Jinsi Uchaguzi wa Rais wa Marekani unavyofanyika

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
Unaweza kushinda kwa kura nyingi dhidi ya mpinzani wako lakini bado usiwe Raisi.Hivi ndivyo sheria ya chuo za wanazuoni wa Marekani inavyofanya kazi.

Katika mjadala huu neno Electoral college nitatumia kwa kiswahili chuo cha wanazuoni

“Kwa kifupi

Wanachama mbali mbali 538 wa chuo cha wanazuoni wa Marekani wanakutana katika miji mikuu ya kila majimbo yao kwa kila jimbo kila baada ya miaka minne baada ya uchaguzi wa raisi kuchagua mshindi.

Kila mgombea uraisi lazima apate jumla ya kura zote au angalau 270 kati ya hizo kura 538 kwa maana hiyo ni zaidi kidogo ya nusu 270 ukigawa kwa 538=0.5 ili uwe umeshinda.

Utaratibu huu ulikuwa kwenye katiba ya Marekani toka mwaka 1787 kuweka sheria madhubuti isiyo ya moja kwa moja kumpata mshindi

Washington,

“Ajabu ni jinsi mgombea wa uraisi Donald Trump alivyomshinda bibi Hillary Clinton tarehe 8th Nov 2016 ni vigumu kuelewa lakini ilikuwa hivyo.Hillary Clinton alimshinda Trump kwa karibu kura millioni tatu lakini Trump alimpiga bao kwenye kura za wanazuoni alifikisha 270 ambazo ni muhimu sana kushinda uraisi wa Marekani.

Hii sheria tata wengine wanadai ni ya kizamani isiyo ya kidemokrasia.

Iliwekwa na watangulizi au mababa wa taifa hilo kubwa la Marekani mwaka huo wa 1787 kuweka sawa mambo kutokana na taifa hilo kubwa historia yake kuwa ni muunganiko wa nchi nyingi na lilipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe hasa kusini na kaskazini wasijitengane wakaona utaratibu huo ndio muhimu zaidi na unatumika hadi sasa hebu tuone mifano mbali mbali.

GORE DHIDI YA BUSH MWAKA 2000

Toka miaka hiyo mabadiliko mamia yamekusudiwa kuifanyia sheria hiyo katika bunge la Marekani au kuiacha kabisa watumie simple majority lakini hakuna aliyeweza kufua dafu kuiondoa sheria hiyo na ndio iliyompa upenyo Trump akamshinda Hillary Clinton.

Kila jimbo lina wapiga kura wengi kama ilivyo kwa wawakilishi wake kwenye chuo cha wanazuoni na hii inategemeana na ukubwa wa jimbo pamoja na idadi ya raia kwenye jimbo husika.

Kwa mfano jimbo kubwa na muhimu la California lina wanazuoni 55; Texas 38; na majimbo yenye watu wachache kabisa mfano Alaska.Delaware,Vermont na Wyoming yote kwa pamoja yana wanazuoni wa 3 tu kila jimbo.

Hii basi ina maana gani tukivuta taswira hii tukaileta hapa kwetu Tanzania.Ukiangalia kiidadi ya watu mikoa ya kanda ya Ziwa ukichukua Mwanza,Tabora,Shinyanga,Mara kwa pamoja kila mkoa mmoja ungepewa upendeleo wa kuwa na wanazuoni wengi zaidi kulingana na wingi wao na ukubwa wa mikoa yao.Mkoa wa Kilimanjaro,Kagera na Mbeya nayo hii mikoa nayo ingekuwa na uwiano mkubwa wa wanazuoni wengi wa kupiga kura za hicho chuo.Mkoa wa Kilimanjaro na Kagera ni midogo lakini ingepata upendeleo maalum kulingana na idadi yake kubwa ya watu.

Mikoa midogo kama Lindi,Mtwara,ingepata idadi ndogo sana wa wanachama wa chuo cha wanazuoni kulingana na uwiano wao.Ndio maana ili mtu ashinde Marekani ni muhimu sana apate kura nyingi za wanazuoni wa majimbo ya California,Florida na Texas.

Majimbo ya Nebraska na Maine yote yameunganishwa kwa pamoja anayeshinda Maine anahesabika ameshinda pia Nebraska.

KUKOSA KURA ZA JUMLA LAKINI BADO UKASHINDA

Mwezi November 2016, Trump alipata kura za wanazuoni 306. Jambo lisilo la kawaida la mwaka 2016 mtu kupata kura chache za wapiga kura na bado tu akawa raisi haikutegemewa.Lakini maraisi watatu huko nyuma waliukwaa uraisi kwa kupita njia hii.

John Quincy Adams alikuwa wa kwanza mwaka 1824, halafu akaja Andrew Jackson. Hivi karibuni mwaka 2000 uchaguzi ulikumbwa na utata huo mtifuano wa kura za wanazuooni wa jimbo muhimu la Florida kati ya George W. Bush wa Republican na Al Gore wa Democrati ndio uliomfanya George Bush akashinda kiti hicho.Hatimaye ikatokea kwa Hillary Clinton wa Democrati na Trump wa Republican ukampa kitu Trump.

Gore alishamshinda mpinzani wake Bush kwa zaidi ya kura 500,000 kitaifa, Lakini jimbo muhimu la Florida wanazuoni wakampa Bush kura nyingi zaidi zikamsukuma akavuka hiyo 270 na akafikia 271 hivyo akapewa yeye ushindi.

Wanazuoni wanakaa baada ya uchaguzi December 14 kupiga kura zao kumchagua raisi na makamu wa raisi.

Kwanini wanakaa tarehe hiyo? Sheria ya Marekani inasema “wanakaa na kupiga kura zao jumatatu ya kwanza baada ya jumatano ya pili ya mwezi December.”

Baada ya kumaliza shughuli hiyo mwezi unaofuata wa January 6, mwaka unaofuata kwa sasa itakuwa 2021, Bunge la uchaguzi (Congress) litamthibitisha mshindi, Ambapo anaapishwa mwezi huo wa January 20.

MAMBO YA KUJIULIZA TUKIJILINGANISHA NA SISI HUKU TANZANIA HAPA KILA MMOJA WETU ANA MAWAZO YAKE TUSAIDIANE KUCHANGIANA

1.Je utaratibu hu kwetu unafaa?-Kwa mawazo yangu kwetu haufai kabisa ikumbukwe wamarekani hawana kitu kinaitwa makabila kama tulivyo sisi huku tuna makabila zaidi ya 125.Kule wote wanaongea lugha moja labda tofauti itakuwa kwenye lafudhi tu labda na makabila ya Wahindi wekundu.Sisi tukileta utaratibu huu badala ya kujenga tutakuwa tunaupalilia ukabila na utengano maana siku zote raisi atatoka kabila flani kubwa lenye watu wengi.

2.Je hawa wanazuoni ni wa kina nani na wako chama gani?.Sisi itatupa shida sana maana wanazuoni wenyewe watajitenga ki vyama na ikumbukwe demokrasia yetu bado ni changa ya vyama vingi.

3.Je utaratibu huu wa Marekani ni mzuri? Jibu kwa mawazo yangu ni mbaya umepitwa na wakati vinginevyo hakuna haja ya wananchi kupiga kura kisha kundi la watu wachache wakawachagulia raisi na nina wasi wasi watakuwa hawa wanazuoni ni mabwanyenye wenye uwezo mkubwa kiuchumi.Kuna usemi wa mtaani kuwa raisi wa marekani huwa anawekwa na matajiri sio watu masikini sina uhakika na hili lakini nadhani kuna ukweli.Ndio maana Marekani wao vyama vikubwa viwili Republican na Democrat wanapeana vijiti kwa zamu.Huwa wanakuwa na malengo yao ya kidunia kwamba chama hiki ni maarufu kwa kufanya hiki kipindi hiki tukichague kwa maslahi yao ya kiuchumi.

Nitatoa mfano lakini kwa mawazo binafsi sio kwamba Bush kipindi cha pili walimpenda sana wananchi ila ukweli baada ya majengo pacha kudondoshwa na Osama kipindi cha Busha wananchi wa Marekani waliingiwa na woga mkubwa mno kuhusu Osama wakatishika mno wakaona chama cha Democrat wasiopenda vita hawatamuweza wakaona ngoja wampe tena Bush kipindi cha pili amdhibiti.Hata hivyo hakuweza Obama akamalizia kazi.

Uzuri wa wamarekani tofauti na sisi watanzania sisi tunashabikia vyama bila kuangalia sera za chama zitanifikisha wapi na je ni chama gani kina sera zinazovutia kwa mwananchi wa kawaida.Sisi bado tuko kwenye mambo madogo maji,barabara,shule na zahanati.Mmarekani mwaka huu anaweza kuwa mshabiki wa chama hiki miaka mingine akaenda chama kingine kulingana na yaliyopita kwa chama husika hakikufanya akaja ingia chama kingine mwaka ufuatao.Mfano mwanamama tajiri Oprah Winfrey alikuwa chama cha Republican lakini wakati Obama anagombea alimuunga mkono kwenye chama cha Democrat.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Colin Powel alikuwa republican lakini Obama wakati anagombea akahamia huko kufuata sera zake nzuri sera za aliyepita zilimkinahisha.

Na sisi watanzania tunatakiwa tuwe na ukomavu wa kisiasa wa hivyo sio kushabikia chama flani kwa kufuata mkumbo kinachongaliwa ni sera zilizokaa vizuri.

=====

Mwandishi wa habari hizi ni mchambuzi wa masuala ya siasa za kimataifa,mchambuzi wa habari za kisayansi na mchambuzi wa mambo ya kale ya kihistoria za kitaifa na kimataifa.
 
Hakika uchaguzi mkuu wa Marekani huwa ni uchaguzi mkuu wa dunia!

USA baby 🇺🇸
 
Back
Top Bottom