Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 261
Katika hotuba yake kwa watanzania kupitia sherehe za Mei Mosi leo, Rais Kikwete amezungumza mengi kuhusu taarifa za CAG na utekelezaji wa mapendekezo ya CAG. Mojawapo ya mambo aliyosema ni kwamba aliagiza CAG aweke taarifa za ukaguzi wazi ili wananchi wazijadili. Sijawahi kusikia hiyo kauli wala waraka unaoelekeza hivyo. Lakini hilo siyo tatizo.
Enzi za utawala wa BWM, idara na Wizara nyingi za serikali ndo ziliwezeshwa kuanzisha tovuti na kuweka taarifa muhimu za serikali. Ofisi ya CAG nayo ilianzisha tovuti yake kipindi hicho, kama ilivyokuwa nyingine, kwa ufadhili wa serikali za nje.
Wakati huo CAG alikuwa akibandika taarifa zote za ukaguzi. Yaani taarifa kuu kama zinazobandikwa sasa (serikali kuu, serikali za mitaa na Mashirika ya umma). Alifanya zaidi, akibandika taarifa za ukaguzi na hesabu za kila Wizara, shirika la umma na kila halmashauri na mkoa. Hakuishia hapo, alitoa nakala zilizosainiwa kwa mtu yeyote (mtu yeyote) aliyeomba nakala ya ukaguzi ya taasisi yoyote ya umma.
Kuanzia mwaka 2006, CAG hajabandika taarifa za ukaguzi za taasisi moja moja na alikataa kutoa nakala za taarifa hizo pale zilipoombwa. Madai yake yalikuwa "Ni maagizo kutoka juu". Pia ukifuatilia taarifa hizo kwenye taasisi husika zimezuiwa kwa maelezo hayo hayo.
Ni vema ikaeleweka kwamba aina ya taarifa anazobandika CAG tangu 2006, hazimuwezeshi mtu kupata picha nzima ya financial management ya taasisi moja moja na hivyo hutaweza kutoa maoni wala kutatua matatizo yaliyopo. Pengine ndiyo maana, kama alivyosema Rais, hati safi zimeongezeka kipindi cha utawala wake, lakini pia amekiri viwango vya ufujaji wa pesa za umma vimepindukia kila ngazi ya serikali.
Swala la pili, Rais amesema aliagiza mjadala wa wazi wa ripoti za CAG bungeni. Hilo niwaachie mpime wenyewe!
Nimeona nitoe maoni yangu tu