IsangulaKG
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 706
- 386
Habari Muhimu Kama hii inahitaji kusomwa Mara Kwa Mara ili ikae ,idumu katika Vichwa vya Wapambanaji
View attachment 22336
Nimetumiwa hii document kwa email, simjui author wake ni nani lakini nampongeza kwa jinsi alivyoweza kuchambua kiini cha sakata zima, ukiisoma between the lines utajua kwa undani ni jinsi gani taifa lilivyoingizwa mkenge na wajanja wachache, ingawaje ni ndefu kidogo lakini it worth reading, just take your time and read it to the end halafu tuunganishe nguvu kupaza sauti za kupinga malipo ya Dowans.
MM,
Utaniwia radhi kwa kuuliza tena na labda tena na tena. Nadhani ni jambo la kawaida na linalokubalika kwamba endapo mahakama imetoa uamuzi ambao wewe huridhiki nao, unaweza ku-appeal ili haki itendeke. Sasa nimewasikia Mzee Sitta na Dr. Mwakyembe wakieleza bayana kuwa Richmond na mrithi wake Dowans ni makampuni ya kitapeli. Binafsi siwezi kupuuza kauli za viongozi hao kwa sababu nina hakika wakati ule wa sakata la Richmond walipata fursa ya kujua mengi kuhusu utapeli huo kuliko hata walichokiandika na kusomwa bungeni. In other words, ninamchukulia Dr. Mwakyembe as a reliable source of data kuhusu utapeli wa hayo makampuni.
Sasa ninachojiuliza, ni je, kama kweli viongozi wetu ni wazalendo, walishindwaje kutumia fursa ya ku-appeal na kupeleka ushahidi mbele ya mahakama unaoonyesha kuwa dowans ni kampuni ya kitapeli tu. Ni kitu gani kimezuia Mwanasheria wetu asichukue hatua hiyo? Je, kipengele ulichogusia kwamba kumbe urithishanaji kati ya Richmond na Dowans ulifanywa kabla hata ya kufikia maridhiano kati ya Tanesco na Richmond, hakiwezi kuwa ni sababu tosha ya kuonesha utapeli wa Dowans? Je, tukiamua kama nchi kutolipa Dowans tutapata madhara gani ambayo wananchi wetu wa kawaida yatawaathiri zaidi ikilinganishwa na madhara watakayopata endapo serikali itajikamua na kulipa mabilioni hayo?
Kwanza kwenye hii kesi tanzania iliwakilishwa na nani? Tumjue ili tujue uelewa wake kwenye masuala ya sheria, na ikiwezekana awajibishwe kwa kukiuka maadili ya kazi kwa kujua au kutojua
Hivi ni nani mhusika mkuu kwenye sakata la RICHMOND?Kama si Lowasa,ni nani sasa ili watanzania tumjue na asutwe.
The most weirdest thing katika huu mjadala wa RICHMOND ambao naona watu wana kila document ni kuwa husikii majina ya:
1. Tender process ilivyokuwa
2. TENDER VALUATION ilivyofanywa
3. Katika Valuation team hakuna anaytajwa
4. Final report ya Valuation team
5. Mapendekezo yaliyopelkwa kwa DG wa TANESCO
6. Majina ya wanasheria wa TANESCO walioridhia haya
7. Majina ya waliokuwa consulted kule WIZARA YA NNISHATI
8. Majina ya waliohusika kule WIZARA YA SHERIA
9. Ushauri wao kwenye hili jambo
10.Role ya PRIVATE law firms kuishauri TANESCO
11. Mchanganuo ulivyofanywa mpaka kuwateua hawa private lawfirms na sababu...PPA ilifuatwa na je PPRA waliridhia?
12.Majina ya hao wahusika from the private law firm
13. Walilipwa Kiasi gani per hour?
14. Comments za DG wa TANESCO zilikuwa zipi?
15. Wanasheria wizara ya NISHATI walikuwa akina nani na walimpa ushauri gani waziri?
16. Wahusika wa PPRA ambao walikuwa consulted na comments zao
naona kila kukicha tunajadili maamuzi ya kesi na hao wanao likisha hizi documents mbona hawaleti full mzigo includi hayo majina?
Unles JF is not as influential as it used to back in the day when people used to trust it with leaked docs...Kulikoni au kitumbua kishaingia mchanga?
Au kama wanavyosema wanywamwezi kuwa the GAME HAS BEEN RIGGED!!
Unless kuwepo public inquiry into this fiasco