JKT na ubaguzi: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

Kimsingi hili swala la JKT linapaswa kuwekewa maandalizi ya kutosha ili vijana wote Tanzania wapate nafasi ya kujiunga na si shule 24 tu

Safi sana..na si kuleta ubabaishaji uso kuwa na maelezo ya kina...Kama Serikali haijafanya maandalizi a kutosha, wangetangaza kwamba, wanafunzi wanaopenda kwenda wa volunteer...na si kuchagua shule 24 tu...

Hakuna anayependa kwenda jeshini kwa mtindo huu wa kulazimishana...tena siku hizi hata ajira hamna...unahenya kulitumkia Taifa...then unakaa kusotea ajira...na Hata ajira zisizo rasmi..serikali haizitengenezi...so kwanini kijana aende Jeshini...? Ni ngono tu kule kwa dada zetu...Hamna lolote.....
 
Kazi kweli kweli, hizi habari nimezisikia hapa Mpanda Girls kwa watoto wangu, yaani wanajiona wenye mkosi kweli, hakuna ambaye amefurahia hata mmoja. Serikali hii bana!!! Sijui hizi akili mbaya huwa wanazitoa wapi? Wameona wanajeshi wengi sana wanaacha kazi wameamua kuwaingiza wengine kwa nguvu. Hivi usipoenda what will happen??
 
Laiti ungejua hawa vijana wa .com wanavyochukia suluba!
Hao vijana watakaobaki nyuma, sasa hivi kwao ni sherehe. Kijana gani anataka kash kash wakati huu?
Hata wale wenzetu waliojulikana ni wapenda jeshi (kina mura!) siku hizi wamestuka.
Shuhudia watavyotoroka kambini!

Nimeipenda ... ni kweli, watoto wa siku hz wamezoea ubwabwa, wasipowakagua vzur siku ya kuripoti watakamata ma-PSP kibao!
 
Vijana wa dot.co, matumbo moto! Wakapige kwata wawe strong, manake, duh, full usharobaro!
 
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetaja shule 24 za sekondari ambazo zitatoa wanafunzi 5,000 waliomaliza kidato cha sita watakaojiunga na jeshi hilo. Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Mahuga alisema katika taarifa yake jana kuwa wanafunzi hao watatakiwa kujiunga na jeshi hilo ifikapo Machi 2, mwaka huu.

Shule hizo za sekondari ni Kibondo, Musoma, Kibaha, Ilboru, Bagamoyo, Jitegemee, Tabora Wavulana na Nganza.Shule nyingine ni Mtwara Wasichana, Ihungo, Kilakala, Benjamin Mkapa, Maswa Wasichana, Dodoma, Tumain-Singida na Galanos.Nyingine ni Ashira, Nangwa-Manyara, Iyunga, Mpanda, Lindi, Iringa Wasichana, Kawawa-Iringa na Ruhuwiko-Songea.

Taarifa hiyo ilisema maofisa wa JKT watakwenda kwenye shule hizo kuanzia Januari 9, mwaka huu kwa ajili ya kutoa utaratibu wa mafunzo na kambi ambazo watakwenda.“Mkuu wa JKT kwa mamlaka aliyopewa kisheria ya mwaka 1964 na kufanyiwa mapitio mwaka 2002, chini ya kifungu cha sheria namba 5,” ilisema taarifa hiyo.
Iliongeza kuwa “Anawaita vijana watakaohitimu kidato cha sita mwaka 2013 kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ifikapo terehe 2, Machi 2013.” Utaratibu wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ulisimamishwa tangu mwaka 1994.Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Julai mwaka jana, Waziri wake, Shamshi Vuai Nahodha alisema kambi zilizopo za JKT zina uwezo wa kuchukua vijana 20,000 kwa wakati mmoja, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka huu wataanza kwa majaribio na vijana 5,000.Alisema wanafunzi 41,348 wanatarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha sita katika mwaka 2013 na kwamba vilikuwa vikiandaliwa vigezo ili kuwapata vijana 5,000 ili kujiunga na JKT.

Kwa mujibu wa jarida la JKT, mafunzo hayo yatakuwa ya miezi sita katika Kambi za JKT Bulombora na Kanembwa mkoani Kigoma.Nyingine ni Mlale (Ruvuma), Mafinga (Iringa), Msange (Tabora) na Oljoro(Arusha).

Maswali yakujiuliza:-
1)Ni vigezo gani walivyotumia kuchagua wanafunzi kutoka shule 24 tu?
2)Ina maana wanafunzi kutoka shule zingine hawana haki au vigezo vya kujiunga na JKT?
3)Wote tunajua kwamba zaidi ya 90% ya shule zote za secondary Tanzania zinapatikana Mkoa wa Kilimanjaro, lakini jambo la kushangaza Kutoka mkoa wa kilimanjaro imechaguliwa shule 1 tu ya weruweru. usawa uko wapi?

Nawasilisha.
Lodrik...
Si kweli ati 90% ya sekondary ziko uchagani,, huo ni ukabila kiasi ya kushindwa hata kuujua ukweli, nilianza kukusoma hadi nilipoona uhoro Wako
 
3)Wote tunajua kwamba zaidi ya 90% ya shule zote za secondary Tanzania zinapatikana Mkoa wa Kilimanjaro, lakini jambo la kushangaza Kutoka mkoa wa kilimanjaro imechaguliwa shule 1 tu ya weruweru. usawa uko wapi?
Bwana lodrick unajua mwenyewe hilo. Bado unasoma magazeti ya miaka ya sabini na themanini mwanzoni? Kama asilimia tisini ya secondari za Tz zipo kilimanjaro, basi angalau katika kila watanzania kumi unaokutana nao takribani tisa wangekwambia wamesoma sekondari Kilimanjaro, tukichukulia sekondari za Tz zinabeba idadi sawa za wanafunzi.
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye 90% umetudanganya hata 20% haifiki jaribu kuangalia vizur labda useme shule nyingi za huko znafanya vizur

Kweli kabisa, shule za secondary Kilimanjaro zipo 222 wakati nchi nzima ni 3200 au 4200 sikumbuki vizuri, ila hii ni kwa O-Level so kwa A-level sijui, labda kutafiti kidogo, but haziwezi kufika 90%
 
hiv mngejickiaje wangepelekwa watoto wote na wasingeweza kuhudumiwa mngesema serikal imekurupuka bila ata kufanya sample au mngewapongeza
 
Unaonaje kama wanaotaka kujiunga na JKT wakahamia kwenye hizo shule...
 
Hivi nyie watoto mnafuata "propaganda" za serikali kuwa jeshi linaongeza ukakamavu na uzalendo? Huo ni uongo kwa sababu wengi wetu tuliokwenda huko hatuna ukakamavu wala uzalendo. Wezi ni sie wenyewe, wazembe ofisini ndo sie vinara. Mie naona JKT ni kupotezeana muda na kuwaongezea wakubwa ulaji. Mie sitaunga mkono mwanangu kwenda JKT. Hata hivyo, enzi hizo tulibanwa kwa kuwa tusingeruhusiwa kujiunga chuo chochote cha elimu ya juu bila kupitia JKT.

Kwa hali ya sasa, ambapo wazazi wanawagharamia watoto wao elimu, sioni sababu ya kufanya JKT iwe ya mujibu wa sheria.


Mlalamikaji, hajui aliombalo.
 
Back
Top Bottom