Jinsi Kampuni za Simu zinavyowaibia wateja wao!

Ahsante Mkuu kwa kutupa taarifa. Kumbe nilikuwa sahihi kutojiunga kwenye promosheni zao. Ila Mkuu umelea tatizo muda mrefu. Ungetutonya mapema. Miaka kumi mingi sana watanzania tumeumizwa.
Asingeweza kufanya hivyo wakati yupo kibaruani alikuwa kwenye system. Alikuwa anamtumikia kafiri ili apate mradi wake baada kuondoka hana cha kupoteza tena
 
Wakuu napenda kuwakumbusha kuwa kuna wizi mpya unaofanywa na kampuni ya vodacom kupitia matumizi ya facebook bila malipo. Hawa watu ni waongo wa kutupwa....hakuna kitu kama hicho...ukifungua facebook isiyokuwa na picha unaliwa fedha kama kawaida. Naomba TCRA muingilie kati wizi huu.
 
Sio simu tu, huduma zote tunanyonywa... Hospital za serikali unambiwa ulete vifaa vya kujifungulia, vya kazi gani sasa wakati huduma bure na tena hapo hapo nesi anaweza ajakwambia yeye anavyo ununue kwake... Anamnunia mgonjwa hadi apewe hela atamuhudumia vizuri hadi ushangae... Si ni tunanyonywa mwanzo mwisho
 
Mimi sina hamu na vodacom , nakumbuka juzi kati kipindi wananidai 1450 ya nipige tafu nikabofya *149*42# ili nijiunge na bando la mb 500 kwa sh 500 kwa wiki nikaweka pesa m pesa kila nikitaka kununua naambiwa mchakato umezuiliwa ile napiga huduma kwa wateja muhudumu wa voda ananiambia heti huwezi kununua bando hili kwa m pesa (kumbuka hapo wananidai ) nikaona isiwe tabu nikanunua jumla vocha ya 2000 ile naweka tu majamaa yakakata 1450 hapo hapo nikabakiwa na 550 haya nikajaribu tena kujiunga naambiwa huduma hii haipatikani kwa sasa jaribu tena baadae, nikapiga huduma kwa wateja kakapokea kamdada flan nikakauliza mbona kila nikijaribu kujinga na bando la net la wiki kwa 500 sifanikiwi naambiwa huduma hii haipatikani kwa sasa ,
Kakanijibu "SASA WEWE UMEAMBIWA HUDUMA HII HAIPATIKANI KWA SASA UNATAKA NIKWAMBIE NINI ZAIDI?"
Kumbuka hapo nimeshaingia mkenge nimelipa deni lao lote la nipige tafu , nikaona isiwe inshu nikakata simu,
BALAA likaja nilipoingia katika kuperuzi tovuti za bure kwenye www.internet.org mzee nikafungua facebook ya bila malipo kama dakika 1 nikatoka nikaenda goal dot com kuangalia matokeo kama sekunde 50 hivi ile nakuja kuangalia salio nakuta limebaki 508 majamaa yameshakula sh 42 wakati yananadi tovuti yoyote inayopatikana kwenye internet.org ni ya bure kumbe ukiwa na salio yanang'amua salio kimya kimya ,
Nikaona huu ni upuuzi huu nikanunua tu bando la siku la internet napo nashangaa napewa mb 70 kwa tsh 500 wakati halotel mb 120 ni 499 aisee kwa kifupi VODACOM TANZANIA ni mafisadi sugu .
 
Nimefanya kazi kwenye kampuni mbali mbali za simu hapa nchini kwa muda wa zaidi ya miaka 10, kabla ya kuamua kujiajiri mwenyewe. Katika muda wote huo nimeshuhudia kampuni hizi zikiwaibia wateja kwa namna mbalimbali.

Nimekaa na huu ushahidi kwa muda sasa lakini naona roho inanisukuma niuanike hadharani mbele za watanzania ili wafunguke macho na kufahamu UFISADI huu unaofanywa na kampuni za simu hapa nchini. Nitaanika wizi wote kadri nitakavyoweza kuukumbuka hapa:

Huduma za bure.

Kuna hizi huduma ambazo wanaziita huduma za "BURE" kana kwamba zinapatikana bure wakati si kweli! Kwa mfano, wateja hutumiwa SMS zinazowadanganya kwamba wanaweza kupata huduma za bure na ili wazipate wanaelekezwa kutuma ujumbe kwenda kwenye namba fulani.

Na mteja akisharogwa akatuma ujumbe kwenda kwenye namba husika, imekula kwake! Nyingi ya huduma hizi zinazoitwa za bure hugharimu fedha na mara ujiungapo hujikuta unakatwa salio lako kimya kimya.

Ni mara nyingi mtakuwa mmewahi kusikia mtu akilalamika kwamba salio lake limepungua&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];.unaweka airtime ya Tsh 1000 leo bila kuitumia, ikifika kesho unakuta zimebaki sh 350! Tsh 650 zimeenda wapi? Zimekatwa kwenye zile huduma za "BURE" ulizotangaziwa.

Promosheni feki.

Promosheni nyingi zinazoanzishwa na makampuni ya simu zinalenga kuwanyonya na kuwakandamzia wateja. Mfano halisi ni pale wateja wanapotangaziwa kwamba huduma ya FESIBUKU inapatika bure! Thubutuuu! Hakuna kitu cha bure nchi hii, ndugu yangu.

Huu ni wizi wa mchana! Kupona kwako ni pale utakapotumia hiyo huduma ukiwa hauna salio kwa kuwa huwezi kupata access ya huduma husika (kama vile fesibuku, twita, nk).

Ikiwa utafungua huduma hiyo ukiwa na salio, salio lako lote litakombwa sawia! Kuna mtandao mmoja wa simu unajinadi kwamba unatoa huduma ya fesibuku bure wakati ni uongo mtupu. Ingia kwenye hiyo fesibuku uone utakavyoliwa fedha! Aidha kuna mtandao mmoja uliwahi kuwa na fesibuku ya bure siku za nyuma (kama mtakumbuka).

Kwa muda fulani huduma hii ilikuwa ikipatikana bure kabisa. Kumbe ilikuwa ni janja ya nyani&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];..baadaye ile "bure" ilifutwa kimya kimya, wateja wakaendelea kukamuliwa kama kawaida na mpaka leo hawajawahi kuwataarifu wateja wao kwamba hiyo "bure" imesitishwa! Kuna wateja wengi sana, hasa wa kule vijijini, ambao wanaendelea kukamuliwa kwa kujidanganya kwamba huduma ni ya bure hadi leo, kumbe ilishasitishwa kitambo sana!

Ulaghai wa Kimangungo.

Kuna wakati ambapo makampuni ya simu hupandisha tariffs kimya kimya bila kuwataarifu wateja wake na kuendelea kuwaibia bila kujua.

Mwaka 2006 gharama za kupiga simu, kutuma sms na kutumia data zilipandishwa kinyemela na wateja wakaendelea kukamuliwa fedha kimya kimya hadi pale baadhi yao waliposhtukia dili na kuja juu. Aidha, prosheni fulani zinapoanzishwa, kama vile punguzo la gharama za kupiga simu nyakati za usiku, pindi zinafikia tamati wateja hawapewi taarifa na kujikuta wakitumia fedha zaidi ya matarajio yao.

Promosheni inapoisha kampuni hizi huwakataza wafanyakazi wake wasiwaambie wateja ili waendelee kukamuliwa fedha kilaghai. Huu ni wizi, tena wa mchana na hauna tofauti na ufisadi wowote ule.

Kutotoa taarifa kwa wateja kwa makusudi.

Wateja wanapojiunga kwenye vifurushi mbalimabli huletewa taarifa immediately via SMS kwamba wamefanikiwa kujiunga lakini kifurushi kikiisha ama wateja huchelewa kutumiwa meseji ya taarifa au hawatumiwi kabisa. Hili tatizo huwakumba zaidi wale wateja wanaopenda kubaki na salio kubwa kwenye simu zao.

Kwa mfano, mtu unanunua vocha ya Tsh 2000 kisha unanunua kifurushi cha Tsh 500 na kubakiwa na Tsh 1500 kwenye simu. Pindi kifurushi cha 500 kikiisha hutatumiwa ujumbe wowote hadi utapokuwa umekausha 1500 zilizosalia kwenye simu.

Huu pia ni wizi wa mchana na unaofanywa kwa makusudi na kampuni za simu hapa nchini. Ninao ushahidi usiokuwa na mashaka katika huu wizi wa makusudi.

Njia nyingine inayotumika kuiba hapa ni kutotoa call details pindi upigapo simu. Ukimaliza kupiga simu ukiangalia call details unakuta inasoma 00:00:00! Details hizi zinafichwa kwa makusudi ili kujenga mazingira ya wizi.

Kwa mfano mtu unaongea kwa dakika 3, wao wanakata dakika 4.30 na kukuibia dakika 1.30! Matokeo yake unakuta muda wa hewani uliopewa wakati wa kujiunga umeibiwa na kampuni kwa maslahi yake binafsi. Lakini pia kuna wizi mwingine huu hapa: &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG];

unaponunua kifurushi hupewa dakika ambazo ungetegemea zitozwe kwa sekunde (per second billing) lakini badala yake hutozwa kwa dakika (per minute billing) kinyume cha mkataba kwa lengo la kumkamua mteja kiujanja. Huu ni wizi na haukubaliki hata kidogo.

Kuvuruga mawasiliano kwa makusudi.

Kuna wakati wahandisi wa kampuni husika hupewa jukumu la kuvuruga mawasiliano ya wateja ili watumie muda mwingi na pesa nyingi kwenye maongezi. Inakuwaje hapa? Inakuwa hivi: Ukimpigia mtu yeye anakuwa anakusikia lakini wewe humsikii au vice versa.

Hii husababisha kutumia muda mwingi kuelewana wakati huo salio likinyonywa kama kawaida &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hata kama mkichukua muda mwingi kuelewana salio hutafunwa sawia! Njia nyingine inayotumika hapa ni kuvuruga access to customer care ili unapokuwa umepatwa na tatizo usiweze kuwafikia watu wa huduma kwa wateja kupata msaada.

Hii ndio sababu 90% ya wateja wenye matatizo genuine hawaipati namba 100. Mtu unaweza kupiga siku nzima na usiunganishwe kuongea na mshauri. Hatimaye wengi wao hukata tamaa na kuamua kukubali "kuliwa"!

Hii ni sehemu ya ushahidi ambao nimeukusanya while working with different mobile companies in Tanzania. Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Nawasilisha.
nitarudi baadae kuchangia
 
Mimi sina hamu na vodacom , nakumbuka juzi kati kipindi wananidai 1450 ya nipige tafu nikabofya *149*42# ili nijiunge na bando la mb 500 kwa sh 500 kwa wiki nikaweka pesa m pesa kila nikitaka kununua naambiwa mchakato umezuiliwa ile napiga huduma kwa wateja muhudumu wa voda ananiambia heti huwezi kununua bando hili kwa m pesa (kumbuka hapo wananidai ) nikaona isiwe tabu nikanunua jumla vocha ya 2000 ile naweka tu majamaa yakakata 1450 hapo hapo nikabakiwa na 550 haya nikajaribu tena kujiunga naambiwa huduma hii haipatikani kwa sasa jaribu tena baadae, nikapiga huduma kwa wateja kakapokea kamdada flan nikakauliza mbona kila nikijaribu kujinga na bando la net la wiki kwa 500 sifanikiwi naambiwa huduma hii haipatikani kwa sasa ,
Kakanijibu "SASA WEWE UMEAMBIWA HUDUMA HII HAIPATIKANI KWA SASA UNATAKA NIKWAMBIE NINI ZAIDI?"
Kumbuka hapo nimeshaingia mkenge nimelipa deni lao lote la nipige tafu , nikaona isiwe inshu nikakata simu,
BALAA likaja nilipoingia katika kuperuzi tovuti za bure kwenye www.internet.org mzee nikafungua facebook ya bila malipo kama dakika 1 nikatoka nikaenda goal dot com kuangalia matokeo kama sekunde 50 hivi ile nakuja kuangalia salio nakuta limebaki 508 majamaa yameshakula sh 42 wakati yananadi tovuti yoyote inayopatikana kwenye internet.org ni ya bure kumbe ukiwa na salio yanang'amua salio kimya kimya ,
Nikaona huu ni upuuzi huu nikanunua tu bando la siku la internet napo nashangaa napewa mb 70 kwa tsh 500 wakati halotel mb 120 ni 499 aisee kwa kifupi VODACOM TANZANIA ni mafisadi sugu .
Mkuu kumbe nawe umeishaibiwa mno na hawa makaburu? Mimi niliwashtukia kitambo sana. Ule ujinga wanaonadi eti facebook isiyokuwa na picha inapatikana bure ni WIZI mtupu. Ukitaka kuprove hili ingia ukiwa na salio la Tsh 0 uone.....huwezi kupata hiyo huduma hadi uongeze salio. Hii maana yake ni nini? Ina maana huduma hii sio ya bure kama wanavyodai...ni utapeli wa kimataifa. Nashangaa hata TCRA wameamua kutuacha tuibiwe kijinga hivi bila kuwachukulia hatua hawa matapeli. Wako busy kukamata watu wanaopost maoni yao dhidi ya mafisadi huku wakituacha wananchi tunaibiwa kila kukicha.
 
Watanzania karibu wote viongozi mbaka wananchi wanalalamika tu,tumegeuka walalamikaji katika nchi yetu
Nini kifanyike:
Kama ushahidi upo namna tunavyo ibiwa sisi kama watumiaji wa hii mitandao tuanze sasa kuchukua hatua
Wanafamilia wa JF kwa umoja wetu tukusanye sahini za wadau wetu wote,tuandikie majina yetu pamoja na namba zetu za simu tumtafute wakili nguli twendeni mahakamani tukafungue mashtaka ya kuibiwa mchana kweupe na haya makampuni ya simu,na endapo sisi kama watanzania hatuna huo ushahidi wa kuibiwa basi tuache kulishana Matango pori
Tuanze sasa kuchukua hatua tuache kulalamika bila sababu..
 
Mkuu kumbe nawe umeishaibiwa mno na hawa makaburu? Mimi niliwashtukia kitambo sana. Ule ujinga wanaonadi eti facebook isiyokuwa na picha inapatikana bure ni WIZI mtupu. Ukitaka kuprove hili ingia ukiwa na salio la Tsh 0 uone.....huwezi kupata hiyo huduma hadi uongeze salio. Hii maana yake ni nini? Ina maana huduma hii sio ya bure kama wanavyodai...ni utapeli wa kimataifa. Nashangaa hata TCRA wameamua kutuacha tuibiwe kijinga hivi bila kuwachukulia hatua hawa matapeli. Wako busy kukamata watu wanaopost maoni yao dhidi ya mafisadi huku wakituacha wananchi tunaibiwa kila kukicha.
tpaul hapa ni shida tupu ndugu yangu mi bora nibaki halotel tu.
 
Asante sana mleta mada. Pia kuna wizi mwingine - nazungumzia Vodacom. Ukijiunga mitandao yote kiasi cha dakika utakachopata hakifikii hata nusu ya dakika za Vodacom-Vodacom. Kwa shilingi 1,000 mitandao yote unapata dakika 22 tu wakati kwenye vodacom-vodacom unapata dakika 50 na dakika 5 mitandao yote (kifurushi cha siku).

Lakini sasa, ukinunua muda wa maongezi kwa mitandao yote ya shilingi 1,000 wakati tayari ulikuwa umeshajiunga kwenye vodacom -vodacom kwa shilingi 1,000 pia, wizi unaanzia hapo. Ukipiga simu kwenye mtandao mwingine ukatumia dakika 7, kwenye salio la mitandao yote unabakia na dakika 15, na kwenye voda-voda unabakia na zile dakika 50. Simu inayofuata ukipiga voda-voda kwa dakika 15, badala ya kupunguza hicho kiasi kwenye dakika 50 za voda-voda, wanakata dakika zote 15 kwenye lile salio la mitandao ingine ambalo ulinunua kwa bei ghali. Wanakutumia ujumbe saa hiyo hiyo kwamba muda wako wa maongezi kwenye mitandao yote umeisha ilhali ulikuwa umepiga voda-voda na sio mtandao mwingine. Huu ni wizi mkubwa. Nadhani hao wafanyakazi wa Vodacom (labda wanashirikiana na wa TCRA) bila shaka ndio wanahusika na wizi huo. Jamani tunawaomba wakurugenzi wa Vodacom na TCRA mliangalie hili !
 
Back
Top Bottom