Jk na 'sijui' na 'nashangaa' zake

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
JK ameendeleza rekodi yake ya kusema hajui na anashangaa kuhusu mambo muhimu kabisa ya maisha haya ya watanzania.Alinukuliwa akisema(na ameungwa mkono na Waziri Mkuu wake,Pinda) kuwa hajui kwanini watanzania ni maskini.Alinukuliwa pia akisema kuwa hawajui wamiliki wa DOWANS ilihali Serikali yake iliingia mkataba nao.Jana alipokuwa anazindua upanuzi na uboreshaji wa Barabara ya New Bagamoyo,amenukuliwa hivi:'Nawashangaa sana wahandisi washauri, wao ndiyo wenye jukumu la kuhakikisha barabara zinajengwa kwa kiwango kinachokubalika, lakini wamekuwa mstari wa mbele kuidhinisha malipo wakati barabara ni mbovu'

Hivi huyu mtu tumfanye nini? Nimeamini maneno ya Mwalimu wangu mmoja pale Mlimani kuwa JK alikuwa mzigo kwa darasa lake....mgumu sana kuelewa(kilaza) na ndio maana alipata Gettleman degree.JK ataingia Guiness Book of Records kwa kauli zake za kijuha
 
Daaaaaaah! Inachosha kweli kweli! waTZ kama ni Rais 2naye, tena mchapa kazi. Mungu ibariki Tz. Mungu wabariki waTz na uwape moyo wa uvumilivu.
JK ameendeleza rekodi yake ya kusema hajui na anashangaa kuhusu mambo muhimu kabisa ya maisha haya ya watanzania.Alinukuliwa akisema(na ameungwa mkono na Waziri Mkuu wake,Pinda) kuwa hajui kwanini watanzania ni maskini.Alinukuliwa pia akisema kuwa hawajui wamiliki wa DOWANS ilihali Serikali yake iliingia mkataba nao.Jana alipokuwa anazindua upanuzi na uboreshaji wa Barabara ya New Bagamoyo,amenukuliwa hivi:'Nawashangaa sana wahandisi washauri, wao ndiyo wenye jukumu la kuhakikisha barabara zinajengwa kwa kiwango kinachokubalika, lakini wamekuwa mstari wa mbele kuidhinisha malipo wakati barabara ni mbovu'

Hivi huyu mtu tumfanye nini? Nimeamini maneno ya Mwalimu wangu mmoja pale Mlimani kuwa JK alikuwa mzigo kwa darasa lake....mgumu sana kuelewa(kilaza) na ndio maana alipata Gettleman degree.JK ataingia Guiness Book of Records kwa kauli zake za kijuha
 
Anashangaa pia kuwa bandari hawajaweza kununua licomputer likubwa la kufanyia kazi kwa ufanisi.

Ameshangaa tanroads wanakuwa wapi mpaka mtu anajenga kwenye road reserve mpaka anahamia.
 
hajui kwa nini kuna msuguano baina ya UVCCM na Elders wao
 
Unajua hata kushangaa nako ni kazi eeh! Only In Tanzania,Mtu anaweza kukaa ikulu kwa miaka 5 akawa anafanya kazi ya kupigwa Bumbuazi tu!!!
 
JK anashangaa kama nami ninavyomshangaa, alipita wizarani miaka mitano iliyopita, akawa kimya leo ndo amezinduka usingizini, mtu unampa changamoto za kiutendaji halafu unamuacha miaka mitano bila kumfuatilia. Unatarajia ukute nini jipya, wakati anajua ulishamsahau. Hajui hata issue ya time management, deadlines, priorities, time span, etc
 
Aaaah yaani ni mambo ya ajabu sana,kama baba mwenyenyumba kazi yake ni kushangaa tu,watotoa wanafanya fyongo we unasema "Nashangaa sana" nenda felly sasa ukashangae vizuri.
 
may b mr. Prezoo bado yuko katka ndoto hajaanza rasmi kaz yake!nawalaumu zaid waliomuandaa ndio wamefuga ubovu!
 
Jakaya anamwambia Magufuli asiwe mbabe aangalie utu wakati wa bomoabomoa ya nyumba zilizojengwa kwenye road reserve na hapo hapo anamuamuru Tibaijuka abomoe nyumba za watu zilizojengwa jangwani!! Hao waliojenga Jangwani ni binadam tofauti na waliojenga kwenye road reserve? Huyu jamaa ni KITUKO.
 
watendaji wengi ni maswahiba wao na hawezi kuwachukulia hatua za kisheria.......jiulize kama kampuni ya consultancy ni ya RA unategemea atahoji kitu chochote?
 
Jakaya anamwambia Magufuli asiwe mbabe aangalie utu wakati wa bomoabomoa ya nyumba zilizojengwa kwenye road reserve na hapo hapo anamuamuru Tibaijuka abomoe nyumba za watu zilizojengwa jangwani!! Hao waliojenga Jangwani ni binadam tofauti na waliojenga kwenye road reserve? Huyu jamaa ni KITUKO.

Wale kuonea huruma ni wa barabara ya msata / bagamoyo.
 
mnajua inawezekana pia anashangaa kwa nini tume na wengine walimsaidia kuchakachua last elections.
 
Anashangaa kwa nini kigoma haijawa dubai wakati alishasema!!!!!!!!!!!
 
Leo mimi nacheka tu hapa, huyu ni kilaza, Nyerere alisema bado akili yake hijawakua at the age of 45, sasa huyo unategemea akue tena? Imetoka hiyo ataendela kushangaaa na sijui zake mpaka israel anamchukua.
 
Back
Top Bottom