Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,170
JK: Ningeboronga CCM ingenitimua
RAIS Jakaya Kikwete amesema anaamini iwapo angekuwa ameshindwa kutekeleza kikamilifu Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyomuingiza madarakani mwaka 2005 asingethubutu kugombea tena.
Kikwete alitoa tambo hizo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM 350 wa Mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kumdhamini.
Inawezekana watu hawaijui vizuri CCM, kama leo ningekuwa nimeboronga ningekuwa nimefukuzwa siku nyingi lakini kutokana na kutekeleza ilani ya chama vizuri, naweza kusimama na kuomba watu wanichague, alisema.
Akizungumzia uamuzi wake wa kumteua mwanaye kuzungusha fomu za kusaka wadhamini, Kikwete alisema hakuna tatizo lolote katika kufanya hivyo.
Kikwete alisema chini ya utaratibu aliouweka, viongozi wa wilaya watakuwa na jukumu la kuandaa fomu za wadhamini zilizoletwa.
Wale waliokuwa wakijiuliza maswali nadhani majibu wameyapata kinachofanywa na hao vijana ni kukusanya fomu ambazo viongozi wamezifanyia kazi kwa kutafuta wadhamini, hivyo kazi ya wanafunzi sio kutafuta wadhamini wao wananiletea wadhamini ambao wamepatikana, alisema.
Kikwete anatoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu tangu Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, amtetee kwa uamuzi wake wa kumteua Ridhiwani ambao baadhi ya makada na viongozi wa juu wa chama hicho wamekuwa wakiuelezea chinichini kuwa unaoonyesha namna rais alivyopoteza imani kwa viongozi wenzake.
Wakati Kikwete mwenyewe akitoa taarifa hiyo, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais nayo imelazimika kukanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku (siyo Tanzania Daima) zilizokuwa zikimtaja waziri wa zamani wa fedha, Zakia Meghji, kuwa ni mtu ambaye yuko katika mawazo ya Kikwete kwa ajili ya kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa Oktoba.
Mbali ya hilo, Ikulu katika taarifa yake hiyo ya maandishi iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salvatory Rweyememu, imekanusha kupata kufanyika kwa mawasiliano yoyote kati ya Rais Kikwete na Meghji kuzungumzia wadhifa huo ambao kiitifaki ni wa pili kimamlaka kitaifa.
Hayo ni mawazo na matakwa binafsi ya waandishi wa habari, huo katu si msimamo wa Rais Kikwete Kwa sasa Rais anashukuru suala la mgombea mwenza hajaanza kulishughulikia kwani wakati wake bado. Hivyo maneno hayo hayana chembe ya ukweli, ilieleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ya Ikulu inakuja wakati kukiwa na vuguvugu la chini chini kuhusiana nafasi ya mgombea mwenza ambayo ndiyo itakayotoa makamu wa rais iwapo watashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Kuibuka kwa ubashiri wa mtu gani anayepaswa kushika nafasi hiyo umekuwa mkubwa tangu ibainike kuwa Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, ambaye ndiye aliyekuwa akitarajia kuwa mgombea mwenza achukue fomu ya kugombea urais wa Zanzibar.
My Take:
1. Ni lini CCM imewahi kumfukuza kiongozi wake katika ngazi ya kitaifa kwa sababu ya kuboronga in the last 30yrs?
2. Ktk vitu vyote vinavyonifurahisha ni jamaa kujittutumua eti ana rekodi ya mafanikio ya miaka mitano. Hivi kwa hali iliyopo Tz sasa haoni hata aibu kulisema hilo?
3. Wa kulaumiwa in huge terms ni wananchi maana wao ndiyo wanaona na kufeel hicho kinachoitwa rekodi lakini hawako tayari kukanusha wala kuhoji........
- Atamba anajivunia rekodi yake ya miaka mitano