Jirani yangu kikojozi,kila mara anaanika godoro,Dawa ya tatizo lake ninaijua.naanzaje kumueleza.

Jun 14, 2016
14
11
Hapa kwenye nyumba nilipopanga tupo wapangaji wawili kama kila mtu upande wake .
Miezi miwili iliyopita nilikua likizo kwa hiyo mara kwa mara nilikua nawahi kurudi nyumbani.

Daah mara nyingi nilikua nakutana na godoro limetolewa nje sehemu ile kuna string za kuanikia nguo,ikumbukwe hiyo sehemu ya kamba za kuanikia nguo tunashare,
Dada ni Sista duu na ni Kauzu so hatunaga story zaidi ya kukumbushana LUKU kama ni necessary kufanya hivyo

Siku moja nikiwa na my g.f,(kabla sijaamua kudate single mom) kumbe naye alikua akijaga na kuona but anapotezea,akaanzisha hiyo maada ya tatizo la jirani.
Binafsi hilo tatizo kuna ndugu yangu ashawahi kuwa kikojozi hadi akiwa form 3 ndipo likizo moja shule tukaendaga kumsalimia shangazi mmoja,akanielekeza miti shamba,ilikua just mizizi ya vimmea fulani,offcourse sijawahi iona hapa mjini ila incase mtu akiihitaji siwezi ikosa nikienda kule tuliitolea,akawa anatafuna na kuloweka kwenye kikombe cha maji anakunywa kadri awezavyo,Siyo chungu according to him,likizo haikuisha akawa kashapona kabisa hadi leo anakimbilia 30's

G.F aliogopa kumwabia yule jirani maana anamfahamu ni cha bangi japo mdada umri umeenda,si unajua hawa dada zetu "wasomi na uzungu na uamerika"
Binafsi siwezi mwambia,itakua unafiki na umbea wa hali ya juu
Wakuu nafanyaje kumsaidia huyu jirani, ikumbukwe ni cha bangi,mie mwenyewe i had a proof of this.

N.B.Tuache theories,kukojoa kitandani ni tatizo la kiafya,lazima utibiwe,hospitali bado hawajagundua dawa,,ooh sijui kutokunywa maji mengi usiku,sijui kumzoesha kumuamsha usiku mhusika akojoe,,it doesn't work
 
Vinakuhusu nini? Wabongo bwana kazi ipo. Rent analipa yeye, hata akitaka nyaku si ni kwake? Respect someone's privacy please, muwe mnatembea hata nje ya Tz kujifunza khaa.

Ngekua mimi ndio huyo Jirani ungekuja ningekuonesha .458 muzzle tu ili ujiheshimu
 
Hiii ndio desturi ya wabongo ya ukarimu na kujali wengine. Au unataka ukarimu na msaada upewe Pale nyumba inapoungua watu waje kuzima? Au kukabwa na vibaka uje kuokoleewa ?
Hapana mkuu hatuishi hivyo.

Privacy ingevunjw endapo huyo dada angeanika ndani kwa siri then jamaa hawe anachungulia.

USHAURI

Hakuna asiyetaka msaada, sema njia unazo tumia hadi kupeleka huo msaada ndo unaweza kuwa tatizo.

Siku mtafute kwa utaratibu tena ukianza na samahani, cheza na akili yake tu muanzie mbali kwa story za huyo ndugu yako na maneno ya kuonesha hiii hali ni ya kawaida mno

Then muahidi kumpa msaada.

Kuna wengine hawapendi kuwa wakaksi au manunda ila wanajisofi tu kwa sababu wana weakness flan flan.
 
mwambie kaka,huenda naye akakusaidia hilo tatizo lako la kubadilisha vimwana coz wewe ndo unalikimbilia tatizo lisilotatulika UKIMWI.
 
Achana na hao akina HAYAKUHUSU hao ndo wale mtu anaumwa hawataki kumsaidia lakini akifa wanajaa kwenye msiba kwa vile wanaogopa watu watawasema kwamna hawahudhurii misiba... SASA SIJUI MSIBA UNAWAHUSUJE..!!!!

Nashauri ufanye hivi;
1. M-face umwambie kuwa unaifahami dawa na utakapokwenda iliko hiyo dawa utarudi nayo au
mweleze ukowa na dawa mkononi
2. Kama la kwanza gumu sana kwako, tafuta ndugu yake yeyote ukiwa na dawa mkononi then mweleze ndugu yake na umpe dawa akampe yeye huku ukimsisitiza kuwa asikutaje
3. Au unaweza ukasubiri yeye ahame au wewe uhame then unalifanya hilo namba moja

NB: Team HAYAKUHU... chukulia wewe ndo kikojozi na akatokea mtu anakupa dawa... UTABAKI KWENYE TEAM HAYAKUHUSU..??!
 
Vinakuhusu nini? Wabongo bwana kazi ipo. Rent analipa yeye, hata akitaka nyaku si ni kwake? Respect someone's privacy please, muwe mnatembea hata nje ya Tz kujifunza khaa.

Ngekua mimi ndio huyo Jirani ungekuja ningekuonesha .458 muzzle tu ili ujiheshimu
Akili ingekuwa ni kiungo cha uzazi ungekuwa huzai...
 
Msaidie huyo dada manake ni bora kikojozi awe mwanaume kuliko shosti! Trust me, mwanamke mwenye hilo tatizo hawezi kuwa na amani hata siku moja. Anaweza kukataa kuolewa na mwanaume ampendae kv tu anaona tatizo lake ni embarrassing!

Ikiwa huwezi kabisa kum-face, basi hiyo dawa ifunge vizuri kwenye gift box kisha ndani weka memo:

Dada Salaam!

Ashakum si matusi na kwa maana hiyo niwie radhi kwa haya nitakayosema. Kimsingi nashawishika kuamini kwamba una tatizo ambalo mimi pia nilikuwa nalo... yaani kukojoa kitandani! Namshukuru Mungu hivi sasa hilo tatizo kwangu ni historia! Ndani ya box kuna dawa ambayo mimi ilinisaidia sana. Nimekosa ujasiri wa kuku-face kwa hofu ya kwamba huenda ungenitafsiri vibaya. Nakuhakikishia dawa hiyo ni salama kabisa ingawaje ni wewe mwenyewe ndie mwenye maamuzi ya kuitumia au kutoitumia.

Nakutakia heri.
 
Hapo inabidi na ww uanze kutoa godoro kama vile unaanika atajua mna tatizo linalifanana baada ya muda kama wiki ivi unaacha kulitoa mwenyewe atakuja kuanza kukuuliza umetumia nn ukaacha tabia kama yake ya kutoa godoro
N:B-madawa ya kulevya humfanya mtu akojoe kitandani ninao ushaidi wa jamaa zangu na sbb ni kwamba akilala anaona uvivu hata wa kuamka na kwenda kukojoa usikute hana shida yeyote ni mavitu anayotumia
 
Hapa kwenye nyumba nilipopanga tupo wapangaji wawili kama kila mtu upande wake .
Miezi miwili iliyopita nilikua likizo kwa hiyo mara kwa mara nilikua nawahi kurudi nyumbani.
Daah mara nyingi nilikua nakutana na godoro limetolewa nje sehemu ile kuna string za kuanikia nguo,ikumbukwe hiyo sehemu ya kamba za kuanikia nguo tunashare,
Dada ni Sista duu na ni Kauzu so hatunaga story zaidi ya kukumbushana LUKU kama ni necessary kufanya hivyo
Siku moja nikiwa na my g.f,(kabla sijaamua kudate single mom) kumbe naye alikua akijaga na kuona but anapotezea,akaanzisha hiyo maada ya tatizo la jirani.
Binafsi hilo tatizo kuna ndugu yangu ashawahi kuwa kikojozi hadi akiwa form 3 ndipo likizo moja shule tukaendaga kumsalimia shangazi mmoja,akanielekeza miti shamba,ilikua just mizizi ya vimmea fulani,offcourse sijawahi iona hapa mjini ila incase mtu akiihitaji siwezi ikosa nikienda kule tuliitolea,akawa anatafuna na kuloweka kwenye kikombe cha maji anakunywa kadri awezavyo,Siyo chungu according to him,likizo haikuisha akawa kashapona kabisa hadi leo anakimbilia 30's
G.F aliogopa kumwabia yule jirani maana anamfahamu ni cha bangi japo mdada umri umeenda,si unajua hawa dada zetu "wasomi na uzungu na uamerika"
Binafsi siwezi mwambia,itakua unafiki na umbea wa hali ya juu
Wakuu nafanyaje kumsaidia huyu jirani,,ikumbukwe ni cha bangi,mie mwenyewe i had a proof of this.
N.B.Tuache theories,kukojoa kitandani ni tatizo la kiafya,lazima utibiwe,hospitali bado hawajagundua dawa,,ooh sijui kutokunywa maji mengi usiku,sijui kumzoesha kumuamsha usiku mhusika akojoe,,it doesn't work
 
jifanye nawe kikojoz anika godoro lako nawe kama wiki hiv mwenyew akiona ataanza kukusemesha kwa kujua naww ni kundi moja apo ndo utamwelekeza dawa
 
Andika bango dawa ya kikojozi inapatina hapa weka na namba yako ya simu
Lakini kuna mawili aje au achukie aone unamchimba.
 
Inaweza kuwa shida sio kukojoa mkojo bali katerero likikolea......... chunguza vizuri
 
Back
Top Bottom