Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,266
- Thread starter
- #121
sheikh Mohamed, nina imani hekima yako ni zaidi ya hilo jawabu lako japo juu.
tafadhali sana soma katikati ya mistari nilichokiandika. ninaweza nisiwe mweledi sana kukuzidi, lakini ninaamnini sauti yangu ya unyonge inaweza kuwa imebeba wito maalumu unaostahili kusikizwa nawe.
tafadhali sana sheikh..
M Mbabe,
Tafadhali sana na mimi nakuomba kwa unyonge, umasikini, kokosa elimu
kwetu na fursa zote hebu nasi tusikize juu ya hii hali yetu.
Naamini nawe una uwezo wa kuelewa historia ya wazee wangu na nini
walifanya, na shida walizobeba kwa matumaini mema ya baadae.
Tuijue historia yetu itatusaidia.
Tafadhali sana ikiwa hujasoma kitabu changu soma na uwaone wazee
wangu.
Ukiwajua wazee wangu utanijua na mimi na ninaposimamia.
Kalamu yangu naamini siku zote inaandika ambayo yanastahili kusikizwa
na watu wakatafakari.
Nasikitika kuwa badala ya jibu kutolewa na wahusika.
Jibu unatoa wewe.
Mimi niko chini ya miguu yako.
Msitupuuze.
Tusikizeni kilio chetu.