Jinsi ya ku-design Blog inayolipa (Part 1)

Asante kwa somo lako zuri, mimi pia nilipata kujifunza humu humu Jamii forum kuhusu blog katika thread zilizopita nashukuru hapa nilipofikia japo si sana lakini sijapata mtu wa kunirekebisha au kunikosoa wapi nilipokosea naomba ukippata mda mkuu upitie Chumbani Lounge

Mkuu, nimeiona, nitakushauri kesho nini cha kufanya.
 
Asante kwa somo lako zuri, mimi pia nilipata kujifunza humu humu Jamii forum kuhusu blog katika thread zilizopita nashukuru hapa nilipofikia japo si sana lakini sijapata mtu wa kunirekebisha au kunikosoa wapi nilipokosea naomba ukippata mda mkuu upitie Chumbani Lounge

Mkuu,

Kosa la kwanza ninaloliona ni namna DESIGNER wako alivyoiweka sheet au uwanja wa hiyo blog.

Utaona sehemu ya makala au uwanja wa kuandikia maneno una upana ulio sawa na uwanja wa menu (right side bar [B to C]). Upana wa kutoka A hadi B ulipaswa uwe mkubwa zaidi kuliko kutoka B kwenda C,

CHUMBANI-SHEET-906x1024.png





Jambo la pili alilokosea ni kutokuweka HORIZONTAL MENU. Utaona pale juu kuna vichwa kama ''Maisha, Michezo, Mahusiano, Mapishi, Habari, Burudani, Mitindo, Urembo, Ajira na Udaku.'' <= hivi vyote vingependeza kama zingekuwa ni CLICKABLE MENU

Chumbani-horizontal-menu-1024x243.png






Jambo la tatu ambalo halipo sawa kwenye hii blog ni kule chini kabisa kwenye blog huwa tunakuita FOOTER. Kule chini kulipaswa kuwekwe COPYRIGHT YAKO au jina lako tu au link zingine kwenda kwenye blog yako. Cha ajabu naona maandishi haya => ''Picture Window template. Template images by Jason Morrow. Powered by Blogger.'' Huyo Jason Morrow na by Blogger wanakupunguzia ubunifu wako na kukuondolea umiliki wa 100% wa hii blog. Bila shaka hii ni template/theme au design ya bure!

chumbani-footer-1024x193.png



Kwa ufupi unahitaji DESIGN nyingine ya hii blog. Unahitaji pia kujifunza namna ya kuandika ndani kwenye kurasa.

Karibu
 
Basi jaribu ku google njia rahisi ya kupata adsense uone kama utapata

Wanadai baadaye zinakuwa disabled na google wenyewe. nime-google, hiyo kitu inawalakini, labda tupate ushahidi wa watu hapa walionunua adsense ac na wamedumu nazo muda wote.
 
Wanadai baadaye zinakuwa disabled na google wenyewe. nime-google, hiyo kitu inawalakini, labda tupate ushahidi wa watu hapa walionunua adsense ac na wamedumu nazo muda wote.

Bro,hii kitu ni full proof

Hizi Adsense ni legit.Hazina matatizo.Zikizingua utakuwa refunded
 
JINSI YA KUDESIGN BLOG INAYOLIPA sehemu ya 3

3. Self Hosted Blog


Ili blog au website ionekane hewani inahitaji vitu viwili


  1. Jina (Domain) <= tumeshajadili kuhusu domain hapo juu kwenye TLD
  2. stoo/hifadhi Host/Server (Host/Server)


Kama ilivyo kwa majina (domain), kuna majina ya bure na majina ya kulipia na tumeshajadili kwa kirefu hapo juu tofauti ya majina ya bure na majina ya kulipia na tukakubaliana kwamba ili uwe na blog inayolipa, unahitaji uwe na jina la kulipia na siyo la bure na sababu tumezieleza.


Hivyo hata stoo ya kuihifadhi hiyo blog ili ionekane hewani popote duniani zipo za aina mbili, za bure na za kulipia. Kwa kawaida kama ulifungulia blog yako kwenye google na ukabadili jina tu bila kubadili hifadhi (server/host) ya hiyo blog bado unahesabika unatumia stoo ya bure.

Kama ilivyo kwa bloggers wengi wanapoanza kuandika kwenye mtandao wengi huanza au hufikiri kutumia server za bure! Lakini ili upate mafanikio katika hiyo blog unalazimika kuwa na server ya kulipia.

Sehemu ya 3 ya vitu mhimu unavyohitaji ili kuwa na blog inayolipa inajikita kwenye Hosting/Server(Stoo).

Kwanini ulipie server?

Kwa sababu unapata uhuru zaidi na blog yako.

Kwa mfano ukiwa kwenye server za bure, mara nyingi

1. Utaambiwa idadi ya watu wanaoweza kutembelea hiyo blog yako kwa siku au kwa mwezi (bandwidth) ni wangapi. Usipolijuwa hili na ukafanya utundu wako siku 1 ukawapeleka watu 1000 au zaidi wakati umeambiwa kwenye hii server ya bure unaweza kuwa na wasomaji 200 tu kwa siku, lazima utaikuta blog yako ipo chini haionekani tena!.

2. Huwezi kuwa na blog yenye uzito (gb) wowote utakao wewe kwa mfano unaweza kuambiwa blog au website yako isizidi ukubwa wa mb 300 (disc space).

3. Unaweza pia ukaambiwa unaweza kuwa na barua pepe/email 1 au 2 au ukaambiwa huwezi kuwa na barua pepe kwa jina la bog yako mfano ukihifadhi blog yako kwenye google basi email yako haiwezi kuwa info@fadhilipaulo.com badala yake utalazimika kutumia email ya gmail! <= sasa kama upo makini na kazi yako huwezi kukubali vitu kama hivi.

Lakini yote hayo ni kwa sababu ya bure.

4. Ukiwa kwenye server ya bure wakati mwingine huwezi kujipangia ni mfumo upi utaumia kusanifu (to design) blog yako mfano kama upo kwenye server za google (blogspot) muundo au design ya blog yako lazima iwe ni zile za blogger tu, huwezi kuwa kwenye blogspot halafu utumie muundo (design) au mfumo wa blog unaotumia wordpress. Kadharika ukiwa .wordpress huwezi kutumia muundo wa blog wa blogger, drupal, joomla na kadharika.

Kumbe ukiwa kwenye server ya kulipia unaweza kuamua mwenyewe blog au website yako iendeshwe kwa mfumo upi ikiwa ni code (html) au utumie mfumo mwingine wowote wa kuendeshea blog (CMS), kama ni wordpress, blogger, html, drupal, Joomla na kadharika na kadharika kadri utakavyo wewe.

Kitu kingine kitakachokugharimu ukiamua kutumia server za bure ni vile namna ya kuifanya blog yako ionekane kirahisi kwenye injini za kutafutia vitu kwenye mtandao kama vile google, bing, nk. Hili tunaliita Search Engine Optimization (S.E.O), kumbe ukiwa kwenye server ya kulipia unakuwa na namna nyingi ya kulifanikisha hili kirahisi zaidi.

Kwa kifupi ukiwa na server yako ya kulipia kila kitu ni chako, haijalishi muundaji wa website kama ni kampuni au mtu binafsi, unao uwezo wa kufanya lolote kuanzia backups and restoration, kubadili mfumo wa blog wakati wowote na bila kumwambia yeyote.

Binafsi nilitumia server za bure mwanzoni mwa safari hii yangu ya kublog lakini baadaaye niliachana na hizo na nikaanza kulipia baada ya kuona kuna vitu vingi navikosa, kisha idadi ya wasomaji wangu waliendelea kuongezeka hivyo isingewezekana tena kukaa kwenye server za bure au server ndogo ndogo za kulipia.

Kuna server za kulipia za aina nyingi, lakini kabla ya kuamua ununuwe au ulipie ipi inakupasa kwanza kujuwa mahitaji yako na umhimu wa hiyo blog kwako na kwa wasomaji wako. Katika yote, nakushauri ulipie server inayokufanya uwe na &#8216;Personal Control Panel'. Control Panel (CPanel) ni aina ya mfumo wa kuhifadhia (host/serve) blog au website kwa namna ya pekee, na unapewa vitu vingi vinavyobaki kuwa vyako na unaweza kuiendesha blog au website yako kwa namna au mfumo wowote uutakao.

Labda utakuwa unajiuliza sasa ni bei gani kuwa na stoo/server yako ambayo ni ya kulipia na siyo ya bure? Jibu ni kama lilivyo kwa domain. Ni bei rahisi sana ingawa bei itaongezeka taratibu kadri blog yako inavyokuwa, kwa sehemu kubwa unaweza ukalipia kuanzia 5000 mpaka laki kadhaa au milioni kadhaa kwa mwezi kutegemea na ukubwa wa hiyo blog na ukubwa hapa huwa ni idadi ya watembeleaji na ukubwa wa faili la blog yako ambalo huongezeka ukubwa kadri unavyoandika makala mpya.

Mwishoni kabisa mwa somo hili nitakuambia kabisa wapi ukanunue jina la blog yako na wapi ukanunue stoo ya blog yako.

Tutaendelea na sehemu ya nne ya somo hili. Tutaenda taratibu walau kila wiki tutapata sehemu 2 za somo hili, hatuna haraka, tunahitaji watu waelewe.
 
Hongera sana mkuu nikijua namna za kujiunga na adsense ntafurahi sana..

Kujiunga na adsense ni bure ila kuna masharti unayotakiwa kuyatimiza. Mara nyingi blog zenye makala au lugha za kiswahili ni shida kuruhusiwa kuwa na adsense na ndiyo maana unaona kuna wadau wanauza account za adsense hapo.

Kuna general guidelines google wanayoiangalia kwenye hiyo blog yako na uki-meet vigezo vyao unapewa account yako bila shida.

Lakini hapa tutajifunza pia namna ya kupata hela kwenye blog bila kutumia adsense ambayo ni mhimu zaidi kuliko yote. Kama blogger adsense iwe ni tegemeo la pili la kukuingizia kipato na siyo jambo la kwanza <= hapa ndiyo mhimu na ndipo inapoleta kazi hii kuwa ni taaluma na siyo jambo la kuamka na kuanza bila kujuwa unaanzia wapi na kuishia wapi.
 
Back
Top Bottom