Jk na 'sijui' na 'nashangaa' zake

JK ameendeleza rekodi yake ya kusema hajui na anashangaa kuhusu mambo muhimu kabisa ya maisha haya ya watanzania.Alinukuliwa akisema(na ameungwa mkono na Waziri Mkuu wake,Pinda) kuwa hajui kwanini watanzania ni maskini.Alinukuliwa pia akisema kuwa hawajui wamiliki wa DOWANS ilihali Serikali yake iliingia mkataba nao.Jana alipokuwa anazindua upanuzi na uboreshaji wa Barabara ya New Bagamoyo,amenukuliwa hivi:'Nawashangaa sana wahandisi washauri, wao ndiyo wenye jukumu la kuhakikisha barabara zinajengwa kwa kiwango kinachokubalika, lakini wamekuwa mstari wa mbele kuidhinisha malipo wakati barabara ni mbovu'

Hivi huyu mtu tumfanye nini? Nimeamini maneno ya Mwalimu wangu mmoja pale Mlimani kuwa JK alikuwa mzigo kwa darasa lake....mgumu sana kuelewa(kilaza) na ndio maana alipata Gettleman degree.JK ataingia Guiness Book of Records kwa kauli zake za kijuha

Ukiwa na rais mswahili lazima uwe tayari kusikia mengi kutoka kwake. Tuvumilie amalize muda wake tutapumzika na kauli za ajabu ajabu za kitoto.
 
Ni kwa vile tunamdekeza kwani Anashangaa amekuwa rais kwa awamu ingine tena Hajui kwanini amechaguliwa huku hakufanya lolote.
 
Back
Top Bottom