Jiji la Mwanza linaongoza kuwa na mbu

Twin Tower

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
2,129
2,982
Nimetembea na kuishi kwenye baadhi ya majiji hapa nchini, ila jiji la Mwanza hapana.

Joto kama Dar, usafi ni changamoto sana. Inabidi vigezo vya majiji vifanyiwe tathmini upya isiwe hizo population na uwezo wa kukusanya mapato.

Hali ya mbu Mwanza ni kama wanafanya ufugaji.
 
Nimetembea na kuishi kwenye baadhi ya majiji hapa nchini, ila jiji la mwanza hapana.

Joto kama dar, usafi ni changamoto sana. Inabidi vigezo vya majiji vifanyiwe tathmini upya isiwe hizo population na uwezo wa kukusanya mapato.

Hali ya mbu mwanza ni kama wanafanya ufugaji.
Ila tuseme ukweli, suala la kwamba Dar kuna joto inategemea unaishi wapi kwenye mazingira yapi Mkuu. Kama wewe unaishi Mburahati, Bugurun na maeneo mengine yaliyobanana bila Mipango Miji utalalama.

Lakini ndugu yangu nenda huko pembezoni Kifuru, Kinyamwezi, Njoo mitaa ya Kishua Obay nk joto hakunaaaa. Mbu vile vilee maaana mazingira machafu yenye maji yaliyosimama huko Uswaz ndio makao ya mbu.

Uwe Mwanza Capripoint nk nk ulie joto na mbu?

Mkuuu tafuta pesa hutolalamika joto na Mbu
 
Kwa vigezo au Standard za kimataifa Tanzania hatuna Majiji

Kwa Africa Mashariki jiji ni Nairobi tu at least

Kwa mpangilio, miundo mbinu na ukosefu wa vitu muhimu bado hatuna majiji

Kama Tanga au Mbeya ndio kabisaa ni miji tu

Kwa Dsm tafuta tu VISA ya kusafiria...hola, barabara katikati ya Dsm ni za hovyo....michanga tu

Management ya kudeal na usafi wa jiji ni hakuna

Just b'se ina population kubwa ndio kigezo?
 
Nimetembea na kuishi kwenye baadhi ya majiji hapa nchini, ila jiji la Mwanza hapana.

Joto kama Dar, usafi ni changamoto sana. Inabidi vigezo vya majiji vifanyiwe tathmini upya isiwe hizo population na uwezo wa kukusanya mapato.

Hali ya mbu Mwanza ni kama wanafanya ufugaji.
Ulifanyanya Sensa ya mbu kwa nchi Nzima hadi ukaja na Conclusion Kuwa Mwanza ndio kuna mbu wengi?

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Hakuna wadudu wanakera kama Mbu,ila nadhani bado hujafika Kyela wewe!
 
Back
Top Bottom