JKT na ubaguzi: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

lodrick

Member
Dec 29, 2010
61
19
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetaja shule 24 za sekondari ambazo zitatoa wanafunzi 5,000 waliomaliza kidato cha sita watakaojiunga na jeshi hilo. Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Mahuga alisema katika taarifa yake jana kuwa wanafunzi hao watatakiwa kujiunga na jeshi hilo ifikapo Machi 2, mwaka huu.

Shule hizo za sekondari ni Kibondo, Musoma, Kibaha, Ilboru, Bagamoyo, Jitegemee, Tabora Wavulana na Nganza.Shule nyingine ni Mtwara Wasichana, Ihungo, Kilakala, Benjamin Mkapa, Maswa Wasichana, Dodoma, Tumain-Singida na Galanos.Nyingine ni Ashira, Nangwa-Manyara, Iyunga, Mpanda, Lindi, Iringa Wasichana, Kawawa-Iringa na Ruhuwiko-Songea.

Taarifa hiyo ilisema maofisa wa JKT watakwenda kwenye shule hizo kuanzia Januari 9, mwaka huu kwa ajili ya kutoa utaratibu wa mafunzo na kambi ambazo watakwenda."Mkuu wa JKT kwa mamlaka aliyopewa kisheria ya mwaka 1964 na kufanyiwa mapitio mwaka 2002, chini ya kifungu cha sheria namba 5," ilisema taarifa hiyo.
Iliongeza kuwa "Anawaita vijana watakaohitimu kidato cha sita mwaka 2013 kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ifikapo terehe 2, Machi 2013." Utaratibu wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ulisimamishwa tangu mwaka 1994.Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Julai mwaka jana, Waziri wake, Shamshi Vuai Nahodha alisema kambi zilizopo za JKT zina uwezo wa kuchukua vijana 20,000 kwa wakati mmoja, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka huu wataanza kwa majaribio na vijana 5,000.Alisema wanafunzi 41,348 wanatarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha sita katika mwaka 2013 na kwamba vilikuwa vikiandaliwa vigezo ili kuwapata vijana 5,000 ili kujiunga na JKT.

Kwa mujibu wa jarida la JKT, mafunzo hayo yatakuwa ya miezi sita katika Kambi za JKT Bulombora na Kanembwa mkoani Kigoma.Nyingine ni Mlale (Ruvuma), Mafinga (Iringa), Msange (Tabora) na Oljoro(Arusha).

Maswali yakujiuliza:-
1)Ni vigezo gani walivyotumia kuchagua wanafunzi kutoka shule 24 tu?
2)Ina maana wanafunzi kutoka shule zingine hawana haki au vigezo vya kujiunga na JKT?
3)Wote tunajua kwamba zaidi ya 90% ya shule zote za secondary Tanzania zinapatikana Mkoa wa Kilimanjaro, lakini jambo la kushangaza Kutoka mkoa wa kilimanjaro imechaguliwa shule 1 tu ya weruweru. usawa uko wapi?

Nawasilisha.
 
Hivi ni kweli kuwa zaidi ya 90% ya shule zote za sekondari Tanzania ziko mkoa wa Kilimanjaro? Naomba ushahidi bwana lodrick, hebu tupatie orodha. Na pili, siamini kuwa JKT ni jambo zuri namna hiyo hata wachagga na wapare wa Kilimanjaro walalamike vijana wao kukosa kuitwa.
 
Hivi ni kweli kuwa zaidi ya 90% ya shule zote za sekondari Tanzania ziko mkoa wa Kilimanjaro? Naomba ushahidi bwana lodrick, hebu tupatie orodha. Na pili, siamini kuwa JKT ni jambo zuri namna hiyo hata wachagga na wapare wa Kilimanjaro walalamike vijana wao kukosa kuitwa.

Kupata idadi ya shule na location zake ingia Tanedu - Home
JKT ni jambo zuri sana kwa vijana wetu wanaohitimu shule za secondary. Kuna mambo mengi wanajifunza huko ikiwepo nidhamu, ukakamavu, etc etc... Kama isingekuwa jambo zuri basi hapakuwa na haja yakurudisha mfumo huu wa vijana kwenda JKT wanapohitimu masomo yao
 
Inawezekana sio mafunzo ya Jeshi La Kujenga Taifa bali ni Jeshi La Kujenga CCM (JKC) wanaandaliwa Green Guard.
 
hzo shule ni za kitafa zna mchanganyiko wa makabila yote uliyeleta hii thread unaendeleza habari za ukanda
 
Kimsingi hili swala la JKT linapaswa kuwekewa maandalizi ya kutosha ili vijana wote Tanzania wapate nafasi ya kujiunga na si shule 24 tu
 
Kumbe suala lako ni ubaguzi na si vigezo, hizo shule ni za Tanzania na waliochaguliwa ni Watanzania. Pia karibu shule zote hizo ni za kitaifa ambamo asilimia kubwa ya wanafunzi wanatoka mikoa yote ya Tz. Kuwa na subra MKUU mwakani wanaweza panua wigo wakuchukua maana wameshasema wapo ktk majaribio na kuna ufinyu wa BAJETI.(Japo mi si msemaji wao).
 
hzo shule ni za kitafa zna mchanganyiko wa makabila yote uliyeleta hii thread unaendeleza habari za ukanda

Kwenye thread yangu nimeongelea wingi wa shule zinazopatikana kilimanjaro, kaa ukijua pamoja na shule nyingi kuwa kilimanjaro bado haimaanishi kwamba ni wachagga na wapare tu wanaosoma hizo shule. Zina mchanganyiko wa wanafunzi from all over the country. Hili la ukanda linakuhusu wewe.
 
Kumbe suala lako ni ubaguzi na si vigezo, hizo shule ni za Tanzania na waliochaguliwa ni Watanzania. Pia karibu shule zote hizo ni za kitaifa ambamo asilimia kubwa ya wanafunzi wanatoka mikoa yote ya Tz. Kuwa na subra MKUU mwakani wanaweza panua wigo wakuchukua maana wameshasema wapo ktk majaribio na kuna ufinyu wa BAJETI.(Japo mi si msemaji wao).

kwa hiyo ambao hawakuchaguliwa si watanzania? Nimeuliza kuhusu vigezo vilivyotumika kuchagua shule 24 tu. Utatusaidia zaidi kama utalijibu hilo manake inaonekana unawajua vizuri
 
Laiti ungejua hawa vijana wa .com wanavyochukia suluba!
Hao vijana watakaobaki nyuma, sasa hivi kwao ni sherehe. Kijana gani anataka kash kash wakati huu?
Hata wale wenzetu waliojulikana ni wapenda jeshi (kina mura!) siku hizi wamestuka.
Shuhudia watavyotoroka kambini!
 
Kupata idadi ya shule na
location zake ingia Tanedu - Home
JKT ni jambo zuri sana kwa vijana wetu wanaohitimu shule za secondary.
Kuna mambo mengi wanajifunza huko ikiwepo nidhamu, ukakamavu, etc etc...
Kama isingekuwa jambo zuri basi hapakuwa na haja yakurudisha mfumo huu
wa vijana kwenda JKT wanapohitimu masomo yao

Kwani Ashira iko mkoa gani mkuu?
 
Kilimanjaro umetaja shule tatu na siyo weruweru tu mana Lyamungo na Ashira pia zipo k/njaro
 
kwa hiyo ambao hawakuchaguliwa si watanzania? Nimeuliza kuhusu vigezo vilivyotumika kuchagua shule 24 tu. Utatusaidia zaidi kama utalijibu hilo manake inaonekana unawajua vizuri

Najua kuwa hata kwenye shule za "Academy" kuna watoto wa vigogo -watanzania. Mbona hizo hazikuguswa? Na ndio maana wengine wanafikiria kuna ubaguzi. Nadhani vigezo vilivyotumika viwekwe wazi hili kuzuia kuwa kuna hisia za ubaguzi.
 
wajitahidi kutushawishi wazazi kwanini shule 24 tu? bila maelezo mazuri mtoto wangu haendi. kama ni jeshi wote waende.
 
JKT isikie tu usije pelekwa wala kumpeleka mtoto wako utamsahau na kama ni kikeni ndio kabisaa anaenda kugegedwa ile mbaya
 
Back
Top Bottom