Elections 2010 JK: Ukosefu wa fedha unakwamisha maendeleo

RAIS Jakaya Kikwete amesema ukuaji wa kasi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika unakwamishwa na ukosefu wa fedha za kutosha za kugharimia miradi ya maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa Kimataifa wa mwaka huu wa Taasisi ya Smart Partnership Dialogue ambao pia unajulikana Langkawi International Dialogue 2011, ulioanzishwa rasmi mwaka 1995.

Rais Kikwete alisema kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha ili kuharakisha ukuaji kasi wa uchumi, hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo.

Rais Kikwete alisema kutokana hali hiyo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya kugharimia maendeleo ya bara hilo na watu wake.

"Tatizo ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi inaweza kuzitoa nchi za Afrika na watu wake katika umasikini kwa haraka zaidi," Rais Kikwete, mjini Kuala Lumpur, Malaysia.

Shabaha kuu ya Smart Partnership ama Langkawi International Dialogue ni kufanya majadiliano ya kimataifa ya jinsi ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi duniani. Mada kuu katika mkutano wa mwaka huu ni ‘Enhancing Smart Partnership for Socio-Economic Transformation'.

Akishiriki katika mjadala huo, Rais Kikwete aliwaambia mamia ya washiriki tatizo kubwa linalokwamisha ukuaji kasi wa uchumi na maendeleo katika Afrika ni ukosefu wa fedha za maendeleo kwenye sekta binafsi, sekta ya umma na kwa Serikali.

Rais alisema chanzo kikuu cha fedha za maendeleo kwa nchi masikini za Afrika ni misaada ya maendeleo (ODA), lakini sasa fedha za ODA zimekuwa zikipungua na wakati mwingine hazipatikani.

"Hata ukitofautiana na kampuni yenye asili ya nchi inayotoa misaada, basi utanyimwa misaada hata kama kampuni yenyewe ndiyo yenye makosa," alisema Rais Kikwete.

Rais alisema wakati mwingine inakuwa vigumu kuvutia fedha za maendeleo kutoka nje.

"Hakuna fedha za kutosha kwenye masoko ya fedha ya ndani na msingi mzima wa kifedha ni dhaifu sana. Msingi wa fedha wa ndani ni dhaifu na hata msingi wa fedha za kigeni wa nchi zetu ni masikini,"alisema Rais Kikwete.

Rais alisema hali hiyo imezifanya nchi za Afrika kujikuta katika wakati mgumu wa kutimiza wajibu na majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

"Hivyo, sisi katika Afrika tunahitaji kutafuta na kuangalia njia nyingine za ubunifu zaidi za jinsi ya kupata fedha za maendeleo," alisema Rais Kikwete.

Mapema mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato' Sri Mohammed Najib Tun Abdul Razak ambaye hotuba yake ilizungumza masuala mengi na matatizo mengi yanayoikabili dunia kwa sasa pamoja na umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea.

Hatuna fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yetu Tanzania kweli.This is a blatant slap in the face.Madini yetu yanakwenda wapi,utalii,pamba,chai,kahawa,mbao,kodi za makampuni ya simu na vitega uchumi vingine vingi, uvuvi nk.Leo tunaambiwa hatuna hela ya kutosha.Nani atakuwa na hela sasa, hao wanaopewa resourses zetu bure.Sawa bwana,iko siku.
 
Tuna raisi ambaye anauongozi wa kiimla na nnadhani anafikiri anaongoza majuha.mmmhh hapa kazi ipo mpaka huo mwaka 2015 tuna huyu mtu
 
Ili tuendelee tunahitaji >>watu, ardhi. siasa safi na uongozi bora.

Yaani inashangaza swali la kwenye siasa darasa la tano mkuu anashindwa kutambua majibu. Kichekesho zaidi eti huyu alikuwa mwalimu wa siasa jeshini kwa miaka kadhaa.
 
This is Kikwete in search of a vision. In search of statesmanship. He is missing both.
 
matatatizoyaliyopo kwenye nchi yetu ni
  • Financial dicspline- Waamuzi wana act kama vile hakuna uhaba wa fedha wakati kwenye bajeti wajua kila siku majibu yao ni ufinyu wa bajeti. Hici huko vyuoni wakati wanajifunza mamneo kama Planning, Organisation walidhani yana maana gani. Hakuna nchi yeyote Duniani yenye financial resources zinatosheleza mahitaji yao . Ndio maana kuna neno bajeti. Budget is plan how effectively and efficently to use scarce financial resource you have.


  • Prioritisation- Kwenye makaratasi Tanzania tunaplan nzuri lakini kiutendaji pesa nyingi zinapotela kwenye administration badala ya kuelekezwa kwenye utekelezaji hasa wa wa sera. Mfano anagalia landcruser za miradi ya kilimo nyingi ziko wapi. ziko mjini badala ya kuwa shemu hasa za kilimo. Watu wanaotakiwa uwa filed wao wamevaa tai. Wizara ya kilimo ina magai mengi ten mikonga yako dar na mijini badala ya rukwa ruvuma iriga an the like.

Bila kubadilsha hayo mambo hata wahisani wangetaoa pesa zote bado mambo yangeuwa yale yale tu.
 
Back
Top Bottom