Jinsi Freeman Mbowe alivyofanyiwa umafia ndani ya nchi yake

Mbowe kasema aliwakuongea na Jpm kuhusu hilo la kukwapuliwa pesa na kubambikiziwa kodi with all in vain.

Itoshe tu kusema mzee baba alikuwa anafurahia wenzake wakiteseka.
Haujawahi kutokea hapa nchini aisee
 
Mungu kapiga penyewe haswaa! Ndiyo maana hata TANZIA nimeacha kuripoti maana yameshatimia!
Yani nipo likizo ya furaha!
Kismati cha kuitoa Chadema kutoka wabunge 100+ walioachwa na Dr Slaa hadi kubaki mbunge mmoja Joyce Mkuya??..
Hovyo kabisa kwa walamba viatu vya Mboe
 
Uchunguzi ufanyike
Inawezekana hata Magufuli hakuwa na details
Za yote yaliyo endelea chini yake
Binasfi nakataa kwani tuliaminishwa mambo ya uonevu, nidhamu ya watumishi na mengineyo yaliboreshwa , ndio maana naamini ilikuwa njia ya kuvuna mapato manene na adhabu wa wenye mawazo mbadala, kama njia kuwataka waunge juhudi.
 
Uchunguzi ufanyike
Inawezekana hata Magufuli hakuwa na details
Za yote yaliyo endelea chini yake
Yes, you are right...

Kama wana akili na nia njema, wafanye hivi...

Lakini kwa maelezo ya Freeman Mbowe Jana, alisema kuwa alifikishaga malalamiko yake kwa Rais Magufuli alipokuwa hai na jibu alilopewa ni;

"....nimesikia, nitashughulikia..."

Halikufanyika lolote, na baada ya siku kadhaa baadaye, akakoswakoswa kuuwawa usiku nyumbani kwake eneo la Area D, Dodoma na watu wasiojulikana...

Hii ni uthibitisho kuwa, Mwendazake Magufuli alikuwa anajua na pengine TRA walifanya yote haya kwa maelekezo yake...

Kwa maoni yangu, kama ni kufanyika uchunguzi uwe ni aidha kweli alikuwa anadaiwa kodi ya serikali au ni uongo bali vita ya kisiasa tu...

Ikigundulika ni uongo, TRA/serikali irejeshe fedha zote za mtu huyu ilizoiba (ndiyo, huu ni wizi) bila masharti yoyote ikiwemo kulipa na hasara iliyosababisha kwa biashara zake...
 
Kwa mwendo huu wa kuongezeka mihemuko,kuna siku itaamuliwa mfuniko wa tiles utandikwe fimbo za kutosha. Tuendelee na kazi zetu,yamepita
 
Rais Samia aliagiza waliofungiwa akaunti na TRA wafunguliwe. Jumanne 06 April 2021, TRA wakafungua akaunti zote za Mbowe, lakini hazina kitu. Kwenye akunti yake binafsi wamekomba zaidi ya 528M ambazo ni malimbikizo ya mshahara na kiinua mgongo chake cha ubunge. TRA wamekomba pia mamilioni ya shilingi kwenye akaunti za kampuni zake. Tayari Mbowe amemjulisha Mhe.Rais Samia kuhusu uharamia huo wa TRA

Kwa kweli Magufuli alikuwa anatupeleka shimoni. Na huu uharamia ulifanywa ndani ya ofisi ya mtu ambaye ni Vice President sasa...
 
Back
Top Bottom