Jinsi Kilimanjaro Natives Cooperative Union (KNCU) kilivyowainua Wachagga na kuwafanya kuwa 'mbele' hata leo hii

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,243
12,766
Ukisoma kitabu Desturi za Wachagga utaelewa kwa nini Wachagga wako mbele kuliko makabila mengi ya Tz. Kwanza kitu kikubwa sana kilichowatoa ni kupanda kahawa na kuwa na hiki chama Kilimanjaro Native Cooperative Union(KNCU) kama chama kikuu cha ushirika. Chama hiki kiliongozwa na mzungu kwa ufanisi sana kwa karibu miaka kumi na nne. Baadaye kikashikwa na Wachagga ambao nao walikiendesha wakiwa na maono makubwa sana. Hata kitabu hiki kilichapwa na kiwanda cha KNCU!! mwaka 1953. KNCU kilipeleka watu Ulaya kusoma biashara, kilihimiza ujengwaji wa shule na hospitali. Ndiyo maana leo Kilimanjaro licha ya kuwa mkoa mdogo tu lakini ndiyo unaongoza kwa kuwa na shule nyingi. Kilihimiza Wachagga kufanya biashara badala ya kutegemea Wahindi ambao ndiyo walikuwa wameshika biashara kilimanjaro wakati huo(Pengine ndiyo maana Wachagga wanafanya biashara pande zote nchini).

Soma sehemu kuhusu KNCU hapa chini. Unaweza kusoma kitabu chote ndani ya maktabaapp.

Desturi za wachagga cover.png

MLANGO WA 23

K.N.C.U. KATIKA SIKU ZIJAZO

Katika siku zijazo chama hiki kitakuwa na uwezo wa kusaidia nchi ya Kilimanjaro kwa njia nyingi kama kikiendelea vizuri. Chama hiki kitailea nchi ya Kilimanjaro mpaka imestarabika kama nchi za Ulaya na Amerika. Nchi hizo zimekua na kuifikia ngazi hiyo baada ya kufanya kazi ngumu kwa jasho kwa miaka mingi. Ustaarabu wa nchi ni kitu kinachochukua muda mrefu kukua. Basi ni juu ya Wachagga wawe na uvumilivu, "haraka haraka haina baraka." Wachagga wanapovumilia namna hiyo ni lazima wawe na uwezo na kuona mbele sana ili wajue siku fulani watafika mahali fulani, ijapokuwa itawachukua muda kuufikia mwisho wa safari hiyo. Watumishi wa chama ni lazima waonyeshe wazi upendo wao wa nchi nzima. Ni lazima Wachagga wote wajibidishe na kupenda nchi yao iendelee. Ni lazima watumishi wa chama waondoe mashaka mioyoni mwa watu kuwa wanazipendelea sehemu fulani za nchi.

Chama hakiwezi kuwa na watumishi ambao hawajaendelea na elimu ya kutosha; ni lazima watumishi hawa wawe na elimu ya juu. Ni lazima wawe watu wapendao ukweli mtupu; watu waaminifu; watu wenye roho ngumu; watu waonao maendeleo ya mbele ya nchi; na zaidi ya yote watu walio na uwezo wa kuona na kuelewa roho za Wachagga na fikira zao ili msaada watakaotoa uwe ule unaotakiwa. Ni lazima wawe watu wapendao chama na nchi kwa maneno na matendo. Hivi ni vitu vigumu na vya lazima ikiwa kila mtumishi ataweza kukisaidia chama ili kiongoze nchi siku za mbele. Watumishi hawa ni kama nguzo za nyumba zenye nguvu, na nguzo zikiingiliwa na mchwa lazima nyumba itaanguka. Hakuna hata Mchagga mmoja anayetaka nchi ianguke; kwa hiyo ni wajibu wa kila Mchagga kufanya kama awezavyo ili nchi iendelee mbele.

Mpaka sasa chama kimekusanya fedha fulani za elimu ya juu. Mwaka 1948 Wachagga wawili walipelekwa Ulaya kujifunza biashara. Mwaka 1949 Wachagga wanne walikwenda tena Ulaya. Hii ni faida kubwa ya nchi ya Kilimanjaro. Bila shaka njia nzuri ya kuzitumia fedha hizo ni kuwaelimisha kwanza watumishi wa chama; na baadaye wanachama. Huko mbeleni itakuwa vizuri zaidi kupeleka Ulaya Wachagga ambao wataweza kufaidia elimu ya juu, yaani wale waliomaliza masomo yao kule Makerere College. Hawa ndio watu watakaopata faida ya kutosha kutoka katika fedha zitakazotumika kwa elimu yao kwa sababu watakuwa na msingi wa elimu. Wanaweza kupelekwa watu wachache waliofanya kazi nzuri ili waongeze elimu yao, lakini wengi wao ni lazima wawe wale waliotoka Makerere. Vile vile itakuwa vizuri wachaguliwe watu wafanyao kazi mbalimbali, kazi ya uganga kwa wanadamu na ng'ombe, elimu, utawala, na biashara.

Kitu ambacho chama hiki hakijafanya ni kutoa fedha za kujenga nyumba za dawa na za shule. Haya ni mambo yanayotakiwa sana katika nchi. Wako watoto wengi wasiokwenda shule kwa kukosa nafasi. Wengi hurudi nyumbani kuishi maisha ya kimaskini. Maisha ya siku zijazo yatakuwa ya taabu sana hasa kwa wale wasiokwenda shule. Ingekuwa vizuri kama chama kingetoa fedha za kujenga shule, halafu Wazungu wa dini na serikali washauriane juu ya walimu na vyombo vya shule.

Nyumba za dawa nazo ni chache. Katika Kilimanjaro nzima iko hospitali moja tu kubwa ya serikali, ile ya Moshi. Ziko nyingine ndogo ndogo lakini hazifai watu kwa magonjwa makubwa. Watu wengi hufa ambao kama wangechukuliwa hospitalini kabla magonjwa hayajazidi wangepona. Nyumba za kuzalisha watoto ni chache sana. Watoto wengi wazaliwao hufariki kwa kuwa mama zao hawapati nyumba za wazazi ambapo wangetunzwa kabla ya uzazi. Chama kingeweza kujenga nyumba halafu serikali iombwe msaada ambao chama hakiwezi kutoa.

Katika Kilimanjaro viko vyama vingine vidogo vilivyoanzishwa na kusaidiwa na Chama Kikuu. Kiko chama cha biashara, chama cha watu walio na motokaa, chama cha wa kulima wa vitunguu na chama cha watu wenye kununua na kuuza ng'ombe wazima. General Chagga Trading Company ni chama kilichoanzishwa na wafanyabiashara wa viduka vya rejareja mwaka 1946. Kusudi lao ni kuuza na kununua vitu kwa jumla na kwa wingi. Kila Mchagga ni lazima ajue kuwa nchi nzima hupata faida kwa njia mbalimbali zinazosaidiwa na Chama Kikuu. Basi ni vizuri siku zijazo fedha ziwekwe kando kwa kusaidia vyama vidogo vya namna hii Ikiwa Chama Kikuu kimekubali kutoa msaada ni lazima kione kuwa Chama hicho kitafaa nchi, na kitengeneze njia maalum za kuzitunza fedha zake. Nchi itarudi nyuma ikiwa fedha za chama kidogo zitapotezwa na watumishi wabaya.

Mwangalizi wa K.N.C.U. siku hizi ni Mchagga. Ni lazima Wachagga wote wamshukuru sana Bwana A. I. B. Bennett ambaye alikuwa kiongozi wa chama kwa miaka kumi na tatu na nusu chini ya halmashauri ya K.N.C.U. Chama kimeweza kushinda taabu na shida nyingi zilizotokea miaka iliyopita kwa ajili ya uongozi mwema wake.

Bwana Bennett sasa ni msimamizi wa chama kingine kidogo kiitwacho Moshi Native Coffee Board. Kazi ya chama hiki ambacho kina Wachagga pia ni kutoa msaada wa namna yo yote kwa K.N.C.U. Chama hiki ni kama mdomo wa serikali na wanachama. Mpaka sasa kimekwisha fanya kazi ya kulea miche ya kahawa na kuwagawia wanachama. Kimejenga mabomba mpaka Rombo ya Kilimanjaro ili wenyeji wapate maji ambayo yalikuwa shida sana kupatikana. Leo maji ni mengi katika sehemu hii na hupatikana kwa urahisi ijapokuwa mapesa mengi yalitumika kwa kazi hii. Shule ya kufundisha watu kuangalia mashamba ya kahawa ya Wachagga imejengwa kule Lyamungo. Inatumainiwa kuwa chama kitaweza kufanya kazi nyingi zaidi za manufaa kwa nchi.
 
View attachment 2519831

Nikiri kwamba sijasoma bandiko lako lote lakini kila nikienda Moshi hupendelea kutembelea mgahawa wa KNCU pale katikati ya mji ! Kuna wazee wana story za zamani tamu hatari !!
 
KNCU ndo iliyimpeleka hayati Reginald Mengi kusoma Scotland na impact yake ni uanzishaji wa bonitte bottlers ambayo inaajiri wachaga wengi. hakika hawa jamaa walipiga step mbali sana nahisi Kilimanjaro ndo mkoa wenye lami mpaka vijijini tangu zamani sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom