JK amewapata wapi 'WASAFI'?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Katibu Mkuu Kiongozi,Mh.Balozi Ombeni Sefue ameueleza umma wa watanzania kuwa eti Rais Jakaya Mrisho Halfan Kikwete anaendelea/ameshalisuka Baraza makini la Mawaziri litakalokonga nyoyo za watanzania.Baraza,kwa mujibu wa Balozi Sefue,litakuwa na watu wasafi na makini.Rais amewatoa wapi wasafi hao? Mara mbili zilizopita hawakuwepo? Sawa,tunasubiri 'surprise'...
 
RAISJakaya Kikwete anakabiliwa na mtihani mgumu. Ana jukumu zito la kuchekecha upyamiongoni mwa wabunge wa CCM kupata “watakatifu” wapya.
Hiini baada ya “watakatifu” wake wa awali kutikiswa. Wametuhumiwa kwa wizi, ubadhirifuna kushindwa kutekeleza majukumu yao. Kwa maneno machache wameonekanawanamwangusha aliyewateua.
RaisKikwete alipochekecha miongoni mwa wabunge wa chama chake baada ya uchaguzi wamwaka 2010, alipata wateule wake takriban 47. Bila shaka aliona wenginehawatoshi kuvaa viatu vya uwaziri, hadi akaamua kuchukua kwenye akiba yake.
Ilikuziba pengo la “watakatifu” lililojitokeza, Rais Kikwete kwenye mkoba wake wapembeni aliwateua Profesa Makame Mbarawa na Shamsi Vuai Nahodha kuwa wabunge,ili kujazia baraza lake.
Hizizilikuwa dalili tosha kuwa kwenye kapu la wabunge wa kuchaguliwa na vitimaalum, “watakatifu” walikuwa wamekwisha hadi akachukua nje ya bunge. Hii simbaya, kwa kuwa katiba inamruhusu kufanya hivyo.
Sasakibao kimegeuka. Wale aliowaona “watakatifu” wakati ule wamechafuka. Wamejaatuhuma na baadhi yao wametajwa hadi bungeni kuwa ni wezi. Wananchi hawawaaminitena. Wabunge wenzao wamewakataa, wanawalazimisha wajiuzulu, si hivyo bosi wao,Waziri Mkuu Mizengo Pinda aachie ngazi.
Mawaziriwanaotuhumiwa ni Mustafa Mkulo (Fedha), Cyril Chami (Viwanda na Biashara),William Ngeleja (Nishati na Madini), Omar Nundu (Uchukuzi), Ezekiel Maige(Maliasili na Utalii), George Mkuchika (Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEAMI),Profesa Jumanne (Kilimo Chakula na Ushirika) na Dk Hadji Mponda (Afya).
Tuhumadhidi ya mawaziri hawa zimeibuliwa katika ripoti za kamati za kudumu za bungeza Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Serikali za Mitaa (LAAC), na Mashirika ya Umma(POAC) zilizotokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Baadaya dalili kuonekana kuwa mawaziri wanaotuhumiwa wasingejiuzulu, hata baada yawenzao wa CCM kuwashinikiza, umeandaliwa mkakati mbadala wa kuwalazimisha –kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Tayarihoja imewasilishwa bungeni, ikiungwa mkono na saini za wabunge zaidi ya 70,kutaka ipigwe kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Kurahiyo ikipigwa, na zaidi ya nusu ya wabunge wakaiafiki, rais anaarifiwa nawaziri mkuu anaachia ngazi.
Wazirimkuu kuachia ngazi si kazi ndogo wala si mchezo. Ni jambo linalomaanisha kwambaBaraza la Mawaziri linakuwa limevunjwa. Kwa maneno mengine, serikali inakuwaimeanguka, isipokuwa rais peke yake.
Wabungewamefikia hatua hiyo baada ya kuona hakuna dalili za mawaziri hao kujiuzulu.Wameamua kuwashinikiza wafanye hivyo, au wajikute wako nje ya baraza, baada yawaziri mkuu kuenguliwa.
Pamojana tuhuma dhidi yao sasa, Rais Kikwete aliona hawa ndio “watakatifu” wakemiongoni mwa wengi. Inawezekana alifanya kazi hii mwenyewe, akachambua naniawemo na yupi asiwemo. Au alisaidiwa na vyombo vya dola vya kuchuja wateulewake.
Mawazirihawa wameshutumiwa waziwazi ndani na nje ya bunge. Wachache kati yaowamejitetea na wengine wamekaa kimya.
Penginehii ndiyo sababu Rais Kikwete amevuta subira akiwa safarini Brazil na baadayeMalawi, ili apate fursa ya kuchambua ili kubaini pumba ipi na mchele ni upi.Labda anachekecha kichwa kwanza, kuona ni wapi atapata “watakatifu” wapya ndaniya muda mfupi wa serikali.
Itakumbukwahata katika kipindi chake cha kwanza, alilazimika kuunda upya serikali baada yakujiuzulu waziri wake mkuu wa kwanza, Edward Lowassa na mawaziri wawili wenginekutokana na kashfa ya kushinikiza mkataba wa ukodishaji wa mitambo ya kufuaumeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond.
Mawaziriwaliojiuzulu pamoja naye ni Dk. Ibrahim Msabaha wa Afrika Mashariki na NazirKaramagi wa Nishati na Madini.
Haiingiiakilini kuona hata kabla ya miaka miwili kupita “watakatifu” wa Kikwetewanafunikwa na uchafu usiosafishika. Miaka miwili ni kipindi kifupi kwakiongozi msafi kubadilika na kuwa mchafu, hasa kama kuna usimamizi makini juuyake.
Kamatuhuma dhidi ya mawaziri hawa ni za kweli, ninashawishika kuamini kwambawateule hawa huenda walikuwa wachafu hata kabla ya kuteuliwa au itakuwa usimamiziuliopo juu yao ni legelege unaotoa mwanya kwao kuchafuka haraka.
Lakinipia, kama mawaziri hawa waliteuliwa wakiwa wachafu, napata mashaka kama nchiyetu ina vyombo makini vya kuchunguza watu na kubaini uwezo na udhaifu waokabla ya kupendekezwa kwa rais wateliwe, hasahasa kwenye nafasi nyeti kamauwaziri.
Wasiwasiwangu ni iwapo Rais Kikwete akichekecha tena kwenye “makapi” aliyoyaacha wakatiule, atapata watu wa namna gani, ikiwa “watakatifu” walimalizika mwaka 2010.
Nirais kusema ohoo bado wabunge kibao, au ukasema Watanzania ni wengi hadimilioni 45. Lakini nani asiyejua kuwa wananchi kwa sasa hawana imani naserikali yake karibu yote?
Naniasiyejua kuwa wabunge waliopo pia hawaaminiki kwa wananchi waliowachagua? Naniasiyesikia kuwa wabunge wengi ni wala rushwa na wengine walitoa rushwa iliwachaguliwe?
Aunani asiyejua kuwa wabunge wengi walifadhiliwa na matajiri wachafu ili kupatanyadhifa walizonazo? Hivi ni nani asiyejua kuwa mtu yeyote aliyetoa rushwakupata ubunge, akipata nafasi ya madaraka kipaumbele chake ni kurejesha fedhaza waliomwingiza madarakani?
Tukiola karibuni la rushwa iliyokithiri kwa wabunge wakati wa mchakato wa kuwaniaubunge wa Afrika Mashariki na mwaka jana wakati wa sakata la aliyekuwa KatibuMkuu wa Nishati na Madini, David Jairo la kutuhumiwa kuhonga wabunge iliwapitishe bajeti ya wizara hiyo, ni mifano michache ya uchafu wa wabunge.
Kutokanana uchafu huo, hapana shaka ni kazi ngumu kwa Rais Kikwete kupata “watakatifu”wapya. Kitakachosaidia, ni “mkoba” wake aliopewa na katiba, ambao bado unanafasi saba za kuteua wabunge.
Kwamujibu wa katiba, Ibara ya 66 (1) (e), Rais Kikwete anazo nafasi 10 za kuteuawabunge. Ametumia tatu kwa kuwateua Nahodha, Profesa Mbarawa na Zakia Meghji.
Bilashaka atalazimika kuingia kwenye mkoba huo kutafuta Watanzania wengine wenyeuwezo ili awateue kuwa wabunge na baadaye mawaziri, vinginevyo itakuwa vigumukwake kupata “watakatifu” wapya.

Wasafi wako ndani ya CCM kwani CCM inawanachama wengi sana wenye nia na malengo madhubuti ya kuitumikia nchi yetu ndio maana watanzania wenye akili na uelewa wa kutosha hawawezi kuchagua upinzani hata siku moja.Ukitaka kujua CCM ni chama tawala subiri uone 2015 CCM itakavyoshinda kwa kura nyingi na kuyachukua majimbo yote muhimu ambayo CDM inajigamba nayo.

KIDUMU CHAMA TAWALA CHA CCM!
 
wasafi wako ndani ya ccm kwani ccm inawanachama wengi sana wenye nia na malengo madhubuti ya kuitumikia nchi yetu ndio maana watanzania wenye akili na uelewa wa kutosha hawawezi kuchagua upinzani hata siku moja.ukitaka kujua ccm ni chama tawala subiri uone 2015 ccm itakavyoshinda kwa kura nyingi na kuyachukua majimbo yote muhimu ambayo cdm inajigamba nayo.

Kidumu chama tawala cha ccm!

kwa mujibu wa katiba yetu ya sasa una haki ya kutoa maoni yako hata kama ni pumba!!
 
Majembe yapo mengi tu. Kama Filikunjombe, Mwakyembe, Magufuli na wengine rundo tu hadi raha. Hivi nyie wapinzani hamjui kuwa CCM ndio baba yenu tena imewalea hadi mmeota masharubu?.
 
Majembe yapo mengi tu. Kama Filikunjombe, Mwakyembe, Magufuli na wengine rundo tu hadi raha. Hivi nyie wapinzani hamjui kuwa CCM ndio baba yenu tena imewalea hadi mmeota masharubu?.

Kwani hao akina Mwakyembe na Magufuri hawako kwenye hilo baraza la sasa?? Mnatapatapa tu. Kama mna majembe mengi tu.......... mbona hamkuyatumia miaka 6 ya nyuma mpaka Zitto alimtishia mtoto wa mkulima na kitumbua chake?? Kwa maana hiyo msha kubali kuwa waliokuwa pale ni vilaza, kazi imewashinda na hawafai kuwa hapo siyo?? Kama kweli Rais amekubali tena kwa kushinikizwa basi ni dhahiri kuwa tazizo siyo baraza lake bali ni yeye mwenyewe.
 
Wasafi wako ndani ya CCM kwani CCM inawanachama wengi sana wenye nia na malengo madhubuti ya kuitumikia nchi yetu ndio maana watanzania wenye akili na uelewa wa kutosha hawawezi kuchagua upinzani hata siku moja.Ukitaka kujua CCM ni chama tawala subiri uone 2015 CCM itakavyoshinda kwa kura nyingi na kuyachukua majimbo yote muhimu ambayo CDM inajigamba nayo.

KIDUMU CHAMA TAWALA CHA CCM!

Na iwe hivyo!
 
wasafi wako ndani ya ccm kwani ccm inawanachama wengi sana wenye nia na malengo madhubuti ya kuitumikia nchi yetu ndio maana watanzania wenye akili na uelewa wa kutosha hawawezi kuchagua upinzani hata siku moja.ukitaka kujua ccm ni chama tawala subiri uone 2015 ccm itakavyoshinda kwa kura nyingi na kuyachukua majimbo yote muhimu ambayo cdm inajigamba nayo.

Kidumu chama tawala cha ccm!

kaya ikikosa usimamizi toka kwa mkuu wa kaya imepoteza mvuto. Watoto watakurudi nyumbani wengine wakiwa wameshikiria hata chupi mkononi. Ndiyo hayo yanayotokea ccm sasa hivi, mkuu wa kaya chali vijamaa hata ambavyo havikuwahi kuiba maishani sasa vinanyakua mchana kweupe, mkuu wa kaya yuko ziara!!
 
Katibu Mkuu Kiongozi,Mh.Balozi Ombeni Sefue ameueleza umma wa watanzania kuwa eti Rais Jakaya Mrisho Halfan Kikwete anaendelea/ameshalisuka Baraza makini la Mawaziri litakalokonga nyoyo za watanzania.Baraza,kwa mujibu wa Balozi Sefue,litakuwa na watu wasafi na makini.Rais amewatoa wapi wasafi hao? Mara mbili zilizopita hawakuwepo? Sawa,tunasubiri 'surprise'...
Tanzania ina wasomi wengi sana na wenye uwezo wa kuongoza, Rais hastahili kulaumiwa hata kidogo pale mtendaji mmoja anapokeuka maadili kwa sababu yeye(Rais) siyo nabii wa kutabiri ya mbeleni, kwani inawezekana akateua watu wazuri sana lakni kwa tamaa zao wakaharibikia mbele ya safari.
 
Kwani hao akina Mwakyembe na Magufuri hawako kwenye hilo baraza la sasa?? Mnatapatapa tu. Kama mna majembe mengi tu.......... mbona hamkuyatumia miaka 6 ya nyuma mpaka Zitto alimtishia mtoto wa mkulima na kitumbua chake?? Kwa maana hiyo msha kubali kuwa waliokuwa pale ni vilaza, kazi imewashinda na hawafai kuwa hapo siyo?? Kama kweli Rais amekubali tena kwa kushinikizwa basi ni dhahiri kuwa tazizo siyo baraza lake bali ni yeye mwenyewe.

Subiri safu mpya ya ukweli ya Mawaziri sikivu na wenye kufanya kazi kwa umoja kama mchwa. Hii miaka miwili iliyobaki wote mtaanza kuipenda CCM kwa mambo mazuri yatakayokuja kama upepo wa kimbunga. Shaka ondoa kaka.
 
kwa mujibu wa katiba yetu ya sasa una haki ya kutoa maoni yako hata kama ni pumba!!
Mkuu mbona jazba asubuhi yote hii? Heshimu maoni ya wenzako. Ni lazima CCM waonekane hawafai kwa sababu wao ndo wanaongoza, lakini siyo kweli kwamba Rais atakosa watu wasafi toka ndani ya CCM hiyo hiyo wa kuunda baraza safi lenye nia ya dhati ya kuwatumikia Watanzania. Huwezi kusema moja kwa moja kuwa wasafi ni lazima watoke nje ya CCM kwa sababu hao unaowadhania kuwa ni wasafi hawajawahi kupewa nyadhifa hizo tunaona uwezo wao. Kumbuka nguvu ya kutaka madaraka siku zote ni kubwa kuliko nguvu ya kuyaenzi madaraka. Mara zote usijione wewe ndo unaweza kabla haujawezeshwa. Hata hao tunaowaona wameshindwa tuliwapokea kwa shangwe na vigele gele.
 
Stela Manyanya, Mwantumu Mahiza, Anna Abdalah, Simba Chawene, Ahmad Rashid ni miongoni mwa mawaziri wapya
 
kaya ikikosa usimamizi toka kwa mkuu wa kaya imepoteza mvuto. Watoto watakurudi nyumbani wengine wakiwa wameshikiria hata chupi mkononi. Ndiyo hayo yanayotokea ccm sasa hivi, mkuu wa kaya chali vijamaa hata ambavyo havikuwahi kuiba maishani sasa vinanyakua mchana kweupe, mkuu wa kaya yuko ziara!!

Unaweza kuwa Mkuu wa kaya ambayo watoto wote si wako. Mama ndo mwenye uhakika na baba wa mtoto. Tusimlaumu Rais bwana, Hakuna Kiongozi anayechagua waziri ili akaibe, tena kama mtoto alikuwa teja, jambazi au mgomvi anatakiwa abadilike pale anapokabidhiwa heshima ya kmsemaji wa familia. Hao wamepewa nafasi na baba yao wameshindwa wao kama wao, na bahati nzuri Kaya ina watoto wengi tena waliokuwa wanajua kaka zao walijifanya kuvaa ngozi za kondoo kumbe ni chui, subiri muone sasa jinsi ambavyo Kaya itapendeza na kupata heshima kwa jamii.
 
Wote watakao changuliwa hakuna msafi, kwani mtoto wa nyoka ni nyoka, wako wapi wafi wanatoka wapi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom