JK amteua Jaji Kiongozi mpya

Mkuu Haki.tupu,

nakubaliana na maoni yako yote isipokuwa hili la kusema ''Ila unapomteua mtu asiyejulikana lazima watu wajiulize na ni haki kujiuliza bila mipaka!''.Kwani wanaostahili kuteuliwa ni wanaojulikana tu? nikiteuliwa mimi Kinyamana utaquestion pia kisa sijulikani? Nafikiri hoja isiwe kujulikana kwasababu kuna wazalendo wazuri kwa nchi hii na wana CV nzuri lakini hawajulikani hivyo haiwezi kunifanya nisipewe uongozi.
 
Aah, yaelekea hii ni recent development kwa nafasi ya JK kutengwa "maalum" kwa ajili ya majaji waislam,. Tukianzia na Amir Manento, akafuatiwa na Salum Massati na sasa Fakihi Jundu.Hii imeanza kujitokeza katika utawala wa awamu hii, ndiyo sababu wanapewa nafasi hiyo huku wakiwa hawana uoefu wa kutosha. Matokeo yake majaji waliopo ambao ni "senior" kuliko Jundu kamwe hawawezi kuheshimu maamuzi yake, naye pia anawagwaya.
KITONZEGU

Bora umekuwa muwazi zaidi na ajenda ya kuwa waislamu hawana uzoefu hivyo hawastahili kuwa majaji,ndio maana una mashaka na uteuzi wa Amir maneto, salum masati na fakih Jandu. Nadhani wewe umethibitisha kuwa wote waliohoji uteuzi huu kwa vigezo vya seniority na uwezo wanaamini kuwa akili na uwezo wa mtu kufanya kazi vinategemea dini yake. Nakushauri pamoja na hao wenye imani kama yako muungane na mzee Mkapa katika safari yake ya kwenda kwa Nyerere kuhiji kama alivyoagizwa na Pengo maana mtachanganyikiwa sana, kwani hali imebadilika na kipindi kile cha uteuzi kwa kuangalia dini kimeondoka. Zama hizi vigezo ni uwezo na si dini wala kabila ya mtu ndio maana hata mtu mwenye asili ya Afrika anaongoza taifa la marekani(nchi iliyokuwa na sifa za ubaguzi). Na hao wasio heshimu maamuzi ya kiongozi wao kisa dini yake watapotea kama upepo. Najua hamkuzoea hili lakini hamuwezi kushindana na wakati, discrimination of any kind is not accepted in any society.
 
Jaji Kiongozi ni kama jina linavyoonekana ni kiongozi wa majaji wa mahakama kuu Tanzania. Actually ni mtawala (Administrator) na wala siyo guru wa sheria. Uteuzi wa Jaji Kiongozi haufuati seniority za namba na miaka ya ujaji bali uwezo wa mtu kiutawala, ambalo nafikiri ni jambo la kawaida kila sehemu kuhusiana na kazi za kiutawala. Labda nimrekebishe MKJ kidogo kwamba mfumo wa kimahakama Tanzania uko kama alivyoupanga lakini kwa marekebisho kidogo; Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya Hakimu Mkazi (wengine huiita mahakama ya mkoa), Mahakama Kuu na mwisho kabisa Mahakama ya Rufani. Mahakama Kuu ndio ina vitengo kwa ajili ya kushughulikia kesi za aina hiyo, na mpaka sasa kuna kitengo cha mahakama kuu (Biashara) Mahakama Kuu (Labour) na Mahakama Kuu (kitengo cha Ardhi). Mahakama kuu imegawanyika katika kanda (kimahakama zinaitwa District Registries) kulingana jiografia na vile vile kwa maoni yangu zilipangwa kutokana na wingi wa kesi katika maeneo hayo. hivyo kuna mahakama kuu kanda ya Dar es salaam, Tanga, Arusha, Moshi, Mwanza, Mtwara, Mbeya, Iringa na Dodoma. Kila Kanda inakuwa na majaji na Jaji mfawidhi. Majaji wafawidhi na wenyewe ni nafasi za kiutawala lakini mara nyingi wafawidhi na majaji senior kwenye kituo/kanda hiyo au anahamishwa kutoka kanda nyingine. Ni kweli Jaji Jundu alikuwa wakili wa kujitegemea (huo uchovu aliosema member fulani sijui alikuwa alikuwa na maan gani) baadaye akateuliwa na rais Mkapa kuwa jaji ambaye alipangiwa kituo cha Moshi na baadaye akapelekwa Iringa kama jaji mfawidhi. SIna uhakika lakini nafikiri alikuwa peke yake kwenye kituo hicho. Kwahiyo hakuna cha ajabu kwa rais kumchagua jaji Jundu kuwa Jaji Kiongozi kama ana uwezo wa kiutawala. Kuna Majaji wengi ambao wana uwezo mkubwa wa kisheria lakini labda siyo wazuri kiutawala na ndio maana wanatoka mahakama kuu bila kuwa hata majaji wafawidhi wala jaji kiongozi na kuwa jaji wa mahakama ya rufani ambako kule panatolewa maamuzi mazito ya kisheria. Kwa taarifa, hata mawakili hawaruhusiwi kuendesha rufani katika mahakama ya rufani kama hajafikisha miaka mitano tangu aapishwe kama wakili wa mahakama kuu.
Sahihisho, ni kweli kwamba rufani mahakama kuu huwa zinakisikilizwa na majaji watatu. lakini vile vile huwa kuna maombi (Applications) ambazo huwa zinasikilizwa na jaji mmoja. Kama hukuridhika na maamuzi ya majaji kwa kuangalia grounds ambazo zipo kisheria (they are specifically provided and not from your case) basi unaweza ukaiomba mahakama ya rufani ikae kama full court. Na full court haina maana kwamba ni majaji wote wa mahakama ra rufani bali majaji watano.

Ahsante
 
Mwanakijiji anasema kama mwaka mmoja uliopita Jandu alikuwa wakili hadi alipoteuliwa kuwa Jaji. Jobo anasema Jandu aliteuliwa kushika wadhifa wa ujaji kama miaka mitano iliyopita. Sasa sijui hapa nani MUONGO.

Hiyo ya mwaka mmoja mleta taarifa ameshasema habari yake ni kwa mujibu wa anavyojua yeye. Hana hakika.

Posted by JMushi: MKJJ nilikuwa nina swali…Je ina maana chini ya mwaka mmoja amepanda ngazi zote mbili toka alipokuwa wakili wa kujitegemea?

Mzee Mwanakijiji: exactly! as far as I know
 
Mwanakijiji anasema kama mwaka mmoja uliopita Jandu alikuwa wakili hadi alipoteuliwa kuwa Jaji. Jobo anasema Jandu aliteuliwa kushika wadhifa wa ujaji kama miaka mitano iliyopita. Sasa sijui hapa nani MUONGO.

Niwie radhi kaka Mfumwa tutumie lugha ya kiungwana/kidiplomasia.Mwanakijiji na Jabo nani KAKOSEA? au NANI YUKO SAWA?
 
Hakuna anayesema ukweli na hakuna anayesema uongo! Ukweli ni kuwa Jundu aliteuliwa kipindi cha Mkapa na si hiki cha Jakaya but ni mwishoni kabisa so it could be less than 5 years ago. Cha muhimu hapa ni kuwa ana muda mfupi katika ujaji. Nakumbuka kituo chake cha kwanza kilikuwa Moshi na alikuwa chini ya Jengafibili Mwaikugile ambaye sasa atakuwa chini yake.
 
Ukweli ni kuwa...so it could be less than 5 years ago.

Kwa hiyo wewe mwenye "ukweli ni kuwa," ni kwamba ukweli wako uko based on "it could be"!

Bado hatuna uhakika na tarehe sahihi za résumé ya bwana huyu.

Mjadala huu waweza kuwa kama mijadala yenye vichwa cha habari vya alama ya kuuliza!
 
Inawezekana uko sahihi. Pale TRA Kamishna wa Forodha alimaliza muda wake wa utumishi tangu mwezi juni 2008. Ilipofika November 2008 wakatangaza nafasi hiyo. Uasili ukafanywa lakini mpaka leo hakuna Kamishna wa Forodha pale TRA.

Labda hawajampata mwenye qualifications
 
hii ni nchi yetu, na hizi ndizo sheria zetu, nimuunge mkono Mwakijiji kuwa tumuache rais wa Jamuhuri ateue ila ipo haja hapa sheria zibadilike ili uteuzi wa raisi wa watumishi nyeti kama hawa uwe unathibitishwa na BUNGE.
Maana kasi ya mheshimiwa rais kumpatia vyeo huyo muungwana inatisha , inawezekana ni mchapa kazi lakini ktk ulimwengu huu wa kujenga jamii pana yenye kuhitaji taarifa sahihi inatosha kuhisi kua uteuzi huu unawalakini kidogo, inamaana hakuna majaji waandamizi pale mahakama kuu.......? walioutumikia umma moja kwa moja kwa miaka kenda na kenda...!
SAWA MHESHMIWA RAIS.
 
Mkuu Haki.tupu,

nakubaliana na maoni yako yote isipokuwa hili la kusema ''Ila unapomteua mtu asiyejulikana lazima watu wajiulize na ni haki kujiuliza bila mipaka!''.Kwani wanaostahili kuteuliwa ni wanaojulikana tu? nikiteuliwa mimi Kinyamana utaquestion pia kisa sijulikani? Nafikiri hoja isiwe kujulikana kwasababu kuna wazalendo wazuri kwa nchi hii na wana CV nzuri lakini hawajulikani hivyo haiwezi kunifanya nisipewe uongozi.

Kinyamana ninaposema kujulikana si maanishi kuwa kama Mrema au Liyumba nk. Nina maanisha kuwa na sifa sitahiki tu. Labda niliteleza kidogo, maana yangu ilikuwa mtu mwenye sifa zisizo na utata wowote - si lazima kwangu mimi ila kwa jamii nzima. Si unajua 'justice should not only be served, it should be seen to be served' Hata kama audience ni illiterate! Kwangu kujulikana ni kwa huyo mkuu ndani ya judiciary. Kama huko jamaa wamefurahi sana kwa kuchaguliwa kwake sisi wote tunaohoji uteuzi huu tutakuwa irrelevant!

Kinyamana, ukiteuliwa tutahoji tu, hata dini yako tunaweza kuhoji tu. Lakini ukiteuliwa hapa JF kuwa moderator/facilitator hatuta hoji kwa sababu kwa tunakujua.
 
Niwie radhi kaka Mfumwa tutumie lugha ya kiungwana/kidiplomasia.Mwanakijiji na Jabo nani KAKOSEA? au NANI YUKO SAWA?

Mkuu Jujuman, kama umesoma vizuri kila mtu kataja miaka yake, Mzee Mwanakijiji anasema "Jaji Jandu alikuwa Wakili wa kujitegemea kama mwaka mmoja uliopita hadi alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na sasa kuwa Jaji kiongozi". Na Jobo anasema "Jaji Jundu ameteuliwa kushika wadhifa wa ujaji kama miaka mitano hivi iliyopita akitokea katika Uwakili wa Kujitegemea".

Ndani ya mwaka kama mmoja uliopita Jaji Jandu alikuwa Wakili, ndio akateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, kwa mujibu wa Mwanakijiji. Hivyo ukitafuta mwaka wa juu na chini kwa kutumia "standard error" ama "standard deviation" (SD), kama utajumlisha mwaka 1 na SD, haiwezi kuwa hata miaka 4 ambayo ni chini ya aliyohisi Jobo. Ndio maana nikasema kuna mmoja hapo MUONGO.

Na muongo unaanza kumuona, Jaji aliyeteuliwa na Mkapa, iweje kateuliwa mwaka jana, labda tuseme bado Mkapa anaendesha nchi kwa "Remote control".

Kuna mada ilianzishwa leo na Lole Gwakisa ikisema WANA JF KUWENI MAKINI (https://www.jamiiforums.com/complaints-congrats-advice/24835-wana-jamii-forums-kuweni-makini.html), sema imefungwa na sijui sababu ya kufungwa kwake, maana ilikuwa inazungumzia haya haya. Mtu anapata habari, badala ya kuripoti tu "Kikwete ateua Jaji Kiongozi", anaongeza na mawazo yake anayohisi bila kufanya uchunguzi. Hii inaharibu sifa ya JF. Tunakaa tunajadili UONGO uliotungwa na mtu badala ya kujikita kwa mambo muhimu ya Taifa letu. Sasa hapa mawazo yetu yote tulikuwa tunajua huyu jamaa ana mwaka kama mmoja tangu ateuliwe kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, kumbe ni mawazo ya mtu anayotunga. Hii ni sawa na ile ya mhindi aliyeua naye kajiua, tunajadili mara jana kaonekana mahakamani. Nadhani Jujuman MUONGO umemjua, ukitaka nitamtaja.
 
Nadhani Jujuman hoja yake ni kuwa si uungwana kumwita mtu 'muongo' kwenye forum hii au popote pengine. Inawezekana wote wawili (MKJJ na Jobo) kile walichokisema sio sahihi kwa ujumla au kwa sehemu tu, lakini sidhani kama hili peke yake linawafanya kuwa 'waongo'. Muongo ni mtu mwenye tabia ya kusema vitu visivyo na ukweli kwa makusudi.

Kama binaadamu ni mara nyingi tunateleza na kujikuta kwa bahati mbaya vile tulivyovisema tukiamini kuwa ni kweli tunakuja kugundua kumbe si vya kweli. Hata hivyo kasoro hii haitufanyi kustahili kuitwa waongo.

Binafsi naamini kumwita mmoja wao muongo kwa kasoro hii iliyojitokeza sio haki na wala si uungwana. JF panapaswa kuwa mahala pa waungwana yaani watu wanaojiheshimu na kuheshimu wengine hata kama mnatofautiana kimtizamo au hoja.
 
...Jaji aliyeteuliwa na Mkapa, iweje kateuliwa mwaka jana, labda tuseme bado Mkapa anaendesha nchi kwa "Remote control".

...Mtu anapata habari, badala ya kuripoti tu "Kikwete ateua Jaji Kiongozi", anaongeza na mawazo yake anayohisi bila kufanya uchunguzi.

...Sasa hapa mawazo yetu yote tulikuwa tunajua huyu jamaa ana mwaka kama mmoja tangu ateuliwe kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, kumbe ni mawazo ya mtu anayotunga. Hii ni sawa na ile ya mhindi aliyeua naye kajiua, tunajadili mara jana kaonekana mahakamani. Nadhani Jujuman MUONGO umemjua, ukitaka nitamtaja.

It tip my hat to you Mfumwa, kwa sababu inahitaji ukakamavu kuyasema hayo.

Sasa huu mjadala ni kituko, maana msingi wake ulikuwa kwenye uelewa kwamba mteule ana kama mwaka mmoja wa uzoefu. Achilia mbali pumba za udini na mashudu ya ukabila na kadhalika, msingi wetu ndio huo, rekodi ya kazi. Come to find out habari yenyewe ni ya "as far as I know." Ndio maana huwa nawambia hawa Wakuu tuwe tunatafuta facts. Yale yale ya "Jamiiforums Yaminywa UDSM?" Tunajenga uninformed society.
 
Last edited:
Nadhani Jujuman hoja yake ni kuwa si uungwana kumwita mtu 'muongo' kwenye forum hii au popote pengine. Inawezekana wote wawili (MKJJ na Jobo) kile walichokisema sio sahihi kwa ujumla au kwa sehemu tu, lakini sidhani kama hili peke yake linawafanya kuwa 'waongo'. Muongo ni mtu mwenye tabia ya kusema vitu visivyo na ukweli kwa makusudi.

Kama binaadamu ni mara nyingi tunateleza na kujikuta kwa bahati mbaya vile tulivyovisema tukiamini kuwa ni kweli tunakuja kugundua kumbe si vya kweli. Hata hivyo kasoro hii haitufanyi kustahili kuitwa waongo.

Binafsi naamini kumwita mmoja wao muongo kwa kasoro hii iliyojitokeza sio haki na wala si uungwana. JF panapaswa kuwa mahala pa waungwana yaani watu wanaojiheshimu na kuheshimu wengine hata kama mnatofautiana kimtizamo au hoja.

Mkuu SMU, niliposema kati ya hao wawili kuna MUONGO, nilikuwa namaana mmoja wao anadanganya. Kumwita mtu Muongo sio TUSI, nikumuonesha kuwa alikuwa akidanganya. Ni sawa na CUF baada ya kuanza kusema wameshakubaliana na CCM, CCM walisema CUF ni waongo. Na CUF nao baada ya kikao cha NEC Butiama wakasema CCM ni waongo wanaposema kuwa hawajamaliza hoja zote. Hili neno uongo linatumika sana kuonesha kudanganya. Jee ningesema mmoja wao ANADANGANYA bado ingekuwa sio lugha ya kistaarabu. Ukinionesha kuwa neno MUONGO (Kudanganya) ni tusi, nitaomba msamaha haraka sana, manake muungwana hukubali kukosolewa.

Kuhusu kutofautiana kimtazamo hii hapa JF iko sana, na si tu JF, ipo mashuleni, makazini nk. Hata watoto wa Baba na Mama mmoja hotofautiana, Kulwa na Doto tena wale waliotoka kwa yai moja hutofautiana, seuze hapa JF. Hivyo kutofautiana na mtu haitanifanya nimtukane, fuatilia “posts” zangu mara ngapi nimetofautiana na watu hapa JF na sikutumia maneno machafu. Kwa hilo la kutofautiana kimitizamo hapa JF liweke kando.

Mtu akisema uongo tumuiteje?. Nisaidie ili nifute neno la UONGO kwa matumizi yangu, na niombe msamaha.

Lakini SMU naona unaelekea kuniripoti kwa Invisible, Painkiller ama Silencer, lakini kabla ya hilo niambie nitumie neno gani mtu akidanganya.
 
natumaini hatakuwa ameteua kwasababu ya udini. kwasababu hizi nyazifa nzuri karibia zote naona majina yao yote ni ya pande moja tu. akumbuke mambo kama hayo yakija kuibuka mwakani wakati wa siasa, wakati ambao hata mambo ambayo yanakuwaga sio ya muhumu huwa yanaibuliwa na wapinzani wake, anaweza akajikuta anapoteza kura nyingi. pamoja na kwamba hiyo itakuwa ndio furaha yangu mimi.
 
Kuna kazi tu anaenda kufanya huyo mchaguliwa ,inaonyesha Kikwete anajipanga kupambana na rungu la 2010.
 
.

Mtu akisema uongo tumuiteje?. Nisaidie ili nifute neno la UONGO kwa matumizi yangu, na niombe msamaha.

Lakini SMU naona unaelekea kuniripoti kwa Invisible, Painkiller ama Silencer, lakini kabla ya hilo niambie nitumie neno gani mtu akidanganya.

Mfumwa,

Ni kweli kumwita mtu Muongo si matusi, lakini ni neno lenye makali na kamwe halipaswi kutumiwa na mtu muungwana kama wewe.

Nadhani Jujuman alitoa pendekezo zuri tu:

Originally Posted by jujuman
Niwie radhi kaka Mfumwa tutumie lugha ya kiungwana/kidiplomasia.Mwanakijiji na Jabo nani KAKOSEA? au NANI YUKO SAWA?

Si lazima mtu akisema kitu ambacho 'sio ukweli' basi ni 'uongo'. Uongo ni upotoshaji wa makusudi (mtu anakuwa maekusudia kupotosha) na tena ni tabia inyojirudia mara kwa mara. Kama mtu amesema kitu ambacho si kweli lakini wakati anakisema aliamini kwa dhati ni ukweli basi huyu hatupaswi kumwita muongo.

Tazama Kaka Mdogo alivyorekebisha kiungwana 'ukweli' kuhusu rufani za mahakama kuu (nimeona umekuwa wa mwanzo kumpa 'Thanks' kwenye hii post yake!)

Sahihisho, ni kweli kwamba rufani mahakama kuu huwa zinakisikilizwa na majaji watatu. lakini vile vile huwa kuna maombi (Applications) ambazo huwa zinasikilizwa na jaji mmoja. Kama hukuridhika na maamuzi ya majaji kwa kuangalia grounds ambazo zipo kisheria (they are specifically provided and not from your case) basi unaweza ukaiomba mahakama ya rufani ikae kama full court. Na full court haina maana kwamba ni majaji wote wa mahakama ra rufani bali majaji watano

Kama angelikuwa si muungwana angeweza tu kuwaita waliochangia mwanzo kwamba ni waongo!Lakini alichgua njia hii ya kiungwana kwa kusema/kutoa ukweli bila kumwita/kuwaita jina lolote wachangaiaji ambao hawakuwa na habari sahihi juu ya taratibu za rufani katika mahakama ya rufaa.
 
Mkuu Jk,

Naomba umpe Uwaziri wa Habari Ndugu Mwanakijiji.Achukue Nafasi ya Mkuchika.

Rais Anateua mtu anyeona anamfaa..Mie nataka Ukurugenzi wa PCCB ili nioneshe Mfano.
 
Aaaahh ENL pia alithibitishwa na Bunge. Bunge la sasa hata Rais akimteua kinyago kitapata kura nyingi na kupita. However, I agree with the wise say that "we cant change the rulers, but we can change the rules"
 
Mkuu Jk,

Naomba umpe Uwaziri wa Habari Ndugu Mwanakijiji.Achukue Nafasi ya Mkuchika.

Rais Anateua mtu anyeona anamfaa..Mie nataka Ukurugenzi wa PCCB ili nioneshe Mfano.

Taratibu Gembe, nafasi hiyo uliyotaka hufanyiwa vetting kwanza na mafisadi je unao wa kukupigia debe?
 
Back
Top Bottom