Jiko la gesi

EPORA

Member
Apr 8, 2012
83
16
Habari wakuu jf!jamani mwenzenu nina swali kwa wale watumiaji wa jiko la gesi,swali ni je?naweza kupikia jiko la gesi afu at the same time liko karibu na jiko la mkaa lenye moto je kuna madhara yoyote ?
 
Epora just out of interest. Kwa nini unatumia vyote mkaa na gesi na sio kimojawapo?
 
Epora just out of interest. Kwa nini unatumia vyote mkaa na gesi na sio kimojawapo?

Ukipika ubwawa kwa mfano, gesi haiwezi kukupatia mahaba, so unatumia mkaa kuyatengeneza
NB, Mahaba= ukoko
 
Ukipika ubwawa kwa mfano, gesi haiwezi kukupatia mahaba, so unatumia mkaa kuyatengeneza
NB, Mahaba= ukoko

Ukoko mbwembwe jamani unatakiwa ukipika ubwabwa sufuria linabakia safi kabisa harafu ukoko ni upotezaji wa resources so ni vyema kuuepuka maana vyakula vinavyopanda bei harafu unaweka na mbwembwe tena aise inakuwa shughuri
 
wadau nashukuru sana hofu ilikuwa madhara yake!
 
Kwa mliotumia gesi kwa muda mrefu hivi mtungi ule wa ujazo wa gesi kg15 kwa makisio unaweza ukapikia kwa muda gani kwa familia ya watu watatu?
 
Gesi si nafuu tena!!! Mkaa ni nafuu kuliko gesi na umeme!!! JAPO KAMPENI ZINASEMA KINYUME CHAKE
 
Kwa mliotumia gesi kwa muda mrefu hivi mtungi ule wa ujazo wa gesi kg15 kwa makisio unaweza ukapikia kwa muda gani kwa familia ya watu watatu?

uneza tumia kwa miezi miwili,. Vinginevyo itategea na matumiz yako uneza ukatumia chini au zaidi miezi miwili
 
Kwa mliotumia gesi kwa muda mrefu hivi mtungi ule wa ujazo wa gesi kg15 kwa makisio unaweza ukapikia kwa muda gani kwa familia ya watu watatu?

kama mnapika milo yote mitatu kwa uhakika bila kubahatisha tena bila kutumia mkaa wala kuchemsha maji ya kunywa ni mwezi mmoja tu...yaani very expensive than we ave thought b4.
 
Gesi si nafuu tena!!! Mkaa ni nafuu kuliko gesi na umeme!!! JAPO KAMPENI ZINASEMA KINYUME CHAKE

uko sawa kabisa, wanatulaghai watz, kuna wakati huku iringa gesi ilifika 62000 kwa kg15 afu nilikuwa na ugeni kdgo ilitumika siku 22 tu, yaani ful uhuni, afu mitungi mingine hawaijazi vzri.
 
acha uongo, anakuwa akipika nn? Labda chai tu!

kwanza koma kuniita muoongo wakati hujui matumizi yangu.....

Pili ndo maana nikasema inategemea na matumizi yake anapika mara ngpi,

tatu kwa nini uchemshe chai kwenye jiko waka jug za umeme zipo?

Nne kutumia gesi muda mrefu au mfupi ni uamuzi wako, mfano wali ni iwenye rice maker, gas ni unaweza chemsha maharage(pressur cooker inahusika) ya wiki nzima then unayaweka kwenye frezer kazi yako ukirudi jioni ni kuunga tu....

Kazungumzia watu 3, nimeassume wanajishughulisha, obvious kupika ni jioni that means gas hutumika jioni tu........

Siku zote kwenye nyumba linapokuja swala la gas au mkaa kutumia ni akili kichwani mwako, mnoga kama nyama au maharage samaki vinaweza kuandaliwa weekend na weekdays ni kuunga tu, viambatanisho iwe wali ugali chapati vinaweza kupikwa kwenye siku husika.....

Mjini mipango, akili kichwani mwako......
Mie nanunua gas mara 2 au 3.
 
vitu viwili vina umuhimu wake mkuu,kuna vitu kama maharage inabid sometime vipatiwe jiko la mkaa

Ukinunua pressure cooker then you will not need chacoal. Cos ma-beans unayaloweka for 6hrs then you pressurerize them. Ikipiga kelele ya kwanza tu. Unazima moto after 15min. funua sufuria ma-beans yameiva.
 
Back
Top Bottom