Joh makini achukizwa na kitendo cha wasanii wa arusha kutoshirikishwa katika uzinduzi wa jiji hilo

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,551
1,777
JOH_MAKINI.jpg

Mweusi Joh Makini ameungana na wasanii wengine wa Arusha waliochukizwa na kitendo cha wasanii wa Arusha kutoshirikishwa kwenye sherehe za kulizindua jiji hilo rasmi.

Joh ambaye huandika mara chache kwenye ukurasa wake wa Facebook ameandika, “Arusha inakua jiji leo huku wasanii wa arusha ambao muziki wetu umekua ukiitangaza nje na ndani ya nchi hatuhusishwi wala kupewa heshima tunayostahili,mweusi.”


Awali Muungano wa wasanii wa muziki Arusha, ukiongozwa na wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Nakaaya Sumari na Chindo Man waliuijia juu uongozi wa Jiji la Arusha kwa kumwalika Diamond katika uzinduzi wa jiji hilo na wao kutelekezwa.

Wasanii hao wanadai kitendo kilichofanywa na waandaaji wa shughuli hiyo kumwalika Diamond na kuwaacha wasanii wa Arusha katika sherehe hizo ni dharau kubwa kwao.
 
ndo hasara za kufanya mziki wa hiphop.....viongozi labda wanahisi ni uhuni
 
Wao si wamekimbilia dsm, wamechukua wasanii wa huko alikokimbilia!
 
MaLyrics yenu yanaichana serikali...sa watawaalikaje? Pangeni tamasha lenu kusherehekea jiji lenu mjialike wanaArusha, na mkitaka watu wajae Mualikeni Slaa, Lema na Sugu!
 
Hata kama wangeshirikishwa ni nini wangebadili? Wasilazimishe watu kuwakubali
 
Usisubiri kualikwa... make your own way kwa mitizamo yako unayo iamini, itakupa uhuru wa ku perform kitu cha maan zaidi,
 
wasanii wengi wa hiphop ni watu wenye misimamo sana na mara nyingi uwa wanaimba maovu yanayofanyika tofaut na wasanii wetu wa bongo fleva uimba mapenzi tu,ndio maana hiphop wamepigwa chini
 
Sasa kuandika kwenye wall yake Facebook inamsaidia nini? Kwa nini wasitumie muziki wao kuupinga uongozi wa Jiji la Arusha hasa ikizingatiwa hata meya mwenyewe wa Jiji hilo yuko kimagumashi tu. Kama kuna watu wa kulaumu katika kuchelewesha mabadiliko nchini basi wasanii wanachukua nafasi pia. Wamekuwa wakiwarubuni wanakijiji kwa nyimbo zenye ujumbe wa uongo wakati wa kampeni na hivyo kuwafanya kufanya machaguo mabovu.

Kwanza wabadilike kifikra, watambue nafasi waliyonayo katika kuleta mabadiliko kwa watanzania.
 
eti anapanda JCB anaanza watu walitapakaa ule mlio ulipolia paa ndo nini?
wengine mbwa mzee anabweka
 
Yeye kama ni mwanaARUSHA aende kwenye uzinduzi, anataka ahusishwe kivip?aandikiwe barua ya mwaliko?kama nan???kwani muziki anafanya bure au biashara?
 
Hata kama wangeshirikishwa ni nini wangebadili? Wasilazimishe watu kuwakubali

katika watu wanaoheshimu CHA kwao ni watu wa Arusha, hawa wana hip hop wanapendwa sana hapa town hata jambo squad tu wangebamba cjui wamefkiria nini kuwatosa shame
 
Waliona wanachanwa sana kwenye hip hop bora wawachukue wa kulialia akina diamond.
 
Waliona wanachanwa sana kwenye hip hop bora wawachukue wa kulialia akina diamond.

Wewe unategemea mistari ya mtu kam ROMA MKATOLIKI inaweza kukaribishwa kwenye hafla za mzee wa white house!.
 
Sote ni watanzania na 2na haki ya kufanyakaz popote, so achen ubaguz wenu wa kijinga usiyo na msing, kwan kuzaliwa Arusha ndo nini? kwenden zenu huko, hamna lolote!
 
Sote ni watanzania na 2na haki ya kufanyakaz popote, so achen ubaguz wenu wa kijinga usiyo na msing, kwan kuzaliwa Arusha ndo nini? kwenden zenu huko, hamna lolote!

Nashukuru kwa kusema nilichotaka sema, mwisho wa siku tutaanza na ukabila
 
Back
Top Bottom