Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 64

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN.”

PREVIOUS
Kwa upande mwingine utamu wa Iryn ulinipagawisha na nilijikuta natamani kuendelea kuwa naye maana utamu nilioupata ni wa kipekee, hivyo niliona bora nimtongoze tu ifahamike moja maana hata yeye ananipenda maybe anasubiri mimi nimfungukie. Ukweli nilikuwa nimetembea na wanawake tofauti lakini sio sana maana mimi sio muhuni, lakini Iryn ana utofauti sana asee ni mlaini, ananyumbulika kitandani, anajua mapenzi afu coochie yake ni hot, Prisca alikuwa ananipagawisha lakini Iryn funga kazi.

CONTINUE

Niliwaza pale Iryn anapataje taarifa za mimi kwenda kwa Asmah?, niliwaza nianze kwanza kuongea na Asmah then mengine yatajulikana, kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Mary akipiga simu na mimi nilipokea simu yake,

“Hi Mary.”

“Poa, Insider hupokei simu zangu are you still hungry with me?”

“No Mary I am really sorry nilikuwa nimebanwa sana jana, tell me unaendeleaje?”

“Niko poa naomba kuonana na wewe please.”

“Kwa leo ngumu labda kwa badae nikipata chance nitakucheki, ukiona kimya bhasi kesho.”

“Okay, byee.”

Mary alikuwa anaomba tuonane lakini sikujua anataka kuongea nini na kwa upande wangu nilihisi lazima litakuwa suala la Prisca, pia sikuona sababu ya kumkatalia maana Mary ni mtu wangu wa karibu sana na alinipa kampani sana kipindi cha Msiba.

Niliingia chumbani na nilimkuta Iryn kalala bado na ilikuwa saa 6 mchana tayari hivyo niliamua kumuamsha na kofi la kalio pale kitandani ili ajiandae tuondoke.

“Mummy ulisema tunatoka mchana jiandae tuondoke saa 6 tayari.”

Iryn alishuka kitandani na alivua nguo zake mbele yangu na akaenda bafuni kuoga, kwa upande mwingine hakuwa na aibu na mimi kabisa. Wakati anajiandaa kwa upande wangu nilitangulia kwenda kuonana na mama mlinzi ili anipe key za gari na tulikuwa tunaongea pale,

“Vipi Mzee hajamind alivyoona gari yangu?”

“Nilimpoza kidogo na yeye hata hajapiga kelele, hakuna asiyependa hela.”

“Mama Ahsante sana maana tumefanikiwa kuyajenga badae nitakupa zawadi yako.”

“Usijali kuwa na amani kabisa.”

Na muda huu Iryn alikuwa ameshuka chini tayari kwa safari na aliniita pale, “Insider…..” na mimi nilimpa ishara asogee mpaka usawa gari ili tuondoke maana gari nilipark upande mwingine.

Tuliondoka pale na break ya kwanza ilikuwa pale Mikocheni kwa Osama, na tulinunua chips kuku sahani 8 na soda, Bossy lady aliamua kuwapa offa ya lunch wafanyakazi wake.

Kwa upande mwingine Lucy alikuwa kanipigia sana simu na mimi sikuzipokea wala kuchat naye maana nilijua lazima tungeonana na kuzungumza haya, kwa upande wangu nilisema siwezi kumwambia kilicho endelea kati yetu.

Baada ya kuwasili pale Salon palikuwa busy sana na nilimuacha Iryn reception akiongea na mimi nilikwenda moja kwa moja mpaka ofisini. Haikuchukua muda Lucy alikuja ofisini na alionekana kuwa na shauku sana ya kujua kinachoendelea na uso wake ulichanua tabasamu kubwa sana,

“Insider you made it?”

“Yeah, tumeyamaliza kwasasa tuko cool.”

“Vipi ume hit? Naona Bossy anafuraha sana leo tena ile halisi.”

“Hahahaha hapana Lucy labda amefurahi tulivyo yamaliza.”

“Insider mimi sio mtoto ujue, jana wote hampokei simu zangu na sio kawaida yenu, pia hamja ni call back, leo nawaona mnakuja pamoja, mlilala pamoja jana.”

“Trust me Lucy jana nilikuwa nakunywa bia huko mbezi si unajua na mastress?”

“I know mshikaji wangu ila wewe ni nyoko kama umefanikiwa kuyamaliza bhasi nakupa respect yangu, najua umemla ila hutaki kunambia but nitafound out soon.”

Wakati tukiendelea kupiga story pale kwa upande mwingine Iryn alikuja ofisini,

“Lucy kumbe umekuja kukaa huku na Insider, tumewaletea chakula kiko kwenye gari, Insider tuondoke.”

“Kila ukiniona na Lucy lazima utuharibie maongezi yetu.”

Tuliondoka pale Mikocheni kwenda Masaki na wakati tuko njiani tulikuwa tunapiga story sana na pia ilibidi nimuulize sababu ya kumuachisha kazi Sumaiya.

“Mummy kwanini umemsimamisha kazi Sumaiya?, kwa hili sijapenda kwakweli unajua mtoto wake amelazwa?.”

“Sijamuachisha kazi ila nime msimamisha kwa muda kutokana na tabia zake, kumbuka yeye ndo incharge pale then anachelewa na hatoi taarifa anajenga nini kwa hawa wengine? ndomana nimechukua hatua.”

“Ulitakiwa uulize kwanza kabla ya kuamua kufanya maamuzi ya kipumbavu kama haya, kumbuka yule ni binadamu afu anamtoto, taarifa alitoa kwangu lakini wewe ulikuwa umeniblock, kwa hili umezingua sana, afu kumbuka hii ni kampuni huwezi kumsimamisha mtu bila barua akienda mahakamani utachomoka.?”

“Nimepata taarifa zake pia anafanya ujanja sana kwenye mauzo ana haribu reputation ya kampuni kumbuka hapa Masaki wateja wetu wengi ni foreigners.”

“Ni sawa unachosema lakini lilikuwa ni suala la kukaa naye chini, Sumaiya nafanya naye kazi vizuri na hakuna kilichoharibika, ifike mahala chuki zako kwa Sumaiya ziishe, tufocus na kampuni. Naomba umrudishe kazini kesho na usipo fanya hivyo na mimi naandika barua ya kuresign position yangu, maana taarifa alitoa kwangu.”

Ilibidi nimtetee Sumaiya muda huu ili kibarua chake kirudi, wivu wa Iryn ndo ulisababisha amsimamishe kazi.

“Sumaiya atarudi kazini na atakwenda kusimamia kampuni ya usafi na sio huku Salon tena, atakuwa manager na mshahara atapandishiwa.”

“Hapo sawa najua hutaki niwe naye karibu but sio mbaya nitampa hizi taarifa badae.”

“Unamtetea sana b*tch wako”

Baada ya kuwasili pale ofisini Masaki nilipark gari na tulikwenda moja kwa moja mpaka ndani na mimi niliamua kwenda ofisini kwa Asmah kumsalimia na sikumwambia kama nimekuja na Iryn. Kwa upande mwingine nilimkuta anachati na baada ya kuniona tulianza kupiga story pale, na mimi kichwani plan zangu nianze kumspy,

Asmah ni mtu ambaye yuko kivyake vyake na sio mtu wa kampani, she is minding her business,

“Baby nakuona umetulia umekula?”

“Nilikuwa na order hapa food bora nimekuona utanilipia.”

“Usijali leo nitakupa offa, naomba tuongee jambo moja maana sielew elewi.”

“Insider jana nimekupigia simu ili tuonane lakini hukupokea nilitaka tuongee haya.“

“Jana nilikuwa busy ndomana, pia kuna kitu hakipo sawa, Iryn amejuaje kama mimi huwa nakuja kwako?.”

“Hata mimi sijui kwakweli au huwa unamuachia simu yako anaikagua.?”

“Iryn hashiki simu yangu, mimi ndo nikuulize wewe labda kuna mtu humu ndani mnashare mambo yenu?.”

“Insider wewe unanijua vizuri sinaga time na mashosti wa humu ndani na ninaanzaje kushare hii kitu?.”

“Huwa una share simu yako na mtu yoyote humu ndani? tuanzie hapa kwanza.”

“Yes!, Rebecca mara nyingi huwa ananiazima simu yangu na ndo yeye ambaye huwa anaomba hakuna mwingine.”

“Rebecca ana snitch? Mbona kama haimake sense.”

“Insider nahisi Rebecca anasnitch atakuwa anaangaliaga chats zetu na anampa Bossy taarifa. Pia kuna siku niliwakuta ofisini wamekaa wanaongea baada ya mimi kuingia wakakatisha maongezi yao, kwa hili leo nimehisi ni yeye.”

“Sawa niachie mimi nitajua ya kudeal naye ila kwasasa uwe unafuta chats na usimpe simu yako.”

“Rebby ni mshenzi sana.”

Mpaka hapo nilihisi Rebecca anahusika moja kwa moja kumpa taarifa Bossy lady kinacho endelea pale ofisini na wakati tukiendelea kupiga story, kwa upande mwingine Iryn alifungua mlango na alituona na Asmah tunacheka, alimsalimia Asmah na akanipa ishara ya kuondoka.

Baada ya kufika parking na kuingia kwa gari Iryn alikuwa ananiangalia sana ni kama alimind kuniona kuwa na Asmah pale ofisini.

“Tunakwenda kula wapi?”

“Chagua mwenyewe sehemu nzuri tukale.”

Na mimi nilindesha gari mpaka Moyo kitchen na baada ya kuingia ndani tuliagiza chakula na tukaanza kupiga story pale, kwa upande wangu
nilikuwa nampango nianze kumtongoza lakini nilikuwa nakosa point, na muda huu wote tulikuwa kimya na yeye alikuwa busy na Iphone yake, muda huu na mimi nilianzisha maongezi,

“Bossy mbona hunambii kama umeniachisha kazi.?”

“Nimekuachisha lini? Mbona sikuelewi Insider.”

“Kitendo cha kumpa Asmah majukumu yangu ulikuwa unamaanisha nini?”

“Insider ulitaka nifanyaje wakati ulikuwa hutumi ripoti?”

“Si umeni block wewe?.”

“Ripoti unatuma kwa whatsapp sikuhizi? na sio kwa mail tena.”

Na mimi nilibidi ninyamaze tu maana kweli nilikuwa nimezingua,

“Hivi kwanini unanichukia na unakuwa na wivu na mimi?”

“Insider mimi siko hivo kama unavyofikiri naona unakuwa hujiamini.”

“Iryn do you love me?”

“Yes I was, but toka nifaham una mke upendo wangu kwako ulikufa na hizi scandals zako zina nisogeza mbali na wewe.”

“Mbona mimi nilivyojua unadate na Grizz upendo wangu ulizidi kuimarika kwako na sikuonesha sign yoyote ile au unafikiri na mimi sikuumia?. So hapa unanionesha ni jinsi gani ulivyo mbinafsi unaangali moyo wako tu.”

Na muda huu Iryn alinyamaza kimya na alikuwa anajifanya kuwa busy na simu yake, baada ya kuona nimemkamata tayari niliendelea kutema sumu kama Koboko,

“Iryn embu niangalie usoni, mimi sipendi dharau ujue, naongea na wewe upo busy kuchezea simu kuonesha mimi naye ongea ni kama fala kwako.”

“Insider nakusikiliza vizuri kabisa… Okay sorry endelea.”

“Mimi nataka tunavyotoka hapa kila mmoja awe hana kinyongo na mwenzake, tuzimalize tofauti zetu. Mimi nakuahidi hutaniona nikifanya mautani na kina Sumaiya, kama hili huwa linakukwaza bhasi kwasasa hapana.”

“A good start, najua una utani nao sana na wamekuzoea sana, but kuwa na mipaka.”

“Pia nataka leo utambue mimi Insider nakupenda sana nataka ikiwezekana uwe mke wangu.”

“Eti what…?” Na muda huu Iryn alinza kucheka maana aliona huyu MTALIBAN anazingua,

“Insider suala la mimi na wewe kuwa kwenye mahusiano haliwezekani kwasasa, nimeachana na Grizzman sababu hii afu tena nianze tena mahusiano na wewe mme wa mtu? na isitoshe mama J ni rafiki yangu unafikiri atajisikiaje akilijua hili?, kumbuka ana Moyo kama mimi. Kuna msemo unasema “what’s goes around comes around “ and karma is bitch.”

“Actually nilitaka wewe uamue kama unaona suala la mimi na wewe kuwa kwenye mahusiano haliwezekani bhasi tuendelee kuwa washikaji tu.”

“Kwa hili nakuunga mkono na wewe utulie na mke wako, unajua unabahati sana ya kuwa na mwanamke mzuri mwenye brain.”

“Haya hayakuhusu, tuondoke mimi nina appointment zangu badae kumbuka niko na wewe toka jana kuna mambo yangu ya kutakecare.”

Tuliondoka pale huku tumeongozana na mimi nilikuwa niko nyuma yake namfanyia mautani ya kumsfia jinsi alivyo na kiuno kizuri pamoja na cut-walks zake. Baada ya kuingia kwa gari tulianza safari na kwa upande wake alisema ni mpeleke kwa Lucy.

Wakati tuko njiani simu yangu ilianza kuita na ile kuangalia alikuwa ni Prisca akipiga na mimi bila wasiwasi niliipokea simu yake. Kwa upande wake Prisca alikuwa bado haamini kama kweli nimemuacha na alikuwa bado ananisisitiza sana tuendelee na mahusiano, lakini mimi niliendelea kumkazia kuwa suala la mahusiano halitojirudia tena.

Kwa upande mwingine Iryn alikuwa makini sana kufuatilia maongezi yetu na alijua ninaongea na Prisca, lakini alinyamaza kimya.

Baada ya kuwasili Mikocheni nilimdrop pale na nikamuaga lakini kwa upande wake alifungua mkoba wake na akatoa noti 3 za $100 na akanipa,

“Insider kaweke mafuta hii nina muda sana sijajaza mafuta byee, takecare.”

Kwanza ilibidi nishangae maana niliona kama utani hivi, ukweli toka nianze kumkera Iryn alipunguza kunipa maokoto, ndomana nilishangaa kuona katoa pesa.

“Bossy unanipa malipo ya kutumika jana nini?Ahsante nashukuru.”

Na muda huu Iryn aliishia kucheka tu na mimi nikaondoka maneno haya kuelekea home. Baada ya kufika home na kupark gari nilikwenda kulala kwani nilikuwa nasikia sana uchovu muda huu.

Nilimka saa 1 usiku na nikiwa bado kitandani niliwaza niwe na mchepuko mmoja wa kunipunguza stress, Iryn alikuwa kachomoa tayari hivyo nilikuwa nina option 2 zimebaki kwa Mary au Asmah. Kwa upande wa Asmah niliona bora huu mpango niachane nao na nikae naye mbali.

Mary ndo alikuwa anafaa kuwa mchepuko lakini sasa niliwaza pale, je Mary atakubali? na atanichukulia mimi kama mwanaume ambaye sijatulia, ukweli alikuwa ananipenda lakini toka afahamu mahusiano yangu na mdogo wake hakuwai tena kuonesha sign yoyote kwangu na hii ndo ilinifanya nimwone Mary ni mwanamke mwenye msimamo. Lakini pia niliwaza kudate na mdogo mtu then dada mtu haitakuwa busara hivyo niliona huu mpango utakuwa mgumu kwangu.

Kwa upande mwingine toka nisex na Iryn nilikuwa nimeridhika kabisa kitendo cha kumla siku nzima kwangu ilikuwa ni ushindi tosha hata alivyonambia hawezi kuwa na mimi niliona sawa tu, hata sikuwa na kinyongo.

Muda huu nilichukua simu yangu na nilimpigia simu Mary na iliita mpaka ikakata bila kupokelewa na mimi nilikwenda zangu kuoga. Wakati nimetoka bafuni simu iliita tena na alikuwa ni yeye akipiga na baada ya kuongea tulikubaliana tukutane Havanna ya pale Mbezi Beach classic Mall.

Saa 2 usiku mapema nilikuwa nimewasili pale kwa upande mwingine yeye alikuwa hajafika bado na ilimchukua kama nusu saa kuwasili maeneo haya na alinikuta nina kunywa taratibu. Tulisalimiana pale na yeye kwa upande wake aliagiza wine na story zilikuwa zikiendelea,

“Insider kwanza niombe radhi kwa ile siku maana nilikuwa na hasira sana juu yako, lakini nimegundua Prisca mwenyewe ndo aliyekubali.”

“Usijali najua wewe kama dada lazima ungeumia lakini Prisca ndo aliyekubali na sikumlazimisha, hata mimba aliibeba bila ridhaa yangu.”

“Ameniambia haya yote lakini nilitaka kusikia kutoka kwako shemu, pia amenambia umemuacha na hajanipa sababu shida ni nini Insider?”

“Ongea na mdogo wako akwambie kila kitu, kavunja makubaliano yetu na mimi nayeye ndo bhasi. I made mistakes lakini sio sasa.”

“I need you guys back together, msiachane.”

“Mary haiwezekani kwakweli acha nifocus na familia yangu kwasasa.”

Kwa upande mwingine Mary aliomba azione picha za familia yangu na mimi bila hiyana nilimwonesha na aliomba siku aje aisalimie familia yangu na mimi nilimkaribisha.

Tulikaa pale na Mary tukiendelea kuongea mambo mbalimbali na kubwa nilimshauri atafute nyumba apange aanze kujitegemea maana ashakuwa mkubwa tayari. Kwa upande wake aliufurahia ushauri huu na akasema ataongea na wazazi wake afu atanipa mrejesho.

Saa 5 usiku tuliagana na yeye alirequest usafiri wa kumrudisha home, kwa upande mwingine wakati niko na Mary, Sumaiya alikuwa amepiga sana simu, baada ya kuachana na Mary ilibidi nimpigie simu.

Baada ya kufanya mazungumzo na Sumaiya nilimpa taarifa za kuamishiwa ofisi nyingine ile ya usafi na yeye kwa upande wake ni alifurahi sana, pia alinishukuru sana.

“Wewe mwanaume unanisaidiaga sana lakini kila nikitaka nikutunuku unaringa.”

“Hahahaa inaonesha umedhamiria sana usije ukaniua bure, afu kuna kitu naomba nikuulize noana kuna something fishy kinaendelea pale ofisini. Nahisi Rebecca ananisnitch kwa Iryn yaani kila nacho fanya anakuwa na taarifa zangu, lakini bado nafuatilia.”

“Huyo ndo snitch sasa na kama hujui, kila kinachofanyika pale ofisini yeye ndo anampa taarifa Queen na suala langu yeye ndo alinichongea. Mimi na yeye hatupatani toka nichukue madaraka yake hili jambo mpaka leo linamuuma, nilitegemea angepewa uongozi lakini kapewa Asmah.”

“Duuh aisee kumbe watu mna mabifu toka muda, usiku mwema tutawasiliana kesho.”

Yalikuwa ni maongezi marefu sana mpaka nafika home getini na wakati naongea na Sumaiya kwa upande mwingine Iryn alipiga simu lakini nilikuwa natumika na baada ya kumaliza maongezi na Sumaiya nilimpigia lakini ilikuwa bado blocked.

********
Jumatatu asubuhi mapema nilikwenda Mbweni kumsalimia Jane pamoja na kumjulia hali, baada ya kuwasili pale kwake nilipokelewa na Vicky lakini yeye alikuwa amelala. Nilikwenda kuangalia maendeleo ya mbwa na niliwaona wakiwa na afya nzuri na nilikwenda kuangalia gari yangu IST na ilionekana kubondwa upande wa nyuma na pembeni kwenye mashavu ilikuwa imebonyea.

Nilirudi ndani na tuliendelea kupiga story na Vicky na alikuwa ananipa maelezo namna jane alivyobamiza gari wakati anarudi reverse. Kwa upande wa gari ilikuwa imebonyea mlango wa buti, taa moja ya nyuma ilikuwa imevunjika pia, kwa upande wa mbele bampa lilikuwa halifai alikuwa kagongesha sana.

Kwa upande mwingine Vicky aliomba nimpe kampani ya sokoni kwenda kununua vitu na alikwenda kujiandaa na mimi nilikuwa pale seblen. Baada ya dakika 10 alitoka na tukaanza safari ya kwenda sokoni na tulikwenda Nyuki sokoni. Njiani tulikuwa tunaongea mambo mengi sana maana vicky ni talkative,

“Insider wewe na Mary mmegombana?”

“Hapana why unauliza?”

“Niliwoana hampo sawa siku ile, shida ni nini?”

“Hamna kitu tuko cool kabisa.”

“Mhh sawa na uliniahidi weekend hii unanitoa out lakini umezingua.”

“Nilikuwa nimebanwa kidogo afu unajua mimi nakuchukulia wewe kama mdogo wangu.”

“Insider umeanza dharau sasa, nimeshakuwa mtoto tayari.”

“Sijasema mtoto nakuchukulia kama mdogo wangu wa karibu, kuna mambo naweza yafanya huko afu kwako yakawa mageni.”

“Wasiwasi wako tu mimi sina utoto wowote.”

“Bhasi tutacheki this week tutoke.”

Baada ya kuwasili pale sokoni nilimpa kampani ya kununua mahitaji na baada ya kumaliza tulirudi Mbweni, kwa upande mwingine Jane alikuwa ameamka tayari na alikua amekaa kibarazani.

“Shem nilisikia sauti yako, nimeamka naambiwa mmetoka.”

“Vicky aliomba kampani ya kwenda sokoni ndo tumetoka huko.”

Tuliendelea kuongea pale kibarazani na pia alizingumzia suala la kuiharibu gari yangu na yeye alisema atanirudishia pesa ili nikanunue Ist nyingine na pia nimpe gharama za matengenezo ya gari. Baada ya kuzisikia hizi taarifa sikutaka kukataa maana gari alikuwa ameibonda sana na kuhusu Dualis alisema niendelee kuitumia mpaka atakapo jifungua ndo ataichukua.

Kwa upande mwingine tumbo lake lilikuwa kubwa sana na alikuwa anaonekana kuchoka sana kipindi hiki. Niliendelea kushinda pale kwa Jane na ile mchana Mzee Mollel alinipigia simu na alinipa taarifa ya kukamilika kwa nyumba na ipo tayari kwa kuhamia. Ofcourse nilifurahi sana kuzisikia hizi taarifa na nilimwambia Mzee Mollel wiki hii Ijumaa nitakwenda Dodoma kwaajili ya hili suala.

Jioni niliondoka maana nilikuwa na Vicky tu pale seblen na wakati natoka tulikuwa tumeongozana mpaka naingia kwa gari, na yeye alikwenda kunifungulia geti. Wakati narudi reverse kwa upande mwingine Jane alionekana akitoka ndani na alinipa ishara ya kusimama na akasogea mpaka usawa wangu na mimi nikashusha kioo nimsikilize,

“Insider nilikuwa na jambo nataka kuzungumza na wewe kwa bahati mbaya nilisahau mpaka nashtuka unaondoka.”

“Una jambo gani shem maana unanitisha.”

“Usiogope but tutaongea next time ukija.”

“Sawa shem haina shida.”

Na mimi nikaondoka maeneo haya lakini njiani nilikuwa nawaza Jane atakuwa na jambo gani?. Na mimi nilirudi home kulala mapema kwa upande mwingine Iryn alikuwa bado ameni block.

Jumanne asubuhi nilikuwa na miadi na mama wa2 na aliniomba kampani ya kwenda Madale kwenye nyumba yake ili akafanye usafi kabla ya kuhamia. Wakati najiandaa pia nilipigiwa simu na mama Janeth na alikuwa anaomba badae tuonane kwani ana mazungumzo muhimu na mimi.

Ilikuwa saa 3 asubuhi na nilikuwa nimewasili tayari kwa mama wa2 na baada ya kuingia ndani nilikaribishwa dining kunywa chai na baada ya hapo tuliondoka kuelekea Madale tukiwa na Rachel pamoja na dada wa nyumbani.

Baada ya kuwasili pale Madale kwa upande mwinginenyumba ilikuwa imekamilika tayari kasoro chini ilikuwa bado kuweka pervings kwa upande wa ndani ilikuwa kila kitu tayari. Pia kwa ndani walionekana mafundi wanaweka fimbo za mapazia na wengine walikuwa wanafunga taa.

“Mama mkwe hongera sana umepambana kwakweli.”

“Nashukuru sana hata siamini kama nimefanikisha, Mungu amenisaidia sana.”

“Kweli kabisa ngoja nitafute mtu atusaidie kufanya usafi wa nje.”

Tulisaidiana kufanya usafi wa ndani na nje na ndani ya masaa 3 tulikuwa tumemaliza na mchana tulitoka kwenda kupata lunch kwenye moja ya mgahawa pale Contena. Muda huu tulikuwa tunaongea mambo mengi sana na mimi kwa upande wangu nilimpa taarifa za kumalizika kwa nyumba yangu kule Dodoma na yeye aliishia kunipongeza sana, na mimi nilimwambia bila yeye nisingeweza kukamilisha.

Kwa upande mwingine tuliongelea suala la usafiri wa kumfuata asubuhi kule Madale maana zoezi lingekuwa gumu sana, hatahivyo ningempa gharama kubwa. Tulishauriana pale awe ana request usafiri wa kumpeleka kazini, pia kwa upande wake alisema anaplan anunue Dualis maana ameipenda sana ile ya Jane.

Muda wa jioni tulitoka pale Madale na nika warudisha home na mimi sikutaka kupoteza muda niliaga maana nilikuwa nasafari ya kwenda Masaki kuonana na Mama Janeth. Niliamua kupitia kwanza Masaki ofisini ili niendelee kubuy time navyosubiri muda ufike.

Baada ya kuwasili pale ofisini nilikwenda moja kwa moja mpaka kwa Rebecca na nikamuomba simu yake ili nimpigie mtu. Rebecca alinipa simu yake hata hakuwa na maswali na mimi nilikwenda nayo moja kwa moja mpaka ofisini kwangu na nilianza kukagua simu yake taratibu, nilikwenda direct kwenye conversation zake na Iryn. Baada ya kufungua chats zao nilikuta ujinga wote mle kuhusu kila kitu kinachoendelea pale ofisini huwa anamwambia Iryn, nilishangaa sana kwakweli maana Rebecca alikuwa TISS wa Iryn.

Kwa upande wangu nilipiga picha baadhi ya chats afu nikaiweka simu yake mezani nikaendelea na mambo yangu. Niliwaza pale nikaona Iryn anafanya ujinga sana kunifuatilia na nilijisemea kwa hili lazima nikamuwashie moto.

Niliendelea kuandaa report na kupitia baadhi ya taarifa incase mama Janeth akiuliza niwe na cha kumwambia, baada ya dakika 10 Rebecca alikuja ofisini kuchukua simu yake na mimi nilimpa ishara ya kukaa chini.

“Rebecca unajua wewe ni mtu wangu wa karibu na ninakuheshimu sana, kwanini unaingilia privacy zangu?”

“Insider mimi niingilie privacy zako kivipi?, mbona sikuelewi?.”

“Rebby usinione mimi ni mtoto najua unanisnitch kwa Iryn, hata Sumaiya umemsnitch kafukuzwa kazi, vipi umeona raha?, ukiendelea kukaza fuvu ninaweza kukuharibia kama ulivyofanya kwa Sumaiya, sasa nataka unambie kwa nini unafanya hivi?.”

Muda huu Rebby alianza kuwa na wasiwasi na alianza kutetemeka ni kama alijua nimecheki simu yake,

“Samahani manager, bossy ndo alinipa hii kazi ili kulinda kibarua changu.”

“Sawa najua sio wewe lakini ulimuuliza kwanini anakupa hii kazi ya kunichunguza mimi?”

“Sikia manager ipo hivi Iryn alikuja akanambia anataka kuwa kwenye mahusiano na wewe hivyo anaomba niwe nakuchunguza movement zako zote za hapa ofisini, hata hio simu kanipa sababu ya hii.”

Inshort Rebby alifunguka mambo mengi sana muda huu kuhusu hili jambo na aliniomba sana msamaha,

“Rebby ukitaka nikusamehe mpigie simu Iryn na umwambie taarifa unazompa mostly sio za kweli ndo utapata msamaha wangu.”

“Insider please atanisimamisha kazi.”

“Unajua ni namna gani nimetumia kurudisha mahusiano yangu karibu na Iryn?. Ulishajaribu kuwaza kuwa unachofanya ni unabomoa na sio kujenga.?”

“Nisamehe sana I had no choice, pia Iryn anafanya kwa mazuri, anakupenda sana Insider.”

“Fanya kama nilivyokwambia Rebby kwaheri.”

Na mimi niliamua kuondoka na nilimuacha pale ofisini amekaa kwenye kiti na alikuwa kama mtu ambaye hajui afanye nini.

Niliondoka pale ofisini kuelekea kwa mama Janeth na nilitumia muda mchache sana kuwasili pale kwake. Baada ya kuwasili nilikaribishwa ndani seblen na kwa upande mwingine nilimkuta Sumaiya amekaa pale seblen akiwa na mama Janeth.

Niliwasalimia wote na mimi nilikaa chini, ofcourse sikutegemea kama ningemkuta Sumaiya pale na kwa upande wake naye alikuwa anashangaa, ilikuwa ni kama surprise. Mama Janeth aliniomba twende kibarazani tukaongee na tulimwacha Sumaiya amekaa sebleni.

Mama Janeth alinambia sababu kubwa ya kuniita ni kunipa taarifa za kuondoka kwa Sumaiya pale ofisini ili akasimamie ofisi ya usafi. Kwa upande wake aliniomba msamaha kwa hili maana alisema anampenda sana Sumaiya na ana muamini sana, kwa upande wangu sikuwa na neno kwanza nilifurahi kusikia maneno ya mama Janeth. Tuliendelea kuzungumza mambo mengine mengi ambayo ni siri siwezi kuyaandika hapa na kubwa lingine aliniomba niwe namsaidia mambo ya uchumi kama budgeting nk, pale ambapo nitahitajika.

Kwa upande mwingine Sumaiya alikuwa amelamba bingo anatoka kwenye balimi anahamia kwenye heineken, na mama Janeth alimtaka Sumaiya afanye kila mbinu kupata wateja wengine wengi wakuingia nao mikataba. Hii kampuni ya usafi wateja wake wengi ni hizi organizations, kuna baadhi ya hotels na offices, japo mama Janeth alikuwa na mipango ya kupenetrate mpaka serikalini.

Mama Janeth alinipongeza sana kwa utendaji kazi wangu na alionekana kunikubali sana, ukweli niliibadilisha sana ofisi hasa kiutendaji na nili implement operating stategies (mbinu za kiutendaji) ambazo zilisaidia sana kufanya vizuri kimauzo na kupelekea kupata wateja wengi. (Siwezi kutaja hizi mbinu kwa maslahi ya kibiashara).

Tulikaa pale mpaka tukapata dinna ya pamoja na wakati tunapata chakula kwa upande mwingine Iryn alikuwa ananipigia sana simu, lakini nilikuwa nashindwa kuipokea maana ingeleta picha mbaya, hivyo nilisubiri nimalize kula then ningempigia.

Saa 2 usiku tuliaga pale kwa upande mwingine mama Janeth alinambia nimpelekee Iryn gari awe anatumia maana mara nyingi zinakuwa amezipark tu pale uwanjani, na yeye anatumia sana gari za ofisi.

“Sasa utaipelekekaje hii gari maana umekuja na gari yako au utakuja kesho?, ni kama saprise nataka mfanyia bint yangu.”

“Kesho ni ngumu, ngoja nimtafute dereva wa Uber nimuombe tuongozane afu nitamlipa, hawezi kukataa.”

“Yes! Good idea son.”

Na mimi nilifanya kurequest bolt na nilimpata dereva alikuwa karibu na baada ya kumpigia simu nilimuelekeza ataendesha gari yangu mpaka Kawe na yeye hata hakubisha na tulikubaliana elfu 30.

Mama Janeth alikwenda ndani na baada ya muda mfupi alirudi ameshikilia funguo na alinikabidhi pamoja na Leseni ya Udereva ya Iryn. Kwa upande wa gari alinipa funguo ya ile gari yake Audi Q7, baada ya dakika 5 dereva wa uber alikuwa kawasili na tuliaga pale.

Mimi nilikuwa nimempa lift Sumaiya ili nikamdrop pale Morocco, na wakati tuko njiani tulikuwa tunaongea masuala mbalimbali na kubwa alifurahi sana kwa kupata mkataba mpya na alinishukuru sana kwa kumpigania kwa Iryn.

“Insider thank you, Queen alinipigia simu na ameniomba msamaha kwa yote na ndo aliyesema nije kwa mama Janeth.”

“Wow nimefurahi sana kusikia hivyo na kingine nimemzingua sana Rebby hana hamu leo, maana nimemdaka vizuri sana.”

Ilibidi nimpe mkanda mzima Sumaiya namna nilivofanya ujasusi wangu mpaka namdaka, na aliishia kunipongeza kwa hili.

“Insider ofisi ipo hapahapa Masaki so hatuko mbali sana na wewe muda wa lunch tutakuwa tunaonana.”

“I told you Mama Janeth anakuelewa sana lakini hukutaka kuniamini rafiki yangu, kwanza hujawai kunambia mlikutanaje na mama Janeth.”

Sumaiya alinipa mkanda mzima namna walivyokutana na mama Janeth, kwa ufupi walikutana Posta kwenye hayahaya masuala ya Salon ndo mpaka leo. Baada ya kuwasili pale Morocco bus stand kwa upande mwingine Sumaiya aliomba nimkope pesa,

“Insider naomba niazime kama laki 2 cash maana mshahara wote nimelipa kodi ya nyumba na suala la mtoto nalo limenimalizia pesa.”

“Mtoto anaendeleaje kwasasa? Na ana umri gani.?

“Anaendelea vizuri ana miaka 4 na anakaa kwa mama yangu mzazi.”

“Sawa kwa sasa mimi sina cash ila nina dollar utaenda kuexchange kesho na utanirudishia pesa yangu mambo yako yakikaa vizuri.”

Na mimi nilitoa noti moja ya $100 kwa zile noti alizonipa Iryn na nikampa pale, kwa upande wake alifurahi sana na wakati anaondoka alinikiss shavuni, na sisi tukaendelea na safari kwenda kwa Iryn nikiwa na jamaa nyuma akiendesha Dualis.

Baada ya kuwasili kwenye zile apartments mlinzi alisogea yule mzee na baada ya kuniona mimi tulisalimiana na akafungua geti, tukaingia ndani. Tulipark gari zote usawa wa apartment ya Iryn na mimi nilimlipa jamaa pesa yake na akaondoka pale.

Baada ya kufika mlangoni nilifungua lakini ulikuwa umefungwa hivyo ilinibidi nigongea pale, niligonga lakini alikuwa hafungui mpaka nihisi labda atakuwa ametoka, nilijaribu kumpigia simu lakini nilikuwa bado niko blocked.

Niliwaza pale labda atakuwa ametoka lakini mzee angekuwa alinambia kama ametoka, hivyo nilihisi atakuwa amelala, niligonga tena kwa nguvu ndo akatoka kunifungulia,

“Mbona nagonga mlango hufungui?”

“Nilikuwa nimekaa kwa balcony ngumu kusikia, mbona hupokei simu zangu toka jumapili?.” Na alionekana kumind sana,

“Kila nikikupigia simu umeniblock afu unalalamika nini? Huoni unafanya utoto?. Nimekuletea gari pamoja na leseni kutoka kwa mama Janeth.” Na mimi nikamkabidhi pale.

“Woow thank you kumbe mama alikuwa serious juu ya kunitafutia Driving licence.”

“Na maongezi nawewe afu, why unanichunguza unaweka mpaka mtu wa kunispy?.”

“Insider umejuaje kama mimi nakuspy?”

“Ina maana hujui ujinga unaofanya sindio?

Na muda huu nilianza kumuwashia moto kwa ujinga wake na nilikuwa na hasira kwelikweli, kwa upande wake alikuwa anaogopa sana.

“Kumbe kwa muda wote huu unanichukia kwa maneno ya kuambiwa na Rebby ambayo hayana ukweli wowote, kwa hili umenikera sana na ushapoteza trust yangu Kwako. Unaweza kuniambia sababu ya wewe kufanya hivi before sija kutia kibao?”

“Insider calm down, please. Let’s talk about this.”

“Talk what?, mimi naondoka sina hata second ya kukusikiliza, kwaheri.”

Na mimi niliondoka pale nimemuacha amekaa kwenye coach na nilisikia akiniita na mimi hata sikuwa na habari naye. Baada ya kufika parking sikutaka kupoteza muda niliwasha gari na wakati natoka pale getini kwa upande mwingine nilimwona ametoka pale nje lakini alikuwa kachelewa tayari na niliondoka kwa kasi sana.

TO BE CONTINUED.
Blessed
 
Hii imeendaa hii!!

Naona ameota mapembe na ameshamjulia Iryn kwake hachomoi!

Nimependa alivokaza pamoja na kuliwa!!
Hapana naenda against na ww kuhusu kuota mapembe ....

Vuta picha ya maisha ya kawaida yaani mtu mnaaminiana afu anakusengenya ni red light kubwa Sana kuwa lolote unaweza fanyiwa msimamo wake ni mzuri pia tupo pamoja
 
IN ADDITION

Sikuwai kuwapa muendelezo kwa kilichotokea kwa Uncle wangu. Alihama pale Mikocheni alijenga nyumba yake huko Bunju. Sasa mwaka 2020 wachina waliondoka Tanzania, sababu kubwa ilikua ni kodi. Kama mnavyojua Wachina ni wakwepaji wakubwa wa kodi.

Uncle wangu ni mhuni sana alificha gari ya kampuni mpaka leo analo, na baadhi ya madeni alokuwa anakusanya alikua anaficha. Kesi ilikua kubwa ikapelekea wachina kuamisha stoo yao ya Mabag ili kuzikwepa mamlaka za serikali.

Walikua wanafanya kazi ya kuuza mabag store pamoja na kukopesha na kupunguza bei ili yatoke haraka wao waondoke.

Baada ya kuona hali so hali wakaondoka chap, Uncle pesa alizobaki nazo pamoja na madeni ilikua ni zaidi ya million 80, hizi ni taarifa za ndani kabisa nilipata. Sio hivyo tu, walimwachia na Godown kile kiwanda cha assembling, hivyo kulikua na assets kibao kama ma AC, ma fan, na mazaga kibao. Nyumba walokua wanakaa waliacha mashine nyingi kama mashine za kufulia, yaani waliacha mazaga kibao.

Mzee baba akalifumua lile Godown akauza Mabati, mbao, nyaya za umeme, ma AC, ma fan na mitambo kibao. Unaambiwa kupitia lile godown aliingiza si chini ya 20 million. Bado vitu vingine vilivyoachwa na wachina mle ndani.

Baada ya hapo mzee baba alishindwa kupanga mipango mizuri ya zile pesa akaanza kula bata na madem zake, unaambiwa hata home akawa harudi, ukifungua gari lake unakutana na machupa ya wine na bia tu.

Zile pesa hatimae zikaisha na hakufanya jambo lolote la maana la kimaendeleo, Since 2021 life ni gumu sana. Aunt yangu alikuaga mtu wa nyumbani tu, kuna kipindi nilimpaga ushauri afungue hata biashara ya Mabag hata hakutaka kunisikiliza sababu pesa zilikuwepo. Hata Uncle nilimshauri afungue biashara ya kuuza jumla na rejareja bag zote lakini hakunielewa kipindi kile.

Life limegeuka now wanahali mbaya sana kiuchumi, wale watoto zake hawasomi shule japo walifaulu form 4, yule mtoto mkubwa niliongea naye nimsapoti arudi shule lakini aligoma kabisa, alisema anataka akomae na mambo yake shule hapana. Dogo nilishamsapoti na kiasi cha pesa tayari, mambo mengine atajua yeye.

Aunt aliyekua ananiona mimi fala, now ndo ananitafuta niwe namsaidia. Kuna jambo moja ambalo anataka kulifanya ni kuhusu yule mtoto wa mwisho wa kike. Tulikua tunapatana sana hivyo nitamsapoti kwenye masomo yake akianza secondary hiyo ndo plan yangu.

Kipindi nakwenda kuwasalimia nilienda na mke wangu na mtoto, maana hata familia yangu walikua hawaijui na pia niliwakaribisha kipindi cha kutoa mahali na hawakutaka kuja. That time nilienda na gari kabisa.

Maisha ni fumbo kubwa sana, yule unayemdharau ndo anakuja kuwa msaada kwako. Muheshim kila unayemwona mbele yako, hakuna anayejua ya kesho. Kesho yetu sote hapa ni fumbo.​

EPISODE 10

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Nimeweka kituo hapa nitarudii,,,,
 
EPISODE 64

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN.”

PREVIOUS
Kwa upande mwingine utamu wa Iryn ulinipagawisha na nilijikuta natamani kuendelea kuwa naye maana utamu nilioupata ni wa kipekee, hivyo niliona bora nimtongoze tu ifahamike moja maana hata yeye ananipenda maybe anasubiri mimi nimfungukie. Ukweli nilikuwa nimetembea na wanawake tofauti lakini sio sana maana mimi sio muhuni, lakini Iryn ana utofauti sana asee ni mlaini, ananyumbulika kitandani, anajua mapenzi afu coochie yake ni hot, Prisca alikuwa ananipagawisha lakini Iryn funga kazi.

CONTINUE

Niliwaza pale Iryn anapataje taarifa za mimi kwenda kwa Asmah?, niliwaza nianze kwanza kuongea na Asmah then mengine yatajulikana, kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Mary akipiga simu na mimi nilipokea simu yake,

“Hi Mary.”

“Poa, Insider hupokei simu zangu are you still hungry with me?”

“No Mary I am really sorry nilikuwa nimebanwa sana jana, tell me unaendeleaje?”

“Niko poa naomba kuonana na wewe please.”

“Kwa leo ngumu labda kwa badae nikipata chance nitakucheki, ukiona kimya bhasi kesho.”

“Okay, byee.”

Mary alikuwa anaomba tuonane lakini sikujua anataka kuongea nini na kwa upande wangu nilihisi lazima litakuwa suala la Prisca, pia sikuona sababu ya kumkatalia maana Mary ni mtu wangu wa karibu sana na alinipa kampani sana kipindi cha Msiba.

Niliingia chumbani na nilimkuta Iryn kalala bado na ilikuwa saa 6 mchana tayari hivyo niliamua kumuamsha na kofi la kalio pale kitandani ili ajiandae tuondoke.

“Mummy ulisema tunatoka mchana jiandae tuondoke saa 6 tayari.”

Iryn alishuka kitandani na alivua nguo zake mbele yangu na akaenda bafuni kuoga, kwa upande mwingine hakuwa na aibu na mimi kabisa. Wakati anajiandaa kwa upande wangu nilitangulia kwenda kuonana na mama mlinzi ili anipe key za gari na tulikuwa tunaongea pale,

“Vipi Mzee hajamind alivyoona gari yangu?”

“Nilimpoza kidogo na yeye hata hajapiga kelele, hakuna asiyependa hela.”

“Mama Ahsante sana maana tumefanikiwa kuyajenga badae nitakupa zawadi yako.”

“Usijali kuwa na amani kabisa.”

Na muda huu Iryn alikuwa ameshuka chini tayari kwa safari na aliniita pale, “Insider…..” na mimi nilimpa ishara asogee mpaka usawa gari ili tuondoke maana gari nilipark upande mwingine.

Tuliondoka pale na break ya kwanza ilikuwa pale Mikocheni kwa Osama, na tulinunua chips kuku sahani 8 na soda, Bossy lady aliamua kuwapa offa ya lunch wafanyakazi wake.

Kwa upande mwingine Lucy alikuwa kanipigia sana simu na mimi sikuzipokea wala kuchat naye maana nilijua lazima tungeonana na kuzungumza haya, kwa upande wangu nilisema siwezi kumwambia kilicho endelea kati yetu.

Baada ya kuwasili pale Salon palikuwa busy sana na nilimuacha Iryn reception akiongea na mimi nilikwenda moja kwa moja mpaka ofisini. Haikuchukua muda Lucy alikuja ofisini na alionekana kuwa na shauku sana ya kujua kinachoendelea na uso wake ulichanua tabasamu kubwa sana,

“Insider you made it?”

“Yeah, tumeyamaliza kwasasa tuko cool.”

“Vipi ume hit? Naona Bossy anafuraha sana leo tena ile halisi.”

“Hahahaha hapana Lucy labda amefurahi tulivyo yamaliza.”

“Insider mimi sio mtoto ujue, jana wote hampokei simu zangu na sio kawaida yenu, pia hamja ni call back, leo nawaona mnakuja pamoja, mlilala pamoja jana.”

“Trust me Lucy jana nilikuwa nakunywa bia huko mbezi si unajua na mastress?”

“I know mshikaji wangu ila wewe ni nyoko kama umefanikiwa kuyamaliza bhasi nakupa respect yangu, najua umemla ila hutaki kunambia but nitafound out soon.”

Wakati tukiendelea kupiga story pale kwa upande mwingine Iryn alikuja ofisini,

“Lucy kumbe umekuja kukaa huku na Insider, tumewaletea chakula kiko kwenye gari, Insider tuondoke.”

“Kila ukiniona na Lucy lazima utuharibie maongezi yetu.”

Tuliondoka pale Mikocheni kwenda Masaki na wakati tuko njiani tulikuwa tunapiga story sana na pia ilibidi nimuulize sababu ya kumuachisha kazi Sumaiya.

“Mummy kwanini umemsimamisha kazi Sumaiya?, kwa hili sijapenda kwakweli unajua mtoto wake amelazwa?.”

“Sijamuachisha kazi ila nime msimamisha kwa muda kutokana na tabia zake, kumbuka yeye ndo incharge pale then anachelewa na hatoi taarifa anajenga nini kwa hawa wengine? ndomana nimechukua hatua.”

“Ulitakiwa uulize kwanza kabla ya kuamua kufanya maamuzi ya kipumbavu kama haya, kumbuka yule ni binadamu afu anamtoto, taarifa alitoa kwangu lakini wewe ulikuwa umeniblock, kwa hili umezingua sana, afu kumbuka hii ni kampuni huwezi kumsimamisha mtu bila barua akienda mahakamani utachomoka.?”

“Nimepata taarifa zake pia anafanya ujanja sana kwenye mauzo ana haribu reputation ya kampuni kumbuka hapa Masaki wateja wetu wengi ni foreigners.”

“Ni sawa unachosema lakini lilikuwa ni suala la kukaa naye chini, Sumaiya nafanya naye kazi vizuri na hakuna kilichoharibika, ifike mahala chuki zako kwa Sumaiya ziishe, tufocus na kampuni. Naomba umrudishe kazini kesho na usipo fanya hivyo na mimi naandika barua ya kuresign position yangu, maana taarifa alitoa kwangu.”

Ilibidi nimtetee Sumaiya muda huu ili kibarua chake kirudi, wivu wa Iryn ndo ulisababisha amsimamishe kazi.

“Sumaiya atarudi kazini na atakwenda kusimamia kampuni ya usafi na sio huku Salon tena, atakuwa manager na mshahara atapandishiwa.”

“Hapo sawa najua hutaki niwe naye karibu but sio mbaya nitampa hizi taarifa badae.”

“Unamtetea sana b*tch wako”

Baada ya kuwasili pale ofisini Masaki nilipark gari na tulikwenda moja kwa moja mpaka ndani na mimi niliamua kwenda ofisini kwa Asmah kumsalimia na sikumwambia kama nimekuja na Iryn. Kwa upande mwingine nilimkuta anachati na baada ya kuniona tulianza kupiga story pale, na mimi kichwani plan zangu nianze kumspy,

Asmah ni mtu ambaye yuko kivyake vyake na sio mtu wa kampani, she is minding her business,

“Baby nakuona umetulia umekula?”

“Nilikuwa na order hapa food bora nimekuona utanilipia.”

“Usijali leo nitakupa offa, naomba tuongee jambo moja maana sielew elewi.”

“Insider jana nimekupigia simu ili tuonane lakini hukupokea nilitaka tuongee haya.“

“Jana nilikuwa busy ndomana, pia kuna kitu hakipo sawa, Iryn amejuaje kama mimi huwa nakuja kwako?.”

“Hata mimi sijui kwakweli au huwa unamuachia simu yako anaikagua.?”

“Iryn hashiki simu yangu, mimi ndo nikuulize wewe labda kuna mtu humu ndani mnashare mambo yenu?.”

“Insider wewe unanijua vizuri sinaga time na mashosti wa humu ndani na ninaanzaje kushare hii kitu?.”

“Huwa una share simu yako na mtu yoyote humu ndani? tuanzie hapa kwanza.”

“Yes!, Rebecca mara nyingi huwa ananiazima simu yangu na ndo yeye ambaye huwa anaomba hakuna mwingine.”

“Rebecca ana snitch? Mbona kama haimake sense.”

“Insider nahisi Rebecca anasnitch atakuwa anaangaliaga chats zetu na anampa Bossy taarifa. Pia kuna siku niliwakuta ofisini wamekaa wanaongea baada ya mimi kuingia wakakatisha maongezi yao, kwa hili leo nimehisi ni yeye.”

“Sawa niachie mimi nitajua ya kudeal naye ila kwasasa uwe unafuta chats na usimpe simu yako.”

“Rebby ni mshenzi sana.”

Mpaka hapo nilihisi Rebecca anahusika moja kwa moja kumpa taarifa Bossy lady kinacho endelea pale ofisini na wakati tukiendelea kupiga story, kwa upande mwingine Iryn alifungua mlango na alituona na Asmah tunacheka, alimsalimia Asmah na akanipa ishara ya kuondoka.

Baada ya kufika parking na kuingia kwa gari Iryn alikuwa ananiangalia sana ni kama alimind kuniona kuwa na Asmah pale ofisini.

“Tunakwenda kula wapi?”

“Chagua mwenyewe sehemu nzuri tukale.”

Na mimi nilindesha gari mpaka Moyo kitchen na baada ya kuingia ndani tuliagiza chakula na tukaanza kupiga story pale, kwa upande wangu
nilikuwa nampango nianze kumtongoza lakini nilikuwa nakosa point, na muda huu wote tulikuwa kimya na yeye alikuwa busy na Iphone yake, muda huu na mimi nilianzisha maongezi,

“Bossy mbona hunambii kama umeniachisha kazi.?”

“Nimekuachisha lini? Mbona sikuelewi Insider.”

“Kitendo cha kumpa Asmah majukumu yangu ulikuwa unamaanisha nini?”

“Insider ulitaka nifanyaje wakati ulikuwa hutumi ripoti?”

“Si umeni block wewe?.”

“Ripoti unatuma kwa whatsapp sikuhizi? na sio kwa mail tena.”

Na mimi nilibidi ninyamaze tu maana kweli nilikuwa nimezingua,

“Hivi kwanini unanichukia na unakuwa na wivu na mimi?”

“Insider mimi siko hivo kama unavyofikiri naona unakuwa hujiamini.”

“Iryn do you love me?”

“Yes I was, but toka nifaham una mke upendo wangu kwako ulikufa na hizi scandals zako zina nisogeza mbali na wewe.”

“Mbona mimi nilivyojua unadate na Grizz upendo wangu ulizidi kuimarika kwako na sikuonesha sign yoyote ile au unafikiri na mimi sikuumia?. So hapa unanionesha ni jinsi gani ulivyo mbinafsi unaangali moyo wako tu.”

Na muda huu Iryn alinyamaza kimya na alikuwa anajifanya kuwa busy na simu yake, baada ya kuona nimemkamata tayari niliendelea kutema sumu kama Koboko,

“Iryn embu niangalie usoni, mimi sipendi dharau ujue, naongea na wewe upo busy kuchezea simu kuonesha mimi naye ongea ni kama fala kwako.”

“Insider nakusikiliza vizuri kabisa… Okay sorry endelea.”

“Mimi nataka tunavyotoka hapa kila mmoja awe hana kinyongo na mwenzake, tuzimalize tofauti zetu. Mimi nakuahidi hutaniona nikifanya mautani na kina Sumaiya, kama hili huwa linakukwaza bhasi kwasasa hapana.”

“A good start, najua una utani nao sana na wamekuzoea sana, but kuwa na mipaka.”

“Pia nataka leo utambue mimi Insider nakupenda sana nataka ikiwezekana uwe mke wangu.”

“Eti what…?” Na muda huu Iryn alinza kucheka maana aliona huyu MTALIBAN anazingua,

“Insider suala la mimi na wewe kuwa kwenye mahusiano haliwezekani kwasasa, nimeachana na Grizzman sababu hii afu tena nianze tena mahusiano na wewe mme wa mtu? na isitoshe mama J ni rafiki yangu unafikiri atajisikiaje akilijua hili?, kumbuka ana Moyo kama mimi. Kuna msemo unasema “what’s goes around comes around “ and karma is bitch.”

“Actually nilitaka wewe uamue kama unaona suala la mimi na wewe kuwa kwenye mahusiano haliwezekani bhasi tuendelee kuwa washikaji tu.”

“Kwa hili nakuunga mkono na wewe utulie na mke wako, unajua unabahati sana ya kuwa na mwanamke mzuri mwenye brain.”

“Haya hayakuhusu, tuondoke mimi nina appointment zangu badae kumbuka niko na wewe toka jana kuna mambo yangu ya kutakecare.”

Tuliondoka pale huku tumeongozana na mimi nilikuwa niko nyuma yake namfanyia mautani ya kumsfia jinsi alivyo na kiuno kizuri pamoja na cut-walks zake. Baada ya kuingia kwa gari tulianza safari na kwa upande wake alisema ni mpeleke kwa Lucy.

Wakati tuko njiani simu yangu ilianza kuita na ile kuangalia alikuwa ni Prisca akipiga na mimi bila wasiwasi niliipokea simu yake. Kwa upande wake Prisca alikuwa bado haamini kama kweli nimemuacha na alikuwa bado ananisisitiza sana tuendelee na mahusiano, lakini mimi niliendelea kumkazia kuwa suala la mahusiano halitojirudia tena.

Kwa upande mwingine Iryn alikuwa makini sana kufuatilia maongezi yetu na alijua ninaongea na Prisca, lakini alinyamaza kimya.

Baada ya kuwasili Mikocheni nilimdrop pale na nikamuaga lakini kwa upande wake alifungua mkoba wake na akatoa noti 3 za $100 na akanipa,

“Insider kaweke mafuta hii nina muda sana sijajaza mafuta byee, takecare.”

Kwanza ilibidi nishangae maana niliona kama utani hivi, ukweli toka nianze kumkera Iryn alipunguza kunipa maokoto, ndomana nilishangaa kuona katoa pesa.

“Bossy unanipa malipo ya kutumika jana nini?Ahsante nashukuru.”

Na muda huu Iryn aliishia kucheka tu na mimi nikaondoka maneno haya kuelekea home. Baada ya kufika home na kupark gari nilikwenda kulala kwani nilikuwa nasikia sana uchovu muda huu.

Nilimka saa 1 usiku na nikiwa bado kitandani niliwaza niwe na mchepuko mmoja wa kunipunguza stress, Iryn alikuwa kachomoa tayari hivyo nilikuwa nina option 2 zimebaki kwa Mary au Asmah. Kwa upande wa Asmah niliona bora huu mpango niachane nao na nikae naye mbali.

Mary ndo alikuwa anafaa kuwa mchepuko lakini sasa niliwaza pale, je Mary atakubali? na atanichukulia mimi kama mwanaume ambaye sijatulia, ukweli alikuwa ananipenda lakini toka afahamu mahusiano yangu na mdogo wake hakuwai tena kuonesha sign yoyote kwangu na hii ndo ilinifanya nimwone Mary ni mwanamke mwenye msimamo. Lakini pia niliwaza kudate na mdogo mtu then dada mtu haitakuwa busara hivyo niliona huu mpango utakuwa mgumu kwangu.

Kwa upande mwingine toka nisex na Iryn nilikuwa nimeridhika kabisa kitendo cha kumla siku nzima kwangu ilikuwa ni ushindi tosha hata alivyonambia hawezi kuwa na mimi niliona sawa tu, hata sikuwa na kinyongo.

Muda huu nilichukua simu yangu na nilimpigia simu Mary na iliita mpaka ikakata bila kupokelewa na mimi nilikwenda zangu kuoga. Wakati nimetoka bafuni simu iliita tena na alikuwa ni yeye akipiga na baada ya kuongea tulikubaliana tukutane Havanna ya pale Mbezi Beach classic Mall.

Saa 2 usiku mapema nilikuwa nimewasili pale kwa upande mwingine yeye alikuwa hajafika bado na ilimchukua kama nusu saa kuwasili maeneo haya na alinikuta nina kunywa taratibu. Tulisalimiana pale na yeye kwa upande wake aliagiza wine na story zilikuwa zikiendelea,

“Insider kwanza niombe radhi kwa ile siku maana nilikuwa na hasira sana juu yako, lakini nimegundua Prisca mwenyewe ndo aliyekubali.”

“Usijali najua wewe kama dada lazima ungeumia lakini Prisca ndo aliyekubali na sikumlazimisha, hata mimba aliibeba bila ridhaa yangu.”

“Ameniambia haya yote lakini nilitaka kusikia kutoka kwako shemu, pia amenambia umemuacha na hajanipa sababu shida ni nini Insider?”

“Ongea na mdogo wako akwambie kila kitu, kavunja makubaliano yetu na mimi nayeye ndo bhasi. I made mistakes lakini sio sasa.”

“I need you guys back together, msiachane.”

“Mary haiwezekani kwakweli acha nifocus na familia yangu kwasasa.”

Kwa upande mwingine Mary aliomba azione picha za familia yangu na mimi bila hiyana nilimwonesha na aliomba siku aje aisalimie familia yangu na mimi nilimkaribisha.

Tulikaa pale na Mary tukiendelea kuongea mambo mbalimbali na kubwa nilimshauri atafute nyumba apange aanze kujitegemea maana ashakuwa mkubwa tayari. Kwa upande wake aliufurahia ushauri huu na akasema ataongea na wazazi wake afu atanipa mrejesho.

Saa 5 usiku tuliagana na yeye alirequest usafiri wa kumrudisha home, kwa upande mwingine wakati niko na Mary, Sumaiya alikuwa amepiga sana simu, baada ya kuachana na Mary ilibidi nimpigie simu.

Baada ya kufanya mazungumzo na Sumaiya nilimpa taarifa za kuamishiwa ofisi nyingine ile ya usafi na yeye kwa upande wake ni alifurahi sana, pia alinishukuru sana.

“Wewe mwanaume unanisaidiaga sana lakini kila nikitaka nikutunuku unaringa.”

“Hahahaa inaonesha umedhamiria sana usije ukaniua bure, afu kuna kitu naomba nikuulize noana kuna something fishy kinaendelea pale ofisini. Nahisi Rebecca ananisnitch kwa Iryn yaani kila nacho fanya anakuwa na taarifa zangu, lakini bado nafuatilia.”

“Huyo ndo snitch sasa na kama hujui, kila kinachofanyika pale ofisini yeye ndo anampa taarifa Queen na suala langu yeye ndo alinichongea. Mimi na yeye hatupatani toka nichukue madaraka yake hili jambo mpaka leo linamuuma, nilitegemea angepewa uongozi lakini kapewa Asmah.”

“Duuh aisee kumbe watu mna mabifu toka muda, usiku mwema tutawasiliana kesho.”

Yalikuwa ni maongezi marefu sana mpaka nafika home getini na wakati naongea na Sumaiya kwa upande mwingine Iryn alipiga simu lakini nilikuwa natumika na baada ya kumaliza maongezi na Sumaiya nilimpigia lakini ilikuwa bado blocked.

********
Jumatatu asubuhi mapema nilikwenda Mbweni kumsalimia Jane pamoja na kumjulia hali, baada ya kuwasili pale kwake nilipokelewa na Vicky lakini yeye alikuwa amelala. Nilikwenda kuangalia maendeleo ya mbwa na niliwaona wakiwa na afya nzuri na nilikwenda kuangalia gari yangu IST na ilionekana kubondwa upande wa nyuma na pembeni kwenye mashavu ilikuwa imebonyea.

Nilirudi ndani na tuliendelea kupiga story na Vicky na alikuwa ananipa maelezo namna jane alivyobamiza gari wakati anarudi reverse. Kwa upande wa gari ilikuwa imebonyea mlango wa buti, taa moja ya nyuma ilikuwa imevunjika pia, kwa upande wa mbele bampa lilikuwa halifai alikuwa kagongesha sana.

Kwa upande mwingine Vicky aliomba nimpe kampani ya sokoni kwenda kununua vitu na alikwenda kujiandaa na mimi nilikuwa pale seblen. Baada ya dakika 10 alitoka na tukaanza safari ya kwenda sokoni na tulikwenda Nyuki sokoni. Njiani tulikuwa tunaongea mambo mengi sana maana vicky ni talkative,

“Insider wewe na Mary mmegombana?”

“Hapana why unauliza?”

“Niliwoana hampo sawa siku ile, shida ni nini?”

“Hamna kitu tuko cool kabisa.”

“Mhh sawa na uliniahidi weekend hii unanitoa out lakini umezingua.”

“Nilikuwa nimebanwa kidogo afu unajua mimi nakuchukulia wewe kama mdogo wangu.”

“Insider umeanza dharau sasa, nimeshakuwa mtoto tayari.”

“Sijasema mtoto nakuchukulia kama mdogo wangu wa karibu, kuna mambo naweza yafanya huko afu kwako yakawa mageni.”

“Wasiwasi wako tu mimi sina utoto wowote.”

“Bhasi tutacheki this week tutoke.”

Baada ya kuwasili pale sokoni nilimpa kampani ya kununua mahitaji na baada ya kumaliza tulirudi Mbweni, kwa upande mwingine Jane alikuwa ameamka tayari na alikua amekaa kibarazani.

“Shem nilisikia sauti yako, nimeamka naambiwa mmetoka.”

“Vicky aliomba kampani ya kwenda sokoni ndo tumetoka huko.”

Tuliendelea kuongea pale kibarazani na pia alizingumzia suala la kuiharibu gari yangu na yeye alisema atanirudishia pesa ili nikanunue Ist nyingine na pia nimpe gharama za matengenezo ya gari. Baada ya kuzisikia hizi taarifa sikutaka kukataa maana gari alikuwa ameibonda sana na kuhusu Dualis alisema niendelee kuitumia mpaka atakapo jifungua ndo ataichukua.

Kwa upande mwingine tumbo lake lilikuwa kubwa sana na alikuwa anaonekana kuchoka sana kipindi hiki. Niliendelea kushinda pale kwa Jane na ile mchana Mzee Mollel alinipigia simu na alinipa taarifa ya kukamilika kwa nyumba na ipo tayari kwa kuhamia. Ofcourse nilifurahi sana kuzisikia hizi taarifa na nilimwambia Mzee Mollel wiki hii Ijumaa nitakwenda Dodoma kwaajili ya hili suala.

Jioni niliondoka maana nilikuwa na Vicky tu pale seblen na wakati natoka tulikuwa tumeongozana mpaka naingia kwa gari, na yeye alikwenda kunifungulia geti. Wakati narudi reverse kwa upande mwingine Jane alionekana akitoka ndani na alinipa ishara ya kusimama na akasogea mpaka usawa wangu na mimi nikashusha kioo nimsikilize,

“Insider nilikuwa na jambo nataka kuzungumza na wewe kwa bahati mbaya nilisahau mpaka nashtuka unaondoka.”

“Una jambo gani shem maana unanitisha.”

“Usiogope but tutaongea next time ukija.”

“Sawa shem haina shida.”

Na mimi nikaondoka maeneo haya lakini njiani nilikuwa nawaza Jane atakuwa na jambo gani?. Na mimi nilirudi home kulala mapema kwa upande mwingine Iryn alikuwa bado ameni block.

Jumanne asubuhi nilikuwa na miadi na mama wa2 na aliniomba kampani ya kwenda Madale kwenye nyumba yake ili akafanye usafi kabla ya kuhamia. Wakati najiandaa pia nilipigiwa simu na mama Janeth na alikuwa anaomba badae tuonane kwani ana mazungumzo muhimu na mimi.

Ilikuwa saa 3 asubuhi na nilikuwa nimewasili tayari kwa mama wa2 na baada ya kuingia ndani nilikaribishwa dining kunywa chai na baada ya hapo tuliondoka kuelekea Madale tukiwa na Rachel pamoja na dada wa nyumbani.

Baada ya kuwasili pale Madale kwa upande mwinginenyumba ilikuwa imekamilika tayari kasoro chini ilikuwa bado kuweka pervings kwa upande wa ndani ilikuwa kila kitu tayari. Pia kwa ndani walionekana mafundi wanaweka fimbo za mapazia na wengine walikuwa wanafunga taa.

“Mama mkwe hongera sana umepambana kwakweli.”

“Nashukuru sana hata siamini kama nimefanikisha, Mungu amenisaidia sana.”

“Kweli kabisa ngoja nitafute mtu atusaidie kufanya usafi wa nje.”

Tulisaidiana kufanya usafi wa ndani na nje na ndani ya masaa 3 tulikuwa tumemaliza na mchana tulitoka kwenda kupata lunch kwenye moja ya mgahawa pale Contena. Muda huu tulikuwa tunaongea mambo mengi sana na mimi kwa upande wangu nilimpa taarifa za kumalizika kwa nyumba yangu kule Dodoma na yeye aliishia kunipongeza sana, na mimi nilimwambia bila yeye nisingeweza kukamilisha.

Kwa upande mwingine tuliongelea suala la usafiri wa kumfuata asubuhi kule Madale maana zoezi lingekuwa gumu sana, hatahivyo ningempa gharama kubwa. Tulishauriana pale awe ana request usafiri wa kumpeleka kazini, pia kwa upande wake alisema anaplan anunue Dualis maana ameipenda sana ile ya Jane.

Muda wa jioni tulitoka pale Madale na nika warudisha home na mimi sikutaka kupoteza muda niliaga maana nilikuwa nasafari ya kwenda Masaki kuonana na Mama Janeth. Niliamua kupitia kwanza Masaki ofisini ili niendelee kubuy time navyosubiri muda ufike.

Baada ya kuwasili pale ofisini nilikwenda moja kwa moja mpaka kwa Rebecca na nikamuomba simu yake ili nimpigie mtu. Rebecca alinipa simu yake hata hakuwa na maswali na mimi nilikwenda nayo moja kwa moja mpaka ofisini kwangu na nilianza kukagua simu yake taratibu, nilikwenda direct kwenye conversation zake na Iryn. Baada ya kufungua chats zao nilikuta ujinga wote mle kuhusu kila kitu kinachoendelea pale ofisini huwa anamwambia Iryn, nilishangaa sana kwakweli maana Rebecca alikuwa TISS wa Iryn.

Kwa upande wangu nilipiga picha baadhi ya chats afu nikaiweka simu yake mezani nikaendelea na mambo yangu. Niliwaza pale nikaona Iryn anafanya ujinga sana kunifuatilia na nilijisemea kwa hili lazima nikamuwashie moto.

Niliendelea kuandaa report na kupitia baadhi ya taarifa incase mama Janeth akiuliza niwe na cha kumwambia, baada ya dakika 10 Rebecca alikuja ofisini kuchukua simu yake na mimi nilimpa ishara ya kukaa chini.

“Rebecca unajua wewe ni mtu wangu wa karibu na ninakuheshimu sana, kwanini unaingilia privacy zangu?”

“Insider mimi niingilie privacy zako kivipi?, mbona sikuelewi?.”

“Rebby usinione mimi ni mtoto najua unanisnitch kwa Iryn, hata Sumaiya umemsnitch kafukuzwa kazi, vipi umeona raha?, ukiendelea kukaza fuvu ninaweza kukuharibia kama ulivyofanya kwa Sumaiya, sasa nataka unambie kwa nini unafanya hivi?.”

Muda huu Rebby alianza kuwa na wasiwasi na alianza kutetemeka ni kama alijua nimecheki simu yake,

“Samahani manager, bossy ndo alinipa hii kazi ili kulinda kibarua changu.”

“Sawa najua sio wewe lakini ulimuuliza kwanini anakupa hii kazi ya kunichunguza mimi?”

“Sikia manager ipo hivi Iryn alikuja akanambia anataka kuwa kwenye mahusiano na wewe hivyo anaomba niwe nakuchunguza movement zako zote za hapa ofisini, hata hio simu kanipa sababu ya hii.”

Inshort Rebby alifunguka mambo mengi sana muda huu kuhusu hili jambo na aliniomba sana msamaha,

“Rebby ukitaka nikusamehe mpigie simu Iryn na umwambie taarifa unazompa mostly sio za kweli ndo utapata msamaha wangu.”

“Insider please atanisimamisha kazi.”

“Unajua ni namna gani nimetumia kurudisha mahusiano yangu karibu na Iryn?. Ulishajaribu kuwaza kuwa unachofanya ni unabomoa na sio kujenga.?”

“Nisamehe sana I had no choice, pia Iryn anafanya kwa mazuri, anakupenda sana Insider.”

“Fanya kama nilivyokwambia Rebby kwaheri.”

Na mimi niliamua kuondoka na nilimuacha pale ofisini amekaa kwenye kiti na alikuwa kama mtu ambaye hajui afanye nini.

Niliondoka pale ofisini kuelekea kwa mama Janeth na nilitumia muda mchache sana kuwasili pale kwake. Baada ya kuwasili nilikaribishwa ndani seblen na kwa upande mwingine nilimkuta Sumaiya amekaa pale seblen akiwa na mama Janeth.

Niliwasalimia wote na mimi nilikaa chini, ofcourse sikutegemea kama ningemkuta Sumaiya pale na kwa upande wake naye alikuwa anashangaa, ilikuwa ni kama surprise. Mama Janeth aliniomba twende kibarazani tukaongee na tulimwacha Sumaiya amekaa sebleni.

Mama Janeth alinambia sababu kubwa ya kuniita ni kunipa taarifa za kuondoka kwa Sumaiya pale ofisini ili akasimamie ofisi ya usafi. Kwa upande wake aliniomba msamaha kwa hili maana alisema anampenda sana Sumaiya na ana muamini sana, kwa upande wangu sikuwa na neno kwanza nilifurahi kusikia maneno ya mama Janeth. Tuliendelea kuzungumza mambo mengine mengi ambayo ni siri siwezi kuyaandika hapa na kubwa lingine aliniomba niwe namsaidia mambo ya uchumi kama budgeting nk, pale ambapo nitahitajika.

Kwa upande mwingine Sumaiya alikuwa amelamba bingo anatoka kwenye balimi anahamia kwenye heineken, na mama Janeth alimtaka Sumaiya afanye kila mbinu kupata wateja wengine wengi wakuingia nao mikataba. Hii kampuni ya usafi wateja wake wengi ni hizi organizations, kuna baadhi ya hotels na offices, japo mama Janeth alikuwa na mipango ya kupenetrate mpaka serikalini.

Mama Janeth alinipongeza sana kwa utendaji kazi wangu na alionekana kunikubali sana, ukweli niliibadilisha sana ofisi hasa kiutendaji na nili implement operating stategies (mbinu za kiutendaji) ambazo zilisaidia sana kufanya vizuri kimauzo na kupelekea kupata wateja wengi. (Siwezi kutaja hizi mbinu kwa maslahi ya kibiashara).

Tulikaa pale mpaka tukapata dinna ya pamoja na wakati tunapata chakula kwa upande mwingine Iryn alikuwa ananipigia sana simu, lakini nilikuwa nashindwa kuipokea maana ingeleta picha mbaya, hivyo nilisubiri nimalize kula then ningempigia.

Saa 2 usiku tuliaga pale kwa upande mwingine mama Janeth alinambia nimpelekee Iryn gari awe anatumia maana mara nyingi zinakuwa amezipark tu pale uwanjani, na yeye anatumia sana gari za ofisi.

“Sasa utaipelekekaje hii gari maana umekuja na gari yako au utakuja kesho?, ni kama saprise nataka mfanyia bint yangu.”

“Kesho ni ngumu, ngoja nimtafute dereva wa Uber nimuombe tuongozane afu nitamlipa, hawezi kukataa.”

“Yes! Good idea son.”

Na mimi nilifanya kurequest bolt na nilimpata dereva alikuwa karibu na baada ya kumpigia simu nilimuelekeza ataendesha gari yangu mpaka Kawe na yeye hata hakubisha na tulikubaliana elfu 30.

Mama Janeth alikwenda ndani na baada ya muda mfupi alirudi ameshikilia funguo na alinikabidhi pamoja na Leseni ya Udereva ya Iryn. Kwa upande wa gari alinipa funguo ya ile gari yake Audi Q7, baada ya dakika 5 dereva wa uber alikuwa kawasili na tuliaga pale.

Mimi nilikuwa nimempa lift Sumaiya ili nikamdrop pale Morocco, na wakati tuko njiani tulikuwa tunaongea masuala mbalimbali na kubwa alifurahi sana kwa kupata mkataba mpya na alinishukuru sana kwa kumpigania kwa Iryn.

“Insider thank you, Queen alinipigia simu na ameniomba msamaha kwa yote na ndo aliyesema nije kwa mama Janeth.”

“Wow nimefurahi sana kusikia hivyo na kingine nimemzingua sana Rebby hana hamu leo, maana nimemdaka vizuri sana.”

Ilibidi nimpe mkanda mzima Sumaiya namna nilivofanya ujasusi wangu mpaka namdaka, na aliishia kunipongeza kwa hili.

“Insider ofisi ipo hapahapa Masaki so hatuko mbali sana na wewe muda wa lunch tutakuwa tunaonana.”

“I told you Mama Janeth anakuelewa sana lakini hukutaka kuniamini rafiki yangu, kwanza hujawai kunambia mlikutanaje na mama Janeth.”

Sumaiya alinipa mkanda mzima namna walivyokutana na mama Janeth, kwa ufupi walikutana Posta kwenye hayahaya masuala ya Salon ndo mpaka leo. Baada ya kuwasili pale Morocco bus stand kwa upande mwingine Sumaiya aliomba nimkope pesa,

“Insider naomba niazime kama laki 2 cash maana mshahara wote nimelipa kodi ya nyumba na suala la mtoto nalo limenimalizia pesa.”

“Mtoto anaendeleaje kwasasa? Na ana umri gani.?

“Anaendelea vizuri ana miaka 4 na anakaa kwa mama yangu mzazi.”

“Sawa kwa sasa mimi sina cash ila nina dollar utaenda kuexchange kesho na utanirudishia pesa yangu mambo yako yakikaa vizuri.”

Na mimi nilitoa noti moja ya $100 kwa zile noti alizonipa Iryn na nikampa pale, kwa upande wake alifurahi sana na wakati anaondoka alinikiss shavuni, na sisi tukaendelea na safari kwenda kwa Iryn nikiwa na jamaa nyuma akiendesha Dualis.

Baada ya kuwasili kwenye zile apartments mlinzi alisogea yule mzee na baada ya kuniona mimi tulisalimiana na akafungua geti, tukaingia ndani. Tulipark gari zote usawa wa apartment ya Iryn na mimi nilimlipa jamaa pesa yake na akaondoka pale.

Baada ya kufika mlangoni nilifungua lakini ulikuwa umefungwa hivyo ilinibidi nigongea pale, niligonga lakini alikuwa hafungui mpaka nihisi labda atakuwa ametoka, nilijaribu kumpigia simu lakini nilikuwa bado niko blocked.

Niliwaza pale labda atakuwa ametoka lakini mzee angekuwa alinambia kama ametoka, hivyo nilihisi atakuwa amelala, niligonga tena kwa nguvu ndo akatoka kunifungulia,

“Mbona nagonga mlango hufungui?”

“Nilikuwa nimekaa kwa balcony ngumu kusikia, mbona hupokei simu zangu toka jumapili?.” Na alionekana kumind sana,

“Kila nikikupigia simu umeniblock afu unalalamika nini? Huoni unafanya utoto?. Nimekuletea gari pamoja na leseni kutoka kwa mama Janeth.” Na mimi nikamkabidhi pale.

“Woow thank you kumbe mama alikuwa serious juu ya kunitafutia Driving licence.”

“Na maongezi nawewe afu, why unanichunguza unaweka mpaka mtu wa kunispy?.”

“Insider umejuaje kama mimi nakuspy?”

“Ina maana hujui ujinga unaofanya sindio?

Na muda huu nilianza kumuwashia moto kwa ujinga wake na nilikuwa na hasira kwelikweli, kwa upande wake alikuwa anaogopa sana.

“Kumbe kwa muda wote huu unanichukia kwa maneno ya kuambiwa na Rebby ambayo hayana ukweli wowote, kwa hili umenikera sana na ushapoteza trust yangu Kwako. Unaweza kuniambia sababu ya wewe kufanya hivi before sija kutia kibao?”

“Insider calm down, please. Let’s talk about this.”

“Talk what?, mimi naondoka sina hata second ya kukusikiliza, kwaheri.”

Na mimi niliondoka pale nimemuacha amekaa kwenye coach na nilisikia akiniita na mimi hata sikuwa na habari naye. Baada ya kufika parking sikutaka kupoteza muda niliwasha gari na wakati natoka pale getini kwa upande mwingine nilimwona ametoka pale nje lakini alikuwa kachelewa tayari na niliondoka kwa kasi sana.

TO BE CONTINUED.
Uuuh sasa ndo huu legend hapo nimekukubali mwambaaaaaa😂😂.
Antonnia ccy asante sana kwa tag
Kaparo
Kalpana
 
Hapana naenda against na ww kuhusu kuota mapembe ....

Vuta picha ya maisha ya kawaida yaani mtu mnaaminiana afu anakusengenya ni red light kubwa Sana kuwa lolote unaweza fanyiwa msimamo wake ni mzuri pia tupo pamoja
Hapana boss lady hamsengenyi Insaida ila anafanya hivo ili ajue ni mwanaume wa aina gani as mtu anaemfeel ukute hizo hekaheka zake za kizinzi za chini chini ndio zilizomtoa Iryn kwenye reli ya insider! True love comes with jealous in it!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom