Elections 2010 JK: Ukosefu wa fedha unakwamisha maendeleo

Dr wa ukweli

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
900
264
RAIS Jakaya Kikwete amesema ukuaji wa kasi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika unakwamishwa na ukosefu wa fedha za kutosha za kugharimia miradi ya maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa Kimataifa wa mwaka huu wa Taasisi ya Smart Partnership Dialogue ambao pia unajulikana Langkawi International Dialogue 2011, ulioanzishwa rasmi mwaka 1995.

Rais Kikwete alisema kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha ili kuharakisha ukuaji kasi wa uchumi, hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo.

Rais Kikwete alisema kutokana hali hiyo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya kugharimia maendeleo ya bara hilo na watu wake.

"Tatizo ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi inaweza kuzitoa nchi za Afrika na watu wake katika umasikini kwa haraka zaidi," Rais Kikwete, mjini Kuala Lumpur, Malaysia.

Shabaha kuu ya Smart Partnership ama Langkawi International Dialogue ni kufanya majadiliano ya kimataifa ya jinsi ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi duniani. Mada kuu katika mkutano wa mwaka huu ni ‘Enhancing Smart Partnership for Socio-Economic Transformation'.

Akishiriki katika mjadala huo, Rais Kikwete aliwaambia mamia ya washiriki tatizo kubwa linalokwamisha ukuaji kasi wa uchumi na maendeleo katika Afrika ni ukosefu wa fedha za maendeleo kwenye sekta binafsi, sekta ya umma na kwa Serikali.

Rais alisema chanzo kikuu cha fedha za maendeleo kwa nchi masikini za Afrika ni misaada ya maendeleo (ODA), lakini sasa fedha za ODA zimekuwa zikipungua na wakati mwingine hazipatikani.

"Hata ukitofautiana na kampuni yenye asili ya nchi inayotoa misaada, basi utanyimwa misaada hata kama kampuni yenyewe ndiyo yenye makosa," alisema Rais Kikwete.

Rais alisema wakati mwingine inakuwa vigumu kuvutia fedha za maendeleo kutoka nje.

"Hakuna fedha za kutosha kwenye masoko ya fedha ya ndani na msingi mzima wa kifedha ni dhaifu sana. Msingi wa fedha wa ndani ni dhaifu na hata msingi wa fedha za kigeni wa nchi zetu ni masikini,"alisema Rais Kikwete.

Rais alisema hali hiyo imezifanya nchi za Afrika kujikuta katika wakati mgumu wa kutimiza wajibu na majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

"Hivyo, sisi katika Afrika tunahitaji kutafuta na kuangalia njia nyingine za ubunifu zaidi za jinsi ya kupata fedha za maendeleo," alisema Rais Kikwete.

Mapema mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato' Sri Mohammed Najib Tun Abdul Razak ambaye hotuba yake ilizungumza masuala mengi na matatizo mengi yanayoikabili dunia kwa sasa pamoja na umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea.
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema ukuaji wa kasi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika unakwamishwa na ukosefu wa fedha za kutosha za kugharimia miradi ya maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa Kimataifa wa mwaka huu wa Taasisi ya Smart Partnership Dialogue ambao pia unajulikana Langkawi International Dialogue 2011, ulioanzishwa rasmi mwaka 1995.

Rais Kikwete alisema kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha ili kuharakisha ukuaji kasi wa uchumi, hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo.

Rais Kikwete alisema kutokana hali hiyo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya kugharimia maendeleo ya bara hilo na watu wake.

“Tatizo ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi inaweza kuzitoa nchi za Afrika na watu wake katika umasikini kwa haraka zaidi,” Rais Kikwete, mjini Kuala Lumpur, Malaysia.

Shabaha kuu ya Smart Partnership ama Langkawi International Dialogue ni kufanya majadiliano ya kimataifa ya jinsi ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi duniani. Mada kuu katika mkutano wa mwaka huu ni ‘Enhancing Smart Partnership for Socio-Economic Transformation’.

Akishiriki katika mjadala huo, Rais Kikwete aliwaambia mamia ya washiriki tatizo kubwa linalokwamisha ukuaji kasi wa uchumi na maendeleo katika Afrika ni ukosefu wa fedha za maendeleo kwenye sekta binafsi, sekta ya umma na kwa Serikali.

Rais alisema chanzo kikuu cha fedha za maendeleo kwa nchi masikini za Afrika ni misaada ya maendeleo (ODA), lakini sasa fedha za ODA zimekuwa zikipungua na wakati mwingine hazipatikani.

“Hata ukitofautiana na kampuni yenye asili ya nchi inayotoa misaada, basi utanyimwa misaada hata kama kampuni yenyewe ndiyo yenye makosa,” alisema Rais Kikwete.

Rais alisema wakati mwingine inakuwa vigumu kuvutia fedha za maendeleo kutoka nje.

“Hakuna fedha za kutosha kwenye masoko ya fedha ya ndani na msingi mzima wa kifedha ni dhaifu sana. Msingi wa fedha wa ndani ni dhaifu na hata msingi wa fedha za kigeni wa nchi zetu ni masikini,”alisema Rais Kikwete.

Rais alisema hali hiyo imezifanya nchi za Afrika kujikuta katika wakati mgumu wa kutimiza wajibu na majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Hivyo, sisi katika Afrika tunahitaji kutafuta na kuangalia njia nyingine za ubunifu zaidi za jinsi ya kupata fedha za maendeleo,” alisema Rais Kikwete.

Mapema mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato’ Sri Mohammed Najib Tun Abdul Razak ambaye hotuba yake ilizungumza masuala mengi na matatizo mengi yanayoikabili dunia kwa sasa pamoja na umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea.
 
Pesa wanazolipana posho
Pesa za kununulia magari ya kifahari ya serikali na idara zake
Pesa za safari mfurulizo ng'ambo
Pesa za Madini
Pesa za maliasili
Pesa za wawekezaji hewa - ATC, TRL, IPTL etc

Hizi si pesa? angesema tatizo ni matumizi na manunuzi ya umma mabovu ndiyo yanasababisha ubutu wa maendeleo wa nchi yetu.
 
Kilio cha pili hiko ndani ya wiki 2 mfululizo
last week akiwa geneva alilia akisema waafrika hawana uzalendo na nchi zao na hawataki kuamini kua afrika imeendelea......this weekenda amekuja na suala la uhaba wa pesa.....slogan ya kulalamika inaendelea as usual
 
Kaenda lini tena huko Malaysia?......duh huyu jamaa kiboko

mchiz anakula bata kishenz wanatumia posho na msafara wake ipasavyo!, juzi knye ziara ya shelisheli aliambatana na msururu wa wabunge kuhudhuria sherehe za uhuru.................. tunapiga kelele kupunguza gharama yeye anatafuta jinzi ya kuzitumia bila mpangilio!
 
Jk F(1).jpg

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete amesema changamoto kubwa inayokwamisha ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi ya maendeleo.

Rais Kikwete amesema kuwa kutokana ukweli kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha za kuharakisha ukuaji wa kasi zaidi hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya ubunifu zaidi ya kugharimia maendeleo ya Bara hilo na watu wake.

Kwa mtazamo wangu Rais hajataja kikwazo halisi, hapa amejaribu tu kudandia hoja mradi aeleweke.
Hoja kubwa ni uongozi bora na viongozi kuacha ubinafsi. Ukiwauliza matajiri wakubwa hawakuanza na mtaji ama anaofikiria Rais, ila uongozi bora pamoja na ubunifu wa kutumia rasilimali zetu ni njia muafaka wa kuondoa kikwazo cha uchumi.
Mbona rasilimali zetu zenye kutuletea utajiri zinasombwa na wageni kwenda kujitajirisha kwao? Sijajua elimu ya uchumi imeeleweka kwa rais wetu au washauri wake. Ndio maana anazunguka duniana kupitisha bakuli la kuomba mikopo?
 
aliambiwa serikali yake imeishiwa akamtuma huyo mmalawi aje akanushe sasa kilo cha nini?
 
Jk%20F%281%29.jpg

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete amesema changamoto kubwa inayokwamisha ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi ya maendeleo.

Rais Kikwete amesema kuwa kutokana ukweli kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha za kuharakisha ukuaji wa kasi zaidi hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya ubunifu zaidi ya kugharimia maendeleo ya Bara hilo na watu wake.

Kujua maeneo ya kujiletea maendeleo ni jambo la muhimu sana. Kuwa na pesa siyo maendeleo, bali matumizi mazuri ya pesa huleta maendeleo. Sasa yakowapi angalau maendeleo kidogo kutokana na hizo pesa kidogo za miradi?
 
[h=4]Haya ni maoni ya wadau - Gazeti Mwananchi [/h]

0#10mchukia majungu2011-06-20 17:05
sad.gif
Ama kweli Tanzania hatuna raisi. Kama hujui tatizo utapataje suluhisho? Tatizo ni uchumi kukaliwa ki[NENO BAYA] na wachache wakiwemo watawala wanazidi kudaganya wananchi kuwa watawaletea maendeleo, matokeo yake watu wamechoka na hawana hamasa tena na maendelea bali wanatibu njaa na matatizo ya kila aina yanayowasonga. Viongozi/watawala acheni maneno, ni wakati wa vitendo. Muungwana akishindwa huwa anaachia siyo kungángánia, utaharibu zaidi na tutafika shimoni ulilochimba tayari, chonde chote
sleeping.gif
.

Quote

+1#9Sam2011-06-20 14:30Hapa ndiyo utaona tofauti ya mwenye akili na asiyenazo, tofauti kati ya JK Nyerere na Jk ******. Wakati Nyrere alissitiza kuwa Fedha si msingi wa maendeleo, ****** anataka tuamini bila fedha hatuendelei.

Badala ya kutuambia kuwa fedha ni matokeo ya maendeleo, matokeo ya kufanya kazi kwa bidii, maarifa na uadilifu, yeye anataka sisi tuamini bila fedha hatuwezi kuendelea,

Hili lilikuwa ni mojawapo ya somo muhimu sana la Nyerere, kuwa fedha si msingi wa maendeleo, Kweli Jk hakumwelewa Nyerere hata kidogo

Quote

0#8m.ali2011-06-20 12:51Rais wetu apotosha fikira jwenye huwo mkutano. bara la afrika ni tajiri sana. Tanzania tuna madani tele, lakini ile mikataba michafu inatufanya wananchi wanaoishi kwenye madini kuwa masikini. Angalieni mji wa Johannesburg kule afrika ya kusini. Ulijengwa na pesaa za dhahabu. Ilikuwa inatakikana shinyanga na kahama kuwa miji ya kisasa, bahati mbaya wanaonufaika sio wananchi bali wale mabepari wa kutoka nje. Itakuwaje mpaka leo mashirika ya madini wanapewa kila kitu tax free, na hawalipi kodi, wakati bei ya dhahbu imefika dola 1500 aunsi moja. wakati walipowekeza bei ya dhahbu ilikuwa dollar 600 aunsi moja. ile faida kwa nini tusawawekee kitu kinachoitwa faida isiyo kawaida ya bei ya dhahbu na watulipe ushuru asilia mia 30. Ndugu zangu nawapiya kwa jina la mungu viongozi ndiyo wabaya. mpaka sasa hawajafanikisha kuinuwa maisha ya watanzania na tuwe watu wanaoitwa middle class ni wachache sana. Tusimameni na vyama vya upinzani na tudai haki zetu hawo investors ni wezi wakubwa na wala hawana faida na nchi. mwisho tutabakiwa na mashimo matupu ambayo madhara yake ni makubwa. hakuna hata kiongozi wa serikali kuwauliza wachimbaji wanpomaliza dhahabu zao wafukiey hayo mashimo.

Quote

0#7fatuma2011-06-20 12:04mheshimiwa rais usijifanye unahuruma sana na maendeleo ya tanzania.Fedha mmezitia vibindoni leo unasemaje?
Futa posho ya wabunge na mawaziri iliyopo kwenye mumzo sasa tutakuona kweli wewe mwanaume

Quote

0#6Gabriel2011-06-20 11:01Siamini kama huyu Rahisi ana washauri na kama anao hafuati ushauri wao. Mikutano kama hiii ni low key na inatosha kumtuma mchumi akajadiliane na wenzake mbinu za kuleta maendeleo. Sasa mama Salma atatusaidiaje kwenye msafara kama huu? Pili, tatizo siyo fedha ila matumizi mbovu na ukosefu wa nguvu mali. Kwa nini tulete wawekezaji kuja kutuulia ndugu zetu Nyamongo badala ya kupeleka vijana wetu wakabobee juu ya uchimbaji madini halafu tuchukue mikopo Benki ya Maendeleo ya Afrika ay Benki ya Dunia kununulia vitendeakazi vya kuchimba madini? Uchumi siyo porojo na kama huna uchangiaji wenye kuleta tija kaa kimya!

Quote

+1#5Musa2011-06-20 07:28“Hivyo, sisi katika Afrika tunahitaji kutafuta na kuangalia njia nyingine za ubunifu zaidi za jinsi ya kupata fedha za maendeleo,” alisema Rais Kikwete.

Katika njia nyingine za ubunifu wa kupata fedha ni kufuta posho zenu viongozi, 987 billion kwa mwaka si haba, ikawekwa kwenye shughuli za maendeleo na ikasimamiwa vizuri kwa kila mwaka miaka mitano ni 4,935 billion, kwa mawazo yangu huu ungekua mwanzo mzuri , TAFADHALI MH NJOO NYUMBANI USIMAMIE HAYA KABLA YA BAJETI KUPITA, ACHA KUENDELEA KUTUMIA PESA ZA WANANCHI KWA KUKAA NJE

Quote

+4#4msemakweli2011-06-20 06:03I cant believe this.
Tatizo siyo Ukosefu wa fedha tatizo ni matumizi mabaya ya fedha na hasa kwa Tanzania.
Pili acha kuongea kana kwamba Afrika yote in matatizo. Hapo kwa watani wa jadi kenya mambo yao yanakuwa biyee kabisa,Rwanda kumekucha,Namib ia, Afrika Kusini, Ethiopia pale pananukia maendeleo,na nchi kibao zimeanza kujiweka sawa. Wewe unawaongelea kivipi. Ongeleamatatizo yako pekee.
Mimi nashangaa kama kweli Mheshimiwa ana washauri..!
Nchi ina watu milioni 42++ ina vitega uchumi kibao, inakusanya kodi kidogo na kuifyeka yote kwa anasa za viongozi, kama hiyo ziara ya umechoma dola ngapi kabla hujasema hakuna hela. Kungekuwa hakuna hela ungesafiria Economy class au usingeenda kabisa na kumtuma balozi wako awakilishe serikali,

Ujumbe huu uwafikie wasaidizi wako wote ambao ndo wakulaumiwa kwa kuipotosha dunia

Quote

-2#3Ludigo2011-06-20 03:28UMATONYA UMEKUWA KAMA WIMBO WA TAIFA KWA NCHI ZETU ZOTE.LAKINI TANZANIA IMEZIDI.SUBIRI KUNA WATU WATAKUJA HAPO MTAONA KAMA PESA ITATOKA WAPI.
 
Jk F(1).jpg

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete amesema changamoto kubwa inayokwamisha ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi ya maendeleo.

Rais Kikwete amesema kuwa kutokana ukweli kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha za kuharakisha ukuaji wa kasi zaidi hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya ubunifu zaidi ya kugharimia maendeleo ya Bara hilo na watu wake.

mimi simwamini kiongozi anayezungumzia sana maswala ya fedha,
nafikiri kiongozi anatakiwa awe mbunifu na sio kulalama hamna pesa
 
Jk F(1).jpg
Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete amesema changamoto kubwa inayokwamisha ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi ya maendeleo.Rais Kikwete amesema kuwa kutokana ukweli kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha za kuharakisha ukuaji wa kasi zaidi hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya ubunifu zaidi ya kugharimia maendeleo ya Bara hilo na watu wake.
Ili tuendelee tunahitaji >>watu, ardhi. siasa safi na uongozi bora.
 
JK ni m.a.t.a.k.o tu. takataka kabisa! kwanza sitakaa nimtambue kama Rais. Na nikipata nafasi ya kumpasua kichwa, sitaipoteza. Fisi mkubwa!!!!
 
Hapa Rais wangu kaniacha hoi na kunichekesha kweli kweli! Hivi haya maneno yanamtoka Rais akijijua au akiwa amepigwa ganzi ya Ubongo? mbona hayaendani na hali halisi ya Tanzania na kauli zake?

Mbona Rais alitoa ahadi lukuki za maendeleo wakati wa Uchaguzi au ndio anathibitisha yale maneno kuwa alikuwa andanganya!? na Je alipokuwa anatoa zile ahadi lukuki hakujuwa kuwa fedha hazipo?

Na je fedha za Madini na maliasili zetu mbona hatuzi-manage vyema kujenga nchni? Mbona hatufanyi mapinduzi kwenye ardhi ambayo mtaji wake ni mdogo sana?! Kweli Rais wetu bado anaamini katika kuwa omba omba!
 
Hata ungempa Kikwete dola trilion kumi, bado hataweza kuifanya tanzania iendelee kwa staili hiyo ya uongozi.
 
Back
Top Bottom