Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,155
- 31,058
Katika ubunifu ambao umefanikiwa sana Afrika ni mobile money hasa ikizaliwa kutoka Safaricom Mpesa. Ubunifu huu tofauti na ubunifu uliozoeleka kuanzia ulaya ukaletwa Afrika, huu ulitengenezwa mahususi kwa mazingira ya kiafrika na ndio maana mbile money imefanikiwa sana afrika.
Vodafone kuona mafanikio haya akaamua kuexpand Mpesa na kuipeleka kwenye sokoa la Ulaya. Mwaka 2014 ikawa launched kwa mara ya kwanza nchini Romania akilenga itumiwe na wateja milion 7 aliokuwa nao huko Romania.
Lakini tofauti na Afrika, Waromania hii huduma hawakuipenda yani waliona haiwezi kuwa mbadala wa huduma nyingone walizonazo za masuala ya pesa.
Kufikia 2018 M-pesa ya Romania ilikuwa ikitengeneza hasarana kupelekea Vodafone kusitisha hii huduma kabisa na mpango wao wa kuisambaza Ulaya.
Funzo ni kwamba, kila product inabidi iendane na mazingira husika na ndio maana developers wengi wanacopy apps za nje wanatengeneza zao tofauti jina baada ya miezi wanaachana nazo amaana watu hawazitumii.