Dondoo Muhimu Kuhusu Nyumba Za Kupangisha Kwa Wawekezaji Wanaoanza Aprili 2023

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
" Owning residential real estate is not a great investment. Over the past 20 years, home prices have risen less than the consumer price index and have returned less than treasury bills." Hayo yalikuwa maneno ya Charles Ellis kwenye kitabu chake kiitwacho Winning The Loser's Game.

Huyu ni mmoja ya waandishi wachache ambao wameandika kwamba majengo ya makazi (residential properties) hupanda thamani kwa kiwango kidogo sana ukilinganisha na ongezeko la gharama za maisha kwa kila mwaka.

Hilo linaweza kuwa kweli kwa kipindi kifupi kwa sababu ya uwepo wa mzunguko wa masoko ya ardhi na majengo. Kuna miaka majengo haya huongeza thamani kwa kasi na kuna miaka majengo hayo huongeza thamani kwa 1% au hata 2% kwa mwaka mzima.

Lakini sababu hii ni sababu ya kiuchumi kama ambavyo ndugu yetu Ellis na wenzake wametuonyesha kupitia maandishi tofauti tofauti. Ongezeko dogo sana (1% au 2%) la majengo haliwezi kumuingiza hasara mwekezaji kwa sababu 4 zifuatazo;-

Moja.

Majengo huongezeka thamani kwa njia mbadala ambayo hutegemea maarifa ya timu ya mwekezaji. Njia hiyo huitwa forced property appreciation. Hii ni pale ambapo nyumba huongezewa thamani kwa kuifanyia ukarabati wa kiurembo.

Mbili.

Kuna nyingine nyingi za kutengeneza fedha kutoka kwenye nyumba za makazi ikiwemo kodi ya mpangaji, kutumia kuingia ubia kwenye biashara nyingine, kuitumia kununua ya pili na kadhalika.

Tatu.

Soko mahalia la majengo (local real estate market) hutofautiana kati ya mtaa na mtaa. Mwekezaji makini hawezi kukubali kumiliki nyumba mtaa ambao kuna kiasi kidogo sana cha ongezeko la thamani. Mwekezaji atatumia kanuni ya 100:10:3:1 ili kumiliki nyumba inayoongezeka thamani kwa kila mwaka.

Nne.

Kutegemea ongezeko la bei (thamani) sio lengo kuu la mwekezaji. Mbali na kwamba mwekezaji anahakikisha anamiliki nyumba inayopanda thamani, hawezi kupigia bajeti ongezeko la mtaji (capital gains) litkanalo na ongezeko la bei ya majengo yake ya makazi.

Tano.

Mwekezaji hutenegeneza faida wakati wa kununua nyumba. Mbinu mojawapo ya kutengeneza fedha kwa mwekezaji ni kununua kwa punguzo la 10% hadi 30% au zaidi kwa kila nyumba anayonunua.

Punguzo hili ni asilimia za thamani ya nyumba kwa wakati wa kufanya mauziano. Kiasi hiki cha punguzo la bei hutegemea mambo makuu mawili. Nayo ni;-

Moja; Mtandao wa mnunuzi na mbinu anazotumia kutafuta na kukagua nyumba anayotaka kununua.

Mbili; Kiwango cha hamasa kutoka kwa muuzaji.

Jinsi hamasa inavyokuwa kubwa kutoka kwa muuzaji ndivyo ambavyo mnunuzi hupata mazingira mazuri ya kupewa punguzo la bei ya nyumba.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711

MUHIMU; Jiunge na kundi la whatsapp liitwalo TZ REAL ESTATE TEAM. Ukiwa hapa utapata masomo na mijadala kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo (real estate investment).

Bofya hapa kujiunga
 
Back
Top Bottom