Hemvumo).

Mwaka 1928 (baba wakati huo akiwa Padre) nilihamia shule ya central school kiwanda kwa kuwa baba alihamishiwa kutoka Magila kwenda kuwa Padre wa Mtaa wa Kizara.

Hapo kiwanda nilisoma na kupata cheti cha Territorial St x (central school leaving certificate) mwaka 1932; na mwaka uliof uata (1933) nilikwenda minaki kusomea kazi ya ualimu. Nilipokuwa hapo minaki nilisomea kwanza cheti cha ualimu wa grade I na kufaulu , mwaka huohuo nikajaribu mtihani wa kwenda Makerere na nikafaulu. Kwa hiyo badala ya kupelekwa kufundisha nilipata nafasi ya kuendelea na masomo zaidi ya Diploma in Educationb kule Makerere.

Mwaka 1940 nilifaulu kupata cheti change cha Diploma in Education pamoja na Cambridge School Certificate na kurudi Tanzania ili kuanza kazi yangu ya Ualimu.

Shule yangu ya kwanza kufundisha ni U.M.C.A Korogwe Middle School ambapo nilianzishwa St. VII. Nilifundishwa Korogwe kwa miaka miwili 1940 na 1941 nikiwa mwalimu mkuu, na mwaka 1942 nikahamishiwa kwenda kufundisha Minaki.

Wakati nikifundisha Minaki nilijiandikisha katika Woolssey Hall College ya London, Uingereza ili kupata masomo kwa njia ya Posta . Masomo hayo pamoja na cheti nilichopata cha London Matriculation ndivvyo vilivyoniwezesha kukuballiwa kupata Scholarship Ya British Council mwaka 1950 kwenda kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Scotland, Uingereza.

Huko Edinburgh nilisoma kwa miaka mitatu na kupata degree yangu ya M.A katika masomo yafuatayo:- Political Economy,Economy History,British History,Constitutional Law, Botanical Science,Moral Philosophy na English Literature. Mwaka 1954 nikarudi nyumbani na kwenda Minaki kuendelea kufundisha wakati huo nikiwa makamu wa mkuu wa chuo.

Niliporudi mwaka 1954 nilikuta chama cha siasa cha TANU (Tanganyika African National Union) kimekwisha kuanzishwa, kwa hiyo nikajiunga nacho na nikachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Tawi la TANU Wilaya ya Kisarawe.

Nilijitahidi kuongoza TANU katika Uzaramo hadi mwaka 1958 wakati nilipoteuliwa na chama kuwa mgombea Mwafrika wa kiti cha ubunge wa Jimbo la Tanga. Nilifaulu na ikabidi kufanya shughuli za ubunge huku nikiendelea na kazi ya ya kufundisha Minaki, baada ya kuafikiana na mkuu wangu wa Chuo (Fr. Nash) kuwa itanilazimu kwenda Tanga ikiwa kkutakuwa na jambo lolote la kisiasa litakalonihitaji jimboni kwangu.

Kwa bahati mbaya kanuni za TANU hazikuruhusu mwanachama kupokea mshahara zaidi ya mmoja ikiimaanisha kuwa mtu kama mimi kupokea mshahara wa ualimu na malipo ya ubunge. Kwa hiyo ilipofika awamu ya pili ya uchaguzi mwaka 1960 sikuweza kugombea tena ubunge, kwa kuwa nilikataa kuacha kazi yangu ya ualimu kwa sababu ambazo nilimweleza Rais Nyerere na akanikubalia.

Mwaka 1961 tulipopata uhuru wetu Rais Nyerere aliniita ofisini kwake Dar es salaam akaniuliza kama niko tayari kwenda Dar es salaam ili kuwa mwenyekiti wa Public Service Commission. Nilimpa sababu zangu nilizopata kupampa huko nyuma zikiwamo uhaba wa walimu kwenye shule yangu ya Minaki, Yeye allinijibu kwamba atanisaidia kuondoa hilo tatizo kwa kutuletea walimu wawili wazungu badala yangu. Kwa hiyo tuliafikiana na nikahama kwenda Dar es Salaam.

Mfumo wa Huduma za pamoja za mawasilano wa Africa ya Mashariki ulipotengenezwa upya. Tanganyika ilipewa huduma ya Posta kwa hiyo mwaka 1964 Rais Nyerere alimtuma waziri Amir Jamal kuja kuniomba niende Nairobi kushika wadhifa wa Postmaster General wa Africa nilikuwa pia mwenyekiti wa kampuni ya Posta na Simu( Post & Telecommunicationb Company Ltd).

Mwaka 1969 baada ya kuundwa kwa Jumuiya ya Africa Mashariki 1967, Makao makuu ya Posta yalihamishwa kwenda Kampala Uganda, Ambako nilikaa mpaka nilipostaafu mwaka 1976 na kurudi nyumbani Tanzania.

Niliporudi nyumbani kwangu Korogwe, Kwamba mwaka 1977 nilikuta Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekwis ha kuanzishwa kwa hiyo nikajiunga na wanachama wengine wa kijiji katika kuhimiza vikao vya chama na kuendesha miradi ya siasa ya kujitegemea kwa mujibu wa miongozo ya Chama. Nilikuwa pia mwanachama wa ushirika wa uzalishaji mali vijijini.

Mwaka 1978 nikapata ujumbe kkutoka magila Muheza kuniomba nikawe mkuu wa Shule ya Hegongo (iliyoitwa Muheza Secondary School hapo awali) badala ya Mw. Stephene Mhando. Nilianzia kazi hiyo tarehe 1/06/1978 nikiwa 1985 nilipostaafu na kurudi Korogwe.

Kwa sasa nipo hapa Majengo nikiwa mwenyekiti wa sehemu ya Wazee wa CCM na mwanachama wa kikundi cha mradi wa kufuga nyuki wa TASAF.

Mungu Uibariki Afrika
Mungu Uibariki Tanzania
…………………..

Majengo Korogwe
10/05/2012

CURRICULUM VITAE
OF
MR. JOHN KETO

1. Date and place of Birth

Born on 15th August, 1917, at Misozwe in Muheza District of Tanga Region.

Married (now widow) with six children, two of them now dead

2. Education

i. At Kiwanda Central School and Minaki

Teacher Training College (1928 – 1937)

Awarded Grade II and Grade I Teachers Certificates

ii. At Makerere College, Uganda(1938 – 1940)

Awarded Cambridge school certificate and Diploma in Education

iii. At Edinburgh University, Scotlad (Oct 1950 – July 1954) awarded M.A degree in following subjects.

· Political History : Constitutional law

· Botanical Science: Moral Philosophy

· English Literature

3. Career

i. Teacher at Korogwe Middle School(1941)

ii. Teacher at Minaki (1942 to Sept 1950) and again 1954 to 1961

iii. Chairman Public Service Commission Tanzania 1961 – 1964

iv. Postmaster General, East Africa 1964 to 1968

v. Director General E.A.P and T. Corporation 1968 TO 1976

vi. Chairman E.A. External Telecoms 1964 to 1976

vii. Headmaster Hegongo Secondary School 1978 to 1985

4. Part Time Activities

a. Member of Council University College

Dar es Salaam

b. Member, East Africa (Swahili) Literature

c. Diwani Muheza and Korogwe District Council

d. Member of Legislative Council

Prepared by Mwalimu John Keto, Majengo Korogwe
 
Mwalimu John Keto huyu ni wazi alikuwa na wito wa ualimu mwanzo hadi mwisho. Alichagua ualimu akaachana na ubunge, bila Nyerere kupeleka walimu wa kuchukua nafasi yake hakuwa tayari kuacha kufundisha. Baada ya kustaafu Posta Africa Mashariki alikubali kuwa headmaster. Saluti kwake.
 
Heshima kwako Keto
Msaga Sumu,
Kaka una jina la ukakasi sharti linanitisha kulitamka na kuliandika.

Wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes nilikutana na John Keto katika
nyaraka kwanza 1955 akiwa kiongozi wa TANU Kisarawe kisha 1958
katika Kura Tatu.

Nakuwekea kitu kutoka Maktaba umsome mzee wetu huyu:

John Keto katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Ilikuwa chini ya hali ya hewa ya kisiasa kama hii ndipo TANU iliingia kwenye uchaguzi wake wa kwanza katika Tanganyika. Tanga ambako UTP ilikuwa imara TANU iliwachagua John Keto, B. Krishna na R. N. Donaldson kama wagombea wake. John Keto akiwa miongoni mwa walimu wa St. Maryís School, Minaki na alikuwa amefanya kazi kubwa katika siku za mwanzo kufungua matawi ya TANU huko Kisarawe. TANU iliamua kumteua Keto kusimama Tanga ambako ndiyo kulikuwa kwao. Katika uchaguzi huu serikali iliacha uandikishaji wa wapiga kura kwa vyama vyenyewe. Mzee Makoko Rashid, mwanasiasa wa makamo mwenye msimamo thabiti wa chama na kijana Mmaka Omari walikuwa maofisa waandikishaji wa wapiga kura katika wa TANU mjini Tanga. Makoko na Mmaka walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kuwaandikisha watu ambao hawakutimiza masharti yaliyoelezwa na ilani ya uchaguzi. Katika ghera yao kwa TANU kushinda ule uchaguzi muhimu, Mzee Makoko alimsajili Mwafrika yoyote aliyetaka kuipigia kura TANU bila kujali sifa zake. Bhoke Munanka alikamatwa vilevile kule Mwanza kwa kosa hilo hilo. Hakukuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya Mmaka Omari kwa hiyo aliachiwa huru mara tu baada ya kukamatwa kwake. Mzee Makoko Rashid alipatikana na hatia na alihukumiwa kufungwa jela. Adhabu ya kifungo ilidhoofisha sana afya yake na mara baada ya kufunguliwa kutoka gereza baya sana la Maweni Mzee Makoko alifariki.''

Moja ya barua za John Keto:
(John Keto kwa J. D. Turner, D. C. Kisarawe, 11 Novemba, 1955 TNA/57/A.6/23).
 
Mmaka yupi huyu?
 
M. Said vitabu vyako vinapatikana duka gani kwa hapa DSM tafadhari
James...
Fika Tanzania Publishing House, Samora Avenue
Elite Bookshop Mbezi
Soma Bookshop Mikocheni
Ibn Hazm Msikiti wa Manyema na Mtoro.

Bei 10, 000.00 Ibn Hazm kwengineko kati ya 13,000.00 na 15,000.00.
 
JOHN KETO
HISTORIA YANGU KUHUSU ELIMU YANGU NA UZOEFU
KATIKA KAZI ZA KUJENGA TAIFA
(Kwa hisani ya Dr. Nzige)

Waliosimama wa nne kulia ni John Keto University of Edinburgh 1953

Nilizaliwa Misozwe katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga (wakati ule ukiitwa Jimbo la Tanga tarehe 15/08/1917.

Kwa kuwa baba yangu alikuwa mwalimu nilipata bahati ya ya kuanza elimu katika shule ya misheni ya U.M.C.A (University Mission to Central Africa)pale Misozwe mwaka 1922.

Baba alipohamia Magila Msalabani kwa ajili ya kusomea kazi ya ushemasi,ikabidi nihamie huko na kuendelea na masomo yangu ya shule ya msingi kwenye shule ya St. Martins (zamani ikiitwa Hemvumo).

Mwaka 1928 (baba wakati huo akiwa Padre) nilihamia shule ya central school kiwanda kwa kuwa baba alihamishiwa kutoka Magila kwenda kuwa Padre wa Mtaa wa Kizara.

Hapo kiwanda nilisoma na kupata cheti cha Territorial St x (central school leaving certificate) mwaka 1932; na mwaka uliof uata (1933) nilikwenda minaki kusomea kazi ya ualimu. Nilipokuwa hapo minaki nilisomea kwanza cheti cha ualimu wa grade I na kufaulu , mwaka huohuo nikajaribu mtihani wa kwenda Makerere na nikafaulu. Kwa hiyo badala ya kupelekwa kufundisha nilipata nafasi ya kuendelea na masomo zaidi ya Diploma in Educationb kule Makerere.

Mwaka 1940 nilifaulu kupata cheti change cha Diploma in Education pamoja na Cambridge School Certificate na kurudi Tanzania ili kuanza kazi yangu ya Ualimu.

Shule yangu ya kwanza kufundisha ni U.M.C.A Korogwe Middle School ambapo nilianzishwa St. VII. Nilifundishwa Korogwe kwa miaka miwili 1940 na 1941 nikiwa mwalimu mkuu, na mwaka 1942 nikahamishiwa kwenda kufundisha Minaki.

Wakati nikifundisha Minaki nilijiandikisha katika Woolssey Hall College ya London, Uingereza ili kupata masomo kwa njia ya Posta . Masomo hayo pamoja na cheti nilichopata cha London Matriculation ndivvyo vilivyoniwezesha kukuballiwa kupata Scholarship Ya British Council mwaka 1950 kwenda kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Scotland, Uingereza.

Huko Edinburgh nilisoma kwa miaka mitatu na kupata degree yangu ya M.A katika masomo yafuatayo:- Political Economy,Economy History,British History,Constitutional Law, Botanical Science,Moral Philosophy na English Literature. Mwaka 1954 nikarudi nyumbani na kwenda Minaki kuendelea kufundisha wakati huo nikiwa makamu wa mkuu wa chuo.

Niliporudi mwaka 1954 nilikuta chama cha siasa cha TANU (Tanganyika African National Union) kimekwisha kuanzishwa, kwa hiyo nikajiunga nacho na nikachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Tawi la TANU Wilaya ya Kisarawe.

Nilijitahidi kuongoza TANU katika Uzaramo hadi mwaka 1958 wakati nilipoteuliwa na chama kuwa mgombea Mwafrika wa kiti cha ubunge wa Jimbo la Tanga. Nilifaulu na ikabidi kufanya shughuli za ubunge huku nikiendelea na kazi ya ya kufundisha Minaki, baada ya kuafikiana na mkuu wangu wa Chuo (Fr. Nash) kuwa itanilazimu kwenda Tanga ikiwa kkutakuwa na jambo lolote la kisiasa litakalonihitaji jimboni kwangu.

Kwa bahati mbaya kanuni za TANU hazikuruhusu mwanachama kupokea mshahara zaidi ya mmoja ikiimaanisha kuwa mtu kama mimi kupokea mshahara wa ualimu na malipo ya ubunge. Kwa hiyo ilipofika awamu ya pili ya uchaguzi mwaka 1960 sikuweza kugombea tena ubunge, kwa kuwa nilikataa kuacha kazi yangu ya ualimu kwa sababu ambazo nilimweleza Rais Nyerere na akanikubalia.

Mwaka 1961 tulipopata uhuru wetu Rais Nyerere aliniita ofisini kwake Dar es salaam akaniuliza kama niko tayari kwenda Dar es salaam ili kuwa mwenyekiti wa Public Service Commission. Nilimpa sababu zangu nilizopata kupampa huko nyuma zikiwamo uhaba wa walimu kwenye shule yangu ya Minaki, Yeye allinijibu kwamba atanisaidia kuondoa hilo tatizo kwa kutuletea walimu wawili wazungu badala yangu. Kwa hiyo tuliafikiana na nikahama kwenda Dar es Salaam.

Mfumo wa Huduma za pamoja za mawasilano wa Africa ya Mashariki ulipotengenezwa upya. Tanganyika ilipewa huduma ya Posta kwa hiyo mwaka 1964 Rais Nyerere alimtuma waziri Amir Jamal kuja kuniomba niende Nairobi kushika wadhifa wa Postmaster General wa Africa nilikuwa pia mwenyekiti wa kampuni ya Posta na Simu( Post & Telecommunicationb Company Ltd).

Mwaka 1969 baada ya kuundwa kwa Jumuiya ya Africa Mashariki 1967, Makao makuu ya Posta yalihamishwa kwenda Kampala Uganda, Ambako nilikaa mpaka nilipostaafu mwaka 1976 na kurudi nyumbani Tanzania.

Niliporudi nyumbani kwangu Korogwe, Kwamba mwaka 1977 nilikuta Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekwis ha kuanzishwa kwa hiyo nikajiunga na wanachama wengine wa kijiji katika kuhimiza vikao vya chama na kuendesha miradi ya siasa ya kujitegemea kwa mujibu wa miongozo ya Chama. Nilikuwa pia mwanachama wa ushirika wa uzalishaji mali vijijini.

Mwaka 1978 nikapata ujumbe kkutoka magila Muheza kuniomba nikawe mkuu wa Shule ya Hegongo (iliyoitwa Muheza Secondary School hapo awali) badala ya Mw. Stephene Mhando. Nilianzia kazi hiyo tarehe 1/06/1978 nikiwa 1985 nilipostaafu na kurudi Korogwe.

Kwa sasa nipo hapa Majengo nikiwa mwenyekiti wa sehemu ya Wazee wa CCM na mwanachama wa kikundi cha mradi wa kufuga nyuki wa TASAF.

Mungu Uibariki Afrika
Mungu Uibariki Tanzania
…………………..

Majengo Korogwe
10/05/2012

CURRICULUM VITAE
OF
MR. JOHN KETO

1. Date and place of Birth

Born on 15th August, 1917, at Misozwe in Muheza District of Tanga Region.

Married (now widow) with six children, two of them now dead

2. Education

i. At Kiwanda Central School and Minaki

Teacher Training College (1928 – 1937)

Awarded Grade II and Grade I Teachers Certificates

ii. At Makerere College, Uganda(1938 – 1940)

Awarded Cambridge school certificate and Diploma in Education

iii. At Edinburgh University, Scotlad (Oct 1950 – July 1954) awarded M.A degree in following subjects.

· Political History : Constitutional law

· Botanical Science: Moral Philosophy

· English Literature

3. Career

i. Teacher at Korogwe Middle School(1941)

ii. Teacher at Minaki (1942 to Sept 1950) and again 1954 to 1961

iii. Chairman Public Service Commission Tanzania 1961 – 1964

iv. Postmaster General, East Africa 1964 to 1968

v. Director General E.A.P and T. Corporation 1968 TO 1976

vi. Chairman E.A. External Telecoms 1964 to 1976

vii. Headmaster Hegongo Secondary School 1978 to 1985

4. Part Time Activities

a. Member of Council University College

Dar es Salaam

b. Member, East Africa (Swahili) Literature

c. Diwani Muheza and Korogwe District Council

d. Member of Legislative Council

Prepared by Mwalimu John Keto, Majengo Korogwe
(Political History : Constitutional law · Botanical Science: Moral Philosophy · English Literature), Is this a single MA. Degree? or six Master's degrees? Wazee wetu kweli walikomaa na kitabu. Siku hizi mtu MA ikos specialized balaa bado inatoa jasho, baaada ya miaka 2 mtu nasoma MA. miaka 6. Wazee hawa wanstahili heshima ya pekee.
 
Back
Top Bottom