- Mawaziri wanaumbuana mbele ya hadhara.Ilianzia Sitta na Nahodha ingawa kabla ya hapo kulijitokeza mgongano wa wazi wa mawaziri katika suala la kulipwa Dowans.
- Jairo amefanya madudu na mkahitilafiana na PM wako wazi kabisa.
- Naibu Waziri wako anatembea na bunduki mbili,laptop tatu,simu tatu na dola 4000 katika ziara ya ndani.Anaibiwa hotelini na bado yupo.Alikuwa katika ziara ndefu na alipitia migodini.
- Exchequer General anauza kiwanja cha serikali kiujanja na pia anataka kuvunja CHC wakati anajua kuwa hiyo bado inashughulikia madai na mambo mbalimbali yaliyokuwa kwenye mashirika ya umma.
Tunakupenda mno,una huruma sana na unaguswa na matatizo ya watu na hapa ndo pakuonyesha vitendo na tutakuwa nyuma yako.