JK atumie Elkopta kwenda na kurudi Airport

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Nadhani ni jambo lisilopingika kwamba foleni za barabarani ktk jiji la Dar zinaongezeka siku hadi siku.

Ninashauri JK na viongozi wengine wanaopenda sana misafara mirefu waanze utaratibu wa kutumia ELIKOPTA kutoka pale kwenye viwanja vya Magogoni/Ikulu kwenda na kurudi AIRPORT.

Vilevile niliwahi kusikia kwamba pale juu kabisa ya TWIN TOWERS palitengenezwa imara sana kwa lengo kama hilo, kwamba Rais anaweza kutoka pale Ikulu akafika kwenye majengo hayo, akapanda lift hadi juu, akaingia kwenye ELIKOPTA akaanza mpaka Air Port na wakati wa kurudi hivyo hivyo.

Je hii itapunguza foleni kwa kiasi gani??????????
 
Hana haja ya kwenda TWIN TOWER hapohapo Ikulu kubwa sana atengenezewe kale kauwanja kadofo ka helkopter
 
--- Helkopta za kiraia kwa matumizi ya kila siku kwa Mh. Rais hazifai. Too risky. Kukiwa na dharura sawa, it's justifiable.

--- Solution ya misongamano siyo wahukika kuikimbia misongamano hiyo, they should find long lasting solutions na siyo njia za mkatomkato zinazoweza kuwa za hatari zaidi na kupinzana na lengo. Cha kusikitisha ni kwamba njia mbadala za utatuzi zinafahamika lakini tunazitupilia kando.

--- Mkuu, ni wazo lenye nia njema kabisa lakini napingana nalo kutokana kwa technicalities chache kama vile uwezo wa kiuchumi na mazingira tuishimo.

SteveD.
 
Ah! Vipi kama akiwa hachelewi sana si itasaidia? Yaani akiwa anaoga bado ikulu huku TAZARA watu wameshapigwa stop! Hii ni aibu jamani, hivi hakuna namna nyingine ya kumhakikishia usalama wake ni mpaka wafunge bara bara na kumkimiza kama nini siju!
 
Alafu hawa watu ubinafsi umewajaa ni kheri aende na Helkopta tuu
 
Kale kandege kununuliwa ilizua mzozo, sasa wazo la helkopta si itakuwa kimbembe
 
Nadhani ni jambo lisilopingika kwamba foleni za barabarani ktk jiji la Dar zinaongezeka siku hadi siku.

Ninashauri JK na viongozi wengine wanaopenda sana misafara mirefu waanze utaratibu wa kutumia ELIKOPTA kutoka pale kwenye viwanja vya Magogoni/Ikulu kwenda na kurudi AIRPORT. Vilevile niliwahi kusikia kwamba pale juu kabisa ya TWIN TOWERS palitengenezwa imara sana kwa lengo kama hilo, kwamba Rais anaweza kutoka pale Ikulu akafika kwenye majengo hayo, akapanda lift hadi juu, akaingia kwenye ELIKOPTA akaanza mpaka Air Port na wakati wa kurudi hivyo hivyo.

Je hii itapunguza foleni kwa kiasi gani??????????

Ni ukweli usiopingika kuwa misafara ya viongozi wa kitaifa inazorotesha sana mwendo kasi ndani ya Jiji la Dar es salam. Viongozi wetu wanakuwa na misafara mirefu na pia huchukua muda kuzisafisha njia hadi wanausalama waridhike kuwa hali ni shwari kwa kiongozi mhusika.

Ni bahati mbaya kuwa mipango miji iliyokuwepo ni ile ileiyoachwa na wakoloni, ambayo maendeleao yaliyofanywa kuipanua ni kidogo sana ili kuweza kutoa nafasi zaidi kurahisisha usafir ndani ya jiji. Barabara zinazoingia na kutoka katikati ya jiji ni zile zile za miaka nenda rudi.

Usafiri wa kutumia ndege ikiwa ni pamoja na helkopta nadhani ndio zinzohesabika kuwa salama sana kuliko usafi mwingine, haswa pale vyombo hivyo vinapokuwa na sifa, achilia mbali zile helkopta za jeshi zilizonunuliwa kwa rushwa, sijui zilitengenezwa chini pamoja na taka nyingine nyingi zilizo jaa Tanzania.

Hivyo basi kama Rais na wateule wengine wasiosongamana na watanzania njiani ingekuwa bora sana kutumia vyombo hivyo vya juu japo kutupunguzia adha ya foleni.

Ukweli unabaki kuwa serikali inahitaji kuliangalia suala la usafiri na miundombinu ya Dar es salaam kwa jicho la karibu kwani sasa JIJI LIPO karibuni KUSIMAMA. Pamoja na kuwa na mabasi makubwa na yanayodaiwa kwenda kwa kasi, bado tunahitaji kuwa na njia zenye viwango za kutosha, hususan madaraja (flyovers) katika makutano korofi, kuanzisha miji mipya nje ya jiji ili kuawanya shughuli za kiofisi na kibiashara kutoka Mjini kati na Kariakoo. Pia kuangalia uwezekano wa kuwa na usafiri kama wa treni, sijui kama za chini ya ardhi tutaweza.

Tatizo la usafiri ni kubwa haswa sasa kuanzia Chalinze hadi Dar es salaam. Kuna haja ya serikali kuwa na barabara za viwango tofauti tanzania. Ni ukweli usiopingika kuwa ajali zimekuwa nyingi eneo hili kwa sababu ya magari ni mengi na kila gari linalotokea upande husika linakuwa na njia moja tu. Nadhani Tunahitaji barabara zote kuu zinazoingia dar ziwe angalao Double, na zikifika Dar ziwe 3 hadi 4. Mfano hakuna sababu ya kuongeza double road kutoka Kimara hadi Kibaha kwa sasa, ila hili inatakiwa Kufika angalao chalinze kama sio morogoro. Huu ndio uwe mwendo mdundo kwa barabara zinzounganisha mikoa na iwe hivi hasa zinapoingia na kutoka.
 
Na huko DOm watalalamikia msongamano wa magari... Tena wa huko utakuwa ni mbaya zaidi kwa jinsi mji huo ulivyojukusanya sehemu moja
 
Kuonekana na kusigishana na wananchi ni hali ambayo huleta zaidi awareness kwamba the president is live and running. Si mbaya kila siku mkuu akipita tukapoteza masaa walau moja na kumpungia.

Ni ishara ya amani pia kama mkuu anaonekana mara kwa mara. Kazi tufanyazo ni muhimu kwetu kwanza kabla ya manufaa ya taifa lakini kazi ya rais ina manufaa kwanza kwa taifa kisha kwake mwenyewe.

Therefore to my views is a matter of priorities here! Heshimu amiri Jeshi Mkuu, movement zake hulinda amani kwani maeneo apitayo yote they are safer than asikopita. Au mnasemaje wanaJF! Ndiyo tumeshampa dhamana atiii! Tusimbanie!
 
Helicopter ndio njia nafuu kusafrisha msafara..lakini watu wa usalama wanaamini zaidi magari kuliko..kujulikana kuwa rais anatumia helicopter ..akiwa na adui anaweza kumuondoa kwa kutumia a simple rpg...anapiga tail..hapo hata apache haina ujanja itaanguka...thats why choppers wanazitumia kwa surprise....

Ila katika siku za karibuni naona serikali kama kenya na uganda ..viongozi wao wanatumia sana choppers...millitary models...kwenda remote.....

Tanzania tutaweza kuamini helicopter kwa rais wetu kama hazitanunuliwa kwa rushwa....we fikiria rais angekuwa anatumia zile augusta bell za vithlani ...si tungeshampoteza????...nadhani vithlani anatakiwa kufunguliwa kesi ya mauwaji...

...serikali itukabidhi jf ...jukumu la kuchagua choppers ambazo zipo cost effective kwa nchi masikini kama yetu..kwa ajili ya matumizi ya viongozi na kijeshi....we can do better..
 
Kutoka Radio Mbao::

JK anatumia less than 3 months in Dar every yr, so sijui lawama za nini humu ndani.

Angekuwa Fulltime president mngesema vipi???
 
Nilienda Dodoma this year kwenye maonesho ya nane 8 kuna pavillion moja ya Capital Development Authority (CDA). Hawa jamaa ndo wana mamlaka ya kustawisha Dodoma na kuufanya mji uwe wa kisasa zaidi.

Kwenye pavillion yao walikua na model (Architectural), inaonesha ofisi zote za serikali zitakavyokua. Its a really good design. Wamepanga wizara zote zikae kwenye eneo moja.

Sasa mi naona wakiamishia Ikulu kule waweke underground tunnel from statehouse str8 to the airport. Haya mambo ya kusimama kila mtu ajue Rais anaenda wapi yamepitwa na wakati. Tatizo Rais mwenyewe ana safari kibao. Akiwa Tz anapokea wageni. Sasa imagine kwa mtu anayekaa Goms alaf anafanya kazi Kamata. Kila siku ni foleni tuuuuuuu.

Alaf safari nyingine atumie helicopter, mbona Mbowe aliweza. Nii misafara inamaliza tu mafuta. These days kunakua na BMW nne zinamsindikiza. I think kila moja in mtu mmoja.
Cant they share a ride???? wanamaliza kodi yetu kwenye mafuta.
 
Kale kandege kununuliwa ilizua mzozo, sasa wazo la helkopta si itakuwa kimbembe
....Tukauze kale kandege tutapa tu-helkopta tutatu wagawane kamoja JK, Kamoja Mzee Cheni na kengine Mzee wa Kupinda tumemaliza kazi.....
 
Back
Top Bottom