Jk anatembelea sabasaba nani anaenda kuwatembelea Wagonjwa waliogomewa na madaktari?

Ataenda Slaa ambaye anatetea mgomo.


Ritz, nimesikia hoja za wabunge wengi sana toka upande wa ccm wakilalamika mgomo wa madaktari una watu nyuma yake. Labda niseme hivi: Kuku mwenye vifaranga akiona akiona mwewe anapitapita karibu, na kama kweli anawajali vifaranga wake atawaficha kwenye mbawa zake ili wasikumbwe na dhoruba la mwewe.

Kama CCM na serikali yake yenye intelligensia hadi ya kubashiri fujo waliona 'mwewe' anaelekea upande wa madaktari walitakiwa wafanye hima na kuhakikisha wanawaweka salama madaktari ili wasichukuliwe na "mwewe". Na kama ni kweli kuna mgomo wa madaktari una watu/mtu nyuma basi serikali ya CCM haifai. Walikuwa wapi mpaka madaktari wakasikiliza upande mwingine? Airport?

Na mambo ya kujiuliza ni haya:
1. Ni lini serikali ya CCM ilijua kuna watu wanawanyemelea madaktari?
2. Na walifanya nini ili kuwazidi ujanja waliokuwa wanawanyemelea madaktari?
3. Madaktari wana akili timamu na utashi wa kuamua mambo bila msukumo?
4. Kwa nini wanafikiri madaktari wamewakiliza 'hao wengine' na sio serikali?
5. Wagonjwa wafanye nini hasa wale ambao hawako karibu na hospitali za jeshi?
6. Madai ya madaktari kuwa hakuna vifaa tiba ya kweli au si kweli?
7. Ni kweli serikali haina uwezo wa kuwalipa madaktari? (ref 50 celebration budget)
8. Nini mpango wa serikali kutatua tatizo hili? Kuendelea kama kawaida as if nothing kimetokea?
9. Wanatanzia bado waendelee kuwa na imani na serikali ya CCM? Kwa sababu zipi?
 
JK ni kipenzi cha watu. Wananchi walikuwa wanagombea kumshika Mkono huko sabasaba. Hakugombea urais kuja kutatua matatizo yenu. Waliomtangulia kwa nini hawakuyatatua? Mwacheni, yeye ni Rais, ale bata lala salama hii
 
Back
Top Bottom