Hizbu Sharifu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2021
- 450
- 884
- Thread starter
- #261
Mtoa mada usidanganye watu...
Kwanza hata Mtume Muhammad (kwa waislamu) aliwaasa sana watu wasipende kumjua adui wa dizaini hizo bali wajilinde na uadui huo (jikinge kwa mujibu wa Qur'an na wala si vinginevyo)
Pili uchawi ni ushirikina (shirk) na uliletwa na kufundishwa na malaika wawili (harut na marut) waliokuja kibinadamu enzi za Mfalme Suleiman, (najua hapa kutazuka hoja nyingine kuwa iweje malaika walete uchawi ila sipo hapa kwa darasa hilo) bali itoshe tu kusema watu walijipeleka wao wenyewe kujifunza uchawi na hao jamaa hawakumfuza mtu pasi na kumuonya na kumuasa kwanza ila kama ujuavyo binadamu... "...wewe nifundishe tu bwana, habari ya madhara sijui nini niachie mwenyewe..."
Tatu kwenye uislamu kinga ya mtu dhidi ya uchawi na maswala mengine kama hayo ya kiroho haiwezi kuwa kitu chenye kubebwa mfano hirizi msahafu nk. Mtu anakula maharage ili apate protini na wala hapati protini kwa kumshikilia samaki mkononi au punje za maharage kadhalika na Qur'an mtu analazimika kuisoma kama kinga wala si vinginevyo, kama dawa basi atachanganya anavyozichanganya kisha atakula basi. Maana yake ni kwamba kama mtu atashikilia msahafu tu ili uwe kinga kwajili fulani mfano wakati wa kulala au kutembea njia za hatari au gizani usiku basi itakuwa kazi bure
Mwisho habari ya kutafsiri ndoto na mambo kama hayo unaingilia elimu ya ghaib ambayo anayo Mola pekee. Elimu hii aliwafafanulia kwa kiduchu tu mitume wake tena kwa nyakati na matukio maalumu. Mkitaka kutangaza biashara zenu msizunguke zunguke kwa kudanganya au hata kusingizia mambo na kuongea uongo
Nimeassume (nimejireassure) wewe ni muislamu kutokana na majina yako na vitu ulivyotaja hivyo kama wewe siyo mwislamu utanisamehe)
Ndugu yangu asante kwa maelezo yako ila maelezo yako mengi uliotoa sijaona dalili zaidi ya kukosea sanna katika kueleza haya masuala kiufupi harut na marut si malaika, iliposwa malakaini haikumaaniisha malaika bali ni milki mbili ya falme mbili za kijini