Mkuu kupeleka bungeni ni suala la kikatiba na lipo wazi kabisa. Alichosisitiza Rais ni kwamba siyo hati ziwekwe mezani tu bali Report ya CAG ipate muda wa kutosha wa kujadiliwa Bungeni.
Jana nimeulizia Report ya CAG yaani general report iliyojadiliwa bungeni nikaelekezwa niende ofisini ama nimtume mtu akanichukulie bila malipo yoyote.
Mtoa mada anasema report zinazotangazwa haziwezi kumfanya mtu kutoa ushauri; ni kweli. wanachoweka pale hasa kwenye magazeti ni sehemu tu ya report yaani Opinion ambayo pale utapata kujua tu kama taasisi imepewa hati safi, ya mashaka ama chafu au mkaguzi alishindwa kabisa kutoa hati (disclaimer). Pale kunakuwa hakuna kitu kinachoitwa management letter ambayo ndiyo inaongelea matatizo ama
Mkuu Kimbunga, hizi ripoti zinapatikana sana, tatizo letu wabongo ni hodari wa kulalamika na kulaumu! CAG report huwa zinapatikana kirahisi kabisa...mathalani, wakati wa maonesho ambapo wananchi wanakusanyika kwa wingi, hizi ripoti huwa zinatolewa kwa anayezihitaji....tena wanaweka hadi kwenye softcopy(CD)!! Wabongo, hatuna utamaduni wa kusoma....leo hii wanajifanya kuzungumzia ripoti za CAG kufanywa siri! Library zetu vyuo vikuu zinageuka Study Room, na unakuta mtu anaanza first year hadi anamaliza, hajawahi azima kitabu!!!!