JK kufanya mahojiano na watoto.

911

Platinum Member
Aug 22, 2008
852
499
Wakati kukiwa na mambo lukuki ambayo wananchi wangependa mh.Rais ayatolee tamko,yeye ameamua 'kupambana' na watoto 14...Ok,swali langu ni kuwa hivi hivyo vituo vya redio na televisheni vitakavyoonesha 'komedi' hiyo vinalipwa?Na nani?I mean kutoka fungu lipi?Yule dogo aliyemuulizaga Eddo kuhusu vijana kuwa taifa la kesho...nilisikia aliandamwa kweli na UwT,nadhani hawa watakuja na hoja soft soft.
Kutoka katika gazeti la Mwananchi;
Na Sadick Mtulya

BAADA ya kufanya mazungumzo na wananchi kwa njia ya redio na televisheni, Rais Jakaya Kikwete sasa atasikiliza hoja na maswali kutoka kwa watoto.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Watoto (Unicef), ambalo limeendaa mpango huo, limesema hiyo ni sehemu ya uhamasishaji nauungaji mkono wa kupitishwa kwa sheria mpya ya watoto nchini.

Sheria hiyo imepitishwa hivi karibuni bungeni na Rais Kikwete anasubiriwa kuisaini ili ianze rasmi kutumika

Kikwete, ambaye alizungumza na taifa kwa mara ya mwisho Septemba 9 mwaka huu alipozungumza na wananchi kwa dakika 90, atapambanana watoto 14 watakaokuwa wamechaguliwa kutoka mikoa saba ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa Unicef, katika mpango huo wa aina yake utakaofanywa katika kipindi ambacho dunia inaadhimisha miaka 20 ya kuanzishwa kwa sheria ya mtoto, Rais ataulizwa na kujadilina na watoto wenye umri kati ya miaka 10 na 18 tu.

Shirika hilo limefafanua kwamba mpango huo ni wenye lengo la kuwapa matarajio watoto katika jitihada zao za kuboresha maisha na haki zao za msingi katika mabadiliko ya maendeleo ya dunia.

"Watoto wenye umri kati ya miaka 10 hadi 18 wakiwakilishwa na wenzao 14 kutoka mikoa saba ya Tanzania Bara na Zanzibar watatumiaaina mpya ya kuwasiliana na Rais Kikwete kwa kusikiliza hoja zao, kwa kujibu maswali yao, kusikiliza ushauri wao na kupata maoni juu ya mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu, serikali yetu na maendeleo yetu," inaeleza taarifa ya Unicef, tawi la Tanzania.

"Mazungumzo hayo yatafanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo baina ya UNICEF na vyombo vya habari vitakavyorusha matangazo hayo moja kwa moja kupitia televisheni na redio."

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watoto hao watazungumza moja kwa moja kupitia vituo vya redio na televisheni vya Shirika la Utangazaji (TBC) na vyombo vingine vya utangazaji nchini.

Taarifa hiyo inafafanua kwamba "mbali na TBC, televisheni nyingine za ITV, Channel Ten na Star Tv zinatarajiwa kuonyesha mazungumzo hayo."

Taarifa hiyo imevitaja vituo vitakavyotangaza moja kwa moja mazungumzo hayo kuwa ni TBC-Taifa, Radio One, Radio Clouds na Radio Free Afrika.

Kipindi hicho kitakachorushwa kwa dakika 30 kitafanyika baada ya watoto hao kuchujwa kutoka Zanzibar na katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Mbeya na Mwanza.

Uchujaji wa watoto hao utafanyika katika tarehe tofauti kuanzia Novemba 10 hadi 19 mwaka huu kupitia vituo vya kulelea watoto.

Katika mkoa wa Mwanza kituo cha Mwanza Children Fund (Mwachif) kitafanya uchujaji huo Novemba 10 na 11, katika mikoa ya Arusha ni kituo cha World Vision Tanzania na Dar es Salaam kituo cha DogoDogo Centre vyote Novemba 12 na 13.

Mkoa wa Lindi ni kituo cha Save the Children na Dodoma ni kituo cha World Vision Tanzania vyote Novemba 14 na 15 na mkoa wa Mbeya ni kituo cha Kiwohede Novemba 17 na 18.
 
Asee, kwa kweli tuna rais! Matatizo mengi tuliyonayo yanamshinda kuyatafutua ufumbuzi sasa amehamia kwa watoto! ni ajabu na kweli! Tunaomba Mungu hii miaka 6 iliyobaki iishe haraka angalau tupate mwingine. Nimesema miaka sita kwa sababu akigombea mwakani atapata tena kwa sababu CCM inajulikana sana na vijijini hawajui udhaifu wake. Hata kwenye jiji kama Dar watampa kwa sababu hata kwenye serikali za mitaa wamewapa. tulitegemea angalau dar waonekane wamepevuka lakini zero wanazidiwa na moshi na kigoma.
 
Nadhani sasa tunakuwa negative bila kuelewa presidency ni zaidi ya jk!!! Ana roles tofauti na hata aipoongea na watoto haimaanishi mda huo atakuwa pale iptl anatengeneza jenereta na mambo kama hayo

jk ana watendaji na unicef wanafahamu hayo, yeye ni role model

hivi unakumbuka sept 11 wakati waarabu wanalipua ndege bush alikuwa nursery school?
 
ila wasije wakawaandalia watoto maswali ya kuiliza maana protocal za bongo noma, wanaweza kuandaliwa hata cha kuongea na kuvaliswa zile nguo zenye rangi ya kifisadi, bongo siasa hadi altare
 
ila wasije wakawaandalia watoto maswali ya kuiliza maana protocal za bongo noma, wanaweza kuandaliwa hata cha kuongea na kuvaliswa zile nguo zenye rangi ya kifisadi, bongo siasa hadi altare

More likely mazee maana inaonekana hivyo ni vipindi na vina themes tofauti so no matter what you wish, tegemea premeditated stuffs
 
Baada ya mahojiano na watoto, ungependa ahojiwe na akina nani wengine?

Note: JK amekuwa akikwepa midahalo kwa bidii sana.
 
Nadhani sasa tunakuwa negative bila kuelewa presidency ni zaidi ya jk!!! Ana roles tofauti na hata aipoongea na watoto haimaanishi mda huo atakuwa pale iptl anatengeneza jenereta na mambo kama hayo

jk ana watendaji na unicef wanafahamu hayo, yeye ni role model

hivi unakumbuka sept 11 wakati waarabu wanalipua ndege bush alikuwa nursery school?
Tatizo sio kuongea na watoto hilo sio swala baya,lakini sasa serikali na chama cha Mafisadi CCM wanaiyumbisha wakati serikali inalipiga chenga bunge kuhusu swala la Richmund,aibu za kikao kamati ya Mh.Mwinyi na rais JK A.k Rostam Aziz yuko kimya tuna tunashindwa kumuelewa sasa ni wakati wa yeye kuwakusanya maprofesa kutoka kati vyuo vikuu au kuongea na wanachuo kutoka vyuo vikuu huko atapata ushauri wa papo kwa hapo(Ana kwa ana)MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Jamani, hii ni aibu. Kwa mawezo yangu angepaswa afanye maojiono na wasomi katika fani zote ili angalau waweze kumshauri la kufanya ili kuinusuru nchi katika janga la ufisadi na mambo mengine yanayo fanana na hayo na si kwenda kuojiana na watoto.
Kama anataka kufahamu matatizo ya watoto, ingekuwa busara kuzungumza na wazazi wao, na kwa upande wa wanafunzi azungumze na waalimu, na kwa upande wa hospitali azungumze na madaktari na wahudumu wengine wa hospitali, na kwenye taasisi nyingine zinazotoa huduma za kijamii, basi azungumze na wahusika.
Huku kuzungumza na watoto sijui anatafuta nini kwa watoto. atabakia kuwapa pipi na kuwafunga kamba za viatu.
 
ukimwambia awekwe midahalo na akina lipumba anakimbia anajifanya anakwenda marekani mara jamaica ,ila mijadala na watoto weeeee wa kwanza..hahaaaaaa
 
hiyo burudani jamani kwa wenye muda wa kuitizama kwenye tv
watoto wameandaliwa na kuchujwa mpaka wakafika 14, inawezekana wamechaguliwa wenye ubongo wa ku kremisha maswali sasa wanajinoa, na raisi nae anapitia pitia majibu...kama mchezo wa kuigiza yaani

wastage of time...
 
More likely mazee maana inaonekana hivyo ni vipindi na vina themes tofauti so no matter what you wish, tegemea premeditated stuffs

"Mwache aongee na watoto kwani yale mengine mazito si yamekataa kutatuliwa na yanapigwa na danadana,Richmond,Ticts,Reli nk.Sasa sahizi yake ni watoto sisi watu wazima tunamboa kila wakati richmond richmond mpeni watoto tena watoto ni wa kuchaguliwa na kujulikana wametoka familia gani, na kwa nani?ambapo maswali mazuurii na majibu yake yatakuwa tayari yameandaliwa ili kufurahisha ze comedy kwenye TV na radio
 
Heshima mbele!
Mawazo yangu ni kwamba kwanza napata hisia kua raisi wetu 'anatumiwa' na hawa UNICEF. Habari ilivyokaa inaonyesha mwenye haja ya kutimiza jambo hapa ni UNICEF ambao kwao watoto na haki zao ndio sehemu yao ya kazi na katika kutimiza programu zao wameona raisi ndio akamilishe lengo kwa kuwa na mahojiano na watoto.

Pia nawaza jinsi watoto hao watakavyochaguliwa. Je vigezo vitakua vipi? Kama ni watoto kunyanyaswa, je wa mjini au wa kijijini wapi wananyanyaswa zaidi? Viongozi wa NGos na mashirika mengine yanayohusika na watoto wataweza kukwepa kishawishi cha kupeleka watoto wao for publicity reasons? Nina hisia kwamba siku hiyo tutaona watoto wa mjini (wasio na matatizo sana) kwenye T.V zetu wakiwa wameshaambiwa cha kusema na cha kujibu!

Kwa kifupi, mheshimiwa raisi, wakati wananchi wanaheshimu mchango wako kama baba na mlezi, taifa linakuhitaji kwenye mambo ya muhimu zaidi. Waziri Mkuu au waziri mwenye dhamana ya mambo ya jamii na watoto angeweza kusimamia hilo.

Naomba kuwakilisha
 
It goest without saying... hata ningekuwa mimi, cha maana ni kutimiza agenda yangu kwahiyo wacha UNICEF watumie nafasi iliyopo

Pia nawaza jinsi watoto hao watakavyochaguliwa. Je vigezo vitakua vipi? Kama ni watoto kunyanyaswa, je wa mjini au wa kijijini wapi wananyanyaswa zaidi? Viongozi wa NGos na mashirika mengine yanayohusika na watoto wataweza kukwepa kishawishi cha kupeleka watoto wao for publicity reasons? Nina hisia kwamba siku hiyo tutaona watoto wa mjini (wasio na matatizo sana) kwenye T.V zetu wakiwa wameshaambiwa cha kusema na cha kujibu!

Watoto wa academy, watoto wa vigogo, watoto wa NGOs, watoto wa wenyewe, na sio kajamba nani!!

Kwa kifupi, mheshimiwa raisi, wakati wananchi wanaheshimu mchango wako kama baba na mlezi, taifa linakuhitaji kwenye mambo ya muhimu zaidi. Waziri Mkuu au waziri mwenye dhamana ya mambo ya jamii na watoto angeweza kusimamia hilo.

Naomba kuwakilisha

Jamani eh!!! Mwacheni aongee na watoto!!
 
Akimaliza mjadala na watoto salva anamwandalia mdahalo na mafisadi wote, baada ya hapo anakuja kwa maalibino wote. Ama kweli Rais tunaye!
 
Akimaliza mjadala na watoto salva anamwandalia mdahalo na mafisadi wote, baada ya hapo anakuja kwa maalibino wote. Ama kweli Rais tunaye!

Hiyo atafanya akitoka safari ya Jamaica, China, Indonesia, Moshi, Mwanza, Malindi, Abuja, India, Kampala, N'twara nk
 
Huyo JK akimalizana na watoto aje hapa JF kujibu hoja zinazomhusu
mbona yuko siku nyingi tu! au hujui ID yake.yeye anachangiaga km raia wa kawaida tu...ila hoja zake nyingi ni za kuitetea na kuibeba sisiem na serikali yake.
 
Back
Top Bottom