Bulesi,Hakuna sababu yeyote ya msingi kwanini Mwalimu Nyerere foundation iwe na ukata; nahisi kuna tatizo katika utendaji wa taasisi hii kwani inaendeshwa kama vile ya kifamiliana ndio maana haishamiri kama vile watu wengi walivyotegemea. Mandela foundation inaendeshwa na professionals walioajiriwa kwa uwezo wao na wale waliofanya kazi na mzee Madiba wao sio watendaji bali wako kwenye board ya foundation; hivyo basi kila kitu kinatekelezwa kiutaalam unlike the Mwalimu foundation where Butiku by virtue of being a relative wa Mwalimu amejiweka kuwa mtendaji mkuu. Pia swala la fedha kutotumika vyema wakati foundation inasimamia mgogoro wa Burundi ilileta credibility problem kwa foundation!
Tatizo la taasisi ya Mwalimu limeanza enzi za utawala wa Mkapa. Sababu zenyewe sizijui lakini nilisikia minong'ono kuwa Mkapa alikuwa amedhamiria kufuta legacy ya Nyerere. Kama nilivyosema ni minong'ono. Wachangiaji wakubwa awali wa taasisi hiyo walikuwa Mandela na Museveni. Butiku alipanga kufanya fundraising nchi nzima baada ya Salim kuchukua uongozi lakini Mpaka akaipiga stop mipango hiyo akidhania ni njama za kumkampeinia Salim. Ilifikia wakati Mkapa alimpigia simu Museveni asimpe Butiku hela za foundation kwa sababu eti Butiku anazitumia vibaya...talk about nyani haoni kundule... Eniwei Mwungana angependa kuona kuna uongozi mpya katika taasisi hiyo kwa kuzingatia kwamba wote Salim na Butiku are over 70. Kagame na Museveni wameshaahidi kutoa msaada wa kuiendesha. So it remains to be seen. Taasisi hiyo ikipangwa vizuri inaweza kuwa chombo kizuri sana cha kusaidia katika utatuzi wa migogoro barani Afrika.