Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Nikweli mkuu,naimani hii simulizi ya huyu jamaa imefanya tugande hapa lln kumbe kuna simulizii zingine au majukwaa mengine
Attention ina utamu wake acha ndugu yetu ajipakulie minyama. Kila akiscroll anakuta notifications kama buku, burudani kabisa.
 
Umepoa Uzi kwa wiki hii..

Kaboa kurudi kwa Asmah or so 🤮

Yaani hakupendi hajitambui huyu mleta mada.. nimerudi Leo naona bado.. haya malizia jinsi usivyo na heshima kwa wanawake wewe.. wanawake wote Duniani unakula hao hao bila kukuheshimu Bosi wako..

Uchafu mtupu.. hujiamini haujitambui kwenye mapenzi.. 😅😅😅 nicheke tu..

Malizia ukasome.. kila la kheri na masomo yako
 
Umepoa Uzi kwa wiki hii..

Kaboa kurudi kwa Asmah or so 🤮

Yaani hakupendi hajitambui huyu mleta mada.. nimerudi Leo naona bado.. haya malizia jinsi usivyo na heshima kwa wanawake wewe.. wanawake wote Duniani unakula hao hao bila kukuheshimu Bosi wako..

Uchafu mtupu.. hujiamini haujitambui kwenye mapenzi.. 😅😅😅 nicheke tu..

Malizia ukasome.. kila la kheri na masomo yako
Makasiriko ya nini tena😃
Hii ilikuwa based on true story huwezi jua kama ni kwel au la vyote vinavyozungumzwa
Mwandishi sometimes anaandika kutokana na hadhira yake inataka kusikia nini mara zote
 
Makasiriko ya nini tena😃
Hii ilikuwa based on true story huwezi jua kama ni kwel au la vyote vinavyozungumzwa
Mwandishi sometimes anaandika kutokana na hadhira yake inataka kusikia nini mara zote

Na mie no msomaji.. lolote naweza sema... Ameboa... Nawe huoni aibu kuandika uliyoandika ..
Nicheke Tu 😅😅😅
 
Kapatwa na nini mzee wa kismati cha bahasha za mamilioni?? Ni kweli amepata ajali au anaumwa kama members wanavyosema?? Mungu amjalie apate nafuu haraka ( kama ni kweli)
 
Kwa upande wangu hii Arosto na huu ukimya Mkuu unatupoteza kabisa ukizingatia na hii hali ya hewa hata wewe mleta uzi kwa upande wako tuangalie na sie kwa hili na hili na kwa upande wa Wajumbe wenzangu humu ndani
 
EPISODE 14

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

Nikamshukuru Iryn kwa out then nikawasha gari tuondoke tukalale, wakati tumevuka geti la Kidimbwi kuna gari ilikuja kwa spidi sana na ikatugonga “BOOM”. Ilisikika sauti ya Iryn “Mamaaaa…….”.

TUNAENDELEA…………….

Lilikua ni tukio la fasta sana ambalo lilitupa mshtuko kupelekea Iryn kutoa sauti ya nguvu. Jamaa alitugonga kwa nyuma na kwa spidi sana, palepale ilibidi nishuke na watu walikua wameanza kusogea pale kwa kasi.

Muda huu magari ndo yalikua yanaingia kwa kasi na kutoka, Uber ndo zilionekana kuwa busy sana hili eneo.

Eneo ambalo jama alitugonga ilikua ni kabla hujafika kwenye corner ya kwanza inayokata kushoto kama umetoka kidimbwi.

Baada ya kushuka niliangalia gari upande wa nyuma nikaona jamaa alikua amevunja bampa la nyuma, taa zote mbili za nyuma na sehemu ya nyuma ya boneti ilikua imebonyea.

Jamaa gari yake ilikua ni Prado zile za zamani ila ilikua na ngao mbele. Jamaa alikua bado hajashuka kwenye gari ikabidi nimgongee dirishani atokee nje, ili tuongee.

Baada ya kumgongea dirishani lakini jamaa hakutoka ni kama alikua na dharau, hichi kitendo kilizidi kunipa hasira sana. Na muda huo askari mgambo wanaolinda eneo hili walikua wameshafika eneo la tukio.

Kwa upande mwingine foleni ilizidi kuwa kubwa sana maana hakuna gari zilizokuwa zinatoka wala kuingia pale Kidimbwi. Na muda huo Iryn alikua kashatoka kwenye gari, akaja akanishika mkono.

Kwa tukio liliokuwa limetokea pale mwenye kosa alikua ni jamaa, maana yeye ndo alinigonga kwa nyuma, napia sheria ziko wazi hivyo hakukuwa na haja ya kumtafuta mchawi ni nani.

“Huyu fala anadharau sana, anamakosa ila hataki kutoka nje. Watu kama hawa ndo wakuwatia makofi”. Ilisika sauti ya dereva wa bodaboda aliyekuwa kwenye bodaboda yake.

Watu walizidi kumiminika hasahasa madereva wa magari walikua wamefika kuona nini tatizo, na wengi walikuwa wanapatwa na hasira kuona jamaa hataki kutoka kwenye gari.

Jama alikuwa na demu wake ambaye alikuwa amekaa upande wa mbele, dem alikuwa kama anamwomba jamaa atoke nje. Kwa upande mwingine Mgambo walikua wamemgongea jamaa ashuke na madereva pia walikua wameanza kumgongea kwa fujo, maana jamaa alikuwa anafanya mambo ya kizamani sana, afu pia ya kishamba.

Baada ya muda jamaa akashuka na alionekana mtu ambaye amelewa hakuwa na akili zake.

“We ms*** unazingua baada ya hili suala mlimalize mapema wewe unaleta mapozi, acha ufala sisi madereva hatuko hivo.” Hii ilikua ni sauti ya jamaa ambaye alikua ni dereva akimwambia jamaa.

Foleni ilizidi kuwa kubwa na kupelekea watu kuzidi kumiminika pale, maana hakukua na gari inayotoka wala kuingia.

MGAMBO: “Bro siku nyingine usifanye ujinga kama huu hili kosa ni lako, ulipaswa kushuka na myajenge haraka.”

JAMAA : “Samahani bro! Tunaweza ongea kuhusu hili private?”

Jamaa alikua akiniomba tuongee private.

MGAMBO : “Hakuna haja kuongea private, cha msingi tumsikilize jamaa hapa atasemaje”

Palepale alitokea jamaa ambaye ni dereva wa Uber na akatoa hesabu na gharama za vifaa na utengenezaji.

“Hii ni IST ya 2006 taa za nyuma moja ni 180,000/= kwa mbili ni 360,000/=. Bampa hilo halifai tena gharama zake ni 250,000/=, kunyoosha hio boneti na kupaka rangi hapo andaa 100,000 kwa jumla hapa ni 710,000/=. Kama jamaa atakuchaji na usumbufu juu yake ila gharama za hapo ni uhakika. Hii gari kali sana bado mpya naona umeshaitia ngeu tayari.”

Muda huu pia Iryn alionekana kunionea huruma sana maana alikua anajua gari itakua ya boss, hakuwai kuuliza kama gari ni yangu au laah! na mimi pia nilikuaga siwaambii wateja kama gari yangu.

IRYN : “Insider unafanyaje sasa?, I can feel you, I’m really sorry.”

MIMI: “Jamaa kama atatoa hizo cost no problem tutatamaliza”

IRYN: “Atakubali sasa?”

Muda huo Mgambo akawa amekuja upande wangu akiniuliza maamuzi yangu ni nini juu ya hili jambo. Upande mwingine madereva walitamani sana hili jambo liishe mapema maana tungesema tusubir traffic kwa muda ule isingekua rahisi kwa Traffic kufika mapema.

Nikamuuliza jamaa alokua anatoa hesabu za matengenezo kama anauhakika na zile bei alizotaja, na madereva wengi wa Uber walikuwepo pale wakasema ni sahihi.

MIMI: “Kama jamaa atakua tayari kutoa hizo gharama sina shida naye anipe 750,000/=. Hio 40,000 iwe kama usumbufu wa kunipotezea muda kwenda garage.”

Kwa upande wa jamaa aliyenigonga ni kama hakua tayari maana alisema hana hela na hicho kiasi ni kikubwa sana kwa upande wake.

DEREVA UBER: “Hivi wewe jamaa una akili kweli? Mshukuru hata jamaa ni mwelewa na mstaarabu sana, kwanza hapo umelewa tukiita traffic hapa unakesi nyingi sana, kama unayo hio amount mpe jamaa tuondoke foleni imeshakua kubwa sana.”

Na muda huu uongozi wa Kidimbwi ulikua umefika pale kutoa usuluhishi.

JAMAA: “Hiki kiasi cha Pesa kwa sasa sina, mpaka niongee na Mzee au tutatumia Bima ya gari, bima yake ni kubwa.”

DEREVA UBER: “Bro embu kuwa serious Kama ni Bima ya gari inamaana tusubiri traffic waje kupima? na Bima inachukua muda mrefu kutoa majibu, jamaa asubiri majibu ya Bima?, hata mimi siwezi kukubalia.”

Kulikua na kelele za madereva wengi walikua ni Uber na walionekana kuwa na hasira sana huu usiku.

MIMI: “Kama jamaa anataka Bima ndo itahusika, bhasi anipe gari yake nimwachie hili akatengeneze, gari ikikamilika na mimi nitakukabidhi lako unaonaje mzee?”

Watu walionesha kufurahishwa na hii kauli yangu na waliiunga mkono. Jamaa baada ya kusikia hii kauli ni kama alishindwa cha kusema.

Uongozi wa pale Kidimbwi, Mgambo walikua wakiongea namna ya kupata solution, palepale Iryn akaanza kuongea.

IRYN: “Bro haya ni maisha tu, leo inaweza kuwa kwako, kesho ikawa kwetu. Hili suala tunataka liishie kirafiki ili kila mtu akaendelee na maisha yake. Hatuwezi kupelekana police kwa jambo dogo kama hili, ukisema utumie Bima kwanza itachukua muda mrefu sana, pili sisi tutaendelea kukusubiri mpaka bima itakapokuwa tayari?. Kwanza hapo umelewa, Traffic wata recommend wewe ndo mwenye makosa do you really think bima watapitisha claim yako?, hata kama ni Comprehensive kwa Tanzania hii sio rahisi. Na huo muda ambao unafuatilia upo tayari kutulipa muda wetu wa kusubiri?, naona unaleta masikhara kwenye vitu serious.”

Iryn aliongea na kila mtu aliona dada kaongea point sana,

JAMAA: “Nimeelewa ila sasa nitapataje hii pesa kwa sasa na muda huu ni usku hata kuwapigia wazazi ni ngumu kwa muda huu.”

IRYN : “Ni simple tu, unatumia simu gani?”

JAMAA : “Iphone”

IRYN : “Ilete tuione”.

Na muda huo dem wa jamaa alikua kashuka kwenye gari. Jamaa alikwenda kwenye gari na akatoka na simu

IRYN : “Hii ni iphone 12 Pro. Unaweza kuweka bond hapa afu kesho ukipata hio hela unapewa simu yako, simple like that.”

Watu walioneshwa kuyakubali mawazo ya Iryn na waliunga mkono hoja kwa 100%. Jamaa alisogea pembeni na demu wake ni kama walikua wanajadili kuhusu hili jambo, baada ya dakika 2 wakarudi.

JAMAA: “Bhasi sawa haina shida acha niweke simu Bond”

IRYN : “Itabidi tuandikishiane”

Palepale zikatafutwa karatasi na peni sijui zilitokea wapi kwa muda mle, jamaa mmoja alikua ameleta notebok na peni. Iryn akaomba leseni zetu za gari, mimi nikaitoa kwenye gari lakini jamaa alikua hana leseni, ikabidii tumwombe NIDA.

Tuliandikishiana pale makubaliano baina yetu na upande wa mashahidi “Mimi nilikua na Iryn, jamaa alikua na demu wake, Mgambo 1, na Dereva wa Uber aliyekuwepo pale kama shahidi”.

“Simu yako utawasiliana na jamaa asubuhi au utawasiliana na mimi kwa namba hizo, Jitahidi uwe mkweli maana ikipita kesho tutakwenda Police maana ushahidi wa Picha na haya makubaliano upo.”

Baada ya kuandikishiana kila mtu alisaini na jamaa akatoa line kwenye simu yake akatukabidhi simu, akapiga picha yale makubaliano kupitia simu ya demu wake na mashahidi wengine wakafanya hivyo, na mchezo ukaisha kihivyo kwa ule usiku.

Ilituchukua kama dakika 45 kutoka eneo la Kidimbwi kutokana na ile foleni kubwa. Tulivyofika kwa Zena pale nikafanya kurequest usafiri kwa ajili ya Iryn, na nikapata Uber pale chap, tukaagana na Mimi nikarudi home kulala.

*********

Asubuhi niliamka mapema sana ili kuwapa taarifa wateja zangu “Maggy na Mama 2” kuhusu ajali niliyopata na wakanielewa. Wakati naongea na Mama wa2 akaomba badae tuonane jioni pale Rainbow.

Saa 2 asubuhi Iryn alinipigia simu kujua maendeleo yangu na pia aliuliza kama jamaa kanicheki na nikamwambia jamaa hajanicheki bado.

Saa4 Jamaa ndo alinipigia simu na saa 6 mchana tukakubaliana tuonane pale Morocco. Jamaa aliomba tuonane pale sababu yeye alikua anakaa Magomeni. Baada ya muda huo tulionana na jamaa na akanikabidhi kiasi changu cha Pesa 750,000/=, nilizihesabu zile Pesa na zilikua zimetimia.

Palepale nilitoa karatasi nikaandika kwa nyuma kuonesha tumekabidhiana tayari. Mimi nikaondoka na uelekeo wa Gerezani kutengeneza gari, sababu nilijua pale Gerezani mimi ni mwenyeji hata sitapata shida kwenye kutengeneza gari.

Baada ya kuachana na jamaa nilimpigia simu Iryn nikamwambia nimeshaonana na jamaa na amenipa pesa tayari, akanambia nipitie kwake navyorudi.

Nilifika pale Gerezani nikamtafuta fundi wangu ambaye nilikuaga nafanya naye kazi kwenye ofisi yangu kipindi kile. Jamaa baada ya kuiona gari akanambia hapa chap leoleo tunaimaliza kazi.

Huyu Fundi wangu ni mtaalam sana kwenye masuala ya upakaji rangi yuko vizuri sana. Tulinunua taa za nyuma OG za mtumba pale Ilala pamoja na bampa ya nyuma.

Nakumbuka taa 2 tulilipia 320,000/= na bampa tulilipia 220,000/=. Mpaka jioni gari ilikua imeshakamilika tayari utafikir sio ile ambayo ilikua imebondwa nyuma.

Baada ya kutoka Gerezani moja kwa moja nilikwenda kwa Iryn maana alinambia nipitie kwake navyotoka mjini. Nilipitia pale Namanga madukani nikanunua mtindi maziwa litre 3, Iryn alinambiaga anapenda sana mtindi, hivyo nikafanya kumsaprizi.

“Nilikua nafanya haya ili kuendelea kumvuta Iryn karibu yangu, maana nilikua naingiza pesa nyingi sana kupitia yeye. Iryn alikua tayari mtu muhimu sana kwangu, nilikua namuheshimu sana.”

Nilifika kwake usiku tayari ulikuwa nikaingiza gari ndani, bhasi na yeye alikua katoka tayari na alikua amezunguka upande wa nyuma kulitizama gari.

Na mimi nilikua nimeshuka na dumu la mtindi, Iryn baada ya kugundua ni mtindi alifurahi sana. Bhasi tukaanza kuondoka kuelekea ndani huku tunapiga story.

IRYN: “Gari imependeza sana utafikiri haikugongwa jana Insider.”

MIMI: “Umeona eeh, jamaa nilompelekea alikuaga Fundi wangu ni mtaalamu”

IRYN: “Kwani ulishawai kuwa na Garage?”

MIMI: “Hapana ilikua kama workshop flani hivi , nilikua napiga piga rangi na kupolish magari.”

IRYN: “Sasa ilikuaje mpaka ukaifunga?”

MIMI: “Nimefunga kwa muda but nitarud tena kwenye business. Nilipisha ujenzi wa barabara”

IRYN: “Pole, unaona sasa una mambo mengi ila hujawai nishirikisha kabisa”

MIMI: “Ndomana hata yule Muajemi niligundua atakuja kuwa asset hapo baadae maana anadili na Lubricants atanisadia huko mbeleni.”

Muda huu tulikua tuko seblen tunaendelea na maongezi…..

IRYN: “So Bossy wako umempa taarifa kuhusu gari?”

MIMI: “Hapana sijamwambia kabisa, kuna vitu unavunga tu. Hata ningemwambia asingekua na msaada angeishia kupata presha tu.”

Iryn alikua hajui kama hii ni gari yangu pia usajili wa gari nilitumia jina la wife. Na mimi sikuwai kumwambia gari kama yangu.

IRYN: “Okay nice, ni uamuzi mzuri. Insider una ni hide mambo yako ujue.”

Muda huu alikua kama amenuna, na mimi ikabidi nimsogelee karibu.

IRYN : “Insider niache bhana..”

MIMI : “Sikia kama unataka kujua kuhusu mimi, nitakwambia tena kwa vitendo sawa?, aya nambie umepika nini?”

Iryn baada ya kusikia maneno hayo aliishia kutabasamu.

IRYN: “Twende jikoni ukaone.”

Alikua amepika tambi na Kuku, kwenye suala la mapishi dada pia alikua yuko vizuri sana. Mimi nikapakua nikaanza kula maana nilikua nina njaa sana, sikula mchana.

IRYN: “Insider unakumbuka kesho?”

MIMI: “Yeah si tunakwenda kwa mama Janeth?”

IRYN : “kumbe unakumbuka”

Na muda huu simu ilianza kuita, kucheki alikua ni mama wa2, nikapokea tukaanza kuongea pale. Mama wa2 alikua ananiuliza niko wapi maana anaona kimya simtafuti. Na mimi nikamwambia ndani ya nusu saa nitakua pale, na yeye akasema nitamkuta Rainbow

IRYN: “Insider huyo nani?”

MIMI: “Mteja wangu huyu”

IRYN: “Seems like mna appointment usikuu huu”

MIMI: “Yeah anataka kunilipa pesa zangu za mshahara huwa namchukua asubuhi kila siku”

IRYN: “Sasa kwanini asikupe hiyo kesho?, mpaka akupe usiku?”

MIMI: “Yuko likizo ndomana, pia amenambia kuna kazi ya kufanya naye tukabargain”

IRYN: “Mmh sawa, watu na appointment zenu za usiku”

Muda huu tena simu yangu ilianza kuita na mama yangu mzazi ndo alikua anapiga simu, sababu nilijua mama atakua anapiga simu kuhusu suala la Mama J sikutaka kuipokea simu yake. Nikasema nitaongea naye nikianza kutoka kwa Iryn, nilijua mama lazima anipe vichambo.

IRYN : “Naona anakupigia tena simu na hutaki kupokea, pokea tu.”

Mimi sikumjibu kitu niliamua kunyamaza, wakati huu nilikua niko busy na msosi. Yeye akaamua kuivuta simu aangalie ni nani anayenipigia.

Sasa Iryn alivyoona Mama ndo anapiga ni kama alipatwa na ka aibu, mawazo yake yote yalikua ni atakua Mama wa2 niliyetoka kuongea naye muda sio mrefu.

IRYN: “Kwanini humpokelei mama simu.?”

MIMI: “Mama kuna kazi alinipa sasa sijaifanikisha ndo nawaza hapa jibu la kumpa, maana hatonielewa kabisa.”

IRYN: “Mmhh sawa bhana, sio vizuri huwezi jua anakupigia akwambie nini.”

MIMI: “Nitampigia soon.”

Nilitoka pale kwa Iryn nikamwaga na yeye alitoka kunifungulia geti, tukakubaliana kesho mchana tukutane kwaajili ya kwenda Masaki.

Muda huo niliendesha gari kwa kasi sana kuelekea pale Rainbow Mbezi Beach. Nilifika pale na nilimkuta akinywa Savannah kama kawaida yake.

MIMI : ”Nakuona Mama mkwe unakimbiza taratibu”

MAMA WA2: “Ndo nini kuniweka hivi utafikiri namsubiri Mr.”

MIMI: “Samahani, hesabu zangu kidogo zilifeli ila sijakuweka sana hata hivyo, nitakuongezea Savannah moja ya kukusubilisha.”

MAMA WA2 : “Insider bhana unajua wewe unavituko sana alokwambia mimi nahitaji Savannah ni nani?”

MIMI : “Sasa unataka nini? Maana kuwa mkwe wako umenikazia”

MAMA WA2 : “Mwanangu mdogo yule wewe ukome.”

MIMI: “Afu sijawai mwona embu nioneshe hata picha ili nianze kuandaa hata posa.”

Mama wa2 akatoa simu akanionesha picha za Bint yake ambaye ndo mtoto wake wa kwanza wa kike. Na huyu mtoto wake alikua Advance form 5. Tuseme Mama wa2 amebarikiwa kuwa na watoto wazuri sana, afu wote baba zao ni tofauti.

MAMA WA2 : “Insider mwanangu mpaka amalize chuo ndo hapo mambo mengine yatafata. Hata wewe huyu sio size yako.”

MIMI: “Sema hutaki kuona bint yako anaolewa na Dereva wa Uber, huyo ni size yangu kabisa”

Muda huo dada alikua kaja pale kunisikiliza bhasi nikamnong’oneza aje na Savanna 2 na Heineken 1.

MAMA WA2 : “Insider unafikir sitamani kuwa na Mkwe kama wewe?, napenda upapambanaji wako. Najua hapo una elimu yako nzuri tu ila uneamua kupambana na Plan B hujataka kuajiriwa kama sisi.”

MIMI: “Unafikiri sipendi kuajiriwa? Sema sina connection tu.”

MAMA WA2 : “Umesomea nini?”

MIMI : “Uchumi”

MAMA WA2 : “Nikikutafutia connection upo tayari kufanya kazi?”

MIMI: “Why not, nikamkonyeza” na yeye akatabasamu.

Na muda huu dada alikua kaleta vinywaji, sasa Mama wa2 alishangaa kuona Savannah 2 kwaajili yake napia kuona mimi nimeagiza Heineken.

MAMA WA2 : “Kwahiyo kweli umeamua kuagiza Savannah?”

MIMI : “Yeah kwani nimefanya vibaya?”

MAMA WA2 : “Ahsante nilijua unanidanganya, na wewe pia kumbe ni mtumiaji wa pombe?”

MIMI : “Hapana leo nimeamua kunywa kwa ajili yako, seems like you don’t need my company here.”

MAMA WA2 : “No I’m happy, hata hivyo nilikua nishakunywa 2 tayari. Nikinywa nyingi zitaenda kunisumbua tu.”

MIMI : “Umeniitia nini kwanza nje na mshahara wangu,?”

MAMA WA2 : “Insider jumamosi nataka unipeleke Bagamoyo kabla sijamaliza likizo yangu.”

MIMI : “Bagamoyo unaenda kula bata?”

MAMA WA2 : “Nataka nikapunguze stress za maisha kule.”

MIMI : “Kwahiyo na mimi niandae pamba?, ili ukanilishe bata.?”

MAMA WA2 : “Ndo maana yake unafikiri nitakwenda na nani? Kama sio wewe?.”

MIMI : “Sawa imeisha hio, Bossy wangu.”

MAMA WA2 : “ I am not your Bossy”

MIMI : “Bhasi mama mkwe wangu kipenzi”

MAMA WA2 : “Gari umefanikiwa kuitengeneza?”

MIMI : “ Yeah muda sana si unajua ile ni ofisi siwezi kuchukua muda mrefu, nitakula wapi?”

MAMA WA2 : “Pole sana, so kesho kama kawaida asubuhi?”

MIMI : “Ndo maana yake, kesho asubuhi nitapita asubuhi kumchukua mtoto.”

Tulikaa na mama wa2 pale, akanikabidhi malipo yangu na mimi nikaondoka kurudi home kulala.

Wakati niko njiani nilimpigia simu mama na tukaongea kuhusu suala la Mama J. Nikamweleza mama ishu ilivyokua na mama aliishia kunilaumu sana kwa lile tukio na kunikanya nisurudie tena ule upumbavu. Akaomba nifanye juu chini tuyamalize mapema maana haileti picha nzuri kabisa. Nilimuahidi mama nitahakikisha tunayamaliza na Mama J na muda huo nilikua nimewasili home tayari.

Baada ya kuingia ndani kama kawaida yangu niliingia kuoga baada ya hapo nikasema acha nimpigie simu Prisca nimjulie hali maana toka jana sijaongea naye na yeye alikua hajanitafuta kabisa.

Nilimpigia simu baada ya kuita kwa sekunde kadhaa akawa amepokea;

PRISCA: “Hi Insider, naona umeamua kunipigia”

MIMI: “Hapana mrembo, Samahani nilikua nimebanwa sana na jana nilipata ajali.”

PRISCA: “Ajali ya nini? Mbona sikuelewi?”

MIMI : “Ya gari ila nishasovu tayari kuna mtu alinigonga kwa nyuma”

PRISCA: “Oohh I am really sorry”

MIMI : “How are you feeling today?”

PRISCA : “Kinda good, Insider do you love me?”

MIMI : “Yes I do, why?”

PRISCA : “I think you do not, nimekwambia jana naumwa but you don’t even care. Uko busy na mambo yako.”

MIMI : “I care about you, kesho nitakuja chuo kukuona sawa?”

PRISCA: “Okay, Goodnite byee”

Muda huu nilikua nawaza kumfanya Prisca kuwa kamchepuko kangu lakini nilibaini huyu mtoto angenisumbua sana. Prisca ni aina ya wale wanawake wanaopenda sana kudekezwa na kupetiwa petiwa, na pia ni aina ya wanawake ambao wakipenda wanapenda kweli.

Sasa mimi wanawake wa dizaini hii siwawezi kwakweli kwenye historia ya maisha yangu. Suala la kumbembeleza na kumdekeza mwanamke kama movie za Kikorea mimi siwezi.

Sasa nilikua nawaza kwa upande mwingine Mama J toka ajifungue ilikua miezi 9 tayari ila kuna muda nilikua sipati mahitaji yangu ya kitandani. Sometimes nilikua namwonea huruma na malezi ya mtoto alikua anachoka sana na ukizingatia Junior alikua analipenda sana nyonyo. Nikawaza nimfanye Prisca kma mchepuko ila nitamwambia ukweli aamue mwenyewe kama yuko in or out.

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Nakuja
 
Back
Top Bottom