Jk aongoza maziko ya shekh yahya hussein

Discussion in 'Celebrities Forum' started by peacebm, May 20, 2011.

 1. p

  peacebm Senior Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Jan 31, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana jf kwa habari nilizopata hivi punde kupitia 88.4FM mtoto wa Sheh Yahya ameongea hewani akisema babake alishamkabidhi mikoba yake yote na ofisi zote zilizopo Tz, Kenya, London na swazland.
  So kinachoniuma zaidi wale ndugu zetu wa magamba bado wanalo kimbilio lao la kuizindika nchi. Jamani Mungu utusaidie tujikomboe kutoka kwenye hizi kamba
  RIP Sheh Yahya Husein
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,305
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Mungu anawaona kuendesha nchi kwa majini

  wote watachukuliwa kwa nguvu na sara za umma
   
 3. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  Kwa Bwana kila goti litapigwa. Jina lake lapita majina yote.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 23,901
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 63
  Amelaaniwa mtu amtegemeaye mwanadamu kuwa ngao na kinga ya maisha yake.
  Je tutaepukaje laana hii iwapo Mkuu wetu wa nji alitegemea ulinzi usio onekana kutoka kwa huyu shehe magirini?
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,069
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 38
  rz 1?au nani?
   
 6. p

  peacebm Senior Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Jan 31, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu azibue akili za watanzania jamani
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  May 20, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 14,268
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 48
  Siku zote biashara za kiafra akifa founder kwishney! Yani shughuli ya kigagula yahaya isiyo na business plan haitadumu kamwe! Labda sasa mademu na wake za watu watamkoma huyo kigagula mtoto!
   
 8. x

  xman JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzee afadhali numenijuza kumbe huyu sheikh alikuwa na ofisi hadi london????mweeeee!!!!
   
 9. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 36,640
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 0
  Junior Yahaya:mimba:
   
 10. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 5,676
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 38
  Tumechoka na hizi nguvu za giza.
   
 11. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 902
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuliza moyo wakooo....

  Kubali mapungufu yakoooo...

  Chunga tamaa mbaya, Chunga Tamaa mbaya ...

  Mtoto wake anaharaka sana ngoja aanze kutoa utabiri hovyo!,

  RIP Sheikh Yahya!
   
 12. Tanganyika1

  Tanganyika1 JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  du huyo mwanae ni noma. Yaani hata dingi hajazikwa yeye anatangaza nia..inaelekea amesubir kwa muda mrefu sana.
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,938
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hakuna lolote.Nguvu za giza zimeshindwa kwa jina la Yesu.
   
 14. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Mnapoleta upuuzi kwenye masuala ya utu huo ni ushenzi
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 27,733
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 63
  Hapa kinachonisikitisha huyu mwanae Hussein ni kamanda wa CHADEMA na aligombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la kinondoni mwaka 2005 na mwaka jana 2010 aligombea Udiwani magomeni kata ya mzimuni kwa tiketi ya CHADEMA lakini kura hazikuosha.
  Namshauri aendeleze yale mema tu ya baba yake, lakini hili la kufuga majini na kutoa tabiri za kuwajaza hofu Watanzania halikubaliki. kama kungekuwa na dawa ya kushinda uchaguzi kweli. basi huyu mwanae Sheikh ubwabwa angekuwa tayari ni mbunge au diwani kwa tiketi ya CHADEMA.
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 37,059
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 83
  Sheikh Yahya afariki dunia


  Aliyekuwa mnajimu maarufu, Sheikh Yahya Hussein
  Mnajimu maarufu Sheikh Yahya Hussein afariki dunia jijini Dar es Sa;laam. Mtoto wa marehemu, Hassan Yahya Hussein, amedhibitisha kwamba baba yake amefariki dunia mnamo saa nne asubuhi ya leo nyumbani kwake Mwembe Chai jijini Dar es Salaam ambapo alikua anasumbuliwa an maradhi ya moyo.

  Hassan amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani Mwembe Chai, na kwamba maziko yanatarajiwa kufanyika kesho hapo nyumbani kwa marehemu.Mola aiweke Roho ya Marehemu pema Peponi
  CHANZO: NIPASHE
   
 17. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Amen! Mungu ashukuriwe kuwa ameamua kutukomboa mwenyewe! Mungu karibu Tanzania uisafishe nchi hii, tumeonewa vya kutosha, vunja kila miungu inayoabudiwa kinyume chako, wakomeshe watawala wanaotusababishia maisha magumu hadi wengine tunakikosea kwa kulazimishwa! Wachukue utumwani watawala wetu kama ulivyomchukua mfalme Nebkadreza porini miaka saba! Hiyo iwe kwa wale unaotaka wajirekebishe, lakini kwa wengine waondolee mbali pamoja na uzao wao kama Ahabu na Sauli! Najua kila aliyemtumainia mchawi akakuacha wewe utamshughulikia kikamilifu na haitakuwa kwa sauli na Ahabu tu, tunataka kukuona ktk hili ili tuamini maneno yako kuwa yaliyoandikwa kutendeka yalitendeka kweli na ni wewe yuleyule jana, leo na hata milele.
  Nakushukuru Mungu kwa kusikia maombi yangu kwa niaba ya WaTanzania wote
  wanaoteseka na kuonewa na jina lako na watumishi wako kutukanwa!
   
 18. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 4,187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 38
  kumbe CHADEMA WAMERITHI MIKOBA YA SHEHE YAHAYA...! HAYA JITABIRIENI SASA
   
 19. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,645
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hofu ni kwa wale alio wawekea ulinzi uso onekana! Kifo ni njia ya kila mmoja wetu kuondoka duniani!
   
 20. N

  Nguto JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,670
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 38
  Amen! Ngome zote za mwovu shetani naziangusha kwa jina la YESU. Uhimidiwe Mungu kwa kuwa umedhihirisha kuwa WEWE ni MUNGU
   
 21. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #21
  May 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 6,240
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 38
  Umemaliza kutukana?, tufafanulie basi ili tuelewe na tufaidike na janvi.
   
 22. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #22
  May 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,059
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Ha ha haaaa... possible!!
   
 23. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #23
  May 21, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 19,301
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 38

  yaani ana haraka utadhani anaoga nje
   
 24. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #24
  May 21, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 48
  Pia mrithi wa Sheikh Yahya ni mwanachama wa CHADEMA....So ondoa hofu yako mkuu...  Mshtuko: Sheikh Yahya kufariki

  • KIKWETE, LIPUMBA, ZITTO WAOMBOLEZA


  na Bakari Kimwanga
  KIFO cha ghafla cha mnajimu mashuhuri Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein (89) kilichotokea katika Hospitali ya Mount Ukombozi jijini Dar es Salaam kimeibua mshtuko mkubwa katika jamii.

  Habari kwamba Sheikh Yahya amefariki dunia zilianza kusambaa kama uvumi dakika chache baada ya tukio hilo kutokea majira ya saa 5:00 za asubuhi jana kabla ya kuthibitishwa muda mfupi baadaye kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na mtoto mkubwa wa mnajimu huyo, Hassan Yahya Hussein.

  Ilikuwa ni vigumu kwa watu waliozisikia taarifa hizo kuziamini kwa haraka hasa ikizingatiwa kwamba hiyo ilikuwa ni mara ya pili katika kipindi kifupi kwa mnajimu huyo kuhusishwa na kifo.

  Akieleza namna baba yake alivyofikwa na mauti, Hassan alisema mnajimu huyo aliamka jana asubuhi akionekana kuwa bukheri wa afya kabla ya hali yake kubadilika ghafla majira ya saa 3:00 za asubuhi.

  Hassan ambaye ndiye aliyerithishwa mikoba ya unajimu na baba yake, alisema mabadiliko hayo ya afya za mnajimu huyo yalisababisha akimbizwe katika hospitali ya Mount Ukombozi, iliyopo Morrocco, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

  Mtoto huyo wa Sheikh Yahya ambaye ndiye aliyesoma unajimu wa mwisho akiwa na baba yake miezi michache tu iliyopita, alisema afya ya mzazi wake huyo ilianza kuzorota miaka mitano iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya moyo.

  Akisimulia, Hassan alisema kutokana na maradhi hayo ya moyo, wakati fulani mwaka jana, mzee wake alilazimika kwenda kutibiwa India.

  “Baba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa miaka mitano sasa … lakini hata umri wake wa utu uzima ni kigezo cha kuitwa na Mwenyezi Mungu. Kilichobaki ni kuwa na subira kwetu.

  “Alikuwa mtu wa watu na kila mara alikuwa akihubiri umoja na mshikamano miongoni mwetu sisi watoto na hata miongoni mwa wanafunzi wake na hakika leo hii imetimu kufuata usia wake,” alisema Hassan.

  Alisema baada ya kufikwa na mauti hayo, walimchukua marehemu na kuupeleka mwili wake hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

  Ratiba ya mazishi yake

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya mnajimu huyo ambaye amekuwa na taswira tofauti katika jamii ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

  Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Sheikh Alhad alisema mwili utaanza kuandaliwa majira ya saa 4:00 asubuhi leo hii na utachukuliwa na kupelekwa nyumbani kwake eneo la Magomeni, Mwembechai kwa ajili ya dua mbalimbali kutoka kwa masheikh na Waislamu wenzake.

  Sheikh Alhad, alisema mara baada ya kumalizika kwa taratibu za dua, mwili utachukuliwa na kupelekwa katika Msikiti wa Mtambani na kuuswalia na hatimaye kuzikwa katika makaburi ya Tambaza majira ya saa saba mchana.

  Alhad, alisema kutokana na kifo cha mwanazuoni huyo mashuhuri wa Korani Afrika Mashariki na Kati hakika ni kigezo chema hasa kwa Watanzania kutathmini na kupenda kufanya yaliyo mema na hata kuijali jamii kwa kutathamini mchango alioutoa katika uhai wake.

  Idadi ya watoto alioacha

  Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Hassan hadi mauti yanamfika, Sheikh Yahya alikuwa ameacha watoto zaidi ya 25 pamoja na mke mwenye umri wa miaka 32.

  Alisema katika kipindi chake cha maisha aliacha usia wa kudumisha umoja na mshikamano baina ya watoto wake na majirani zao ili kuweza kuwa kigezo chema ndani na nje ya familia.

  Neno lake la mwisho kabla ya kifo

  Mtoto huyo mkubwa wa marehemu alisema kuwa jana majira ya saa 12:00 asubuhi alikwenda kumjulia hali na kuhitaji taarifa za ulimwengu juu ya hatima ya Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF), Dominique Strauss-Kahn anayekabiliwa na tuhuma za kubaka na akataka kujua iwapo alikuwa amejiuzulu au ala.

  “Nilipokwenda asubuhi kwa Sheikh kumjulia hali alinihoji kuhusu sakata la Mkurugenzi wa IMF kama amejiuzulu au la. Hilo ndilo lilikuwa neno lake la mwisho kwangu na baada ya hapo nilipata simu ya hali yake kubadilidilika nikiwa studio za Radio Uhuru katika kipindi cha Nyota Zetu,” alisema Hassan.

  Utabiri wake wa mwisho

  Kwa mujibu wa msemaji huyo wa familia alisema kuwa pamoja na harakati za Sheikh katika utabiri hadi mara ya mwisho aliweza kutabiri juu ya vifo vya wasanii, machafuko katika nchi za Kiarabu na kifo cha kiongozi wa Al Qaeda Osama Bin Laden aliyeuawa mwanzoni mwa mwezi huu.

  Amkabidhi mtoto wake mikoba

  Hassan alisema kuwa shughuli alizokuwa akizifanya marehemu baba yake zitaendelea kutolewa kama kawaida kwani kabla ya kufikwa kwa umauti tayari sheikh huyo alikuwa ameshamkabidhbi mikoba ya utabiri wa nyota na hata kutoa dawa.

  “Kabla baba hajafariki alikuwa akitoa elimu kwa watu mbalimbali na mikoba yake aliniachia na hivi sasa huduma zinatolewa na hili tutakuwa tukishirikiana na wasaidizi wake aliokuwa akiwatumia wakati wa uhai wake,” alisema Hassan.


  Nafasi alizowahi kuongoza

  Kiongozi huyo wa familia alisema kuwa Sheikh Yahya Hussein, aliwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Ulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Msemaji wa Mufti wa Tanzania Marehemu Sheikh Hemed Bin Jumaa Bin Hemed.

  Alizitaja nafasi nyingine kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa mali (Nyumba) za Bakwata na Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wasoma Korani nchini huku yeye mwenyewe alikuwa ndiye msomaji mashuhuri.

  Kikwete aomboleza

  Saa chache baada ya taarifa hizo kuthibitishwa, Rais Jakaya Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi wa mwanzo kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Sheikh Yahya.

  “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sheikh Yahya Hussein ambaye enzi za uhai wake alijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kipaji chake katika masuala ya unajimu wa nyota ambao ulimpatia sifa kubwa.

  “Naomba, kama familia, mpokee salamu zangu za pole kwa kuondokewa na kiongozi muhimu na tegemeo kubwa la familia. Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu. Amina.”
  Kikwete alikielezea kifo cha Sheikh Yahya kuwa ni pengo kubwa kwani alikuwa mzazi, baba, babu, mlezi na tegemeo kubwa la familia yake.

  “Najua ameacha pengo kubwa ambalo litakuwa gumu kuzibika. Najua mko katika kipindi kigumu na cha majaribio. Hivyo nawaombeni muwe na moyo wa uvumilivu na subira. Yote ni mapenzi ya Mola. Napenda kuwahakikishieni kuwa niko nanyi katika kipindi hiki cha maombolezo ya msiba wa mpendwa wenu,” alisema.


  Mufti, Waislamu wamlilia

  Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaaban Bin Simba alisema alikuwa amepokea taarifa za kifo cha Sheikh Yahya kwa masikito makubwa kwa sababu alikuwa msomaji mashuhuri wa Korani.

  Aliyekuwa Imamu wa msikiti wa Mtoro jijini Dar es salaam Sheikh Khalifa Hamis ambaye jana alikuwapo msibani hapo alisema huo ni somo tosha kwa watanzania hasa jamii ya Waislamu ambao wanatakiwa kufanya mambo mema ya kumpendeza Mungu.

  Mbowe kushiriki msiba

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kimepokea kwa masikitiko msiba wa Sheikh Yahya Hussen na kimeahidi kushirikina na wafiwa katika msiba huo.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana katika eneo la msiba Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Tanzania Bara), Zitto Kabwe, alisema kuwa chama chao kinatoa pole kwa wafiwa na Watanzania kwa ujumla.

  Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema: “Mtoto wa Mkubwa wa Sheikh Yahya (Hassan) ni mwanachama wetu na kutokana na msiba huu CHADEMA itashiriki kwa hali na mali na kesho Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atashiriki msiba huu.”
  Aidha alisema mnajimu huyo mashuhuri atakumbukwa na Watanzania wengi na kifo chake ni pigo kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla.

  CCM watoa pole

  Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa wafiwa na familia kwa ujumla kutokana na msiba wa Sheikh Yahya.

  Akizungumza na Tanzania Daima Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema msiba ni jambo la kila mmoja na kifo cha sheikh Yahya kimegusa hisia za Watanzania kila kona ya nchi.

  “Tunawapa pole wafiwa kwa msiba na Mungu awape subira wafiwa kutokana na msiba huo mzito kwa familia na jamii ya Watanzania kwa ujumla,” alisema Nape.

  Prof. Lipumba amzungumzia Sheikh Yahya

  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema kuwa msiba huo wa Sheikh ni pigo kwa Watanzania na Waislamu kwa ujumla.

  “Yapo mengi aliyoyafanya nchini na mchango wake kuonekana na hakika CUF tunawapa pole wafiwa kwa msiba mzito wa kufiwa na Sheikh Yahya tutamkumbuka kwa mengi,” alisema Profesa Lipumba

  Source: Gazeti la Tanzania Daima.
   
 25. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #25
  May 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,505
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  hivi hili nalo ni tangazo la biashara?.......
   
 26. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #26
  May 21, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 22,716
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 83
  MziziMkavu.....hii habari mbona ilishatoka toka jana saa tano asubuhi hapa hapa JF......au wewe ndio umeisikia leo?
   
 27. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #27
  May 21, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,782
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo mwanawe si yule "diwani" wa CHADEMA?
   
 28. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #28
  May 21, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo nadhani anaishi Loliondo
   
 29. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #29
  May 21, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ...basi na dogo ane atawawekea mazindiko hao CHADEMA ili mambo yawanyokeee....:pound::pound::pound:
   
 30. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #30
  May 21, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dah! barabara ya morogoro ili fungwa kwa saa zima leo majira ya saa nane hadi saa tisa ili kuruhusu waandamanaji walio kuwa wameubeba mwili wa Sheikh Yahya kupita ukitokea msikitini kuelekea makaburini maeneo ya karibu na hospital ya Muhimbili.

  Hakika safari yake imefana sana hasa kutokana na wasindikizaji wengi walio msindikiza kwenye safari yake ya mwisho, wengi wa wasindikizaji walikuwa wamevaa vibarakashia, sijui ndio kusema hawa watu ndio walikuwa wafuasi wake au kutokana na imani yake?

  Napenda kutoa pole yangu kwa mh.Jakaya M.Kikwete kwa kuondokewa na mlizi wake hodari, hakika nipengo kubwa sana ambalo wakuliziba hayupo kwa sasa! Hofu yangu ni kwamba rais wetu usalama wake kwa sasa utakuwa mashakani...

  Hivyo basi watanzania tuzidishe ulinzi kwa mpendwa wetu Jakaya Kikwete ili wabaya wake wasimzuru... Kwa wale wenye huwezo kama wa Sheikh Yahya jitokezeni kutoa ulinzi tafadhali...


  R.I.P Sheikh Yahya
   

Share This Page