GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
JK aponzwa na Msimamo tete wa Tanzania kuhusu LIBYA Wiki Leaks yatumika Kumfunga Mdomo
Tuhuma ambazo zinasambazwa kwa sasa na Mtandao wa Wiki leaks ni juhudi za wazi za idara ya ujasusi ya Marekani kuhakikisha kuwa inamfunga mdomo jumla JK ambaye katika siku za karibuni serikali yake imekuwa na msimamo usioegemea upande wowote katika kadhia ya NATO na serikali inayoondoshwa madarakani ya Muamar Gaddafi.
Sikubaliani na Udhaifu wa Serikali ya JK katika masuala mengi ya msingi ambayo watendaji wake wanamunagusha kwa kiwango kikubwa na yeye kushindwa kuthubutu kutoa maamuzi mazito, lakini kwa hili la WIKI Leaks nashawishika kusimama upande wa pili wa mstari na kusema enough of these none sense from western world.
Haiwezekani tuhuma hizo mmezikalia muda wote huo na leo ndo mnakuja kuzitoa kama lengo ilikuwa kuonyesha madhaifu haya, yalikuwa msaada mzuri kwa watanzania hapo Oktoba 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba tunakwenda kuchagua kiongozi ambaye si safi, na si leo huu ni unafiki na kutaka kutuchanganya watanzania.
Binafsi huu ni upuuzi na nadhani Acheni Afrika ifanye mambo yake yenyewe na Viongozi waendeshe serikali zao kwa uhuru na Demokrasia. Mkisimamia mawazo ya kuongeza transparency, Accountability na Democracy nitawaelewa.
Kuna UN Democracy charter ambayo ni suluhisho la siasa mbovu za Tanzania, hili ndilo ambalo lingesikika leo mkilipigia kelele tuiridhie charter hii ambayo Tanzania mpaka sasa wanajiuliza waridhie ama la maana itawapa safari ya mapema kuachia madaraka na si design ya suti na rushwa za kuibua muda huu.
Hili linafanyika ili kuficha wizi wa mafuta unaofanywa na kampuni za BP, SHELL na miamba wengine huko LIBYA Mwizi anampigia kelele mwizi mwenzie kwa kuwa yeye ana mbwa nayeweza kubweka kwa sauti kubwa zaidi.
HAPANA,Sidanganyiki kwa hili.
ADIOS