Jinsi ya ku-design Blog inayolipa (Part 1)

Binafsi sijui, utatengenezaje pesa kupitia blog? Km mtu ametembelea blog yako mfano ya kitaaluma, wewe utanufaikaje?
 
Kuhusu adsense… hawa ni google ambao wana act kama madalali wa matangazo mfano hapa tz kuna pinpoint…

Hivyo ili uweze kupata hiyo acc ya adsense waweze kufanya kazi na wewe kuna masharti kwanza web/blog yako angalau iwe na miezi 3… iwe na post angalau 50… . iwe na template yenye muonekano mzuri na rafiki kwa matangazo… hivyo kwa mtu ambae hajawahi kupata acc inakuwa ngumu kukubaliwa na google.

Wazee wa fursa wanaamua kukusaidia kwa kukulipisha kidogo kwa ajili ya hiyo service… kwanza anakuwa na ready blog na template ambazo akitumia tu kesho unapata acc. Wengi wanaanzia elfu 30, 40, 50 nakuendelea.

Kama unataka adsense acc, plus domain site, plus good template design na support and service ili uweze kupost kiswahili na stil utengeneze pesa hadi dola 100 kwa siku call this number 0713774746.
 
mwalimu fadhil Paulo nini muhimu zaidi
kati Domain au Host/Server kuanza nayo kulingana na mfuko/pesa
unavyoruhusu. Je nikiamua kuwa na Domain tu kuna athari sana?
samahani kama nimeuliza maswali yasiyo na msingi ndio najifunza.

Mkuu poposindege

Kama unataka kwa ajili ya kuanza kujifunza na kupata uzoefu tu, basi anza na domain (jina) halafu server unaweza kutumia ya bure

ila kama ndiyo unataka kuwa na blog inayolipa au unatarajia ianze kukulipa hivi karibuni basi anza na vyote. Siyo bei kwa sababu domain ukinunua kwa 25000 ni mara moja tu kwa mwaka, sasa ukipata server ya kulipia 5000 kwa mwezi na unapata support kuna ubaya gani?. Hizi za bure wakati mwingine hawatoi support, kuna tatizo linakusibu unataka ushauri au mwongozo unaweza usipewe. Hata ukipata server ya kulipia 10000 kwa mwezi sioni gharama hapo.

Karibu
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo adsense ni mpaka post za kingezera tu

Post au website/blog kwa ujumla lazima iwe ya kiingereza au lugha zingine kubwa duniani ambazo google wameshazipitisha kwa ajili ya huduma ya adsense, utaona hata wakati unaomba kujisajiri unapochagua lugha ya blog yako Kiswahili hakipo! Kiswahili bado hakipo supported kwa adsense

Halafu siyo adsense tu, nimegunduwa kiswahili kimeachwa sana kwenye upande huu wa I.T, nadhani kuna haja ya developers wa Tanzania wakae wajitafakari katika hili

Kuna namna ya kumwingiza mjini google akubali adsense kwa website au blog yenye content za kiswahili ikubaliwe kwenye adsense, tricky hii itakulazimu kuwa na blog au website ambayo ndani yake content ni za kiswahili au mchanganyiko wa kiswahili na kiingereza lakini Menu zake kuu zimeandikwa kwa kiingereza na wanahitaji pia pages kama TERMS & CONDITIONS, ABOUT US, SITE MAP, CONTACT US nk

Nini cha kufanya, ama tuendelee kusubiri google waanze kusupport lugha ya kiswahili kwenye adsense na hatujuwi itakuwa lini au tunajibidiisha kupata hela kwenye blog bila kutegemea adsense. Na blogger atakayefauru ni yule atakayeweza kuwaza namna ya kupata hela bila kutegemea adsense
 
Binafsi sijui, utatengenezaje pesa kupitia blog? Km mtu ametembelea blog yako mfano ya kitaaluma, wewe utanufaikaje?

Ni rahisi sana.

Hakuna hela inayopatikana tu hivi hivi. Nguvu ya hela ipo kwenye mabadilishano ... 'A value of money is in exchange'.

Siku hizi ukienda kwenye shule nyingi iwe ni msingi au sekondari utaona walimu wanafundisha lakini pia wana biashara fulani pembeni, labda huyu anauza kokoto, huyu maandazi nk. Hakuna ubaya katika hilo mhimu atimize majukumu yake.

Ili upate hela lazima uuze kitu. Hata hizo adsense ni matangazo ya biashara kuhusiana na bidhaa au huduma fulani.

Unaweza kuuza nini kwenye mtandao? jibu ni chochote. Kuanzia viatu, nguo, vyombo vya majumbani, unaweza kuuuza baiskeli, pikipiki, magari, nyumba, huduma kuhusiana na taaluma yako na kadharika na kadharika bila idadi, unaweza kuuza chochote. Na unachouza siyo lazima kiwe chako, mfano kama unapenda kuuza nguo unaweza kumuona mwenye duka la nguo na mkaingia makubaliano, unapiga picha nguo weka kwenye blog yako, mtu akiagiza unapita dukani kwa huyu rafiki yako unachukuwa nguo unapeleka kwa mteja wako.

Mwalimu wa msingi anauza kokoto na wanafunzi wananunua kwa sababu wanamfahamu, ni mwalimu wao, wanampenda na wana imani naye.

Hizi kokoto sijuwi lugha rahisi ni ipi, ni aina fulani ya maandazi magumu sana.

Sasa kwenye blog na darasani kwa mwalimu tofauti yake ipoje? Ni kuwa kwenye blog utakuwa kuna somo unafundisha lakini unafundisha bure, watembeleaji wako wanapita huko wanasoma masomo unayowafundisha bure, labda iwe ni online classroom au course au tution nk

Kwahiyo utakuwa unawafundisha bure. Wakati unawafundisha bure hilo somo ulilolichagua wewe, pembeni usisahau kuweka kokoto zako na wewe kama ni huduma yako au bidhaa yako fulani.

Sasa kuna ushindani, kwanza uandike kweli kweli tena hizo notisi zako ziwe haziwezi kupatikana sehemu nyingine kirahisi rahisi na mhimu kuliko yote ziwe zinamsaidia msomaji kutatua matatizo yake au kumwendeleza zaidi.

Tutajadili zaidi huko mbeleni .....
 
Somo liendelee ticha

Somo lazima liendelee hakuna namna nyingine.

Halafu sasa nimeona tuwe tunafanya hata mazoezi kwa vitendo kabisa kwa baadhi ya mambo hasa namna ya kuandika vizuri kwenye ukurasa wa blog, kama ujuavyo uandishi wa kwenye blog ni tofauti kabisa na ule wa kwenye gazeti au kitabu, huku kwenye blog kabla huja-publish post yako kuna vitu vingi sana vya kuvizingatia.

Kwa sababu hiyo nimenunua jina la tovuti (domain) siku kama tatu zilizopita. Hapo naomba bloggers wote tukutane hapo tupeane uzoefu na kuelimishana. Nimeiweka kwenye server yangu. Jina au domain hii nimenunua dola 1, kama Tsh 2200 hivi. Ingawa bado naimalizia kuiunganisha, bado unaweza kuiona ikiwa kwenye 'underconstruction mode' kupitia link hii hapa chini;

http://www.bongobloggers.xyz
 
Ni rahisi sana.

Hakuna hela inayopatikana tu hivi hivi. Nguvu ya hela ipo kwenye mabadilishano ... 'A value of money is in exchange'.

Siku hizi ukienda kwenye shule nyingi iwe ni msingi au sekondari utaona walimu wanafundisha lakini pia wana biashara fulani pembeni, labda huyu anauza kokoto, huyu maandazi nk. Hakuna ubaya katika hilo mhimu atimize majukumu yake.

Ili upate hela lazima uuze kitu. Hata hizo adsense ni matangazo ya biashara kuhusiana na bidhaa au huduma fulani.

Unaweza kuuza nini kwenye mtandao? jibu ni chochote. Kuanzia viatu, nguo, vyombo vya majumbani, unaweza kuuuza baiskeli, pikipiki, magari, nyumba, huduma kuhusiana na taaluma yako na kadharika na kadharika bila idadi, unaweza kuuza chochote. Na unachouza siyo lazima kiwe chako, mfano kama unapenda kuuza nguo unaweza kumuona mwenye duka la nguo na mkaingia makubaliano, unapiga picha nguo weka kwenye blog yako, mtu akiagiza unapita dukani kwa huyu rafiki yako unachukuwa nguo unapeleka kwa mteja wako.

Mwalimu wa msingi anauza kokoto na wanafunzi wananunua kwa sababu wanamfahamu, ni mwalimu wao, wanampenda na wana imani naye.

Hizi kokoto sijuwi lugha rahisi ni ipi, ni aina fulani ya maandazi magumu sana.

Sasa kwenye blog na darasani kwa mwalimu tofauti yake ipoje? Ni kuwa kwenye blog utakuwa kuna somo unafundisha lakini unafundisha bure, watembeleaji wako wanapita huko wanasoma masomo unayowafundisha bure, labda iwe ni online classroom au course au tution nk

Kwahiyo utakuwa unawafundisha bure. Wakati unawafundisha bure hilo somo ulilolichagua wewe, pembeni usisahau kuweka kokoto zako na wewe kama ni huduma yako au bidhaa yako fulani.

Sasa kuna ushindani, kwanza uandike kweli kweli tena hizo notisi zako ziwe haziwezi kupatikana sehemu nyingine kirahisi rahisi na mhimu kuliko yote ziwe zinamsaidia msomaji kutatua matatizo yake au kumwendeleza zaidi.

Tutajadili zaidi huko mbeleni .....

Asante sana ticha!! Naomba niulize tena,
Unaweza nunua domain au server online!? Au lazma ununue CD uinstall?
Na je ni hatua zipi za muhimu ambazo unazifuata ukiwa unatengeneza blog au website!? Asante sana
 
JINSI YA KUDESIGN BLOG INAYOLIPA sehemu ya 4

4. CONSISTENCE/KUDUMU KWENYE MADA

Hebu fikiria labda ulikuwa ukitafuta somo linalofundisha ‘Namna ya kufuga Mbwa' na unakutana anuani ya blog inayoelezea somo hilo kupitia injini za kutafuatia vitu kwenye mtandao (search engines).

Siku ya pili unarudi kwenye ile blog unakuta kuna masomo ya namna ya kutengeneza keki!. Keshokutwa yake unajaribu kurudi tena uone ni kweli ulichoona jana, mara unakuta post yao ya mwisho inazungumzia namna ya kulima vitunguu swaumu!!!

Hakika, siku ya nne hutarudi tena hapo kutafuta habari juu ya ‘Namna ya kufuga Mbwa'.

Ni vigumu kuwa na blog inayolipa kwa staili ya uendeshaji wa blog wa namna hii.

Fanya blog yako ijulikane ipo hasa kwa ajiri ya nini, wafanye wasomaji wako wawe wazi kujuwa wakija kwako watapata nini.

Blog lazima iwe na mada au topic maalumu moja inayojitambulisha nayo. Blog zipo hasa kwa ajili ya kufundishana jambo au somo fulani moja. Kama ni blog kuhusu michezo, andika habari za michezo, kama inahusu mapenzi, andika mapenzi, kama inahusu biolojia, andika biolojia, kama inahusu teknolojia andika teknolojia, na kadharika na kadharika. Huhitaji kuzungumzia kila jambo kwenye blog yako ili kupata wasomaji wengi na hatimaye ikulipe.

Hizi mada au topic, kwenye ulimwengu huu wa ku-blog huitwa ‘NICHE'.

Kuna NICHE kubwa na niche ndogo ndogo, na kutoka kwenye hiyo niche kubwa bado unaweza kuivunjavunja na kupata kipande kidogo cha sehemu ya hiyo niche kubwa na ikawa ndiyo mada au topic kuu ya blog yako.

Mfano, NICHE KUBWA ni ‘AFYA'. Kutoka niche au mada kubwa au kuu AFYA unaweza kuivunjavunja na ukapata niche ndogo ndogo kama ‘UZITO NA UNENE KUPITA KIASI'. Blog yako kuanzia post ya kwanza hadi ya mwisho zinazungumzia mada moja tu ambayo ni UZITO NA UNENE KUPITA KIASI. Yaani nikihitaji kila kitu kuhusu uzito na unene kupita kiasi basi nikienda blog fulani au blog ya fulani kila kitu kuhusu UZITO NA UNENE KUPITA KIASI nitakipata hapo.

Sasa unakuta blog mara ina post za stori za mapenzi, mara michezo, mara afya, mara teknolojia. Yaani ni vurugu. Blog siyo forum au siyo tovuti ya gazeti. Wewe kama blogger chagua mada moja utakayodumu nayo na watu wakutambuwe kwa hilo.

Kama unapenda magari, blog kuhusu magari. Kama unapenda kilimo, blog kuhusu kilimo, kama unapenda siasa, blog kuhusu siasa, unapenda habari, blog kuhusu habari, unapenda muziki, blog kuhusu muziki …. Na kadharika na kadharika.

Na hii kudumu kwenye mada (being consistent) inahusu vitu viwili kwenye blog, ambavyo ni;

1. Kudumu kwenye mada au topic ya blog, (niche). Yaani kama inahusu kilimo basi udumu na masuala ya kilimo na

2. Kudumu kutoa makala mpya kwa muda na mpangilio maalumu (persistence). Wasomaji wako watarudi tena na tena kwenye blog yako kama kuna makala mpya kila mara. Hapa JF unaona kuna wasomaji wengi ni kwa sababu kuna mada mpya kila siku na tena ni nyingi maana kila mtu popote alipo anaweza kuanzisha mada tena wakati wowote na mbaya zaidi hao waanzisha mada ni wengi na mada zimepangwa kimajukwaa sababu hii ni forum na siyo blog.

Sasa, sijakushauri ukaanzishe jamiiforum nyingine, wewe kaanzishe blog, dumu kwenye mada ya blog na uandike makala mpya kila mara bila kupumzika. Siyo kila siku! Unielewe hapo. Kama ni blog inayohusu habari, ndiyo unaweza kuandika makala mpya kila siku sababu habari zinatokea kila siku.

Ili kutowachosha wasomaji wako unaweza kufanya makala mpya moja kila baada ya siku 1 au makala mpya 2 kwa wiki. Hii itakusaidia pia kupata traffic toka search engines kama google sababu google anapenda blogs ambazo zinakuwa na makala mpya kila mara (updated) na kwa mpangilio maalumu.

Hii siri nawapa pia website au tovuti za makampuni ambazo website zao ni static na hawana sehemu ya blog kwenye tovuti zao. Kila website sasa inahitaji kuwa na sehemu ya blog ambako wataandika matukio au elimu yoyote kuhusu huduma zao kila mara ili waweze kupata watembeleaji (traffic) kirahisi kutoka kwenye injini za kutafutia vitu kwenye mtandao (search engines). Itawapunguzia hata gharama zao wanazotumia upande wa masoko (marketing).

Mengine ya haya ninayoyasema hapa yananichoma hata mimi sababu hata mimi nimewahi kukosea staili hii mwanzoni wakati naanza ku-blog kwenye mtandao. Lakini kama elimu na kama kukusaidia wewe usije kupoteza muda na pesa basi uyaepuke ikiwa unataka kutumia mtandao kwa manufaa ya jamii na yako. Kwa maana ya kusanifu (design) na kuwa na blog inayolipa.

Kuna wakati inaweza ikakutokea unao uwezo wa ku-blog au kufundisha mada (niche) zaidi ya moja labda hata 3, yaani mtu ana vipawa vingi Mungu kamjaalia, utafanya nini?. Hapa jaribu, nimesema ‘jaribu' ku-blog kuhusu vyote halafu uone wapi wasomaji wako wanakupenda zaidi na uwekeze muda zaidi upande huo.

Kwahiyo sehemu hii ya nne ya namna ya kudesign blog inayolipa inazungumzia umhimu wa kudumu kwenye mada, ‘CONSISTENCE'. Kudumu kwenye mada inayoitambulisha blog yako (niche) na kudumu kwenye mada kwa maana ya kuleta makala au post mpya kila mara kwa mpangilio maalumu (persistence).

Tutaendelea na sehemu ya 5 ….
 
Asante sana ticha!! Naomba niulize tena,
Unaweza nunua domain au server online!? Au lazma ununue CD uinstall?

Mkuu aupa

Yes, unaweza kununua server online. Unahitaji kuwa na credit au debit card na account ya paypal kwa usalama wa fedha zako ufanyapo manunuzi online

Na je ni hatua zipi za muhimu ambazo unazifuata ukiwa unatengeneza blog au website!? Asante sana

Hili nitakujibu siku zijazo kwa maelezo ya kina zaidi
 
Last edited by a moderator:
Tutaendelea na somo letu muda wowote leo, mnisamehe nilikuwa na tatizo la network
 
Hongera zako mkuu

Nimependa signature yako mkuu imenifunza kitu flani hivi kiongozi.

Hongera sana kwa somo lenye manufaa na lisilo na uchoyo coz elimu ukiitoa inazidi kuongezeka maradufu.

Ni wachache sana wanaoweza kujitolea kwa muda wao na moyo wao wote na hasa kama ulivyosema sababu ni neno ambalo unaweza kulisoma kutokea kushoto au kulia na likaleta maana ileile "UVIVU".

Hongera sana mkuu.
 
Ahsante sana mkuu, ila zaidi ya miezi miwili sasa nimetingwa vibaya mno, niahidi tu kuwa tutaendelea na somo hili mwanzoni mwa mwezi disemba sababu bado nimetingwa sana
 
Ahsante sana mkuu, ila zaidi ya miezi miwili sasa nimetingwa vibaya mno, niahidi tu kuwa tutaendelea na somo hili mwanzoni mwa mwezi disemba sababu bado nimetingwa sana

Asante nawe pia kwa maarifa yako mkuu. Na nakutakia kila la heri na MUNGU akutie nguvu na abariki pia kazi za mikono yako kiongozi.

MUNGU AKUTANGULIE MKUU.
 
JINSI YA KUDESIGN BLOG INAYOLIPA

Habari ya wakati huu wakuu,

Ni siku nyingi niliahidi ningeleta somo hili hapa na leo kwa mapenzi ya Mungu tutaanza kulisoma taratibu.
Awali ya yote ijulikane wazi mimi binafsi sina blog inayolipa bali nitakufundisha yale ambayo nimepata kuyasoma ili kuwa na blog inayolipa.

Na wakati huo huo nitoe angalizo kwamba usiache kazi yako ya kuajiriwa au kazi nyingine uliyojiajiri na ukahamia kublog ukitegemea utapata hela za kukutosha kuendelea na maisha yako! Ni kweli unaweza kupata pesa kwa kuwa na blog lakini ni jambo linalohitaji muda, miezi kadhaa na hata miaka wakati mwingine mpaka uje uone hela ikitoka kwenye hiyo blog na kuja kwako.

Blog ni nini?

Neno Blog linatokana na maneno mawili ya kiingereza ambayo ni ‘web logs',. Neno ‘Logs' tafsiri yake ni ‘ni kuweka kwenye rekodi'. Hivyo Blog ni aina ya tovuti au website ambayo inaongezwa makala mpya kila mara kwa mpangilio maalumu. Kuna aina kuu 2 za blog, blog za bure na bure za kulipia.

Kwenye makala hii tutajadili zaidi kuhusiana na blog za kulipia sababu ndizo zinazoweza kulipa.

Ili kudesign blog inayolipa unahitaji vitu hivi kwa kuanzia;

1. Top Level Domain (T.L.D)

Domain ni nini?

Domain ni JINA LA BLOG. Hivyo jamiiforums.com au millardayo.com/ yote haya ni majina ya blog au tovuti.

Domain au jina la blog huwa na sehemu kuu mbili, mzizi (jina) na kiambishi tamati (extension)

Hivyo jamiiforums na millardayo haya yote mawili ni sehemu ya mzizi wa jina
na .com ndiyo kiambishi tamati au domain extension kama tulivyozoea

Sasa, top level domain ni domain za namna gani?

Ili uwe na blog inayolipa kitu cha kwanza ni kuwa na top level domain, hizi domain ambazo kwanza hazipatikani bure, ili kuwa nayo ni lazima ununue na mara nyingi unaweza kununua na kuimiliki kwa mwaka mmoja au miwili au hata zaidi kadri utakavyolipia wewe.

Pili, hizi top level domain mara nyingi ni kuwa, mara tu baada ya jina basi kinachofuatia ni kiambishi tamati (extension), mfano jamiiforums baada tu ya jina mwisho ni .com hivyo unasoma jamiiforums.com

Kumbe zile ambazo siyo top level domain kwanza ni bure na unakuwa huna umiliki wake kwa asilimia 100, hivyo unaweza ukaamka tu siku moja na usiione blog yako hewani na ukiuliza utaambiwa inakiuka vigezo na masharti yetu, hata kama si kweli!

Siyo hivyo tu, zile ambazo siyo top level domain huwa pia ni ndefu zaidi kuliko hizi top level domain kwa sababu katika hilo hilo jina lako kutatakiwa kuwepo pia jina la aliyekupa hiyo domain bure au wakati mwingine unaweza ukalazimishwa kiambishi tamati (extension) kiweje.

Hivyo ukitaka kuwa na blog inayolipa sahau kuhusu .blogspot.com, .wordpress.com, .webly.com na mengine mengi kama hayo.

Tuchukulie mfano kama hawa jamiiforums wangeamua kutumia jina la bure kutoka google kwa mfano, jina lao lingekuwa linasomeka hivi => jamiiforums.blogspot.com !!!

Umeona tofauti ya jamiiforums.com na jamiiforums.blogspot.com?

Hivyo top level domain kwanza ni fupi na hivyo linakuwa rahisi hata kutamkwa na kukumbukika kirahisi. Ni rahisi kutaja au kutamka jamiiforums.com kuliko kutaja au kutamka na kukumbuka jamiiforums.blogspot.com

Watu wengi wanaotaka kuwa waandishi wa kujitegemea kwenye mtandao (bloggers) wengi hukosea kwa kutumia muda mrefu wakiwa na domain au majina ya blog ya bure. Haidhuru kutumia jina la bure lakini iwe ni kwa ajili ya kujifunza na kupata uzoefu tu kwa muda mchache, baada ya muda au hata mwanzoni kabisa kama unataka kuwa na blog inayolipa ni vema kuwa na top level domain mapema. Siyo gharama, top level domain unaweza kuipata kuanzia Tsh 10000 na haizidi Tsh 30000 labda iwe ni special sana kama zilivyo za .academy

VITU VYA KUZINGATIA UNAPONUNUA DOMAIN

Domain au jina zuri la blog lazima liwe na sifa zifuatazo;

1. Liwe Fupi, kwanini liwe fupi? ili iwe rahisi kutamkwa na kukumbukwa

2. Liendane na maudhui ya blog. Mfano unaona jamiiforums limebeba maudhui au malengo ya blog, jamii ni sisi watumiaji wote na forums ndivyo yalivyo majukwaa. Hii si kanuni hasa kwa blog binafsi zile mtu anaweza kuamua kutumia jina lake kamili na ndani yake akaandika lolote analolipenda au kuhusiana na taaluma au kazi yake.

Mara nyingi nikipata mtu anataka nimshauri kuhusu blog yake afanye nini iende mbele, cha kwanza nawaambia nitajie blog yako, nikiona tu ni jina la bure basi cha kwanza hata kabla sijaitembelea hiyo blog nitakuambia nunua jina.

Hatua ya kwanza katika kuwa na blog inayolipa ni kuwa na blog yenye jina la kulipia na siyo la bure. Na sababu ni nyingi, kwanza linakuwa ni la kwako kwa asilimia 100, unaweza kulifupisha kadri uwezavyo na linakufanya uonekane upo makini na kazi yako.

Kwa leo tuishie hapa, somo litaendelea na sehemu ya pili. Pia mnipe ushauri kama niwe nafungua uzi mpya kwa kila sehemu ya somo au niwe naendelea nayo kwenye uzi huu huu.

sehemu ya pili;

Jinsi ya ku-design Blog inayolipa (Part 2):

Tunaendelea na sehemu ya pili ya somo letu

2. UNIQUENESS (UPEKEE)

Blog inayolipa lazima iwe ni ya kipekee (Unique). Hapa uwe makini kidogo maana hili ndilo lililo mhimu kuliko yote. Kama huwezi kumshawishi mtembeleaji mpya wa blog yako kuiona blog yako ni ya tofauti, nini kitamfanya aendelee kubaki hapo akisoma au arudi tena kesho kuona kama kuna jipya?

Njia pekee ya uhakika ya kuifanya blog yako ni tofauti na blog nyingine ni UPEKEE. Kama hakuna vitu vya kipekee kwenye blog yako usitegemee mtembeleaji wa kwanza au mpya wa blog yako kurudi tena au kuitafuta tena hiyo blog.

Ninaposema upekee kwenye blog naongelea vitu vikuu viwili ambavyo ni;
1. UNIQUE DESIGN/MUONEKANO WA KIPEKEE

Blog yako ili ilipe lazima iwe na muonekano wa kipekee. Muonekano wake kwa maana ya rangi, menu zake, namna inavyowasiliana na kujibizana na watembeleaji uwe ni wa kipekee na usiobadilika kila mara, mfano leo nimetembelea blog yako nakuta in background ya blue, kesho nakuta ina background nyekundu!, hapana, haiwi hivi. Unaweza kubadili muonekano wa blog yako baada ya miezi 6 au mwaka mmoja au miaka kadhaa, lakini siyo kila mara kwa sababu inaweza hata kuathiri kiasi cha uaminifu wa wasomaji wako kwako.

Hivyo unapofikiria kuanzisha blog yako fikiria pia juu ya kumpata mtengenezaji au designer wa blog atakayekutengenezea blog yenye muonekano wa pekee kwa maana kwamba blog yako haifanani fanani na blog nyingine kirahisi ili kukufanya wa tofauti.
2. UNIQUE CONTENT/MAKALA ZA KIPEKEE ORIJINO

Hapa ndiyo penye shida sana hasa kwa bloggers wengi wa Tanzania. Yaani Bloggers wengi wanachofanya ni kusubiri website ya gazeti fulani au blogger fulani aandike makala na wengine wote wana-copy na ku-paste kwenye blog zao kwa kichwa cha habari kile kile na maelezo yale yale!. Ni vigumu kuwa na blog inayolipa kwa staili hii.

Ili kuwa na Blog inayolipa, blogger unatakiwa ushiriki kwenye kutayarisha, kuandaa na kuandika makala za blog yako wewe mwenyewe. Sasa kuna sababu gani ya mimi kutembelea blog yako kama makala zako zote una-copy toka blog ya Shigongo?, ni heri nifunguwe kila siku blog ya Shigongo ambako nitapata orijino stori badala ya kuja kwako. Hii inaathari nyingi ikiwemo kukosa traffic kutoka search engines kama vile google.

Kuna vitu vingi sana unavyoweza kuviandika. Lakini wengi wanapenda kuandika tu juu ya mapenzi, michezo na siasa. Unaweza kuandika juu ya somo lolote iwe ni hesabu au biolojia, unaweza kuandika kuhusu kilimo, ufugaji, ujasiriamali, uchumi, afya, utalii, hoteli, shule, saikolojia, ushauri, malezi, na mengine mengi bila idadi na ukaeleimisha jamii inayokuzunguka.

Kwanini watu wanatembelea blog yako? Kwa sababu kuna jambo wanataka kusoma au kujifunza. Ukiwa blogger huna tofauti na mwalimu. Mwalimu au profesa wa chuo kikuu analipwa mshahara kwa sababu kuna kitu fulani anachofundisha.

Anzisha blog, chagua mada maalumu na udumu kwenye mada hiyo ukiifundisha kila mara kidogo kidogo. Andika habari au makala ambayo haifanani na wengine lakini yenye msaada kwa msomaji. Andika jambo likakamilika.

Kuna ushindani mkubwa na unaozidi kuongezeka siku hadi siku kwenye sekta hii ya uandishi. Andika kitu cha pekee (unique story) na mhimu kuliko yote, stori iwe ni yenye kumsaidia au kumuongezea thamani msomaji wako.

Kwa ufupi, sehemu hii ya pili inagusia kwenye jambo la UPEKEE, Upekee kwenye muonekano wa blog, kazi ambayo siyo yako wewe blogger bali ni kazi ya msanifu/designer wako na upekee kwenye makala au stori zako, kazi ambayo ni yako moja kwa moja.

UVIVU ndilo neno pekee linaloweza kusomeka na likaleta maana ukianzia kulisoma upande wowote iwe ni kushoto au kulia.

sehemu ya 3

3. Self Hosted Blog

Ili blog au website ionekane hewani inahitaji vitu viwili

  1. Jina (Domain) <= tumeshajadili kuhusu domain hapo juu kwenye TLD
  2. stoo/hifadhi Host/Server (Host/Server)

Kama ilivyo kwa majina (domain), kuna majina ya bure na majina ya kulipia na tumeshajadili kwa kirefu hapo juu tofauti ya majina ya bure na majina ya kulipia na tukakubaliana kwamba ili uwe na blog inayolipa, unahitaji uwe na jina la kulipia na siyo la bure na sababu tumezieleza.

Hivyo hata stoo ya kuihifadhi hiyo blog ili ionekane hewani popote duniani zipo za aina mbili, za bure na za kulipia. Kwa kawaida kama ulifungulia blog yako kwenye google na ukabadili jina tu bila kubadili hifadhi (server/host) ya hiyo blog bado unahesabika unatumia stoo ya bure.

Kama ilivyo kwa bloggers wengi wanapoanza kuandika kwenye mtandao wengi huanza au hufikiri kutumia server za bure! Lakini ili upate mafanikio katika hiyo blog unalazimika kuwa na server ya kulipia.

Sehemu ya 3 ya vitu mhimu unavyohitaji ili kuwa na blog inayolipa inajikita kwenye Hosting/Server(Stoo).

Kwanini ulipie server?

Kwa sababu unapata uhuru zaidi na blog yako.

Kwa mfano ukiwa kwenye server za bure, mara nyingi

1. Utaambiwa idadi ya watu wanaoweza kutembelea hiyo blog yako kwa siku au kwa mwezi (bandwidth) ni wangapi. Usipolijuwa hili na ukafanya utundu wako siku 1 ukawapeleka watu 1000 au zaidi wakati umeambiwa kwenye hii server ya bure unaweza kuwa na wasomaji 200 tu kwa siku, lazima utaikuta blog yako ipo chini haionekani tena!.

2. Huwezi kuwa na blog yenye uzito (gb) wowote utakao wewe kwa mfano unaweza kuambiwa blog au website yako isizidi ukubwa wa mb 300 (disc space).

3. Unaweza pia ukaambiwa unaweza kuwa na barua pepe/email 1 au 2 au ukaambiwa huwezi kuwa na barua pepe kwa jina la bog yako mfano ukihifadhi blog yako kwenye google basi email yako haiwezi kuwa info@fadhilipaulo.com badala yake utalazimika kutumia email ya gmail! <= sasa kama upo makini na kazi yako huwezi kukubali vitu kama hivi.

Lakini yote hayo ni kwa sababu ya bure.

4. Ukiwa kwenye server ya bure wakati mwingine huwezi kujipangia ni mfumo upi utaumia kusanifu (to design) blog yako mfano kama upo kwenye server za google (blogspot) muundo au design ya blog yako lazima iwe ni zile za blogger tu, huwezi kuwa kwenye blogspot halafu utumie muundo (design) au mfumo wa blog unaotumia wordpress. Kadharika ukiwa .wordpress huwezi kutumia muundo wa blog wa blogger, drupal, joomla na kadharika.

Kumbe ukiwa kwenye server ya kulipia unaweza kuamua mwenyewe blog au website yako iendeshwe kwa mfumo upi ikiwa ni code (html) au utumie mfumo mwingine wowote wa kuendeshea blog (CMS), kama ni wordpress, blogger, html, drupal, Joomla na kadharika na kadharika kadri utakavyo wewe.

Kitu kingine kitakachokugharimu ukiamua kutumia server za bure ni vile namna ya kuifanya blog yako ionekane kirahisi kwenye injini za kutafutia vitu kwenye mtandao kama vile google, bing, nk. Hili tunaliita Search Engine Optimization (S.E.O), kumbe ukiwa kwenye server ya kulipia unakuwa na namna nyingi ya kulifanikisha hili kirahisi zaidi.

Kwa kifupi ukiwa na server yako ya kulipia kila kitu ni chako, haijalishi muundaji wa website kama ni kampuni au mtu binafsi, unao uwezo wa kufanya lolote kuanzia backups and restoration, kubadili mfumo wa blog wakati wowote na bila kumwambia yeyote.

Binafsi nilitumia server za bure mwanzoni mwa safari hii yangu ya kublog lakini baadaaye niliachana na hizo na nikaanza kulipia baada ya kuona kuna vitu vingi navikosa, kisha idadi ya wasomaji wangu waliendelea kuongezeka hivyo isingewezekana tena kukaa kwenye server za bure au server ndogo ndogo za kulipia.

Kuna server za kulipia za aina nyingi, lakini kabla ya kuamua ununuwe au ulipie ipi inakupasa kwanza kujuwa mahitaji yako na umhimu wa hiyo blog kwako na kwa wasomaji wako. Katika yote, nakushauri ulipie server inayokufanya uwe na &#8216;Personal Control Panel'. Control Panel (CPanel) ni aina ya mfumo wa kuhifadhia (host/serve) blog au website kwa namna ya pekee, na unapewa vitu vingi vinavyobaki kuwa vyako na unaweza kuiendesha blog au website yako kwa namna au mfumo wowote uutakao.

Labda utakuwa unajiuliza sasa ni bei gani kuwa na stoo/server yako ambayo ni ya kulipia na siyo ya bure? Jibu ni kama lilivyo kwa domain. Ni bei rahisi sana ingawa bei itaongezeka taratibu kadri blog yako inavyokuwa, kwa sehemu kubwa unaweza ukalipia kuanzia 5000 mpaka laki kadhaa au milioni kadhaa kwa mwezi kutegemea na ukubwa wa hiyo blog na ukubwa hapa huwa ni idadi ya watembeleaji na ukubwa wa faili la blog yako ambalo huongezeka ukubwa kadri unavyoandika makala mpya.

Mwishoni kabisa mwa somo hili nitakuambia kabisa wapi ukanunue jina la blog yako na wapi ukanunue stoo ya blog yako.

JINSI YA KUDESIGN BLOG INAYOLIPA sehemu ya 4

4. CONSISTENCE/KUDUMU KWENYE MADA

Hebu fikiria labda ulikuwa ukitafuta somo linalofundisha &#8216;Namna ya kufuga Mbwa' na unakutana anuani ya blog inayoelezea somo hilo kupitia injini za kutafuatia vitu kwenye mtandao (search engines).

Siku ya pili unarudi kwenye ile blog unakuta kuna masomo ya namna ya kutengeneza keki!. Keshokutwa yake unajaribu kurudi tena uone ni kweli ulichoona jana, mara unakuta post yao ya mwisho inazungumzia namna ya kulima vitunguu swaumu!!!

Hakika, siku ya nne hutarudi tena hapo kutafuta habari juu ya &#8216;Namna ya kufuga Mbwa'.

Ni vigumu kuwa na blog inayolipa kwa staili ya uendeshaji wa blog wa namna hii.

Fanya blog yako ijulikane ipo hasa kwa ajiri ya nini, wafanye wasomaji wako wawe wazi kujuwa wakija kwako watapata nini.

Blog lazima iwe na mada au topic maalumu moja inayojitambulisha nayo. Blog zipo hasa kwa ajili ya kufundishana jambo au somo fulani moja. Kama ni blog kuhusu michezo, andika habari za michezo, kama inahusu mapenzi, andika mapenzi, kama inahusu biolojia, andika biolojia, kama inahusu teknolojia andika teknolojia, na kadharika na kadharika. Huhitaji kuzungumzia kila jambo kwenye blog yako ili kupata wasomaji wengi na hatimaye ikulipe.

Hizi mada au topic, kwenye ulimwengu huu wa ku-blog huitwa &#8216;NICHE'.

Kuna NICHE kubwa na niche ndogo ndogo, na kutoka kwenye hiyo niche kubwa bado unaweza kuivunjavunja na kupata kipande kidogo cha sehemu ya hiyo niche kubwa na ikawa ndiyo mada au topic kuu ya blog yako.

Mfano, NICHE KUBWA ni &#8216;AFYA'. Kutoka niche au mada kubwa au kuu AFYA unaweza kuivunjavunja na ukapata niche ndogo ndogo kama &#8216;UZITO NA UNENE KUPITA KIASI'. Blog yako kuanzia post ya kwanza hadi ya mwisho zinazungumzia mada moja tu ambayo ni UZITO NA UNENE KUPITA KIASI. Yaani nikihitaji kila kitu kuhusu uzito na unene kupita kiasi basi nikienda blog fulani au blog ya fulani kila kitu kuhusu UZITO NA UNENE KUPITA KIASI nitakipata hapo.

Sasa unakuta blog mara ina post za stori za mapenzi, mara michezo, mara afya, mara teknolojia. Yaani ni vurugu. Blog siyo forum au siyo tovuti ya gazeti. Wewe kama blogger chagua mada moja utakayodumu nayo na watu wakutambuwe kwa hilo.

Kama unapenda magari, blog kuhusu magari. Kama unapenda kilimo, blog kuhusu kilimo, kama unapenda siasa, blog kuhusu siasa, unapenda habari, blog kuhusu habari, unapenda muziki, blog kuhusu muziki &#8230;. Na kadharika na kadharika.

Na hii kudumu kwenye mada (being consistent) inahusu vitu viwili kwenye blog, ambavyo ni;
1. Kudumu kwenye mada au topic ya blog, (niche). Yaani kama inahusu kilimo basi udumu na masuala ya kilimo na

2. Kudumu kutoa makala mpya kwa muda na mpangilio maalumu (persistence). Wasomaji wako watarudi tena na tena kwenye blog yako kama kuna makala mpya kila mara. Hapa JF unaona kuna wasomaji wengi ni kwa sababu kuna mada mpya kila siku na tena ni nyingi maana kila mtu popote alipo anaweza kuanzisha mada tena wakati wowote na mbaya zaidi hao waanzisha mada ni wengi na mada zimepangwa kimajukwaa sababu hii ni forum na siyo blog

Sasa, sijakushauri ukaanzishe jamiiforum nyingine, wewe kaanzishe blog, dumu kwenye mada ya blog na uandike makala mpya kila mara bila kupumzika. Siyo kila siku! Unielewe hapo. Kama ni blog inayohusu habari, ndiyo unaweza kuandika makala mpya kila siku sababu habari zinatokea kila siku.

Ili kutowachosha wasomaji wako unaweza kufanya makala mpya moja kila baada ya siku 1 au makala mpya 2 kwa wiki. Hii itakusaidia pia kupata traffic toka search engines kama google sababu google anapenda blogs ambazo zinakuwa na makala mpya kila mara (updated) na kwa mpangilio maalumu.

Hii siri nawapa pia website au tovuti za makampuni ambazo website zao ni static na hawana sehemu ya blog kwenye tovuti zao. Kila website sasa inahitaji kuwa na sehemu ya blog ambako wataandika matukio au elimu yoyote kuhusu huduma zao kila mara ili waweze kupata watembeleaji (traffic) kirahisi kutoka kwenye injini za kutafutia vitu kwenye mtandao (search engines). Itawapunguzia hata gharama zao wanazotumia upande wa masoko (marketing).

Mengine ya haya ninayoyasema hapa yananichoma hata mimi sababu hata mimi nimewahi kukosea staili hii mwanzoni wakati naanza ku-blog kwenye mtandao. Lakini kama elimu na kama kukusaidia wewe usije kupoteza muda na pesa basi uyaepuke ikiwa unataka kutumia mtandao kwa manufaa ya jamii na yako. Kwa maana ya kusanifu (design) na kuwa na blog inayolipa.

Kuna wakati inaweza ikakutokea unao uwezo wa ku-blog au kufundisha mada (niche) zaidi ya moja labda hata 3, yaani mtu ana vipawa vingi Mungu kamjaalia, utafanya nini?. Hapa jaribu, nimesema &#8216;jaribu' ku-blog kuhusu vyote halafu uone wapi wasomaji wako wanakupenda zaidi na uwekeze muda zaidi upande huo.

Kwahiyo sehemu hii ya nne ya namna ya kudesign blog inayolipa inazungumzia umhimu wa kudumu kwenye mada, &#8216;CONSISTENCE'. Kudumu kwenye mada inayoitambulisha blog yako (niche) na kudumu kwenye mada kwa maana ya kuleta makala au post mpya kila mara kwa mpangilio maalumu (persistence).

Tutaendelea na sehemu ya 5 &#8230;.

Tutaendelea na sehemu ya tano ya somo hili. Tutaenda taratibu walau kila wiki tutapata sehemu 2 za somo hili, hatuna haraka, tunahitaji watu waelewe.

WhatsApp natumia namba hii => +255769142586

orthodox, Aqua, crunkstaa, Chris41, ladyfurahia, Murano, Health and Life Tz,
Nashukuru sana hili somo limenisaidia sana hata kufanya designing ya kablog kangu,MTILAH BLOG
 
Back
Top Bottom