Elections 2010 JK ametufanyia nini miaka hii 5 hadi tumchague?

AMETUWAKILISHA KWENYE FACEBOOK; atakosa muda wa kushughulikia matatizo ya wananchi ila hawezi kukosa muda wa lucheki ukurasa wake kwenye FB kuona chekibob gani mwingine kampa BIG UP:angry:
Login | Facebook
 
Kikwete again!!!???
Tujiulize CCM imetufanyia nini kwa miaka zaidi ya 40 iliyokaa madarakani kaitka kutibu njaa, ujinga na maradhi ya watanzania...Kikwete ni kitu kidgo sana katika matatizo lukuki yanayolikabili taifa, baada ya miaka kumi ya utawala wake hali itakuwa ndiyo ile ile kama ya miaka 40 iliyopita.
 
Wadau, miaka 5 ya kwanza awamu ya Rais Kikwete iko ukingoni. Kila kiongozi hupimwa na mazuri na mabaya yake ili aweze kuaminiwa na kupewa kipindi kingine cha uchaguzi. Viongozi wa Taifa letu tangu uhuru wamekuwa 4 sasa na kila awamu imekuwa na jema la kujivunia ambalo imetuachia.

Rais wa 1, Nyerere: Kaleta Uhuru na katuachia mshikamano na uzalendo ambao sasa unaporomoka

Rais wa 2, Mwinyi: Katuletea soko huria na kutuondoa kwenye upungufu mkubwa wa bidhaa

Rais wa 3, Mkapa: Alisaidia sana kuukuza uchumi wa nchi yetu, kuongeza mapato ya ndani, kurejesha nidhamu ya matumizi ya pesa za umma, kujenga mitandao ya barabara za lami, daraja la Mkapa na Umoja.

Rais wa 4, Kikwete: Ametufanyia nini hadi sasa hivi ambalo angalau twaweza kumwamini kwa awamu nyingine?

1. Amejenga Chuo kikuu cha Dodoma
2. ..............
 
Nusura ailete timu ya Real Madrid...naamini nikimpa kura October 2010 atalifanikisha hili!!
 
Ukweli ninaouona, unashawishi niamini ni rais Kikwete anayeweza kuwa amevunja rekodi kwa kuwa kiongozi aliyeongoza serikali iliyoshindwa kuliko watangulizi wake.

Mfano Elimu/shule za kata ambazo badala ya kutoa wana-taaluma inatoa wajanja wa baadae.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Tunapoongelea kupanua elimu ya sekondari, tunaharakisha sana kusema watu watachangia ujenzi kwa juhudi zao. Lakini majengo hayana umuhimu wa kwanza…vitu muhimu katika elimu ni walimu, vitabu, na kwa sayansi ni maabara."

Jamani kushindwa kwa Kikwete na chama chake hakuhitaji sana taarifa za uchumi wala utafiti mpana. Mtanzania hahitaji kuambiwa na serikali kama ahadi ya "Maisha bora kwa kila Mtanzania" imetekelezeka au imeshindwa.

Chukua mifano rahisi. Wakati rais Kikwete anaingia madarakani, kilo moja ya sukari ilikuwa ikiuzwa kwa Sh. 600. Hivi sasa inauzwa hadi Sh. 1,500.

Hii ni kauli ya kutusi mtu. Ni dharau na kebehi kwa Watanzania. Ndani ya upinzani wapo viongozi wazuri, wenye kufikiri vema, walio wazalendo kwelikweli kwa nchi yao kuliko walivyo wa CCM.
 
Back
Top Bottom