Jinamizi ni nini? Kwanini hutokea wakati wa kulala tu?

Pia kisayansi ukilala chali unadisturb equilibrium ya ubongo na moyo ndo sababu ya kisayansi ya hayo mauzauza. Inashauriwa usilale usingizi ukiwa chali position. Vifo vya ghafla usingizini pia usababishwa na kulala chali
atoto na we unalalaga chali dada'ngu? njoo huku umsikie shostito cute b na mauzauza yake, kumbe siku ile tunamtafuta alipatwa na mauzauza ya kulala chali bana

Yes name sayansi hii niliwahi kuisikia. Inahusiana na ubongo. Mimi pia nikilala chali ( mara nyingi huwa bila ya kujua) nikiamka kichwa huwa kinauma sana. Naamini ni kuhusiana na masula ya ubongo!
 
Habari zenu wakuu,

Kuna vitu ambavyo naviwaza sivipati majibu mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie.

Ni kwanini mtu unapolala kwa kuangalia juu yani bati anakuwa anaota ndoto mbaya za kutisha na kama vile kuna kukabwa flani hivi na hii sio kwangu tu nimewasikia watu wengi pia wakilalamika.

Je, jambo hili linahusiana na mambo ya kichawi kama wengi wanavyozani? Au kuna namna kisayansi lazima itokee endapo mtu akilala hivyo labla kuna vitu vinaforce ubongo kuhisi hivyo?

Wataalam naombeni msaada wenu

Mmh! Ni imani tu
Kama ilivyo ukiwa na imani hata mlima ukiuambia ng'oka unang'oka.
Kikukaacho moyoni ndicho kikutokacho.
Jamani hata mimi kabla niliwaza hivyo lakini kwenye safari ya maisha nikapata tatizo katika moja ya ushauri wa kitiba niliopewa ni kulala chali. Tena mwanzoni ilikua kulala chali 24/7 kwa hiyo hata kula nilikula nikiwa chali bila kuinua hata kitanda watu walijaribu vyote na mirija ya aina zote but kula ni kula na kuna imani ukila huku umelala chakula sijui kitakupalia sijui nini mambo mengi. Lakini hakuna kitu.
Nina 7yrs now ninalala chali sioti wala nini. Mwanzoni nilikua nachoka tu lakini nimeshazoea.

Kwahiyo hakuna jipya wala lolote kwahilo zaidi ya imani.
 
Kisayansi ukilala chali ulimi unaweza kurudi nyuma na kuziba koo la hewa, na ndio maana unahisi kukabwa (kukosa hewa/kushindwa kupumua) kwa kuwa upo usingizini hauwezi kujitambua hivyo utahangaika hadi utakapoamka utaweza kuurudisha ulimi na utasikia ile hali imeondoka.

Huo ndio ukweli ukilala chali ulimi unarudi nyuma na kuziba koo pia intake ya oxygeni inakuwa ndogo hali inayosababisha ubongo kupata oxygen kidogo matokeo yake ni hizo ndoto za mauza uza ni sawa na vidudu aina fulani vya malaria vinapokuwa kwenye damu na damu hiyo inapoenda kwenye ubongo husababisha hali fulani ya kuchanganyikiwa wataalamu huita celebral maralia
 
Kwanza lazima uelewe kuwa dunia ina pande tisa , nane Zinajulikana na kutajwatajwa lakini nne ndio maarufu zaidi nazo ni kaskazini kusini mashariki na magharibi na upande wa tisa usiotajwa sana ni kile kitovu au Shina linalounganisha hizo pande linaitwa central axis

Pili hili anga limejaa roho na mapepo yaliyozagaa kila mahali na kama ujuavyo roho/pepo ni energy kitu chepesi kabisa kisichoonekana wala kushikika

Kwahiyo kinachotokea ni kwamba unapolala chali na kuangalia juu ni kama unakuwa kwenye central axis ya dunia yanapopita roho na mapepo yote lakini vilevile ni kama unayaalika kwakuwa unakuwa kama uko kwenye cental gravity ya dunia

Yale yanapopita yatakuachia upepo fulani ndio hayo mauzauza yale yanayovutika kuja ndio majinamizi
Kwahiyo haishauriwi kulala chali kwakuwa unaalika nguvu zisizofaa kualikwa

Angalia ibada nyingi za kishetani humlaza mtu akiwa uchi chali ameangalia juu

Mkuuu asante yaan umenifundisha jambo.
Ila mkuu mmmhhhhh wew noumaaaa
 
Pia kisayansi ukilala chali unadisturb equilibrium ya ubongo na moyo ndo sababu ya kisayansi ya hayo mauzauza. Inashauriwa usilale usingizi ukiwa chali position. Vifo vya ghafla usingizini pia usababishwa na kulala chali
atoto na we unalalaga chali dada'ngu? njoo huku umsikie shostito cute b na mauzauza yake, kumbe siku ile tunamtafuta alipatwa na mauzauza ya kulala chali bana

Acha tuu ndugu sijapata usingiziii wiki nzima ni mauza uza tuu
 
Last edited by a moderator:
Watu maneno kweli,ila ni sayansi ndogo tu kwamba tumbo linasaga chakula kama mashine kumbe ni suala la digestion system. Haliusiani na mengine kabisa.
 
Ukitaka kuota ndoto za kugegedana na demu chukua kanga isokote vizuri halafu itupe chini ya ufungu mwa kitanda kesho yake asubuh utakuta umetoboa godoro kwa kuligegeda!

18+ only

Duuuhhh mkuu umekomesha mbavu zangu kwa kicheko
 
Kisayansi ukilala chali ulimi unaweza kurudi nyuma na kuziba koo la hewa, na ndio maana unahisi kukabwa (kukosa hewa/kushindwa kupumua) kwa kuwa upo usingizini hauwezi kujitambua hivyo utahangaika hadi utakapoamka utaweza kuurudisha ulimi na utasikia ile hali imeondoka.

Asante mkuu maana nahisigi nakabwa na macho siwezi kuyafungua nateseka sanaaa
 
Mimi ni Sheikh Kifyatu na huu ndio utabiri wangu:

Katika siku za nyuma wewe ulimkwaza binti mmoja, mzuri sana, maji ya kunde, mtanashati, na anaishi kaskazini ya hapo ulipo.

Huyu binti alikwenda kwao kijijini hivi karibuni (na alikuaga), na aliporudi tu ndio hizo njozi zako mbaya zilipoanza.

Kafara lake:
Vunja nazi mbili mbata, weka vipingili viwili vya muwa hapo juu, kata miche saba ya mmea uitwao mvunja-hukumu na uiweke pamoja na hizo nazi na hiyo miwa.

Mishale ya saa saba usiku, nenda njia panda yoyote ile ilioko karibu na makazi ya huyu binti. Weka hili kafara halafu washa miche miwili ya UDI. Wakati unaondoka basi usiangalie nyuma. Matatizo yako yote yatakua kwishney.

Kama ukifanikiwa na nilichokwambia basi wape JF mchango wako sawa na mshahara wako wa mwezi mmoja.

Just kidding folks.

Leo niko kwenye mood nzuri ile mbaya.

Hahahahahahaaa
 
Kula vizuri, kunywa maji ya kutosha, oga kwa sabuni sahihii ya kuogea, lalia shuka safi, kitanda kiwe kizuri, chumba kiwe na hewa ya kutosha, na akili iwe na uhakika wa kesho, hata ulale kichwa chini miguu juu huwezi ota ndoto za ajabu.

Mkuuu mimi haijalishiii aisee nitaota tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom