Jinsi kupiga pesa kwenye karasha la madini(dhahabu) mgodini

Jan 26, 2019
67
86
HABARI ZA MUDA HUU WANA JUKWAA,Natumai ni wazima waafya ,lengo la kuandika uzi huu ni kutaka kujua jinsi ya kupiga pesa nyingi ikiwa kama ni MENEJA MKUU wa KARASHA(Crusher) la kusaga mawe yaliyo na dhahabu pia ningependa kujua kama ni mmiliki wa karasha kuna changamoto gani na pia faida inapatikana kweli?. Nimetaka kujua coz Mzee ameniambia nikasimamie karasha kwenye mgodi uliopo kahama mpakan na nzega..
 
Kaka naomba tu kuelekezwa jaman
Okay

Kwanza uhakika wa ku make hela unakuja kutegemea na eneo la crem linavyotoa mawe yake.

Kipimo kinachotumiwa kama makadirio ni idadi ya pointi kwa"dumu"

Kwa hiyo kama crem yenu au mgodi wenu unatoa walau ratio ya pointi 3 kwa dumu basi hiyo ni sehemu nzuri.

Kwa maana hiyo ukijaza rudio within 1 Year utakuwa unauhakika wa kuwa na zaidi ya 50M.

Ila kama crem yako haitoi jiwe la maana basi kuna namna utapata changamoto.
 
Wabongo Shida sana. Mzee kakupa kazi badala ku focus na kazi unawaza jinsi ya kupiga pesa. Ukishampiga pesa mzee wako Hilo karasha litakuwepo kweli?
Mkuu swala la kupiga pesa sehemu yoyote hutakuta mtoto akifanya kazi bila kupiga hata ya chai kwo hapo ni kawaida ila lengo si kuharibu ni kujenga
 
Hayo mambo mepesi mepesi ndio yanatufanya vijana wa kitanzania tuonekane wapumbavu,,ww aliyekwambia kwenye kusimamia karasha la baba yako utapiga pesa ni nani?

Karasha unalipwa kwa mzunguko unaosagwa,km unataka kufa mapema njoo na hiyo akili ya kutaka kutuibia mawe wachimbaji,tutakusukumiza kwenye ma longobesi na tukufukie humo humo,

Km lengo ni kujifunza kazi za uchimbaji na ununuzi nenda kajifunze upate maarifa ila kama unakuja kupiga pesa ya haraka ukatambie mademu njoo tukuoneshe
 
Nina ushahidi wa watu waliopewa kazi ya usimamizi wa karasha kutoka kwa madingi zao na saizi wametusua.

Kama eneo lina mawe yenye sample nzuri basi ipo nafasi tena kubwa tu ya kutoboa.

Ila kama mawe yakusua sua halafu hayatoi basi simshauri hata kwenda
 
Najua ataupuuza huu ushauri lakini ni one of the best to move with....napakumbuka shilalo,mwakitolio na masumbwe....pesa kumamayoooo
 
HABARI ZA MUDA HUU WANA JUKWAA,Natumai ni wazima waafya ,lengo la kuandika uzi huu ni kutaka kujua jinsi ya kupiga pesa nyingi ikiwa kama ni MENEJA MKUU wa KARASHA(Crusher) la kusaga mawe yaliyo na dhahabu pia ningependa kujua kama ni mmiliki wa karasha kuna changamoto gani na pia faida inapatikana kweli?. Nimetaka kujua coz Mzee ameniambia nikasimamie karasha kwenye mgodi uliopo kahama mpakan na nzega..
Deborah9007
 
Nina ushahidi wa watu waliopewa kazi ya usimamizi wa karasha kutoka kwa madingi zao na saizi wametusua.

Kama eneo lina mawe yenye sample nzuri basi ipo nafasi tena kubwa tu ya kutoboa.

Ila kama mawe yakusua sua halafu hayatoi basi simshauri hata kwenda
Kinachokutoa sio usimamizi wa karasha bali ni uzalishaji mzuri wa eneo hilo,mm nina karasha 5 nipo Mpanda hapa,mzunguko mmoja tunasaga 10000,sasa hapa kuna gharama ya mafuta na opareta,hiyo pesa nyingi unaipataje kwa mkupuo bila ya ww kukuza senga?pesa ipo kutokana na uzalishaji wa eneo kwa ww kuchimbisha au kununua mawe na kusaga kutumia karasha la baba
 
Uzalishaji ni matokeo ya kuwa na kelemu yenye kutoa mawe yenye sample nzuri.

Labda wewe una miliki karasha halafu huna kelemu yenye mwamba mkubwa wa kutoa mawe na ndio maana unaona upande wako hili swala haliwezekani.

Sijaelewa unaposema mzunguko mmoja mnasaga 10,000 ume maanisha nini
 
Najua ataupuuza huu ushauri lakini ni one of the best to move with....napakumbuka shilalo,mwakitolio na masumbwe....pesa kumamayoooo
Haya mambo ya haraka haraka yanatufanya tushindwe kupata vijana wazuri huko mbeleni wa kusimamia na kuendesha miradi,kabla hajafika hata kazini anataka ushauri wa kupiga pesa haraka haraka ampite hata baba yake mwenye karasha,km baba yake ndie mwenye karasha maana yake ni kwamba baba yake ni mpambanaji mwenzetu sasa huyu dogo anashindwaje kukaa na baba yake akampa ushauri wa uendeshaji?huyu ni Mchoji au Manyani sasa mwache aje tumtupe longobesi
 
Uzalishaji ni matokeo ya kuwa na kelemu yenye kutoa mawe yenye sample nzuri.

Labda wewe una miliki karasha halafu huna kelemu yenye mwamba mkubwa wa kutoa mawe na ndio maana unaona upande wako hili swala haliwezekani.

Sijaelewa unaposema mzunguko mmoja mnasaga 10,000 ume maanisha nini
Mkuu mbona tunabishana vitu vidogo?hakuna pesa ya kusimamia karasha,soma vizuri maelezo yangu,mm sihadithiwi hii kazi nina PML na PL juu,,hakuna pesa ya haraka kwenye kusimamia karasha,achimbe mawe asage kwenye karashala baba yake au anunue mawe na kusaga,,nimemaliza!
 
Nahisi dogo alikua anamaanisha ajue jinsi ya kupiga ili asipigwe yeye kama msimamizi wa baba yake.

Ila Kama anataka kumpiga baba huyu Haifai hata kusafiri na dingi maana atamsukia mipango hasi buree.
 
Mkuu mbona tunabishana vitu vidogo?hakuna pesa ya kusimamia karasha,soma vizuri maelezo yangu,mm sihadithiwi hii kazi nina PML na PL juu,,hakuna pesa ya haraka kwenye kusimamia karasha,achimbe mawe asage kwenye karashala baba yake au anunue mawe na kusaga,,nimemaliza!
Sio kama na mimi sijui nacho kiandika ipo maana ya mimi kwanini naandika hivi.

Nadhani tutakuwa tunapishana hapo wenye msamiati wa "pesa ya kusimamia karasha"

Target ya hiyo pesa nimeielezea huko juu kuwa akiwa yupo kwenye mgodi wenye kutoa sample nzuri ya mawe basi swala la ku make hela haliwezi kuwa kipengele kwake.

Hayo mawe unayomuelekeza akachimbe ina maana akisaga hayamuingizii hela kabla ya kuuza au kuchenjua rudio?

Au ndio aina ya mawe ya kutoa nusu point kwa dumu mbili?
 
Back
Top Bottom