Jinsi Umimi lism Katika biashara za Kibongo utakavyo tuangamiza

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,915
Wakuu, Mkijaribu kufuatilia triend ya Biashara Duniani, Ushindani ni wa Hali ya Juu kabisa, na si kwa makampuni madogo tu, No makampuni makubwa ndo wako katika hatari zaidi, Na kwa sasa Kampuni nyingi sana zina ungana ili waweze kuhimili ushindani wa Kibiashara, Mfano KAMPUNI YA BP YA UK WANA MPANGO WA KUUNGANA NA KAMPUNI YA URUSI YA GAZPROM, hii kwa sasa ndo kampuni yenye profit kubwa sana kwa mjibu wa Ripot ya juzijuzi, imezipiku hata Exon mobile ya USA

- So kampuni nyingi sana kwa sasa zina angalia uwezekano wa Kuungana kwa ajili ya kuimarisha mitaji yao na kuweza kushindana vyema, na kuungana hakumanishi kuua kampuni moja na kubakia nyingine

NJOO SASA KWA UMIMI WA WATANZANIA

1. Watanzania ni Moja ya watu ambao Umimi uko juu sana kila mmoja anataka awe na chake, kila mmoja anataka aonekane, kila mmoja anataka sifa, Kila mmoja anataka aonekane yeye ndo yeye,

2. Watanzania Kila mmoja anataka awe na Tax, kila mmoja awe na Haice/daladala, kila mmoja awe na Mabasi yake, Kila mmoja afuge kuku wake, Kila mmoja awe na Ng'ombe wake, Kila mmoja awe supermarket yake, kila mmoja awe na Mgahawa wake, Kila mmoja awe na Baa yake, Kila mmoja awe na Gest yake, Kila mmoja awe na Kampuni yake ya Ujenzi

ORODHA NI NYINGI SANA ILA HUO NI MFANO WA UMIMI HAPA BONGO

- Kwa Triend ya Biashara ilivyo, tutakuja lia sana tena kulia na kuswaga meno, najua wako watakao beza hili, ila kulia kupo sana, Dunia inakuwa kijiji na Nirango inafunguliwa kwa kila Biashara, Na msidhani kwamba WACHINA WANAO KUJA TANZANIA KUNA SIKU WATAONDOKA, NO NDO WANAZIDI KUONGEZEKA,

-Watanzania tunapenda sana tuonekane na Kila mtu yuko bise kivyake, ilimuradi kila mtu ana kampuni yake halafu mwisho wa siku tunaanza kulilia serikali kwamba haiwajari wazawa,

MIFANO

1. KAMPUNI ZA UJENZI- Hizi kampuni za Ujenzi za Tanznaia zinauwezo wa Kupambana na Kampuni za Nje na kupata tanda, Tatizo ni UMIMI, hizi kampuni za China zinazo pata Tenda huku nyingi ukifuiatilia historia yao ziliyngana Kampuni zaidi ya Tano na Kuunda Kampuni kubwa sana

- Kampuni zetu za Wazawa ndo zinaelekea Kaburini, zitabakia kusubiria tenda za kujenda Barabara za Vijijini ambazo hazina Tija sana kwao na Tenda kubwa wanapewa Wachina na Wazungu

2. USAFIRI

- Hii itakuwa sekta ya Pili kula kwao, hii sekta musa si mrefu watu watalia sana, Na yote ni kutokana na kila mtu kutaka awe na DALADALA LAKE, AWE NA TAX YAKE AWE NA FUSO LAKE NA KAZALIKA, tuulizane je MABASI YAENDAYO KASI YAKIKAMILIKA KUNA MTANZANIA ATAWEZA KUSHINDANA NAYO KIBIASHARA?

3. SEKTA YA MADUKA YA REJAREJA
- Kwenye hizi supermarket nako kazi ipo sana, Ushindani ni mkubwa na kutokana na UMIMI WETU ITAKULA KWETU MUDA SI MREFU

wakuu orodha ni ndefu ila kwa leo naishia hapa

Wakuu kwa Kifupi, UMIMI utatuangamiza na Watanzania wengi sana Hawataweza Kuhimili kushindana na Kampuni za Nje pindi zitakapo anza kumiminika huku kwetu, Tiyali Kariakoo Wachina wameisha anza kuonyesha hivyo, Na hawa jamaa wanakuja kuwekeza kwenye sekta nyingi sana zikiwemo za UFUGAJI, KILIMO, USAFIRI NA KAZALIKA
 
Asante sana mm niko tayari kungana na wenzangu kibiashara naomba mnitafutie wabia wa daladala, hardware na kadhalika, hongera sana kwa wazo zuri sana,...
 
Back
Top Bottom