SoC03 Jinsi furaha yangu ilivyopotea

Stories of Change - 2023 Competition

Yese Kajange

New Member
Oct 24, 2018
4
12
Ilikuwa ni usiku wa tarehe 30/3/2022. Muda wa saa 4:15 usiku ambapo mke wangu alipata uchungu na alikuwa tayari kwa ajili ya kujifungua. Usiku huo ulikuwa ni usiku usiosaulika katika maisha yangu kutokana na misukosuko mingi sana ambapo tulikutana na changamoto nyingi. Changamoto nyingine tuliweza kuzitatua na nyingine zilishindikana mpaka zikapelekea kifo kwa mama mjamzito pamoja na mtoto aliekuwa tumboni.

Changamoto zilianza pale ambapo kwa muda ule mvua zilikuwa zinanyesha na hakukuwa na uwezekano wa kuondoka kwa muda huo kwasababu ya barabara za kijijini kwetu zilikuwa ni mbovu na ilikuwa ni ngumu kupitika kama mvua imenyesha na usafiri ambao tulikuwa tunautegemea ni pikipiki ambayo ilikuwa inatakiwa kutufikisha mtoni ili tuweze kuvushwa na mtumbwi ili kufika ng'ambo ya pili ya kijiji cha jirani ambacho ndio kulikuwa na kituo cha afya.

Safari yetu mimi na mke wangu ilianza muda wa saa 3:06 usiku ambapo tuliongozana na mama mzazi wa mke wangu. Ilituchukua muda wa saa moja na nusu mpaka kufika kwenye mto ambao ndio ulikuwa ukituvusha kwenda kwenye kituo cha afya. Tulichelewa kufika mtoni kwasababu barabara tuliyopita ilikuwa na utelezi uliomfanya dereva aende mwendo wa taratibu.

Tulifika mtoni ambapo ndio tulipanda mtumbwi kwaajili ya kuanza safari ya kwenda kwenye kituo cha afya. Muda wawa saa 9:15 ndio tulifika kwenye kituo cha afya na kupokelewa na nesi aliekuwa zamu kwa muda ule wa usiku.

Baada ya yule nesi kutupokea alitupa kitanda ambacho ndio alilala mke wangu huku akiwa anapitia maumivu makali ya uchungu lakini kitu kibaya zaidi damu nyingi zilikuwa zikimtoka. "daktari hayupo na kituo chao cha afya kina daktari mmoja ambaye yupo nyumbani kwake na umbali kutoka kwenye kituo cha afya mpaka nyumbani kwake ilikuwa ni 2km na kwenye mawasiliano hapatikani" hayo ndio yalikuwa maneno ya yule nesi. Maneno yale yalizidi kunichanganya huku nikiangalia hali ya mke wangu ndio ilizidi kuwa mbaya.

Tuliendelea kumsubiri daktari mpaka ilipofika muda wa saa kumi kasoro dakika saba (9:53). Daktari alipofika tulimbeba mke wangu mpaka kwenye chumba cha kujifungulia lakini baada ya muda daktari alitoka na kuniita pembeni tulijadili kwa muda kidogo lakini maneno alioniambia mwili uliniisha nguvu. " mke wako anatakiwa kufanyiwa kufanyiwa upasuaji na katika kituo chetu cha afya huduma ya upasuaji atuwezi kwasababu ya ukosefu wa vitendea kazi,umeme aupo na jenereta halina mafuta,ukosefu wa madaktari bingwa pamoja na uhaba wa wafanyakazi.

Kutokana na haya inabidi uchangie pesa ya mafuta ili mke wako apelekwe kwenye hospitali ya wilaya. Pia gari iyo itafika hapa saa 11:30 alfajili". Hayo ndio yalikuwa maneno alioniambia yule daktari wa ile zahanati ya kijiji cha pili na umbali kutoka kwenye kile kijiji mpaka hospitali ya wilaya ni 10km. Kweli baada ya kufika saa 11:30 gari la wagonjwa lilifika kutoka wilayani ambapo lilimbeba mke wangu ili limuwaishe kwenye hospitali ya wilaya.

Safari ilianza ya kwenda kwenye hospitali ya wilaya huku mimi na mama yake (mama mkwe) tukiwa tunamfuata kwa nyuma kwa kutumia usafiri wa bodaboda. Baada ya muda muda kidogo tulifika kwenye hospitali ya wilaya ambapo tulikuka wahudumu wa pale wameshampokea na tayari wameshaanza kumpatia huduma.

Ama kweli huduma za pale mjini ni tofauti sana na za kule kijijini kwetu. Miundombinu ya kwenye hospitali ya wilaya ilikuwa bora sana kulikuwa hakuna uhaba wa wafanyakazi wala witendea kazi kama kule kijijini kwetu.

Lakini kisicho ridhiki hakiliki madaktari walitoka kwenye chumba cha upasuaji huku sura zao zikiwa hazina furaha. Hata mimi na mama mkwe tulistuka. Kiongozi wa lile jopo la madaktari aliniita pembeni " kijana wewe ndio muhusika wa huyu mama mjamzito aliekuwa kwenye chumba cha upasuaji" nilimjibu "ndio ni mimi daktari" aliniambia nifuate ofisini kwangu. Nikamfuata yule daktari kwenye ofisi yake kisha tukaanza mazungumzo "pole sana kijana kwa hii taarifa. Mimi na jopo langu la madaktari tumejitahidi kwa uwezo wetu imeshindikana.

Tumeshindwa kumuokoa mama pamoja na mtoto kutokana na mama alipoteza damu nyingi sana ambazo ndio zilipelekea kuwapoteza wote wawili. Pole sana ndugu yangu". Hayo yalikuwa maneno ya yule daktari ambae tulimkuta kwenye hospitali ya wilaya. Nguvu ziliniisha huku machozi yalianza kunitoka taratibu nilitamani nipige kelele lakini ilishindikana kwasababu nilikuwa kwenye ofisi ya daktari.

Nilimpoteza mke na mtoto wangu kwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile;
- ubovu wa miundombinu kama barabara (rami) pamoja na madaraja (kwenye mito).
- umbali wa kituo cha afya; kwa mfano umbali wa kutoka kijijini mpaka hospitali ni kama 12km.
- watumishi wa afya kukaa mbali na maeneo ya kazi kutokana na ukosefu wa huduma za kijamii kama maji na umeme.
- uhaba wa madaktari bingwa pamoja na wafanyakazi katika sekta ya afya.

Hayo ndo mambo yaliyopelekea kifo cha mama (mke) pamoja na mtoto wangu. Ilipofika kesho yake tulikabidhiwa mwili kwa ajili ya kuendelea na shughuli ya mazishi. Tukaanza safari ya kurudi kijijini kwetu tukiwa tumetokea kwenye hospitali ya wilaya. Tulivyofika kijijini tulimpunzisha mke na huo ndio ukawa mwisho wangu na mwanamke niliempenda.

Ombi langu kwa serikali ni kujitahidi kuwafikia wananchi walio kwenye maeneo mbalimbali ambapo huduma za kijamii azipatikani.
 
Pole kwa Kipoteza familia. Nchi yetu inakumbwa na changamoto nyingi.
Kwa upande wako ulishawahi kuhudhuria kiliniki hata mara moja? Kuna kitu chaitwa individual birth plan preparation ulipaswa ufanye hiyo mapema na ingesaidia sana mkeo kujifungua salama
 
Pole sana mkuu kwa mapito uliyopitia, pole pia kupoteza wapendwa wako.
 
Ilikuwa ni usiku wa tarehe 30/3/2022. Muda wa saa 4:15 usiku ambapo mke wangu alipata uchungu na alikuwa tayari kwa ajili ya kujifungua. Usiku huo ulikuwa ni usiku usiosaulika katika maisha yangu kutokana na misukosuko mingi sana ambapo tulikutana na changamoto nyingi. Changamoto nyingine tuliweza kuzitatua na nyingine zilishindikana mpaka zikapelekea kifo kwa mama mjamzito pamoja na mtoto aliekuwa tumboni. Changamoto zilianza pale ambapo kwa muda ule mvua zilikuwa zinanyesha na hakukuwa na uwezekano wa kuondoka kwa muda huo kwasababu ya barabara za kijijini kwetu zilikuwa ni mbovu na ilikuwa ni ngumu kupitika kama mvua imenyesha na usafiri ambao tulikuwa tunautegemea ni pikipiki ambayo ilikuwa inatakiwa kutufikisha mtoni ili tuweze kuvushwa na mtumbwi ili kufika ng'ambo ya pili ya kijiji cha jirani ambacho ndio kulikuwa na kituo cha afya.

Safari yetu mimi na mke wangu ilianza muda wa saa 3:06 usiku ambapo tuliongozana na mama mzazi wa mke wangu. Ilituchukua muda wa saa moja na nusu mpaka kufika kwenye mto ambao ndio ulikuwa ukituvusha kwenda kwenye kituo cha afya. Tulichelewa kufika mtoni kwasababu barabara tuliyopita ilikuwa na utelezi uliomfanya dereva aende mwendo wa taratibu. Tulifika mtoni ambapo ndio tulipanda mtumbwi kwaajili ya kuanza safari ya kwenda kwenye kituo cha afya. Muda wawa saa 9:15 ndio tulifika kwenye kituo cha afya na kupokelewa na nesi aliekuwa zamu kwa muda ule wa usiku. Baada ya yule nesi kutupokea alitupa kitanda ambacho ndio alilala mke wangu huku akiwa anapitia maumivu makali ya uchungu lakini kitu kibaya zaidi damu nyingi zilikuwa zikimtoka. "daktari hayupo na kituo chao cha afya kina daktari mmoja ambaye yupo nyumbani kwake na umbali kutoka kwenye kituo cha afya mpaka nyumbani kwake ilikuwa ni 2km na kwenye mawasiliano hapatikani" hayo ndio yalikuwa maneno ya yule nesi. Maneno yale yalizidi kunichanganya huku nikiangalia hali ya mke wangu ndio ilizidi kuwa mbaya. Tuliendelea kumsubiri daktari mpaka ilipofika muda wa saa kumi kasoro dakika saba (9:53). Daktari alipofika tulimbeba mke wangu mpaka kwenye chumba cha kujifungulia lakini baada ya muda daktari alitoka na kuniita pembeni tulijadili kwa muda kidogo lakini maneno alioniambia mwili uliniisha nguvu. " mke wako anatakiwa kufanyiwa kufanyiwa upasuaji na katika kituo chetu cha afya huduma ya upasuaji atuwezi kwasababu ya ukosefu wa vitendea kazi,umeme aupo na jenereta halina mafuta,ukosefu wa madaktari bingwa pamoja na uhaba wa wafanyakazi. Kutokana na haya inabidi uchangie pesa ya mafuta ili mke wako apelekwe kwenye hospitali ya wilaya. Pia gari iyo itafika hapa saa 11:30 alfajili". Hayo ndio yalikuwa maneno alioniambia yule daktari wa ile zahanati ya kijiji cha pili na umbali kutoka kwenye kile kijiji mpaka hospitali ya wilaya ni 10km. Kweli baada ya kufika saa 11:30 gari la wagonjwa lilifika kutoka wilayani ambapo lilimbeba mke wangu ili limuwaishe kwenye hospitali ya wilaya.

Safari ilianza ya kwenda kwenye hospitali ya wilaya huku mimi na mama yake (mama mkwe) tukiwa tunamfuata kwa nyuma kwa kutumia usafiri wa bodaboda. Baada ya muda muda kidogo tulifika kwenye hospitali ya wilaya ambapo tulikuka wahudumu wa pale wameshampokea na tayari wameshaanza kumpatia huduma. Ama kweli huduma za pale mjini ni tofauti sana na za kule kijijini kwetu. Miundombinu ya kwenye hospitali ya wilaya ilikuwa bora sana kulikuwa hakuna uhaba wa wafanyakazi wala witendea kazi kama kule kijijini kwetu. Lakini kisicho ridhiki hakiliki madaktari walitoka kwenye chumba cha upasuaji huku sura zao zikiwa hazina furaha. Hata mimi na mama mkwe tulistuka. Kiongozi wa lile jopo la madaktari aliniita pembeni " kijana wewe ndio muhusika wa huyu mama mjamzito aliekuwa kwenye chumba cha upasuaji" nilimjibu "ndio ni mimi daktari" aliniambia nifuate ofisini kwangu. Nikamfuata yule daktari kwenye ofisi yake kisha tukaanza mazungumzo "pole sana kijana kwa hii taarifa. Mimi na jopo langu la madaktari tumejitahidi kwa uwezo wetu imeshindikana. Tumeshindwa kumuokoa mama pamoja na mtoto kutokana na mama alipoteza damu nyingi sana ambazo ndio zilipelekea kuwapoteza wote wawili. Pole sana ndugu yangu". Hayo yalikuwa maneno ya yule daktari ambae tulimkuta kwenye hospitali ya wilaya. Nguvu ziliniisha huku machozi yalianza kunitoka taratibu nilitamani nipige kelele lakini ilishindikana kwasababu nilikuwa kwenye ofisi ya daktari.

Nilimpoteza mke na mtoto wangu kwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile;
- ubovu wa miundombinu kama barabara (rami) pamoja na madaraja (kwenye mito).
- umbali wa kituo cha afya; kwa mfano umbali wa kutoka kijijini mpaka hospitali ni kama 12km.
- watumishi wa afya kukaa mbali na maeneo ya kazi kutokana na ukosefu wa huduma za kijamii kama maji na umeme.
- uhaba wa madaktari bingwa pamoja na wafanyakazi katika sekta ya afya.

Hayo ndo mambo yaliyopelekea kifo cha mama (mke) pamoja na mtoto wangu. Ilipofika kesho yake tulikabidhiwa mwili kwa ajili ya kuendelea na shughuli ya mazishi. Tukaanza safari ya kurudi kijijini kwetu tukiwa tumetokea kwenye hospitali ya wilaya. Tulivyofika kijijini tulimpunzisha mke na huo ndio ukawa mwisho wangu na mwanamke niliempenda.

Ombi langu kwa serikali ni kujitahidi kuwafikia wananchi walio kwenye maeneo mbalimbali ambapo huduma za kijamii azipatikani.
Pole sana mkuu ndio maana mabinti wa siku hizi wanaprefer Kisu kuliko kusubiri uchungi.

Anafuatilia siku za matarajio na kuweka appointment na Dk. Siku zikifika ni kisu (operations)
 
Back
Top Bottom