Jinsi ya kufanya biashara ya kununua na kuuza majengo yanayolipa bila kumiliki

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Masomo yanayofundishwa:

✓ Utangulizi wa makala (maana ya wholesaling real estate).

✓ Tofauti kati ya udalali wa majengo na kuuza majengo ambayo huyamiliki.

✓ Jinsi ya kuuza kwa uhalali.

✓ Kuwa mkaguzi wa nyumba inayouzwa.

Utangulizi
Kununua na kuuza nyumba ndani ya muda mfupi bila kuifanyia ukarabati inaitwa wholesaling real estate. Mambo matano (05) ya msingi kwenye kununua na kuuza majengo bila kumiliki ni kama ifuatavyo;-

✓ Kutafuta jengo ambalo lina thamani kubwa na hutapata shida kumuuzia mwekezaji kwenye majengo.

✓ Saini makubaliano ya mauziano kati yako na muuzaji wa jengo husika.

✓ Kutafuta mnunuzi wa jengo ulilosaini mkataba wa mauziano.

✓ Kukamilisha mkataba kati ya muuzaji na mnunuzi (Complete a double closing).

Hizo ni hatua muhimu za kununua na kuuza majengo bila kuwa na umiliki wa majengo hayo. Anayetengeza faida ni lazima aweke tofauti ya bei kati ya mnunuzi na muuzaji. Hii itakusaidia kuongeza uwekezaji wako kwenye ardhi na majengo.

Njia nyingine ya kujiingizia ni kujipangia kiasi cha kamisheni ambacho mwenye nyumba anaweza kukulipa au mnunuzi anaweza kukulipa. Kiasi kizuri ni 10% ya bei ya kuuzia hadi 5% ya bei ya kuuzia kutegemeana na aina jengo na hamasa ya muuzaji au mnunuzi wa nyumba.

Kuwa wazi na uwe mwaminifu kwa pande zote mbili. Unayepata faida ni mtu wa kati ya mnunuzi wa nyumba na muuzaji. Ingawa muuzaji wa nyumba naye anaweza kutengeneza faida kutegemeana na jinsi alivyokuwa amenunua.

Njia hii inafaa sana kwa wawekezaji ambao hawana mtaji wa kutosha kununua nyumba wanayotaka.

Kwa kuwa ni kanuni ya ukarabati wa nyumba kutokarabati nyumba ambayo hauna umiliki halali wa nyumba husika.

Ni kosa kubwa kuifanyia ukarabati nyumba ambayo hauna umiliki wake. Pengine kuwe na makubaliano maalum ya kati yako na muuzaji wa nyumba.

Kwa maneno mengine, hutakiwi kukarabati nyumba endapo unatumia njia hii kuwekeza kwenye ardhi na majengo.

Kununua na kuuza nyumba bila kumiliki nyumba inaweza kukufanya utengeneze kiasi kikubwa cha mtaji fedha ndani ya muda mfupi.

Ingawa sio kazi rahisi. Ni kazi ngumu. Ni kazi inayohitaji uwe na uzoefu na maarifa sahihi, unahitaji mbinu bora za mazungumzo na unahitaji kuwa mtandao bora wa uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Hapo juu nimekushirikisha hatua nne (04) ambazo ni muhimu sana kwenye kununua na kuuza nyumba bila kuwa na umiliki wa nyumba.

Hatua ya kwanza ni muhimu sana ili uweze kutengeneza kiasi kikubwa cha mtaji fedha kwenye kununua na kuuza nyumba bila kuimiliki.

Tafuta nyumba nzuri ambazo utaweza kuuza bila kutumia nguvu nyingi na muda mwingi.

Fokasi kwenye kununua na kuuza nyumba, tengeneza mfumo na kuwa na muendelezo wa kutafuta nyumba za kipato kikubwa.

Mfano kama umenunua nyumba kwa milioni kumi (Tshs.10,000,000/=). Unasaink mkataba wa kununua nyumba. Kisha unatafuta mteja wako wa kununua nyumba ambayo hauna umiliki wake.

Unasaini mkataba na mnunuzi wa nyumba hiyo kwa Tshs.12,000,000/=. Mwisho wa mauzo unapata faida ghafi (gross profit) ya Tshs.2,000,000/=.

Faida hiyo unaweza kuipata ndani ya wiki tu au mwezi mmoja tu. Kazi ya kufanya hivi inakutaka uwe vizuri sana kwenye mtandao wako.

Kama hauna mtandao mzuri utatumia nguvu nyingi, na muda mwingi kuwafikia wanunuzi sahihi.

Tofauti Nne (04) Kati Ya Udalali Dhidi Ya Kuuza Nyumba Bila Kumiliki (Real estate agency versus Wholesaling real estate).

Moja; kwenye udalali wa nyumba unauza nyumba na sio mkataba wa mauziano ya nyumba.

Wakati kwenye kuuza nyumba bila kuimiliki, unakuwa unauza mkataba wa mauziano kati ya mnunuzi wa nyumba na mmiliki wa nyumba.

Pili; kwenye udalali wa nyumba unaruhusiwa kutangaza kuuzwa kwa nyumba.

Wakati kwenye kuuza nyumba bila kuimiliki, unatakiwa kumshawishi mnunuzi wa nyumba kupitia mkataba ambao unao kati yako na mmiliki wa nyumba.

Tatu; kwenye udalali wa nyumba unakuwa mwakilishi wa mmiliki wa nyumba na mnunuzi wa nyumba.

Wakati kwenye kuuza nyumba bila kuimiliki, unatakiwa kusimama pekee yako. Husimami badala ya mwenye nyumba na muuzaji wa nyumba.

Nne; Kwenye udalali wa majengo, unalipwa kwa kamisheni au kwa mshahara au gawio kufautana na utaratibu unaotumika kwenye shughuli zako za udalali wa nyumba.

Kwenye kuuza nyumba bila kuimiliki, unatengeneza faida itokanayo na tofauti ya bei ya mmiliki wa nyumba na bei anayonunulia mwenye nyumba.

Kujenga Uaminifu Kwa Wateja Wako.

Unatakiwa kuwa mwaminifu katika hatua zote za kukamilisha malipo na kusainisha mikataba.

Mmiliki wa nyumba anatakiwa alipwe kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kusaini mkataba wa mauziano kati yako na yeye ili uweze kuuza mkataba huo kwa mwekezaji mnunuzi wa majengo.

Unaweza kusajili kampuni au kuingia ubia kampuni ya kusaidia kupata hati miliki ya nyumba. Hii itakusaidia kufanya mauzo pasipokuwa na shaka yoyote.

Vitu Viwili (02) Ili Upate Mafanikio Makubwa

Moja; uwe na orodha ya wateja wengi. Unatakiwa kuwa na kundi kubwa la wanunuzi wa nyumba ambayo watakuwa tayari kununua nyumba kwa bei ya juu kidogo kutoka kwa mwenye nyumba.

Ukiwa na orodha kubwa itakusaidia kupata wanunuzi kwa haraka zaidi na utapata wanunuzi washindani. Ni muhimu sana kuweka nguvu nyingi na mtaji fedha kwa ajili ya kuwafikia wanunuzi wengi wa nyumba.

Pili; Uza kwa wanunuzi waliohamasika (motivated buyers). Hawa ni wanunuzi ambao wapo tayari kufanya kulipa kiasi ambacho unawambia.

Ni vibaya kumuuzia mwekezaji ambaye anaona kama umemwibia. Tumia vigezo vya kiuwekezaji kumshawishi mnunuzi mwekezaji kununua nyumba.

Muonyeshe faida zote na baadhi ya changamoto atakazokutana nazo kwenye nyumba unayonunua.

Kuwa Mkaguzi Wa Nyumba Unayouza.

Andika ripoti nzuri ya nyumba unayouza. Ripoti hii mkabidhi mwekezaji mnunuzi wa nyumba. Kwa ripoti yako itakuwa rahisi sana kushawishika, badala ya kuuza kienyeji.

Pia, mpe nafasi ya mwekezaji mnunuzi kuandaa ripoti ya ukaguzi wa nyumba kwa kutumia timu yake anayoiamini ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Ni muhimu sana kuwa na wakili ambaye atakusaidia kwenye hatua fulani fulani za uuzaji wa mikataba ya nyumba ambayo huna umiliki wake.

Ni muhimu ukawa na mfano wa mkataba ambao umeandaliwa na wakili mbobezi kwenye ardhi na majengo ambao utautumia kama mkataba rejea.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Masomo yanayofundishwa:

✓ Utangulizi wa makala (maana ya wholesaling real estate)...
Hi biashara bado sana hapa Tanzania. Madalali wengi hawajaenda shule, wanaishi kwa ujanjaujanja, na pili hamna mwenye jengo atakae muamini mbongo afanye mkataba wa mauzo kabla ya kuona cash money......kwanza 90% ya madalali watanzania ni waingo matapeli, ata ukiwa na nia nzuri ya kufanya nae biashara atakuibia tu.
 
Hatua ya kwanza ni muhimu sana ili uweze kutengeneza kiasi kikubwa cha mtaji fedha kwenye kununua na kuuza nyumba bila kuimiliki.,

Real estate inalipa
 
Kuna mzee alikuwa anauza nyumba yake kwa bei ya milioni 55 hapo na dalali atapata mgao wake. Dalali akasema yeye atajitambulisha kama m'miliki wa nyumba so mzee asijiingize katika makubaliano mengine yoyote na mtu mwingine isipokuwa na dalali.

Sasa mwisho wa siku dalali akawa anapambana huko mzee akatokea mtu na milioni 75,mzee hakupoteza muda fasta akauza akalala mbele.

Dalali kaja na mteja wa 65 akajua anakuja kutoboa. Anakuta eneo limezungushiwa mabati kuna ujenzi unaendelea, kumtafuta mzee hapokei. Akapata namba ya mtoto wa mzee kumuuliza nini kinaendelea dogo anamjibu kwa dharau kabisa kwamba pameuzwa.

Shida ya kufanya biashara na watanzania. Kuheshimu mikataba ni ngumu sana na tamaa wameweka mbele.
 
Hi biashara bado sana hapa Tanzania. Madalali wengi hawajaenda shule, wanaishi kwa ujanjaujanja, na pili hamna mwenye jengo atakae muamini mbongo afanye mkataba wa mauzo kabla ya kuona cash money......kwanza 90% ya madalali watanzania ni waingo matapeli, ata ukiwa na nia nzuri ya kufanya nae biashara atakuibia tu.
Hapa ni pagumu sana ni lazima dalali afunge mkataba wa kuuza jengo kwa kiasi fulani cha fedha na kwa specific time!, yaani unipe million 10 kwamba mimi nisijishughulishe na wateja lakini ni lazima nikupe siku 90,endapo kama utakuwa hujafanikiwa kuuza mkataba udisolve automatically.
 
Back
Top Bottom