Ngolinda
Senior Member
- Apr 12, 2010
- 125
- 25
Katika pitapita zangu kwenye blogs..nilikutana na swali au maoni yaloandikwa na mmoja wa wadau na yanasomeka hivi:
"Ninagusia suala moja tu, 'agizo' la Raisi kwa Wakala. Nawaza na kujiuliza ikiwa agizo hili la Raisi latolewa kama Raisi katika shughuli zake za Kiserikali au kama Mgombea wa Uraisi kupitia CCM katika kampeni?
Sina ufahamu wa miiko ya Katiba na Sheria ya Uchaguzi, hivyo mniwie radhi kwa kuwaza hivi, pengine ikipelekwa kesi mahakamani au ukapotolewa ufafanuzi, nitapata uelewa wa kunisaidia kutofautisha kauli za Raisi wa nchi kwa sasa dhidi ya kauli za Mgombea wa Uraisi kupitia CCM ambaye ni Raisi wa nchi kwa sasa.
Nasema hivi kufuatia kauli ya CHADEMA kuishitaki CCM/Raisi Kikwete kwa anaosema na kuagiza ndani ya kipindi hiki cha kampeni, inakuwa kama "unfair advantage" kwa kuwa yeye ni Raisi kisha anagombea Uraisi.
Yaani ni sawa na kusema kwamba, kwa vile yeye kwa sasa ni Raisi na vile vile yeye ni mgombea Uraisi, basi anatumia kofia mbili kama msumeno kukata kuwili, yaani kutoa agizo kama Raisi na kisha kufanya kampeni kama Raisi mtarajiwa. Unakosekana mpaka (a clear demarcation) wa hili ni agizo haliingiliani na sera. Je, ilipaswa auze sera za CCM Tunduma kisha aondoke, na apange safari nyingine upya, au akiwa katika ofisi yake ya Kitawala, atoe agizo kama Raisi kuhusu Wakala wa ununuzi Tunduma? (waweza kubadili pia kuwa alipaswa atoe agizo kama Raisi na kisha afunge safari ya kampeni ambayo hapaswi kutoa maagizo bali kunadi sera zake). Kwa ilivyo sasa, ni vigumu sana kutofautisha (1) Aliyefika hapa na kutoa agizo ni Raisi wa nchi Jakaya Kikwete na (2) Aliyefika hapa ni Mgombea wa Uraisi Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete."
Maswali haya yanatokana na Mgombea huyo wa urais Jakaya Kikwete kumuagiza Wakala wa Hifadhi ya Chakula (SGR) kuongeza kiwango cha ununuzi wa nafaka kutoka tani 150,000 hadi 400,000 ili kuwapa soko la uhakika wakulima huko Tunduma.