Jinsi ya kuiibia Serikali bila kukamatwa!

Kuwa mjasiriamali kupitia mkakati wa mkurabita ndani ya Ikulu kwa kurasimisha biashara ndogondogo za kibenki na nyumba za kupanga.
 
Ukweli ni kwamba serikali yenyewe haioni shida kuibiwa,,, kwa kuwa kama ingekuwa inataka kuziba mianya... ni hivi hata ukiwa na document zote za safari na nk. kuna kipengele cha good governance, kinatamuka kwamba lazima kuonekane hali ya "value for money" kwenye miradi

sasa kingekuwa kinatumika vizuri hiki kipengele wangeweza sana kupunguza matumiza mabaya ya fedha!!!
 
hiyo aliyosema mzee ES ni kweli kabisa, mkurugenzi analilia safari ya afisa wa chini matokeo yake hawezi kuingia mkutanoni au akiingia hawezi kudeliver ideas since mtendaji hayupo, the end results ni mkutano wote hauna faida kwasababu hakukuwa na watendaji wanaohusika.

Ila tusisahau wahasibu wa serikali wanavyokula pesa kwa kuweka majina ya watu hewa halafu cheki ya malipo ikitoka wanaenda kuongea na watu wa benki wakatiane hiyo pesa ya waajiriwa hewa.
 
Kwa hiyo namna nyingine ya kujisaidia na fedha za umma ina husisha kamtandao ka aina fulani hivi na wenyewe wanajuana. ?
 
Kule TRA kodi hasa toka kwa wafanyabiashara wakubwa.
Konteiner limejaa perfume lakini dokument inayoungia strongroom inaonyesha mitumba.Inspecta anakula chake na mkadiria mahesabu anakula chake mzigo unatona.Transit Cargo.wafanyabiashara wengi wakubwa wanaingiza mizigo kwa system hii. Wanafanya collaboration hasa na Waganda. Kontainer halilipiwi kodi kwa kuwa ølinajulikana kuwa linakwenda Uganda.Kinachofanyika baada ya kupakiwa ndani ya lori documents zinawahishwa mpakani na kugongwa mihuri ya kuonyesha mzigo umetoka then kontainer linapakuliwa nchini.Fanya utafiti.huwezi kupata nafasi ya kuwa ofisa TRA mpakani bila ya kuwa ndani ya system.
 
Posho za vikao vya Board. Kuitisha vikao vya Voard vya dharura hata pale ajenda yake inapokuwa haina kichwa wala miguu. Bahasha za vikalio, per diem safari, mambo swafiiii
 
sasa haya ndiyo maisha ya kawaida? Ikitokea mtu akaanza kuzima mianya hiyo inawezekana kukomesha kutafuna nchi namna hiyo na wale waliozoea kuishi kwa mtindo huo kwali wataweza kuishi?
 
Mzee Mwanakijiji we ulie tu.

Nani mwenye ubavu hata wa kujaribu tu wa kuziba hiyo mianya?
 
Ukiona budget ya matumizi ya fedha zinazotolewa na wafadhili, hautaamini, nimehudhuria workshops nyingi, vikao vingi vya "kupanga mikakati ya kusaidia jamii maskini za Tanzania," kusaidia matumizi endelevu ya natural resourses, kinachoendelea huko naomba niseme, karibu asilimia 60 ya budget zote inakuwa kwa ajili ya vikao, tea, lunch, dinner accomodation, fuel bila kusahau sitting allowances za waliohudhuria.

in the end pesa yote inaishia katika kupanga mipango na walengwa waliokuwa wafaidike wanaambulia patupu. Kinachonishanagaza hawa wanajustify vipi hizo budget kwa hawa waliozitoa kwa serikali ya Tanzania?

Kosa ni pale wewe uliye na uchungu wa nchi hii unyanyuke na kuanza kuhoji kwa nini matumizi haya yasielekezwe zaidi kwa walengwa, Hapo ndio utajua kwamba kuna watu hawataki mchezo hasa kwenye pesa za shushi kama hizi.
 
U.S. Millennium Challenge Threshold Program Supports Training for Prevention of Corruption Bureau (USDAID)

Investigators from the Prevention of Corruption Bureau (PCB) will gain in-depth knowledge during a week-long course on procurement fraud and corruption. The U.S. Government-provided training, supported by USAID/Tanzania’s Millennium Challenge Threshold Program will help strengthen the capacity of the PCB to ensure transparent public procurement. PCB Director General Edward Hoseah will provide opening remarks on Monday, March 26, at 9 a.m. at the Sea Cliff Hotel.

“According to a World Bank Report, it is estimated that 20% of the Tanzanian government's expenditure on procurement is lost through corruption,” said Pamela White USAID/Tanzania Director. The training will also be attended by officers from the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA), and a special presentation will be made by the PPRA Chief Executive Officer, Dr. Ramadhani Mlinga. “With the support of Mr. Hoseah and Dr. Mlinga, we are helping to build the linkages between PPRA and PCB so that the two agencies can better fight corruption in public procurement,” said Ms.White.

The Government of Tanzania became eligible for U.S. Millennium Challenge Threshold Program assistance in November 2004. The primary objective of the Threshold Program as committed to by the Government of Tanzania is to reduce corruption in half the country's local districts and in central government agencies. The procurement fraud and corruption training program will help the government reach its objective by enhancing the PCB’s technical capabilities.

USAID has hired a three-person independent consulting firm team comprised of individuals from the U.S., U.K., and Tanzania to conduct and prepare materials designed specifically for this comprehensive course. The course will include materials for the training, a workbook and instructor's guide, PowerPoint presentations, exercises, role-plays and case studies. A second two-week training for another group of PCB officers is scheduled for later in the year.

My Take:

Kama ni kweli kusa asilimia 20 ya manunuzi ya serikali hupotea mikononi mwa "wajanja" kwa mbali inawezekana ikaonekana ni kidogo hasa ukizingatia kuwa asilimia 80 inatumika ipasavyo. Ina maana kwenye tenda ndogo ya kama milioni 20, milioni 4 zinaingia mifukoni mwa wajanja... !
 
Mzee Mwanakijiji,

Huu mpango wa kuibia serikali bila kukamatwa mbona ni biashara ndogo sana mjomba!.. hizi ni biashara ama wizi unaoogopa sheria ni rahisi sana kuzimwa. Kwa nini tusizungumzie UHUJUMU UCHUMI wa hawa viongozi wetu bila wananchi kushtuka!..The untouchables!
Mfano mdogo ni Ununuzi wa Rada...Mchezo huu umechezwa katika mashirika mengi ya serikali yaliyouziwa wawekeshaji toka nje, ikiwa ni pamoja na NBC.
Tukiondoa Commission kuna mchezo mwingine wa kununua hisa ndani ya shirika hilo
pale tunapotaka kuuza shirika la Umma ama kuanzisha mradi mpya wa serikali - Billions of Dollars involved!!
1. Kwanza anatafutwa Tapeli mwekekezaji kupitia kwa wajanja mafia ( kama tulivyoona ktk mchezo wa Rada).
2. Mikataba miwili hutengenezwa mmoja unaotengenezwa kwa maslahi ya mwekeshaji husajiliwa ndani ya nchi yetu kama tulivyoona ktk Mkataba wa Buswagi na pia pekee ndio unajulikana nchini.
3. Ule wa pili ambao unasajiliwa nje na kusainiwa hotelini (Lol) una makubaliano ya mgawanyo wa hisa kulingana na makubaliano kisha kampuni moja husajiliwa ndani ya nchi kama ni subsidiary ya kampuni mama na yenye kumilikiwa 100%... Kama unavyoona uhusiano wa hizo kampuni kina Pangea Goldfields Inc na Barricks!
Mzee katika makubaliano ya awali na kampuni mama ya nje humweka mtu wake ktk BoD kuhakikisha mafao yapo salama, wengine ndio huweka watoto zao n.k
Baada ya hapo tambarareeee... fweza zinaingia huku ukijifanya una uchungu sana na maslahi ya Taifa Ukisema we have no choice!.. tutafanya nini ndio matatizo ya Umaskini wetu inabidi tukubali kupokea angalau kidogo toka kwa hawa wawekeshaji!.
 

..... HATA mchongoma ANAJUA KWANINI AFRICA NI MASIKINI!!


SteveD.

"...Kiwi cha yule ni chema cha;hata ulimwengu uwishe kwani Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua!"

...naomba unitafsirie maneno yako ya chini, lugha yangu hii sitobisha, saa nyingine inanichenga vibaya sana, na mambo huwa noma kweli kweli kama mafumbo yananijia kutoka kwa wataalam wa lugha kama wewe. Naomba nitangulize shukrani.

SteveD.

Steve D.

Tafsiri sahihi ni; HATA mchongoma '(na upofu wake)' ANAJUA KWANINI AFRICA NI MASIKINI '(kwa makali ya maisha anayokumbana nayo!)'

Tuendelee na issues nyingine.
 
Hivi naomba kuulizwa swali ambayo sio popular kama ilivyokawaida yangu?

Kwa hali hii ya wizi uliowazi kwenye serikali kutoka kwa watumishi wake na wanasiasa, je ni kiongozi/mwanasiasa gani mzuri? Maskini au Tajiri? assuming mambo mengine yote yako constant?

My take:
Napenda sana siasa za Kenya maana wanasiasa wana hela,,, yaani kinachowafanya waingie kwenye siasa ni uchungu sio ujasiriamali kama huu wa kwetu!

Wabunge wetu wengi wanapenda vikao bungeni wanaouliza maswali ambayo hata ukiwa kijijini unakua unajibu nia na madhumuni vikao vichukue muda mwingi posho iingie!

Issue nyingine kwa wanasiasa vijana, wale wenye shughuli zao zingine nawapongeza wale wanaotegemea vikao vya kamati na mialiko ya vikao vya ubalozini nakadhalika ni wezi pia...
 
Je, wabunge wanapochaguliwa kila mmoja akikatiwa shilindi milioni 50 ya kuzuia kula rushwa itamtosha ili afanye kazi yake yaani ni bonus ya kuchaguliwa...
 
Je, wabunge wanapochaguliwa kila mmoja akikatiwa shilindi milioni 50 ya kuzuia kula rushwa itamtosha ili afanye kazi yake yaani ni bonus ya kuchaguliwa...

Mzee Mwanakijiji, wabunge tayari wanalipwa posho nzuri za vikao, tayari wanakopeshwa mashangingi kwa masharti nafuu kuliko mwananchi wa kawaida, tayari mbunge anauhakika wa kiinua mgongo kizuri baada ya kumaliza ubunge wake, tayari wabunge wana uhakika wa matibabu nje ya nchi kwa gharama za serikali kila mwaka, sidhani kama kwa vigezo vyote wapewavyo bado kuna litalokata 'njaa' ya asili ya binadamu kutotaka zaidi! Hawa hawafai!

Watu pekee nionavyo mimi wanaoweza kujaribu kukomesha Rushwa nchini ni kuunda kikosi huru toka ofisi ya Rais -'mwadilifu'- ambacho kitakuwa kinapambana na Rushwa. Naamini 'Anti Corruption Squad' hiyo ikipewa meno ya kikweli kweli' wataweza kwa kiwango kikubwa kupunguza makali ya wala rushwa nchini.

Muhimu tu watendaji wake wapewe mishahara minono, posho, motisha, vitendea kazi vya kisasa na ikiwezekana hata mafao ya uzeeni yanayolingana na kazi kubwa watayoifanya. Naamini kikosi kama hicho kwasababu tu kitakuwa na watendaji 'untouchables' wanao report moja kwa moja kwa Rais, wataweza kupenya ndani ya mashina na mizizi ya wala rushwa wa ngazi zote katika jamii, either directly au indirectly ( hata through informers) kupata incriminatory evidence, na kuhakikisha mianya ya rushwa inazibwa, na wataobainika wametoa na kupokea rushwa wanahukumiwa kwa mujibu wa sheria.

Taasisi kama TAKURU (sijui ipo chini ya wizara gani) nadhani bado inachukuliwa kama taasisi tu nyingine ya umma isiyokuwa na meno 'kamili', yaani ni kama taasisi tu ilowekwa kuonyesha 'nasi' tupo tunapigana na rushwa!

Kwa nchi kama Tanzania, anti corruption officer atapendeza zaidi akiwa ni mtu 'undercover' kuliko mtaa mzima kumjua 'yule jirani' ni askari wa kikosi maalum.

Ni maoni yangu tu.
 
Labda tuwalipe milioni 50 kama signing bonus hao maafisa wa hiyo squad ili wasiwe na tamaa ya rushwa...
 
Nyingine ni kuunda kampuni yako kama wewe ni mtumishi wa sirikali. Unampa umeneja rafiki ama ndugu yako ambaye unajua atalinda maslahi yako. Lengo la kampuni ni kupata tenda zote ambazo zinatoka katika sirikali, kwa sababu wafunguaji wa tenda ni nyie wenyewe. Katika tenda hizi mnapiga cha juu kuliko gharama halisi huku mkifanya kazi chini ya kiwango. Mkaguzi wa kazi akileta zake zipi mnampa bahasha anakauka.
 
mtupori, halafu mkifanya kazi chini ya kiwango vikiharibika si lazima waje kwenu tena?
 
..tafuta zile ajira za kufika ofisini asubuhi,unasoma magazeti,saa nne chai pale ferry,mchana wali nyama hapo hapo ferry,jioni huyooo posta ya zamani unapanda basi lako kurudi nyumbani!

..ukikaribia mwisho wa mwezi,we unakuwa wa kwanza kuulizia kama voucher zimeandikwa!na lini wataenda benki!na lini wataziweka kwenye account!

..baada ya hapo ni kuhakikisha semina za bagamoyo,morogoro,arusha na zanzibar hazikupitii mbali,unakula night yako kiulaini!

..baada ya hapo ni kusubiri promotion!

...kiulaini unaiibia serikali!
 
Nimekaa najiuliza ni jinsi gani watumishi wa serikali kuanzia wa ngazi za chini hadi za juu kabisa wanaweza kuibia serikali na serikali isitambue au ishindwe kuchukua hatua? Inawezekana vipi watu wakawa wanachota fedha za umma kama kuchota maji kwa kata na wakazimeza hata bila ya kuzitafuna? Bila ya shaka kuna mbinu mbalimbali ambazo zinatumika na wajanja hao kula fedha za umma "bila kunawa". Hivi ni mbinu gani zinatumika kuuibia serikali bila ya hata kukamatwa?

NB: Mada hii haina lengo la kufundisha wizi au mbinu za kuuibia serikali bali inataka kuonesha ni mbinu gani zinatumika kuubia serikali. Kama unataka kujua jinsi ya kula fedha za umma, tafadhali jiunge na utumishi wa serikali kwani wapo watu ambao watakuwa tayari kukupa somo "live" as you go along.

...Mnh, Mzee Mwanakijiji wengine hawa!... yaani habari ile kwamba huyu Mkubwa 'alijikatia chajuu' katika ununuzi wa jumba la kibalozi kule Italy, halafu na makelele yote yale oooh, kesi itasikilizwa October matokeo yake ndio haya... pesa za kodi za WANANCHI zilizotumika kuendesha kesi hii mpaka hapa ndio zinaishia wapi kama sio mfukoni kwa wajanja wachache? ndio kusema 'huyo 'sirikali'' alomshitaki kafuta kesi?... au ndio kuna walofaidika na 'bingo ya hapo kwa papo!'?

Maajabu kesi ya Balozi Mahalu
By Marshy Abdu | Published 10/6/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Maajabu kesi ya Balozi Mahalu
na Happiness Katabazi

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya kuhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Ricky Mahalu na mwenzake, umekiri kwamba hakuna mlalamikaji katika kesi hiyo.
 
Back
Top Bottom