Jinsi ya kupika tambi

Chukua tambi zako chemsha mpaaka ziwe zimelainika, zitoe na uziweke kwenye chombo kingine na kuziacha zichuje maji, then chukua sufuria nyingine weka jikoni then weka nazi au mafuta kiasi kidogo kama vijiko v3 then chukua hiliki zisage na kuchanganya kiasi kidogo cha sukari weka, then baada huo mchanganyiko kuchemka kidogo ingiza zile tambi zako na kuzichanganya taratibu ili zisivurugike kama dakika 3 zinatosha, ipua pakua kwenye sahani. Hapo tambi zako ziko tayari kuliwa.

Ahsante mkuu
 
Inategemea na aina ya tambi ndugu.

Kama ni zile ndefuu, just kwa wewe vikate urefu unaotaka then weka kwenye sufuria. Tia maji kiasi, ama kama una nazi, weka sukari kiasi, chumvi kidogo, mafuta kiasi. Ichemke iive. Ipua ule

Kwa wewe beginner achana na viungo sijui hiliki....

Kama ni zile tambi zinaitwa pasta ndogondogo hivi.... Weka mafuta jikoni, yakipata moto ziweke hizo tambi zichemke kidogo, zikiwa za brown zitoe kwenye mafuta. Weka kwenye sufuria ingine, then weka sukari kidogo, chumvi kidogo,.... Weka maji kidogo.. Then weka jikoni. Baada ya muda mchache zitakua zimeiva.
Kama unatumia jiko la mkaa unaweza kupalia baada ya maji kwisha nawewe kuzigeuza kidogo.
 
Mkuu nilifanikiwa Ahsante sana
 
chukua tambi zako zioshe vizur weka kwenyesufuri tia maji chemsha weka karanga za kusaga na mafuta zinafaa kuliwa kwa wali au ugali teh!
 
Tambi
Mahitaji:
1. Kitunguu kikubwa kimoja
2. Nyanya mbili kubwa
3. Karoti kubwa moja.
4. Pilipili Hoho Nusu
5. Tambi gram 250
6. Mafuta ya kupikia
7. Chumvi
8. Nyama ya kusaga 1/4 Kg
9. Tangawizi
10. Limao
11. Kitunguu swaumu

Matayarisho
1. Weka sufuria jikoni, weka mafuta na ukaange vitunguu maji vikifatiwa na vitunguu swaumu
2. Baada ya hapo, chukua nyama yako ya kusaga na uitie kwenye sufuria yenye vitunguu vyote.
3. Kisha tia tangawizi kwenye nyama huku unaendelea kuikaanga, baadae tia nyanya, hoho na karoti
4. Ipua na uweke pembeni
5. Chukua sufuria nyingine, weka maji na uibandike jikoni mpaka maji yachemke
6. Maji yakisha chemka, weka chumvi kiasi na uzitie tambi zako
7. Ukiona zimelainika kiasi, yachuje maji yoote na tambi zibaki kavu.
8. Chukua ule mchanganyiko wako wa viungo na tia tambi zako na uziache jikoni kwa dakika 5 hivi..
gharama hiyo Bibi yanga ina maana siwezi kula tambi mpaka vitu vyote hivyo viwepo
 
Mahitaji
Tambi
images.jpg

Maji\maziwa\tui la nazi
Chumvi\sukari
Mafuta ya kupikia
Viungo mfano hiliki
Soseji
IMG_20170601_143344.jpg

Chemsha maji\maziwa au tui la nazi kiasi jikoni weka hiliki,chumvi na sukari kidogo

Chukua soseji kata vipande vitatu,chomeka tambi kama inavyoonekana pichani,fanya hivyo kwa soseji zote.
18723366_824507997697533_3019737011272548352_n.jpg

Weka mchanganyiko wako wa tambi na soseji kwenye maji yaliyochemka jikoni

Tambi zikishalegea weka mafuta ya kupikia humo humo kisha pika au kaangiza kama kawaida mpaka msosi uive.

unaweza ongezea pia ujuzi kwa aina hii ya upishi
 
Mahitaji
TambiView attachment 519162
Maji\maziwa\tui la nazi
Chumvi\sukari
Mafuta ya kupikia
Viungo mfano hiliki
SosejiView attachment 519161

Chemsha maji\maziwa au tui la nazi kiasi jikoni weka hiliki,chumvi na sukari kidogo

Chukua soseji kata vipande vitatu,chomeka tambi kama inavyoonekana pichani,fanya hivyo kwa soseji zote.View attachment 519163

Weka mchanganyiko wako wa tambi na soseji kwenye maji yaliyochemka jikoni

Tambi zikishalegea weka mafuta ya kupikia humo humo kisha pika au kaangiza kama kawaida mpaka msosi uive.

unaweza ongezea pia ujuzi kwa aina hii ya upishi

Jana nilikula kitu aiseeh..sema mimi yangu ilikuwa na nyama ya kusaga alooo

Nilichanganya viongo kama vitunguu nilikata julian,carrot pia julian,nyanya niliblend,hoho nilikata julian pia,soy source,black pepper aiseeh niliufurahia msosi sana kwa jana loh!!!

Natamani nipike tena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom