Jk aongoza maziko ya shekh yahya hussein

Tuliza moyo wakooo....

Kubali mapungufu yakoooo...

Chunga tamaa mbaya, Chunga Tamaa mbaya ...

Mtoto wake anaharaka sana ngoja aanze kutoa utabiri hovyo!,

RIP Sheikh Yahya!


yaani ana haraka utadhani anaoga nje
 
Wana jf kwa habari nilizopata hivi punde kupitia 88.4FM mtoto wa Sheh Yahya ameongea hewani akisema babake alishamkabidhi mikoba yake yote na ofisi zote zilizopo Tz, Kenya, London na swazland.
So kinachoniuma zaidi wale ndugu zetu wa magamba bado wanalo kimbilio lao la kuizindika nchi. Jamani Mungu utusaidie tujikomboe kutoka kwenye hizi kamba
RIP Sheh Yahya Husein

Pia mrithi wa Sheikh Yahya ni mwanachama wa CHADEMA....So ondoa hofu yako mkuu...



Mshtuko: Sheikh Yahya kufariki

• KIKWETE, LIPUMBA, ZITTO WAOMBOLEZA


na Bakari Kimwanga




KIFO cha ghafla cha mnajimu mashuhuri Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein (89) kilichotokea katika Hospitali ya Mount Ukombozi jijini Dar es Salaam kimeibua mshtuko mkubwa katika jamii.

Habari kwamba Sheikh Yahya amefariki dunia zilianza kusambaa kama uvumi dakika chache baada ya tukio hilo kutokea majira ya saa 5:00 za asubuhi jana kabla ya kuthibitishwa muda mfupi baadaye kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na mtoto mkubwa wa mnajimu huyo, Hassan Yahya Hussein.

Ilikuwa ni vigumu kwa watu waliozisikia taarifa hizo kuziamini kwa haraka hasa ikizingatiwa kwamba hiyo ilikuwa ni mara ya pili katika kipindi kifupi kwa mnajimu huyo kuhusishwa na kifo.

Akieleza namna baba yake alivyofikwa na mauti, Hassan alisema mnajimu huyo aliamka jana asubuhi akionekana kuwa bukheri wa afya kabla ya hali yake kubadilika ghafla majira ya saa 3:00 za asubuhi.

Hassan ambaye ndiye aliyerithishwa mikoba ya unajimu na baba yake, alisema mabadiliko hayo ya afya za mnajimu huyo yalisababisha akimbizwe katika hospitali ya Mount Ukombozi, iliyopo Morrocco, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Mtoto huyo wa Sheikh Yahya ambaye ndiye aliyesoma unajimu wa mwisho akiwa na baba yake miezi michache tu iliyopita, alisema afya ya mzazi wake huyo ilianza kuzorota miaka mitano iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya moyo.

Akisimulia, Hassan alisema kutokana na maradhi hayo ya moyo, wakati fulani mwaka jana, mzee wake alilazimika kwenda kutibiwa India.

“Baba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa miaka mitano sasa … lakini hata umri wake wa utu uzima ni kigezo cha kuitwa na Mwenyezi Mungu. Kilichobaki ni kuwa na subira kwetu.

“Alikuwa mtu wa watu na kila mara alikuwa akihubiri umoja na mshikamano miongoni mwetu sisi watoto na hata miongoni mwa wanafunzi wake na hakika leo hii imetimu kufuata usia wake,” alisema Hassan.

Alisema baada ya kufikwa na mauti hayo, walimchukua marehemu na kuupeleka mwili wake hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Ratiba ya mazishi yake

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya mnajimu huyo ambaye amekuwa na taswira tofauti katika jamii ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Sheikh Alhad alisema mwili utaanza kuandaliwa majira ya saa 4:00 asubuhi leo hii na utachukuliwa na kupelekwa nyumbani kwake eneo la Magomeni, Mwembechai kwa ajili ya dua mbalimbali kutoka kwa masheikh na Waislamu wenzake.

Sheikh Alhad, alisema mara baada ya kumalizika kwa taratibu za dua, mwili utachukuliwa na kupelekwa katika Msikiti wa Mtambani na kuuswalia na hatimaye kuzikwa katika makaburi ya Tambaza majira ya saa saba mchana.

Alhad, alisema kutokana na kifo cha mwanazuoni huyo mashuhuri wa Korani Afrika Mashariki na Kati hakika ni kigezo chema hasa kwa Watanzania kutathmini na kupenda kufanya yaliyo mema na hata kuijali jamii kwa kutathamini mchango alioutoa katika uhai wake.

Idadi ya watoto alioacha

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Hassan hadi mauti yanamfika, Sheikh Yahya alikuwa ameacha watoto zaidi ya 25 pamoja na mke mwenye umri wa miaka 32.

Alisema katika kipindi chake cha maisha aliacha usia wa kudumisha umoja na mshikamano baina ya watoto wake na majirani zao ili kuweza kuwa kigezo chema ndani na nje ya familia.

Neno lake la mwisho kabla ya kifo

Mtoto huyo mkubwa wa marehemu alisema kuwa jana majira ya saa 12:00 asubuhi alikwenda kumjulia hali na kuhitaji taarifa za ulimwengu juu ya hatima ya Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF), Dominique Strauss-Kahn anayekabiliwa na tuhuma za kubaka na akataka kujua iwapo alikuwa amejiuzulu au ala.

“Nilipokwenda asubuhi kwa Sheikh kumjulia hali alinihoji kuhusu sakata la Mkurugenzi wa IMF kama amejiuzulu au la. Hilo ndilo lilikuwa neno lake la mwisho kwangu na baada ya hapo nilipata simu ya hali yake kubadilidilika nikiwa studio za Radio Uhuru katika kipindi cha Nyota Zetu,” alisema Hassan.

Utabiri wake wa mwisho

Kwa mujibu wa msemaji huyo wa familia alisema kuwa pamoja na harakati za Sheikh katika utabiri hadi mara ya mwisho aliweza kutabiri juu ya vifo vya wasanii, machafuko katika nchi za Kiarabu na kifo cha kiongozi wa Al Qaeda Osama Bin Laden aliyeuawa mwanzoni mwa mwezi huu.

Amkabidhi mtoto wake mikoba

Hassan alisema kuwa shughuli alizokuwa akizifanya marehemu baba yake zitaendelea kutolewa kama kawaida kwani kabla ya kufikwa kwa umauti tayari sheikh huyo alikuwa ameshamkabidhbi mikoba ya utabiri wa nyota na hata kutoa dawa.

“Kabla baba hajafariki alikuwa akitoa elimu kwa watu mbalimbali na mikoba yake aliniachia na hivi sasa huduma zinatolewa na hili tutakuwa tukishirikiana na wasaidizi wake aliokuwa akiwatumia wakati wa uhai wake,” alisema Hassan.


Nafasi alizowahi kuongoza

Kiongozi huyo wa familia alisema kuwa Sheikh Yahya Hussein, aliwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Ulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Msemaji wa Mufti wa Tanzania Marehemu Sheikh Hemed Bin Jumaa Bin Hemed.

Alizitaja nafasi nyingine kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa mali (Nyumba) za Bakwata na Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wasoma Korani nchini huku yeye mwenyewe alikuwa ndiye msomaji mashuhuri.

Kikwete aomboleza

Saa chache baada ya taarifa hizo kuthibitishwa, Rais Jakaya Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi wa mwanzo kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Sheikh Yahya.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sheikh Yahya Hussein ambaye enzi za uhai wake alijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kipaji chake katika masuala ya unajimu wa nyota ambao ulimpatia sifa kubwa.

“Naomba, kama familia, mpokee salamu zangu za pole kwa kuondokewa na kiongozi muhimu na tegemeo kubwa la familia. Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu. Amina.”
Kikwete alikielezea kifo cha Sheikh Yahya kuwa ni pengo kubwa kwani alikuwa mzazi, baba, babu, mlezi na tegemeo kubwa la familia yake.

“Najua ameacha pengo kubwa ambalo litakuwa gumu kuzibika. Najua mko katika kipindi kigumu na cha majaribio. Hivyo nawaombeni muwe na moyo wa uvumilivu na subira. Yote ni mapenzi ya Mola. Napenda kuwahakikishieni kuwa niko nanyi katika kipindi hiki cha maombolezo ya msiba wa mpendwa wenu,” alisema.


Mufti, Waislamu wamlilia

Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaaban Bin Simba alisema alikuwa amepokea taarifa za kifo cha Sheikh Yahya kwa masikito makubwa kwa sababu alikuwa msomaji mashuhuri wa Korani.

Aliyekuwa Imamu wa msikiti wa Mtoro jijini Dar es salaam Sheikh Khalifa Hamis ambaye jana alikuwapo msibani hapo alisema huo ni somo tosha kwa watanzania hasa jamii ya Waislamu ambao wanatakiwa kufanya mambo mema ya kumpendeza Mungu.

Mbowe kushiriki msiba

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kimepokea kwa masikitiko msiba wa Sheikh Yahya Hussen na kimeahidi kushirikina na wafiwa katika msiba huo.

Akizungumza na Tanzania Daima jana katika eneo la msiba Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Tanzania Bara), Zitto Kabwe, alisema kuwa chama chao kinatoa pole kwa wafiwa na Watanzania kwa ujumla.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema: “Mtoto wa Mkubwa wa Sheikh Yahya (Hassan) ni mwanachama wetu na kutokana na msiba huu CHADEMA itashiriki kwa hali na mali na kesho Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atashiriki msiba huu.”
Aidha alisema mnajimu huyo mashuhuri atakumbukwa na Watanzania wengi na kifo chake ni pigo kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla.

CCM watoa pole

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa wafiwa na familia kwa ujumla kutokana na msiba wa Sheikh Yahya.

Akizungumza na Tanzania Daima Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema msiba ni jambo la kila mmoja na kifo cha sheikh Yahya kimegusa hisia za Watanzania kila kona ya nchi.

“Tunawapa pole wafiwa kwa msiba na Mungu awape subira wafiwa kutokana na msiba huo mzito kwa familia na jamii ya Watanzania kwa ujumla,” alisema Nape.

Prof. Lipumba amzungumzia Sheikh Yahya

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema kuwa msiba huo wa Sheikh ni pigo kwa Watanzania na Waislamu kwa ujumla.

“Yapo mengi aliyoyafanya nchini na mchango wake kuonekana na hakika CUF tunawapa pole wafiwa kwa msiba mzito wa kufiwa na Sheikh Yahya tutamkumbuka kwa mengi,” alisema Profesa Lipumba

Source: Gazeti la Tanzania Daima.
 
MziziMkavu.....hii habari mbona ilishatoka toka jana saa tano asubuhi hapa hapa JF......au wewe ndio umeisikia leo?
 
Hapa kinachonisikitisha huyu mwanae Hussein ni kamanda wa CHADEMA na aligombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la kinondoni mwaka 2005 na mwaka jana 2010 aligombea Udiwani magomeni kata ya mzimuni kwa tiketi ya CHADEMA lakini kura hazikuosha.
Namshauri aendeleze yale mema tu ya baba yake, lakini hili la kufuga majini na kutoa tabiri za kuwajaza hofu Watanzania halikubaliki. kama kungekuwa na dawa ya kushinda uchaguzi kweli. basi huyu mwanae Sheikh ubwabwa angekuwa tayari ni mbunge au diwani kwa tiketi ya CHADEMA.
...basi na dogo ane atawawekea mazindiko hao CHADEMA ili mambo yawanyokeee....:pound::pound::pound:
 
dah! barabara ya morogoro ili fungwa kwa saa zima leo majira ya saa nane hadi saa tisa ili kuruhusu waandamanaji walio kuwa wameubeba mwili wa Sheikh Yahya kupita ukitokea msikitini kuelekea makaburini maeneo ya karibu na hospital ya Muhimbili.

Hakika safari yake imefana sana hasa kutokana na wasindikizaji wengi walio msindikiza kwenye safari yake ya mwisho, wengi wa wasindikizaji walikuwa wamevaa vibarakashia, sijui ndio kusema hawa watu ndio walikuwa wafuasi wake au kutokana na imani yake?

Napenda kutoa pole yangu kwa mh.Jakaya M.Kikwete kwa kuondokewa na mlizi wake hodari, hakika nipengo kubwa sana ambalo wakuliziba hayupo kwa sasa! Hofu yangu ni kwamba rais wetu usalama wake kwa sasa utakuwa mashakani...

Hivyo basi watanzania tuzidishe ulinzi kwa mpendwa wetu Jakaya Kikwete ili wabaya wake wasimzuru... Kwa wale wenye huwezo kama wa Sheikh Yahya jitokezeni kutoa ulinzi tafadhali...


R.I.P Sheikh Yahya
 
''.......napenda kutoa pole yangu kwa mh.Jakaya M.Kikwete kwa kuondokewa na mlizi wake hodari, hakika nipengo kubwa sana ambalo wakuliziba hayupo kwa sasa! Hofu yangu ni kwamba rais wetu usalama wake kwa sasa utakuwa mashakani...

Hivyo basi watanzania tuzidishe ulinzi kwa mpendwa wetu Jakaya Kikwete ili wabaya wake wasimzuru... Kwa wale wenye huwezo kama wa Sheikh Yahya jitokezeni kutoa ulinzi tafadhali...''

Hatari kweli kweli! Labda wa Loliondo atachukua nafasi!
 
dah! barabara ya morogoro ili fungwa kwa saa zima leo majira ya saa nane hadi saa tisa ili kuruhusu waandamanaji walio kuwa wameubeba mwili wa Sheikh Yahya kupita ukitokea msikitini kuelekea makaburini maeneo ya karibu na hospital ya Muhimbili.

Hakika safari yake imefana sana hasa kutokana na wasindikizaji wengi walio msindikiza kwenye safari yake ya mwisho, wengi wa wasindikizaji walikuwa wamevaa vibarakashia, sijui ndio kusema hawa watu ndio walikuwa wafuasi wake au kutokana na imani yake?

Napenda kutoa pole yangu kwa mh.Jakaya M.Kikwete kwa kuondokewa na mlizi wake hodari, hakika nipengo kubwa sana ambalo wakuliziba hayupo kwa sasa! Hofu yangu ni kwamba rais wetu usalama wake kwa sasa utakuwa mashakani...

Hivyo basi watanzania tuzidishe ulinzi kwa mpendwa wetu Jakaya Kikwete ili wabaya wake wasimzuru... Kwa wale wenye huwezo kama wa Sheikh Yahya jitokezeni kutoa ulinzi tafadhali...


R.I.P Sheikh Yahya

hakika unaonyesha jinsi ulivyomdini kwa kuhusisha mavazi ya watu na imani za dini yao lakini sikushangai kwa sababu mfumo kiristo tanzania umeota mizizi mpaka watu kama nyinyi hamna mnachowaza bali kubaguwa watu kwa kutegemea vazi gani mtu kavaa.
 
hakika unaonyesha jinsi ulivyomdini kwa kuhusisha mavazi ya watu na imani za dini yao lakini sikushangai kwa sababu mfumo kiristo tanzania umeota mizizi mpaka watu kama nyinyi hamna mnachowaza bali kubaguwa watu kwa kutegemea vazi gani mtu kavaa.

kwani unadhani ni uongo kua wavaa vile vikofia majority ni Waislamu ? Acha kufikiri ndani ya box.
 
Nadhani makombora ya ulinzi amemwachia mwanae japo ni vigumu kujua kama ana uwezo wa kuyatumia kama ilivyokuwa baba yake.
 
05_11_hz8cha.jpg

Rais Jakaya Kikwete akiweka mchanga katika kabuli la Sheikh Yahya Husein wakati wa mazishi yake leo hii kwenye makaburi ya Tambaza jijini Dar es salaam.
 
Lazima aende manake huyo alikuwa mtabiri na kiongozi wake. Ukiweka matumain kwa mtu katu huwezi kufaulu.Ona sirikali ilivyo, imekuwa ikiongozwa kwa utabiri (uchawi tu).

Jamani Mungu pekee atumainiwe
 
Ni mtu maarufu,ni raia wake na sasa yuko mbele ya Mungu,naona si vema sisi kumhukumu wala kuhukumu wanaohudhuria mazishi yake.Ana ubaya na uzuri wake ila historia itahukumu
 
Hivi Mheshimiwa amerudi lini toka Namibia.... Duuhh!!! ILA NAOMBA SAMAHANI MWENZENU NILIKUWA NIMELALA!!!!
 
Back
Top Bottom