Elections 2010 JK: ilani niachieni mimi

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,366
6,492
JK alipokuwa Kawe aliwaambia wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM kuwa wenyewe wajibu kero za wananchi na ilani ya uchaguzi ya CCM wamwachie yeye. Sasa tofauti iko wapi? Hivi kazi ya mbunge na diwani ni kujibu kero za wananchi au kuisimamia serikali, kuwakilisha wananchi zikiwemo kero na kutunga sheria? JK anajua kweli kazi za mbunge na diwani?
 
katika miaka mitano aliyokaa ikulu alikuwa akizungukwa na wapambe wakimdanganya tuu;

sasa baada ya kukutana uso kwa uso na wananchi katika kampeni amegundua kuwa watendaji wa serikali,wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa halamashauri n.k walikuwa wakivurunda tuu ndio maana ameamua kila mtu ajibu tuhuma katika eneo lake
.

mfano hai ni pale alipokuwa katika kampeni kule kagera na akakiri hadharani kuwa wakuu wa mkoa wa ikagera na wilaya ya misenyi walimpotosha kuwa katika ranchi ya kakunyu hakuna makazi ya watu. Hali kama hiyo imejitokeza katika sehemu nyingi katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wa j k na wananchi kwa maelfu kunyang'anywa ardhi zao, kubomolewa nyumba zao n.k.
 
Back
Top Bottom